Kwanini "Service charge" ya TANESCO ni tatizo linalohitaji utatuzi wa haraka!

Ni kweli ni unyonyaji sana lakin siku hzi tanesco wamepunguza gharama kwa watu wanaotumia chini ya unit 75 per month unatolewa service charge ewura na rea na unit moja unanunua 150 per month nenden mchekiwe kwenye system issue ni nyumba za kupanga matumiz huwa makubwa sana kuliko mwenye nyumba yake
Mbona sehemu nyingine ukienda unaambiwa kwamba huduma hiyo ilishafungwa.
Why?
 
Really terrible, tunanyonywa mpaka tumezoea! Kwa hakika inahitajika waondoe vijigharama fichama hivi ambavyo wanyonge ambao makato haya ni regressive wanaumia sana.

Ni wakati sasa watambue kwamba wananchi wanafahamu haya mambo. Na hizi gharama za kificho zikipungua watu watanunua umeme, hakutakuwa na mtu anaiba umeme, watu wataipenda kampuni hii ya umma, wakisikia transformer inataka kuhujumiwa watashiriki kuokoa hasara, LAKINI ni mpaka hawa na TRA watambue kwamba kila pande iwe na haki pamoja na kutimiza wajibu...
Ukweli haya ndiyo mambo ysnayopaswa kupigiwa kelele ssna na wabunge wote bila kujaki itikadi za vyama vyao. Servicr ni wizi kwsni toka nimefinga umeme miaka 18 iliyopita sijawahi kuons tanesco wakija kufanya service yoyote lskini nakatwa kila mwezi 5,520 eyi ni service au fixed cost. Huu ni wizi. Waziri kivili wa nishati ns madini hii ndio ongekuwa hoja yake kubwa bunge likiaanza. Mtu akiitisha maaandamano ya amani kupinga wizi nami lazima niwemo hata kama wstatumia mgari yso ys wshawasha waliyonunua kwa ajili ya uchaguzi hakafu yskakosa kazi. Yale sasa ndiyo yatumike kuzoa marundo ya taka mitaani kwani vinginevyo yatakuwa yanaoza tu kwa kukosa kaxi labda wayakodishe kwenye nchi zenye vurugu
 
Kwanza naomba usipotezwe na maneno ''service charge'' ufikirie ni gharama ya Tanesco kuja nyumbani kwako kufanya service. Hizi fedha zinatozwa kwa sababu ya gharama za ku-mantain zile line za umeme kutoka kwenye source ya umeme mpaka pale nyumbani kwako. Kwa kifupi ni gharama za ku-transmit umeme kutoka from the source to the end point. Ni kama unavyoagiza pizza ukiwa nyumbani... inabidi ulipe gharama ya pizza na gharama ya kuletewa. Na hii service charge ipo sehemu nyingi duniani. Mara yangu ya kwanza kuishi nchi moja Europe nilichukua likizo ya miezi mitatu. Niliporudi nilikuta bill ya umeme inanisubiri (tulikuwa tunalipa bill kila baada ya miezi mitatu). Ilikuwa ni bill ya kipindi kile ambacho sikuwepo. Nikaenda kuulizia vipi nichajiwe umeme ambao sijatumia? Jibu nililopata ni ''hizi ni gharama za service! Yaani utumie umeme au usitumia, lakini kama umeingia contract ya kununua umeme wao ni laizima kuna basic cost ambayo utalipa plus gharama ya umeme. Labda uniambia kuwa hizo gharama za service ni kubwa sana Tanzania nitakubali...

Maelezo mazuri but the logic is inflammatory wanayo maintenance budget, tena very specific kutoka kwenye normal revenue hii tunayonunulia umeme; Pesa nying tena nyingi mno inautumika kulipia makampuni yanayo wapa umeme; Songas, ;na wale wa Tegeta ni mfano. Kwa uhalisia, na taarifa zote zinaonyesha kwamba hawapati faida (Net profit) kwa sababu ya gharama ya uendeshaji, lakini, wanaweza kuwalipa hawa jamaa, first thing in hand... Jiulize!

Hii siyo sahihi kabisa, kama wana guts basi waweke mapato na matumizi yao pale uone pesa inavyogaiwa kwa wenye mikono mirifu, tena wengi wapo katika nafasi za juu ki siasa.
 
Service Charge bila VAT ni 5520, ukiweka VAT 5520+(22%) Jumla ya service charge Tsh. 6734.4 NA SIO Tsh. 7400 KAMA ULIVYOSEMA.
Basi anayewekaga umeme ananidananyaga,maana nampa hela ananiambia makato n 7400
 
Kwa ufupi ni gharama za uendeshaji kwa kiswahili sahihi, je ni nani anayetakiwa kulipa gharama hizo ? Ni mtumiaji wa hiyo bidhaa husika na upande Wa Tanesco ni mteja.

Hizo gharama kama mita imeharibika kuvadilisha, kuna gharama nyingi ambapo mteja hupata huduma bila kutozwa kiwango chochote na pesa ya service charge ndio inayogharamikia.
Koleba,
Nimependa sana jinsi ulivyojitoa kuelimisha watumiaji wa umeme,
Hiyo service charge umejaribu sana kuitetea na kwa upande wako uko sawa. Unasema matumizi yake ni kama kwa mfano mita imeharibika mteja hubadirishiwa, naomba nikuulize swali, hiyo mita ni ya nani....Ni mali ya mteja wa TANESCO au ni mali ya TANESCO? Kama ni mali ya TANESCO unataka kuniambia mteja ndiye anatakiwa kuingia ghalama ya kuitengeneza? Natoa mfano kwa mfanya biashara ya Hotel,mteja anatakiwa kulipia service charge ya kulalia kitanda(Nje ya bei ya room) kwamba hata kama kitanda kitaharibika kitatengenezwa bila mteja kutozwa pesa?
Tusaidie pia tujue kwa nini mnatulipisha ghalama za EWURA na REA?
 
TANESCO waliwahi kupeleka hati ya maombi ya kuongeza bei kwa muda ( Sikumbuki lilikuwa bunge la ngapi), wabunge walikuikubalia TANESCO kuongeza bei kwa makubaliano ya baada ya muda washushe. Nafikiri muda haujafika.

Binafsi umenikuna sana kwanza,huwa sipati jibu ya hizo tozo zitozwazo na TANESCO.

18% VAT haina tatizo inaeleweka
1% EWURA ya kazi gani? Kama ni kitengo kilianzishwa na serikali kwa nini serikali isiwajibike na vitengo vyake kwa hiyo 18%?
3% REA ili iweje,kama mtu unapanua biashara, mtaji si uwe wa kwako? Watumiaji kulipia umeme vijijini,kwani hao watu wa vijijini hawaliipii service line?

Service charge kwa siku hizi ni wizi mtupu.

Mabenki (baadhi) wana account zinazofanana na LUKU, kwa mfano Standard Chartred bank wanayoinaitwa HIFADHI current account- Pay as much as you consume", hii account haina charge yoyote ya mwezi( No single cent charged) wanakucharge tu pale unapotumia.

LUKU ni the same, walitakiwa watucharge tu pale tunapotumia plus 18% VAT hizo charges nyingine ni wizi mtupu!
Tanesco ni janga la Taifa,Muhongo katoa Tamko juzi juzi hapa hata sijui nchi hii lini itaunda mahakama ya kusimamia matamko ya serikali.
 
Koleba,
Nimependa sana jinsi ulivyojitoa kuelimisha watumiaji wa umeme,
Hiyo service charge umejaribu sana kuitetea na kwa upande wako uko sawa. Unasema matumizi yake ni kama kwa mfano mita imeharibika mteja hubadirishiwa, naomba nikuulize swali, hiyo mita ni ya nani....Ni mali ya mteja wa TANESCO au ni mali ya TANESCO? Kama ni mali ya TANESCO unataka kuniambia mteja ndiye anatakiwa kuingia ghalama ya kuitengeneza? Natoa mfano kwa mfanya biashara ya Hotel,mteja anatakiwa kulipia service charge ya kulalia kitanda(Nje ya bei ya room) kwamba hata kama kitanda kitaharibika kitatengenezwa bila mteja kutozwa pesa?
Tusaidie pia tujue kwa nini mnatulipisha ghalama za EWURA na REA?

Asante Mkuu kwa swali zuri, ni kweli kabisa mita ni mali ya TANESCO, lakini kumbuka TANESCO haitengenezi hizo mita, mita zinanunuliwa na mbali ya hivyo kunavitu vingi Kama cable, mafundi wanapokuja kwa mteja pia mafuta, kuna vifaa vingi, matatizo ya kiufundi mteja anaweza kuyapata ya aina mbalimbali na sio mita tu.

Fikiria upige simu TANESCO unatatizo uambiwe ili mafundi wafike unatakiwa ku gharamia 50,000 kama gharama ya ufundi ingekuwaje?

SERVICE CHARGE haina tatizo na ipo kisheria nafikiri mada ingejikita zaidi kwenye kuboresha huduma.
 
Wanatakiwa wabuni jinsi ya kuongeza kipato siyo kuwaibia wananchi. Hili ndio tatizo la kuwa na kampuni moja ya umeme (Monopolies) na sithani kama regulator wananguvu za kutetea wananchi. Nchi kama UK wana regulator OFGEM ambaye anahakikisha fair price na fine pale umeme unapokatika katika bila sababu za msingi.
Service charge inafanana sana na Capacity charge wanayotoza kina Symbion. Sema wenzetu akina Symbion,IPTL na Aggreko wanaitoza Tanesco kwa mabilioni.
Sasa hizo Capacity charge Tanesco watafidiaje ? Ndo walalahoi inabidi tutozwe ,tunalipa Capacity Charge kwa njia hii ya service charge. Kwa kweli ni uonevu.
 
Mkuu hapa Arusha tumejaza fom siku nyingi kubadili hiyo tariff lakini hakuna kitu nimruliza naambiwa watu ni wengi wameomba kubadilisha ila wamegoma ili wapate hela
Na mimi nimeuliza ..wanasema wataanza mwezi wa tatu.Ni mwendo wa kupigwa tarehe tu.
Hili la tarriff Prof. Muhongo naomba uingilie. tunaumia.Kama haiwezekani basi wapunguze bei ya unit. Mbona mafuta yameshuka bei ?
 
MKUU HAKUNA GHARAMA HIYO
1kwh = Tzs 298 (umeme bila vat)
Service charge = Tzs 5520 (bila vat)

Service charge inakatwa mara moja kwa mwezi

Mfano

Una shilingi 10,000

TANESCO SVC = 5520 + Vat (22% ya 5520)
Kwa hiyo jumla itakuwa = 6734.4

Kununua umeme unachukua 10,000 - 6734.4 = 3265.6 tuki approximate unapata Tzs 3266

Kila manunuzi yanakuwa na vat

3266 * 22% unapata 718.4

Kwa maana hiyo unachukua 3266 - 718.4 = 2547.568 tuki approxmate tunapata Tzs 2548.

Energy ( UMEME) 2548/ 298( 298 ni bei ya umeme kwa unit)
= unapata unit 8.5 uki approximate 9 Kwh
Hizo unit 8 zinatoka wapi? Basi kama ni hivyo tunatozwa tofauti!
Mbona EWURA (1%) na REA (3%) hujaweka??
Umeme wa elfu kumi si zaidi ya unit 3 kama unanunua mwanzo wa mwezi.
 
Hizo unit 8 zinatoka wapi? Basi kama ni hivyo tunatozwa tofauti!
Mbona EWURA (1%) na REA (3%) hujaweka??
Umeme wa elfu kumi si zaidi ya unit 3 kama unanunua mwanzo wa mwezi.
Mkuu hayo mahesabu niliyaweka nakuwekea tena kwa mara nyingine.

Unaweza kufanya pia hesabu inavyokuwa.

1kwh = Tzs 298 (umeme bila vat)
Service charge = Tzs 5520 (bila vat)

Service charge inakatwa mara moja kwa mwezi

Mfano

Una shilingi 10,000

TANESCO SVC = 5520 + Vat (22% ya 5520)
Kwa hiyo jumla itakuwa = 6734.4 hii ndio service charge inayokatwa ukiweka vat.

Kununua umeme unachukua 10,000 - 6734.4 = 3265.6 tuki approximate unapata Tzs 3266

Kila manunuzi yanakuwa na vat na vat hapo namaanisha ( VAT 18%, EWURA 1%, na REA 3% ukijumlisha unapata 22% kwa ujumla ndio nasema vat)

3266 * 22% unapata 718.4

Kwa maana hiyo unachukua 3266 - 718.4 = 2547.568 tuki approxmate tunapata Tzs 2548.

Kwa hiyo katika 10,000 yako kiasi utakachotumia kununua umeme ni 2548.

Energy ( UMEME) 2548/ 298( 298 ni bei ya umeme kwa unit)
= unapata unit 8.5 uki approximate 9 Kwh
 
Pia tunawashauri TANESCO waache na wao kulipa capacity charges ,ukiiangalia kiundani ndio inazaa services charges kwa wananchi ..
 
Back
Top Bottom