Kwanini mkutano wa juzi wa CHADEMA Arusha hatukuona kwenye vituo vyote vya TV?

loiluda

Member
Jun 15, 2011
25
3
Nimejaribu kucheki vyombo vya habari hivyo cku ambako viongozi wa cdm walifika arusha na kufanya mkutano kuhusu maamuzi ya kamati kuu ya kuwafukuza madiwani watano.Vyombo vya habari ambavyo vilipata ujasiri wa kuandika yaliyojiri ni magazeti tu,kulikoni?
Je huu kweli haukuwa ni mpango wa kuwafanya watu wasione msimamo na mwitkio wa watu wa Arusha kuhusu maamuzi yale ya kamati kuu?
Napata msukumo wa kufikiri hivyo haswa ukizingatia kuwa aliyekuwa amepewa nafasi ya unaibu meya wa arusha alisikika akijaribu kuhonga polisi ili mkutano huo usipate kibali cha kufanyika.
Nyie wenzangu wana-jf mwasemaje?

Star tv walirusha kesho yake kwenye taarifa ya habari.

yes its true, hata mimi nilishuhudia star tv tena waliwapa muda mwingi tu, hii tv inarusha sana mikutona ya chadema na matukio mengi ya upinzani ikiwa tu yule mbunge wa cdm ilemela hataonekana knye tukio.
 
Itv walirusha saa 4 usiku siku ile ile.Niliona watu wengi kama mchanga wa bahari.Hakika ilipendeza.
 
Nimejaribu kucheki vyombo vya habari hivyo cku ambako viongozi wa cdm walifika arusha na kufanya mkutano kuhusu maamuzi ya kamati kuu ya kuwafukuza madiwani watano.Vyombo vya habari ambavyo vilipata ujasiri wa kuandika yaliyojiri ni magazeti tu,kulikoni?
Je huu kweli haukuwa ni mpango wa kuwafanya watu wasione msimamo na mwitkio wa watu wa Arusha kuhusu maamuzi yale ya kamati kuu?
Napata msukumo wa kufikiri hivyo haswa ukizingatia kuwa aliyekuwa amepewa nafasi ya unaibu meya wa arusha alisikika akijaribu kuhonga polisi ili mkutano huo usipate kibali cha kufanyika.
Nyie wenzangu wana-jf mwasemaje?

Ni kawaida! tumezoea kwa demokrasia kandamizi upendeleo ni jambo la kawaida hasa vyombo vya habari. mumeona kila siku kile kipindi cha kupre-empty wapinzani asubuhi kuhusu kutoka bungeni. hurushwa na TBC. lengo ni kutaka wabunge wa upinzania waonyeshe alignment ya hoja zao ili kuifaidisha chama tawala katika majibu.
 
Ni jambo la kusikitisha sana ndugu zangu,nadhani mafisadi walizuia tv zisionyeshe ila habari tumezipata kwenye magazeti.Hii ni changamoto kwa chadema,inabidi kuwepo na mpango wa kuanzisha kituo cha tv,na kimilikiwe na chadema,hii itasaidia katika ukombozi wa nchi hii.Na ingekuwa ni vyema kama chadema wakifungua tv kabla ya uchaguzi mkuu 2015,hili jambo linawezekana kabisa,kama ishu ni pesa watu tuko tayari kuchanga.
 
Kwani kuna ulazima gani vyombo hivi kurusha habari za CDM? Tumeshauri mara kwa mara CDM ianzisha vyombo vyake vya habari ambavyo sisi wapenzi wa mabadiliko tutanunua hisa ili viweze kuendeshwa kibishara. Nina uhakika vitapata biashara kubwa sana.
 
ITV walionyesha saa tano usiku na asubuhi,Star TV walionyesha kesho yake na kwenye marudio ya wiki Jumapili walionyesha,TBC hawakuonyesha kabisa ila walionyesha mkutano wa CCM kata sijui wilaya gani sikumbuki vizuri
 
Nimejaribu kucheki vyombo vya habari hivyo cku ambako viongozi wa cdm walifika arusha na kufanya mkutano kuhusu maamuzi ya kamati kuu ya kuwafukuza madiwani watano.Vyombo vya habari ambavyo vilipata ujasiri wa kuandika yaliyojiri ni magazeti tu,kulikoni?
Je huu kweli haukuwa ni mpango wa kuwafanya watu wasione msimamo na mwitkio wa watu wa Arusha kuhusu maamuzi yale ya kamati kuu?
Napata msukumo wa kufikiri hivyo haswa ukizingatia kuwa aliyekuwa amepewa nafasi ya unaibu meya wa arusha alisikika akijaribu kuhonga polisi ili mkutano huo usipate kibali cha kufanyika.
Nyie wenzangu wana-jf mwasemaje?

Kwenye taarifa ya habari ya saa 4-5 usiku wa siku hiyo ITV waliionyesha tena vizuri sana..
 
Kwani kuna ulazima gani vyombo hivi kurusha habari za CDM? Tumeshauri mara kwa mara CDM ianzisha vyombo vyake vya habari ambavyo sisi wapenzi wa mabadiliko tutanunua hisa ili viweze kuendeshwa kibishara. Nina uhakika vitapata biashara kubwa sana.
Vipaumbele mkuu.....vyombo vya habari ni kweli zina umhimu lakini siyo kivile angalia magamba vyombo karibu vyote hapa nchini ama ni vyao au vya makada wao lakini vina wasaidia kiasi gani? kuna vijiji siku hizi wana lipa 300 mpaka 500 ili wangalie bunge kwenye vibanda umiza ili wawasikilize wabunge hasa wa upinzani lakini wakisha tajwa wabunge wa CCM wanafatana watu wanafata shughuli zao mpaka mbunge wa upinzania atakapo anza kuongea wanaitana ndiyo wanaanza kutanzama tena cha msingi CDM wafanye kazi...iko siku uhuru uzalendo utawashinda wataandika mema ya chadema...
 
Back
Top Bottom