Kwanini Mwalimu Nyerere aling'oa reli ya Dar-Lindi, Mtwara, Nachingwea?

Hii reli wakati ule ilikuwa uneconomical.

Halafu eneo hilo lilikuwa uwanja wa mapambano wa vita mbali mbali vya Msumbiji.
 
Mimibaba; Ni kweli Mkuu, nchi hii ilifanyiwa master plan karibia mikoa yote.Binafsi siamini kwamba makabidhiano ya miundombinu na mipango ya maendeleo haikufanywa kwa umakini mkubwa kwani tumeshuhudia hata sasa, mbona safari za treni kutoka Dar kwenda Mwanza zimeota mbawa kwa 95%? Mimi nadhani tunacho kibarua cha kujifunza zaidi tulipojikwaa kuliko kujifanya mabingwa wa mikakati (Big Results...) bila kuangalia miaka mingi ijayo.Tusiwe na mawazo mgando, tujiulize ng'ombe wa maziwa kule Kitulo mkoani Njombe au Mpwapwa huko Dodoma bado wanafugwa kwa wingi? Tumepunguzaje tatizo la utapiamlo? Nirudi kwenye mada, tatizo la kuficha kumbukumbu muhimu ni chanzo cha kushindwa kufanikiwa katika masuala ya maendeleo.

Dhana ya kuficha kumbukumbuku nadhani hukuitoa vizuri; kupoteza kumbukumbu ni tofauti kabisa na kuficha kumbukukmbu. Moja ni matokeo ya carelessness na nyingine ni deliberate action.

Master plani kuu ya Dar es Salaam ilifanywa mwaka 1963 wakati Dereck Bryceson akiwa mbunge wa Dar es Salaam. Magomeni Mapipa ni moja ya vitongoji vilivyojengwa chini ya master plan ile; mwishoni mwa miaka ya sabini, serikali iliweka mkazo zaidi mambo ya vijiji vya ujamaa na ikaacha swala la maendeleo ya mijini kuwa chini ya National Housing Corporation. Pale ndipo maendeleo ya miji yalipoanza kuporomoka sana na zile master plans kusahahulika.
 
View attachment 415981
Hili ni jambo ambalo ukimuuliza Nyerereist yoyote hatokupa jibu

Mindhali humu kuna GREAT THINKERS naamini tutapata data tuu kwa nini the so called baba wa taifa alimua hii reli ingolewe

Nawasilisha

Reli hii ilijengwa kwa ajili ya mradi wa katani (mkonge) Nachingwea, ilianzia Mtwara sio Dar kwenda Nachingwea SP RLY (Southern Province Railway) Mradi haukuwa na mafanikio hivyo hakukua na mkonge wa kutosha ili faida ya reli hiyo ionekane, bahati mbaya hatujui kuwa reli hujengwa kwa ajili ya kusafirisha mizigo, CCM kwa kutumia ujinga wetu wanajaribu kutuaminisha kuwa reli inajengwa kwa ajili ya abiria! Hapana.
 
Hii reli wakati ule ilikuwa uneconomical.

Halafu eneo hilo lilikuwa uwanja wa mapambano wa vita mbali mbali vya Msumbiji.

Reli haikung'olewa kwa sababu ya vita, iling'olewa kutoa spea parts za kuripea reli ya Tanga-line chini yauamuzi wa East African Railways Corporation waliokuwa wamiliki wakati huo, hayakuwa maamuzi ya serikali. Uamuzi huo ulitokea baada ya reli hiyo kuwa idle kwa muda mrefu sana bila kuwa na mizigo yoyote; na ilikuwa haibebi zaidi ya behewa moja la abiria kutokana na kutokuwapo kwa abiria wa kutosha. Kwa hiyo plani ya serikali ikawa ni kujenga barabara ya lami Mtwara hadi Songea, lakini sijui plani hiyo iliishia wapi.
 
Hivi kama hakuna tena uzalishaji ndio in'golewe njia? Hee ama kweli nyerere alikua ni adui mkubwa wa waislam. Aliwahi pia kusema kua kama ana uwezo angevitupa visiwa vya zanzibar ktk bahari ya hindi.
Aliona jinsi mlivyo wehu
 
Reli haikung'olewa kwa sababu ya vita, iling'olewa kutoa spea parts za kuripea reli ya Tanga-line chini yauamuzi wa East African Railways Corporation waliokuwa wamiliki wakati huo, hayakuwa maamuzi ya serikali. Uamuzi huo ulitokea baada ya reli hiyo kuwa idle kwa muda mrefu sana bila kuwa na mizigo yoyote; na ilikuwa haibebi zaidi ya behewa moja la abiria kutokana na kutokuwapo kwa abiria wa kutosha. Kwa hiyo plani ya serikali ikawa ni kujenga barabara ya lami Mtwara hadi Songea, lakini sijui plani hiyo iliishia wapi.

Hoja zetu hazipingani. Nimesema at that time the railway was uneconomical.

Vile vile serikali iliogopa kuendeleza miundombinu ya mikoa hiyo kwasababu za kiusalama na kiulinzi zinazohusiana na vita vya Msumbiji.
 
Back
Top Bottom