Megawatt B
JF-Expert Member
- Aug 23, 2011
- 259
- 69
Nimewahi kusikia kuwa kabla ya uhuru wa Tanganyika kusini mwa Tanzania Mkoa wa Mtwara kuliwahi na Railway line iliokua inaunganisha Mtwara na Wilaya ya Nachingwea. Aiadha mara baada ya uhuru wa Tanganyika serikali ya Mwalimu ikaamua kung'oa reli hiyo na kwenda kujenga reli ya Dar/Moshi. Kwa ufahamu wangu naamini kuwa wazungu (wakoloni) walioamua kujenga reli hiyo walikua na madhumuni yao kwa mikoa ya kusini mwa Tanganyika. Lakini mpaka hivi sasa sijui kwa nini Wazungu waliamua kujenga Reli kusini na Kwa nini serikali ya Mwalimu iliamua kung'oa reli hiyo?........Naomba wan jf kwa yeyote ambae ana ufhamu mzuri kuhus hili basi anifahamishe na mimi niongeze ufahamu wangu.....nawakilisha.
Wakoloni walijenga reli hiyo (Mtwara- Nachingwea) kwa ajili ya mashamba makubwa ya karanga yaliyofunguliwa kule Nachingwea. Lengo lilikuwa kusafirisha mazao hayo toka Nachingwea hadi Mtwara - bandarini. Mashamba hayo hayakufanikiwa kama ambavyo walitarajia kutokana na matatizo kadhaa. reli hiyo ikawa haina kazi iliyokusudiwa ikang'olewa mwaka 1953. Kwa wale amabao wamefika kusini bado unaweza kuona alama mpaka leo, kwa mfano tuta la reli, madaraja na majina ya stesheni. Bado wakazi wa Nachingwea wanafahamu mashamba hayo yaliyotelekezwa na wakoloni, yalijulikana sana kuanzia farm one (Farm 1)hadi farm twenty one(21) yalikuwa mashamba makubwa sana. maeneo haya sasa yamekuwa mapori na wanavijiji wanalima. Kwa wale waliofuatilia ukombozi wa wa kusini mwa Afrika miaka ya 60-70- 80, kambi za wapigania uhuru ziliwekwa katika lilipokuwa shamba namba 17 (farm 17). Nji wa Nachingwea haukuwa kitovu tu cha wakoloni tu, bali ni mji unaojulikana sana kwa mafunzo ya kijeshi katika ukombozi wa kusini mwa Afrika, na nadhani ni mji pekee wenye kambi nyingi za jeshi (pamoja na JKT)