Asema atakufa kulinda haki za wananchi
MBUNGE wa Jimbo la Arusha Mjini Godbless Lema (CHADEMA), ameonya juu ya uwezekano wa kuzuka kwa ghasia nyingine kubwa ikiwa uongozi wa halmashauri ya jiji hili unaoundwa kwa sasa na watendaji wa Chama cha Mapinduzi (CCM) utawahamisha kwa nguvu wakazi zaidi ya 24,000 wa eneo la Kaloleni kupisha ujenzi wa mji wa kisasa.
Lema akizungumza na Tanzania Daima juu ya mradi mkubwa wa ujenzi wa mji wa kisasa wa kibiashara katika eneo la Kaloleni jijini Arusha, unaotarajiwa kukamilika ndani ya miaka mitano ambapo jumla ya wakazi 24,000 watalazimika kuhama, alisema hawezi kukubaliana na mpango huo mbovu wa kutaka kuwahamisha wakazi wa eneo hilo kabla ya kufikiwa kwa mambo ya msingi na pande zote zinazohusika.
Mbunge huyo alisema kinachotaka kufanywa na uongozi wa jiji ni cha hatari na yeye kama mwakilishi wa wananchi wote hatakubaliana na mpango huo, badala yake ataungana na wananchi kuchukua hatua nzito na madhubuti za kuzuia jaribio lolote la kuwahamisha wananchi hao wa Kaloleni.
Aliutuhumu uongozi wa jiji chini ya meya mwenye mgogoro, Gaudence Lyimo, kwa kutumia mabavu kuamua mambo yanayohusiana na uhai na utu wa mtu kwa sababu ya fedha za wawekezaji.
Akifafanua juu ya jambo hilo, Lema alisema madiwani na uongozi wa jiji wamefikia uamuzi huo kutokana na kiwewe baada ya kupewa ufadhili wa kwenda Dubai na kulipiwa mamilioni ya fedha na mwekezaji huyo kwa kile kinachodaiwa kuwa ni kujifunza namna miji ya wengine ilivyojengwa kibiashara.
Mimi siko tayari kupokea fedha hizo chafu ili kuwasaliti wananchi wangu. Nitasimama imara na masikini wenzangu kutetea haki, utu na heshima yetu kama wanadamu katika ardhi aliyotupatia Mwenyezi Mungu, alisema.
Hata hivyo, mbunge huyo alisema kimsingi hapingi kuwapo kwa shughuli za maendeleo katika jiji hilo, lakini akadai kutokubaliana na taratibu zote zilizofikiwa kumpata mwekezaji huyo, ikiwa ni pamoja na kutowashirikisha wawekezaji wazawa katika mchakato mzima wa zabuni.
Nieleweke tangu awali kuwa mimi sipingi kuanzishwa kwa eneo la mji wa kisasa, wala shughuli za maendeleo kwa watu wa arusha. Nikifanya hivyo nitakuwa mbunge wa ajabu sana na hata chama changu kitanishangaa. Ninachokataa ni ukikukwaji wa mambo mengi ya msingi, ikiwa ni pamoja na kutowashirikisha wananchi watakaohama kupisha mradi huu.
Kwanza huyo meya wao aseme lini tenda hii ilitangazwa na ni Watanzania wakazi wa Arusha wangapi walishirikishwa. Kama hilo halikufanyika, siwezi kukubaliana na mpango mzima na lazima tuanze upya, alisema Lema.
Aliongeza kuwa ni jambo la kushangaza kwa chama kinachodai kujali wananchi wake kwenda kuwabeba wawekezaji wa kigeni na kuwaacha Watanzania wenye uwezo mkubwa wa kujiendeleza na kuendeleza nchi yao.
Mji huu umejengwa na kuendelezwa na wananchi wenyewe, na hata ule wa Moshi. Sasa imekuwaje hata katika mradi huu wasihusishwe na wadharaulike?
Lema alidai kuwa mapema wiki hii, kuliitishwa kikao maalumu cha madiwani na viongozi wa halmashauri na kuhudhuriwa na mwekezaji huyo kikiwa na nia ya kupanga mikakati ya kuanza kwa ujenzi huo.
Nimepokea taarifa kwamba baadhi ya madiwani wa Chama Cha Mapinduzi, wakiongozwa na mtu anayejiita meya pamoja na wakurugenzi wa kampuni hiyo wamekubaliana kuanza ujenzi katika eneo la Kaloleni haraka iwezekanavyo.
Huu ni usaliti kwa wananchi kwa sababu, hakuna maandalizi yoyote makini yaliyofanywa, wala mimi kama mbunge sijashirikishwa na wananchi wangu hawajakubaliana na mamlaka hiyo katika mambo mengi ya msingi, alisema Lema.
Aliongeza kuwa suala la kuwahamisha watu si la mzaha na linahitaji maandalizi makini, ya haki, yenye masilahi na yaliyokubaliwa na kila upande unaohusika.
Haiwezekani kuhamisha watu bila kwanza kukaa na kukubaliana nao wapi wanakoenda, wanakwenda kwa utaratibu gani na wanalipwa kiasi gani, lini na kwa njia gani fidia ya nyumba na mali zao, alisema.
SOURCE:TANZANIA DAIMA