Laptop ya JK yatoweka kiutatanishi!

Wanabodi,
Jamani hizi habari za kweli ama ndio habari za jioni kijiweni na moja baridiii pembeni..
Kama kweli imetokea hivyo wakuu msifanye mzaha hata kidogo, hili linawezekana kuwa swala zito na gumu kuliko mnavyofikiria.. Kwanza tukizingatia maneno ya Mtanzania - Laptop iliyopotea ni ya RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA na sio ya JK.
Na yote mliyoyazungumza iwe kuna bongo flava, picha za Utamu na kadhalika kitu muhimu nikuelewa kwanza Ndivyo Tulivyo...
Rais wetu kutembea na laptop ni moja ya Ulimbukeni wetu ulotokana na Umaskini wa hali na mali..Nasema hivyo kwa sababu sijawahi kuona kiongozi akitembea na Laptop mkononi ama imebebwa na mtu wakati wa msafara wa rais isipokuwa Bongo tu. Viongozi wengi kama sio wote hubeba Laptop kila waendapo wengine huziacha mahotelini na kadhalika..na uwezekano wa kuwemo habari nyeti za Kitaifa ambazo zinaweza kuhatarisha Usalama wa taifa ni kubwa sana..
Kumbukeni marehemu Chacha Wangwe na hadi leo kilichoibiwa ktk ajali ile ni laptop tu..Pia nilisikia karamagi ewakati anafunga deal la Buzwagi hotelini laptop ilitumiwa sana tu na wajanja waliweza ku access info za mkataba huo kutokana na hiyo laptop yake..(msije nisulubu hivyo ndivyo nilivyosikia) sina hakika na maneno haya..
Mimi nadhani swala hili ni zito sana kuliko tunavyofikiria na kuna haja kubwa ya kufanya msako mkubwa iwe kama mtu kaingia ktk server ya FBI ama CIA..
 
ndiyo imepotea tangu jana; hadi hivi sasa sijui kama imepatikana au vipi. Jana walisema ilikuwa "misplaced" na walikuwa wanajaribu kui "locate"...
 
Mkandara kwa chacha wangwe hata simu ya mkononi iliyeyuka sio laptop tu , hiyo laptop ilikuwa imeunganishwa na zantel cdma sasa nashangaa kwanini line hiyo bado iko wazi ni nani anaitumia email address ziko active nani anazitumia ?
 
Siijui sana lugha ya Malkia lakini tofauti ni nini hasa ? "Misplaced," "lost", "unlocated," "unfound"....yiddy yaddy yiddy....comical Ali Rweyemamu sijui ata spin vipi.
 
Si nasikia magereza yao maalum yalishajengwa? Tatizo ni VIP ones!

Mkuu inawezekana wenye lap top ni mafisadi wanaotaka kujuwa whats going on in terms of their fate?
Kama nilivyosema hapo awali...Grupu mbili zinaitaka lap top..Lakini kwa jinsi mjadala huu unavyokwenda....Naweza kudhani kuwa ni mafisadi wanataka kunusa nusa assuming habari hizo za jela nzuri wanazojengewa ni za kweli.
 
Mkandara kwa chacha wangwe hata simu ya mkononi iliyeyuka sio laptop tu , hiyo laptop ilikuwa imeunganishwa na zantel cdma sasa nashangaa kwanini line hiyo bado iko wazi ni nani anaitumia email address ziko active nani anazitumia ?

Usalama umegawanyika mkuu...Sasa ni tit fo tat.
Kama lap top ya Wangwe someone anayo..Then ni mwendo wa kufuatiliana kijasusi...Ni source yote inatafutwa...Watu hawajui wanadai movie...Kuna mambo yanaendelea sasa hivi ambayo ni kama movie tu.
Unashangaa Rais mwenyewe anaambiwa awahi ikulu faster faster kabla ya giza halafu manaona ni easy?
Kiutaratibu wananchi ndio huambiwa wawe ndani ya nyumba zao kabla ya giza endapo nchi iko kwenye hali ya hatari.
Sasa aliye na lap top ya Wangwe anajuwa kila kitu kuhusu mpango mzima wa upinzani pamoja na mambo binafsi ya wangwe na kuhusiana na chama chake nk.
Na aliye na lap top ya mkuu wa nchi naye ana uwezo wa kuona mambo mengi sana na pia kujuwa current and future plans.
Ni sawa na mtu mwenye uwezo wa kutizama through ya clothes magically licha ya kwamba everybody else sees you with outfits.
Mpambano uko ndani kwa ndani....Kama ningekuwa movie producer sasa hivi ningeshakuwa na bonge la movie nisikufiche.
Hata hapa jf unaweza kutumia mijadala humu ndani na kupata bonge la movie lenye kubeba ujumbe wenye reality....For sure it has been done.
History iko hapa.
 
Kuna umuhimu sana sasa kwa watu muhimu katika serikali wawe wanatumia hizo laptop kama client za kulogin katika system tu ila kazi na mambo yote yawe yanahifadhiwa katika server maalumu online kwahiyo hata wakichukuwa laptop watakuwa wamekosa mengi na hizi laptop na vyombo vingine vya mawasiliano viwekewe vitu muhimu vya kuzilanda na kuzitambua popote zinapokuwa
 
Kuna umuhimu sana sasa kwa watu muhimu katika serikali wawe wanatumia hizo laptop kama client za kulogin katika system tu ila kazi na mambo yote yawe yanahifadhiwa katika server maalumu online kwahiyo hata wakichukuwa laptop watakuwa wamekosa mengi na hizi laptop na vyombo vingine vya mawasiliano viwekewe vitu muhimu vya kuzilanda na kuzitambua popote zinapokuwa

....hiyo server ukifanikiwa kui-hack utatujulisha, au?!!
 
Steve naomba msipotoshe jamii kuhusu mimi , mimi sina uwezo wala ujuzi wa kufanya vitendo hivyo natoa ushauri tu ila kama ikiwa hacked au kufanywa chochote na wanahitaji kusaidiwa katika kuhakikisha wahusika wanatafutwa basi tunaweza kushauriana katika kuhakikisha wanapatikana popote walipo ------------ hii ni dunia ya habari na mawasiliano wabongo lazima wajiandae na mambo kama wenzetu rwanda wako mbali sana
 
Shy ameonekana kama ni mtu mwenye wasiwasi mkubwa toka member mmoja amwambie kuwa Shy aliwahi kuanzisha topic kuwa lap top zinaibiwa sana na pia yeye kudai kuwa kuna movies kibao kwenye lap top ya Mh Rais.
Shy lazima utakuwa unajuwa mambo mengi sana ila acha kupanic.
Kama si wewe, si wewe na kama ni wewe, ni wewe...At the same time kama unajuwa, unajuwa na kama hujui, hujui.
Hivyo basi inawezekana kuna movies ndani ya lap top kama ulivyosema na inawezekana hakuna...Pia unaweza ukawa unajuwa siri.
 
Jmushi -- mimi najaribu kufanya suala hili liwe la kitaalamu zaidi kuliko kulifanya la kisiasa , ndio imeibiwa sasa tuafanye nini kitaalamu kwa siku zijazo incase kukitokea mambo kama hayo ? Tusifanye suala hili ni la kisiasa hamna kisiasa hapo , wataalamu njooni tujadili au mada ipelekwe kule kwenye it
 
Inawezekana wewe uko mbele zaidi kwasababu labda una more info zaidi ya wengi wetu hapa.
Watu bado tunatafakari kilichomo kwenye lap top wewe unazungumzia kuprevent...Uko very fast.
Hujawahi kujuwa mambo ya investigative report? Kwanza lazima tuwe na feedback.
 
Hiyo imeshatokea sasa tujilinde wasije kuiba kingine na kingine zaidi na zaidi , kama wameweza hiyo watakuwa na mipango kabambe zaidi lazima wenye kuwa na hizo vitu wahakikishiwe usalama navyo kwanza wakati mengine yanaendelea
 
Yes inawezekana ndio maana nikasema mada hii ihamishiwe sehemu husika ili tuweze kulichambua vizuri , tutembelee hata katika office hizo tujue wanaziprotect vipi na tunaweza kusaidia vipi

kuna wakati laptop ya system administrator wa celtel iliibiwa , ilivyopatikana ikawa haina pwd na acont yake ni administrator unaona mambo kama haya ? Watu wanafanya nini huko makazini ??
 
Mara nyingi watu wanapoongelea Security kwenye IT wanafikiria zaidi network security, nikiwa na maana vitu kama Firewalls, Anti-virus, anti-spyware etc. Kosa kubwa sana watu wanalofanya ni kuto consider physical security na kuweka policies madhubuti kwa usalama wa data na vifaa.

Katika information security kuna vitu vitano:
1. Physical security
2: Access security
3: OS security
4: Network security
5: Personal security

Mara nyingi physical security na personal security watu hawazingatii na ndiyo zina madhara makubwa. Kwa mfano utakuta mtu anabeba laptop begani kila siku anaenda nayo kazini jioni anarudi nayo wakati nyumbani hafanyi kazi kila usiku. Akipita baa anapita nayo anaweka chini ya meza, au anaacha kwenye gari inaonekana kupitia vioo. Haya mambo yote ni uzembe wa hali wa juu. Ukisoma kwenye tovuti ya jeshi la polisi, utakuta kuna tips nzuri kuhusu usalama wa mali na ofisi.

Pili, personal security - Je ni kwa kiasi gani una wa trust watu wanaokuzunguka au wanahusika na mambo ya information management kazini? Je watu hao wamepewa au wanayo elimu ya usalama? Je ni waaminifu? Ulifanya uchunguzi kabla ya kuawaajiri? Ni wa ajiri wangapi kabla ya kumuajiri mtu wanaenda kucheki record polisi au usalama wa taifa? Ukweli ni kwamba 90% ya wizi au upotevu au kuvuja kwa data kunafanikishwa na watu wa ndani. Je kampuni/taasisi ina code of conducts kuhusu usalama na mali za kampuni? Ni kuna mechanism ya kuhakikisha kuwa zinafuatwa? Hayo ni mambo ambayo na uhakika yakifuatwa jambo kama hili haliwezi kutokei. Amina
 
Steve naomba msipotoshe jamii kuhusu mimi , mimi sina uwezo wala ujuzi wa kufanya vitendo hivyo natoa ushauri tu ila kama ikiwa hacked au kufanywa chochote na wanahitaji kusaidiwa katika kuhakikisha wahusika wanatafutwa basi tunaweza kushauriana katika kuhakikisha wanapatikana popote walipo ------------ hii ni dunia ya habari na mawasiliano wabongo lazima wajiandae na mambo kama wenzetu rwanda wako mbali sana

Sawa Shy nimekuelewa. Tutashirikiana ipasavyo, kukiwemo kule kukosoana sisi kwa sisi maana hamna binadamu asiye na hitilafu, sema hitilafu hizo zinatofautiana tu.
 
Serikali na idara zake naamini wana policy maalumu ya kulinda yote hayo kama hawana basi itakuwa hatari sana na maajabu ya kipekee , kama hawana policy inabidi ziandaliwe na kila mfanyakazi asome na kuweka sahihi kabla ya kuajiriwa au kabla hajaamua kujihusisha na mambo kama hayo

hivi bwana mnyama kuna database ambayo naweza kupata majina ya wahalifu yote bila kukosea ? Kwa uzoefu wangu kesi nyingi za uhalifu unakuta wanaandika majina tofauti na hazifiki kwa wakuu wao

mfano kijana mmoja anayeitwa darskendo ni maarufu sana kwa wizi wa laptop huyu akipelekwa polisi huwa haandiki jina pale , polisi wakienda kuita majina huwa wanasema( sina jina ndio nani ? ) unaona mtu baada ya siku anadunda mitaani mambo kama hayo
 
Back
Top Bottom