Anna Nkya
Member
- Oct 21, 2021
- 69
- 341
Jana Lema alikuwa Serena Hoteli kwenye mjadala uliohusu uwekezaji kwenye maeneo mbalimbali ya nchi yetu ikiwemo bandari. Alikuwa pale na kina Mzee Ulimwengu, Rostam Aziz, Wasira na watu wengu wengine. Kwenye meza yake, Lema alikaa na Zito Kabwe na watu wengine mashuhuri.
Lema alipochangia, alianza kwa kutete kauli ya Mbowe ambayo baadhi ya watu wameitafsiri kama ubaguzi. Lema hakupindisha maneno kusema kwamba watu wanatumia kauli za Mbowe kukwepesha mada.
Kuhusu uwekezaji unaotaka kufanyika bandarini, Lema alionekana wazi kwamba anaunga mkono uamuzi wa kuleta wawekezaji katika bandari ya Dar es Salaam. Baadhi ya kauli za Lema zinazodhibitisha hilo;
1. "Nchi hii inahitaji muwekezaji zaidi Bandarini"
2. "Hakuna mtu anakataa uwekezaji, na hakuna namna Tanzania inaweza ikasurvive bila uwekezaji"
3. "Kukataa uwekezaji ni jambo baya sana"
Kisha Lema alichangia kwamba mkataba unaotarajiwa kuipa DP World kazi, ni vyema ukatazamwa na kuboreshwa.
Alitolea mfano wa vifungu vinavyodaiwa kwamba vitaipa DP World bandari zote za Tanzania, lakini alieleweshwa kwamba haiko hivyo; DP World wanapewa baadhi ya maeneo ya bandari ya Dar es Salaam na hawawezi kwenda kwenye bandari nyingine mpaka pale Mamlaka ya bandari Tanzania itakapojiridhisha na kuchagua maeneo tunayohitaji uwekezaji zaidi.