Kwanini "Service charge" ya TANESCO ni tatizo linalohitaji utatuzi wa haraka!

service charge kwa mtumiaji wa mwisho ni mzigo mkubwa sana ziangaliwe upya

Vipi ikitolewa mteja anapopata tatizo kama nguzo kuanguaka,nyaya kukatika,meter kuharibika mafundi wa TANESCO wakuja kutoa huduma wamchaji mteja wateja wangapi watamudu gharama?
 
Naomba kisahihisha kwa wanao tumia umeme chini ya unit 75 kwa mwezi gharama ya umeme ni Tsh 100, na hawa ni wateja wa Tariff4 (T4). Unit zikizodi 75 wakati yupo T4 zile unit zilizozidi mteja analipia Tsh 350.

Na mteja wa T4 hana service charge na hawa ni low usage customer.

a
Nimekuelewa mkuu ila kwenye LUKU mteja anaetumia zaidi ya unit 75 anapatikanaje, je ni wakati wa kununua umeme yaani let say nanunua unit 40 hazijaisha nakuja nanunua tena unit 40 zingine na kufanya unit 80 kwa mwezi au kuna system ina count vipi, unajua kwa mita hii issue ya zaidi ya 75 unit inaeleweka zaidi kwa kuwa umeme ulikuwa ni postpaid yaani unalipa unachotumia kwahiyo zikizidi 75 tu unit price inachange sasa kwa luku ambao unalipa in advance hapa ndo nachanganyikiwa

Ila kwa uzoefu wangu wa kutumia umeme wa LUKU nimejifunza ukitaka kupata unit nyingi usinunue umeme mara kwa mara (nahisi system ya LUKU inamtambua mteja wakati wa kuweka zile token mfano niliwahi nunua unit nyingi ambazo zilikaa kama miezi miwili hivi nilipokuja nunua umeme wa 10,000 nikapewa unit 9 hapo walikata service charge yao ya buku 5 ya miezi miwili baada ya siku 10 nikanunua umeme wa 30,000 nikapata unit zaidi ya 80 kitu ambacho kwa haraka haraka nimepewa unit nyingi kwa kuwa tayari nimeonekana kama mtumiaji mdogo kutokana na jinsi navyoweka umeme (nielimishwe hapa ila concept yako nimeielewa vizuri hasa kipindi kile cha mita nilikuwa ninazingatia sana ila kwa LUKU hakuna calculation inayoeleweka mfano hapo umeme wa mwekundu nikapata unit 9 of course service charge ilipunguza kwa kuwa nilikaa na umeme zaidi ya mwezi bila kununua lakini nikanunua umeme wa 30,000 nikapata zaidi ya 80 unit kitu ambacho mteja mwingine nae angepata tofauti na mie kwa umeme huo huo wa 30,000
 
Vipi ikitolewa mteja anapopata tatizo kama nguzo kuanguaka,nyaya kukatika,meter kuharibika mafundi wa TANESCO wakuja kutoa huduma wamchaji mteja wateja wangapi watamudu gharama?
Well hapa ndipo issue ilipo. Kama mteja hawezi kumudu service, asitumie umeme mpaka hapo serikali itakapokaa na kuona njia bora za kuzalisha umeme ambao wateja wataumudu.

Ninachokiona hapa ni kuwa Tanesco service zao ni kubwa sana na ili kuzificha wamelazimisha kila mtu alipe ili kuweka load sharing. Lakini huu ni wizi. Ina maana kama sina uwezo wa kulipia gharama za daladala basi ianzishwe special charges ili kuwezesha asiye na uwezo kulipia daladala kwa sh 50?

That is completely insane! Yaani kazi nifanye mimi mshahara wangu nimgawiye mtu kwa lazima kisa hawezi ku afford service ambayo anaweza ku opt out? Why?

Kama ni hivyo mbona wengi wanakufa kwa kukosa matibabu, basi na tuweke charges maalum maana uhai wa mtu ni muhimu kuliko kuwasha friji au feni.
 
Nimekuelewa mkuu ila kwenye LUKU mteja anaetumia zaidi ya unit 75 anapatikanaje, je ni wakati wa kununua umeme yaani let say nanunua unit 40 hazijaisha nakuja nanunua tena unit 40 zingine na kufanya unit 80 kwa mwezi au kuna system ina count vipi, unajua kwa mita hii issue ya zaidi ya 75 unit inaeleweka zaidi kwa kuwa umeme ulikuwa ni postpaid yaani unalipa unachotumia kwahiyo zikizidi 75 tu unit price inachange sasa kwa luku ambao unalipa in advance hapa ndo nachanganyikiwa

Ila kwa uzoefu wangu wa kutumia umeme wa LUKU nimejifunza ukitaka kupata unit nyingi usinunue umeme mara kwa mara (nahisi system ya LUKU inamtambua mteja wakati wa kuweka zile token mfano niliwahi nunua unit nyingi ambazo zilikaa kama miezi miwili hivi nilipokuja nunua umeme wa 10,000 nikapewa unit 9 hapo walikata service charge yao ya buku 5 ya miezi miwili baada ya siku 10 nikanunua umeme wa 30,000 nikapata unit zaidi ya 80 kitu ambacho kwa haraka haraka nimepewa unit nyingi kwa kuwa tayari nimeonekana kama mtumiaji mdogo kutokana na jinsi navyoweka umeme (nielimishwe hapa ila concept yako nimeielewa vizuri hasa kipindi kile cha mita nilikuwa ninazingatia sana ila kwa LUKU hakuna calculation inayoeleweka mfano hapo umeme wa mwekundu nikapata unit 9 of course service charge ilipunguza kwa kuwa nilikaa na umeme zaidi ya mwezi bila kununua lakini nikanunua umeme wa 30,000 nikapata zaidi ya 80 unit kitu ambacho mteja mwingine nae angepata tofauti na mie kwa umeme huo huo wa 30,000

Mkuu ni kwamba system ya LUKU inaangalia pale unaponunua umeme, tuseme umenunua wa 40,000 na ndani ya mwezi huo ukanunua tena wa 40,000 kwenye sustem tukiangalia tunaangalia jumla ya unit ndani ya mwezi huo ulizo nunua na zinavuka unit 75 kwa maana hiyo hufai kuwa katika watumiaji wa umeme chini ya unit 75, naomba ieleweke kuwa tariff 4 ipo kwa ajiri ya low usage customers ( wateja wa hali chini).

Pia service charge inakatwa kila mwezi, usipo nunua umeme mwezi huu mwezi ujao utakatwa service charge Mara mbili ya mwezi huu na mwezi uliopita.

Nilishaweka mfano inavyokuwa nakuwekea tena uangalie. Uliyo yaandika sio kweli

Service charge inakatwa mara moja kwa mwezi, usipo ilipa mwezi huu mwezi ujao unakatwa mara mbili

Mfano

Una shilingi 10,000

Service charge bila vat ni Tah. 5520 kwa maana hiyo unaweka na vat inakuwa hivi.

TANESCO SVC = 5520 + Vat (22% ya 5520)
Kwa hiyo jumla itakuwa = 6734.4

Kununua umeme unachukua 10,000 - 6734.4 = 3265.6 tuki approximate unapata Tzs 3266

Kila manunuzi yanakuwa na vat

3266 * 22% unapata 718.4

Kwa maana hiyo unachukua 3266 - 718.4 = 2547.568 tuki approxmate tunapata Tzs 2548.

Energy ( UMEME) 2548/ 298( 298 ni bei ya umeme kwa unit)
= unapata unit 8.5 uki approximate 9 Kwh

Ninapo ongelea vat namaanisha ( REA 3%, EWURA 1% na VAT 18%) kwa Ujumla wake ndio tunapata 22% of vat
 
Kwani mafundi hao wa tanesco hawalipwi mishahara? Futeni kauli ya "bure"
ndani ya kila unit ninayonunua kwa producer mimi kama mteja najua nalipia service charge, tax, na gharama zingine za usafirishajia(transport costs) hapo inakujaje nilipe service charge, VAT, REA etc. Wakati nimenunua units zangu kulingana na uwezo wangu?
 
tanesco.jpg
tanesco.jpg
 
Service charge ni Uharamia, Kila Unit ninayonunua najua tayari humo ndani Tanesco wameshapiga gharama za uendeshaji mitambo yao na service ya mitambo yao, iweje wanikamue mimi niwalipie gharama za kugharamia huduma zao ambazo ilipaswa iwe ni sehemu ya mtaji wao?
Ni sawa na biashara ya Usafiri, unanitoza nauli halafu baadae unanitoza gharama za service ya gari yako hii inaingia akilini?
 
TANESCO waliwahi kupeleka hati ya maombi ya kuongeza bei kwa muda ( Sikumbuki lilikuwa bunge la ngapi), wabunge walikuikubalia TANESCO kuongeza bei kwa makubaliano ya baada ya muda washushe. Nafikiri muda haujafika.

Binafsi umenikuna sana kwanza,huwa sipati jibu ya hizo tozo zitozwazo na TANESCO.

18% VAT haina tatizo inaeleweka
1% EWURA ya kazi gani? Kama ni kitengo kilianzishwa na serikali kwa nini serikali isiwajibike na vitengo vyake kwa hiyo 18%?
3% REA ili iweje,kama mtu unapanua biashara, mtaji si uwe wa kwako? Watumiaji kulipia umeme vijijini,kwani hao watu wa vijijini hawaliipii service line?

Service charge kwa siku hizi ni wizi mtupu.

Mabenki (baadhi) wana account zinazofanana na LUKU, kwa mfano Standard Chartred bank wanayoinaitwa HIFADHI current account- Pay as much as you consume", hii account haina charge yoyote ya mwezi( No single cent charged) wanakucharge tu pale unapotumia.

LUKU ni the same, walitakiwa watucharge tu pale tunapotumia plus 18% VAT hizo charges nyingine ni wizi mtupu!

Alafu akina Muhongo kujisifia na Jasho letu as if pesa wanazotumia ni Kodi kumbe uwizi kupitia Mgongo wa Sheria Kandamizi!
Vijijini wakulima wanauza Mazao na Mifugo mbona hakuna hiyo hiyo 3% ?.

Kiufipi kwenye Umeme unakuta tunalipa Kodi isiyopungua 25%= 1%+18%+3%+5000tsh/mwezi (???%)
 
Mkuu Msabila, nilishatoa maelezo ya service charge ukipitia comments za nyuma.
What is service charge?

A type of fee charged to cover services related to the primary product or service being purchased. For example, a concert venue may charge a service fee in addition to the initial price of a ticket in order to cover the cost of security or for allowing electronic purchases. Another example would be a fee for using theATM of a competing bank.
Mimi nadhani Service charge ni muhimu kwa shirika hila la uma kwa sababu zifuatazo

  1. Gharama kubwa za uwekezaji kuanzia kuzalisha,kusafirisha na kusambaza umeme,Gharama hizi kubwa zinapelekea wawekezaji kuona kuwa kuwekeza kwenye umeme kunachelewa sana kulipa (Long payback period),Hivyo shirika hili la uma limejitahidi kufikisha umeme hata maeneo yasiyo na faida hivyo kulichangia service charge ni kulipa nguvu Zaidi
  2. Mteja anapopata tatizo kama nguzo kuanguaka,nyaya kukatika,meter kuharibika mafundi wa TANESCO wamekuwa wakitoa huduma bura kabisa kitu ambacho ingekuwa private company ingeingizwa kwenye gharama za mteja ,Service charge imesaidia hili
  3. Service charge ni kama bima ambayo tunawekeza kwenye shirika la umeme nchini ili liweze kuhudumia wateja wote pale wanapopata hitilafu ya umeme.
  4. Sio wateja wote wanaolipa service charge bali na kwa wateja wa kundi la T,Wanaotumia umeme kuanzia unit 75 mpaka 7500 kwa mwezi,Waleo wanaotumia umeme chini ya unit 75 wanalipa kwa bei ya ruzuku naamini kabisa service charge inawasaidia watanzania wenzetu wa hali ya chini.
Kuingiza gharama za uwekzaji, endapo wewe ni msemaji wa TANESCO, basi dhana nzima ya service charge haipo je kwenye bei ya umememe utaweka nini. Hilo la pili kuhusu bure si sahihi ni moja ya gharama za service charge. Service charge kama ulivyoeleza
ina
inasaidia kgharimia matukio yasio ya kila siku.
Asante kwa maelezo. Bado kwngu kiasi tunacholipia regulator wa umeme ni ubwa nchi nyingine ni0.015 YA BEI. jE ewura PESA YOTE HIYO WANAITUMIA KWA NINI?
 
Serikali wavunje mkataba na IPTL nashindwa kuelewa Tanesco washindwe kuzalisha MW 300 mpaka wawape dili IPTL,Umeme tanesco wanauziwa kwa Tsh 90 kwa unit iweje watuuzie bei karibu mara nne? 395? Kwanini wasituuzie kwa 120? REA,EWURA,IPTL,SERVICE CHARGE ni wizi tu.
 
Nilinunua umeme wa elfu kumi nikaambulia units 9 tu makato yalikuwa mengi zaidi yaani karibia elfu nane ilikatwa dah tanesco ni jibu
 
Back
Top Bottom