Silent watcher
Member
- Oct 20, 2011
- 25
- 3
Wasallam!Kama mwanajukwaa nitumie nafasi hii kutoa maoni yangu kwa kutumia elimu ya sayansi ya jamiii niliyoipata pale Mlimani pamoja na exprience yangu ya maisha juu ya kifo cha mpendwa na mwanaharakati mwenzetu Daud Mwangosi. Kwanza nianze kwa kutoa salamu zangu za rambirambi kwa familia yake na wapenda haki na wanaharakati wa mageuzi hapa nchini.Pili nitumie fursa hii kutoa maoni yangu.Ndugu wanajamii,serikali ya CCM kama ilivyo kwa mfumo wowote wa kisiasa umekwisha zeeka na hivyo ni kuukuu.Mfumo huu umeshindwa kuwateka wananchi kifikra kwa kuwaletea maendeleo na hivyo badala yake njia pekee iliyobakia kwao ni matumizi ya rushwa,vitisho na mauaji.Nchi kwa sasa haijiwezi imefilisika,makarani wa sensa wanalipwa ujira wao kwa mafungu katika nchi ijaayo maziwa na asali.Mfumo huu mpaka utakapokuwa unafika mwaka wa ukombozi 2015 utakuwa umegharikisha raia wasikuwa na hatia wengi sana lakini hilo halitawasaidia wala kuwafaa maana mwisho wao utafika kama ilivyo ada. Kwa upande wa kifo cha Mwangosi ni kweli inasikitisha kwa familia ya marehemu na kwa umma wa Watanzania wapenda haki lakini kifo chake ni sadaka ya ukombozi kwa wanyonge na walalahoi wa nchi hii.Tukumbuke waandishi wa habari ni askari wa kwenye uwanja wa mbele wa mapigano licha ya kutokuvaa sare(yaani SOLDIERS WITHOUT COMBAT UNIFORMS).Waandishi wa habari na mafanani ni wapiganaji wanaotumia KALAMU NA KARATASI kama BUNDUKI NA RISASI.Tukumbuke A PEN IS MIGHTIER THAN A SWORD.Na hao waliofanya mauaji pamoja na mwajiri wao wakumbuke ya kwamba HAKI YA MTU HAINYIMWI KABISA BALI INAWEZA KUCHELEWESHWA TU.Damu ya Mwangosi pamoja na wanaharakati wengine haijamwagika bure!Surely, they havent died in vain!