Puppy
JF-Expert Member
- Oct 6, 2011
- 2,995
- 2,494
Kwanza kwa Masikitiko makubwa natoa salamu zangu za Rambirambi kwa familia ya Marehemu Bwanaa Daudi Mwangosi, Channel Ten, Waandishi Wa Habari na Wapenda maendeleo wote. Mungu aipumzishe roho ya marehem mahali pema peponi.
Naanza kwa kuwaambia wanataaluma ya habari, Ni Heri umfadhili Punda atakubebea mizigo kuliko kufadhili fisadi.
Ni katika matukio mengi tu toka napopata akili ya kujua jema na baya waandishi mmekuwa mkilalamikiwa kupindisha ukweli au kuuficha kabisa. Na hilo nimelidhihirisha mwenyewe katika baadhi ya matukio niliyoyashuhudia LIVE tukioni. Kama lile Tarehe 5 Januari 2011 Arusha. (Sitorudia maelezo yake, asante to JF ukweli ulifahamika).
Hao mlokuwa mkiwasaidia either sababu
1. Mnapewa rushwa
2. Mnamlinda mwajiri wenu
3. Mnajipendekeza kwa mwajiri
Etc,
sasa wameanza kuwafanyia nyie yale walotufanyia na mkawasaidia kuyaficha.
"Bomu la Machozi", "kitu kizito" au "flying object" sasa limelenga na kumuua hapo hapo kipenzi chetu mwaandishi mwenzenu ndugu Daudi Mwangosi (R.I.P), kaa ukijua kwa ishara hiyo lolote lawezekana. Maana wanajua ninyi hamna guts za kufanya uchunguzi wala kuhoji, so wataweza ku-claim chochote kile apendacho kusema ndio kiliua au si ajabu hata ku-pin hii kesi kwa mmoja wenu.
Nguvu mlio nayo ni kubwa mpaka mkaitwa the "4th Estate" nyuma ya Executive(1st Estate),
Legislature (2nd estate) na Judiciary (3rd estate), mbele ya
Organised Crime (5th Estate).
Lakini ninyi kwa njaa au uoga mmekuwa wadogo mkawa dependants wa wadogo zenu the 5th Estate, mmeshindwa kujiamini na kujitegemea, hamuwezi kusema kweli. Ninyi wenyewe mnakatishana tamaa, msema kweli anatengwa.
Gazeti la MwanaHalisi limefungiwa mmekaa tu kimya, Jerry kashikishwa kesi mmekaa tu. Na sasa mwenzenu, Mtanzania mwenzetu kauwawa tena on field, mtafanyaje?
Je Mtakaa kimya upepo upite?
Je Mtakubali pesa muudanganye Umma?
Je Mtageuza kifo cha Daudi mtaji wa kupokea na kuomba rushwa a.k.a vibahasha?
Je sasa mtaona kama wakati umefika na kusimamia kweli na haki??
Sisi wananchi tunangoja kuona nini itakuwa reaction yenu, na je ina manufaa kwetu sisi na Taifa.
Msiogope, Tunachopigania leo ni kwa ajili ya maisha yetu na watoto wetu kesho. Wengi tutaumia, tutalemaa, tutafungwa na wengine kuuwawa lakini tusitishike tusonge mbele. Hata wazazi wako walijinyima ndio mana leo angalau unaweza hata kusoma hii post.
Watoto wanaozaliwa kwa siku ni zaidi ya mara mia ya risasi zinazotengenezwa kwa siku, Hatutaisha wote, kuna watakaobaki kuelezea Stori hizi za ukombozi.
Rest In Peace Daudi Mwangosi.