Mwana Kwetu
JF-Expert Member
- Jul 12, 2011
- 652
- 562
Nazungumza kama supporter mkubwa wa CHADEMA na niliyemchagua Godbless Lema kama mbunge wangu. Niko mjini na niko mobile sana huwa nazunguka katika kata kadhaa za hapa mjini. Wananchi wengi ukiwasikia wanasema lazima waonyeshe support kwa madiwani wao waliowachagua kutokana na uamuzi waliotangaza jana. Mambo ya kamati kuu ya CDM haimsaidii mwananchi wa Kata ya Kimandolu, Sekei, Kaloleni n.k. ambao wanachotaka ni maendeleo na si migogoro ambayo haimaliziki. Wananchi walio wengi including viongozi wa dini wanaunga mkono muafaka na dhamira safi ya madiwani ya kutaka kuendelea mbele katika kuwatumikia wananchi na kuachana na malumbano.
Kutokana na mgogoro huu Lema ameanza si tu kupoteza umaarufu bali hata ushawishi kwa wakazi wa manispaa ya Arusha. Wengi tunaanza kumwona yeye na CHADEMA taifa kama watu wanaotafuta mambo yao binafsi na si kuwatumikia waliowachagua.
Naomba wajue wananchi wamechoka na hakuna mtu yuko tena interested na mvutano ambao siyo tu hauna mwisho bali ambao hauchangii hata asilimia 1% ya maendeleo katika kata zao.
Madiwani wameshikamana na wananchi kuliko Kamati kuu ya CDM inavyofikiri na kama watakosea wakawafukuza hawa madiwani basi wajue wamepoteza jimbo la Arusha kwa sababu watu hawa hawa ndio waliompigia Lema kura na hawatakuwa tayari kumpigia tena 2015.
Watu wanataka iwepo way forward na wasahau ya nyuma tujenge manispaa yetu na siyo kila wakati kutaka kuonyeshana misuli ya kisiasa kana kwamba ndilo lengo kuu la kuingia madarakani.
Please Lema anza kushughulikia malengo makuu ya maendeleo kama mbunge kwa mustakabali wa watu waliokuchagua kinyume na hapo tutakuona uliingia kwenye ubunge kwa personally motivated agenda na si vinginevyo. Kama hautafanya kazi kwa matakwa ya wananchi ndugu yetu hatutakuwa na jinsi zaidi ya kumtafuta mtu atakayeweza kufanya hiyo kazi.
Lastly but not the least namuomba sana Dr. Slaa asiwatishe tishe madiwani tuliowachagua kwani hakuwachagua yeye na hii ni sawa na kututisha sisi tuliowachagua. Dr. Slaa ni mtu mzima na atumie hekima na busara kulishughulikia hili suala haraka iwezekanavyo na kwa manufaa ya wananchi waliowachagua hawa madiwani. Tutaendelea kumheshimu Dr. Slaa kama atatuheshimu na kuelewa wale madiwani wana watu nyuma yao waliowachagua.
Sioni dhambi kukaa meza moja na CCM wakati huko bungeni mko na CCM na mnacheka nao. Sisi tuko nao pia huku mitaani, mahotelini, kwenye mabasi, kwenye nyumba za ibada n.k. Hawa ni wenzetu na tumetofautiana tu itikadi lakini hatuna uadui mkubwa kiasi hicho ambacho Lema anataka kuonyesha hapa Arusha. Ninamuomba Lema akue na aache mambo ya kuonyeshana ubabe ili tujenge nchi yetu kwani safari iliyoko mbele ni ndefu na kazi bado ni kubwa. Nitakuwa na uchungu mkubwa sana kama uzembe wa CDM utalifanya jimbo hili kurudi tena mikononi mwa CCM na mtakuwa mmepoteza sana credibility na support kwa jinsi ambayo itakuwa ngumu ku- reverse.
Mungu Ibariki Tanzania