Tunduma: Yanayojiri kwenye Mkutano Mkubwa wa hadhara wa CHADEMA

Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
117,752
218,339
Kwa Mujibu wa Ratiba ya Mikutano ya hadhara iliyotangazwa na Chadema kanda ya Nyasa , Leo ni zamu ya Tunduma.

Labda kwa wageni na wenyeji wasahaulifu ni kwamba , Jimbo la Tunduma ni miongoni mwa majimbo machache yaliyokombolewa muda mrefu kutoka kwenye makucha ya utumwa wa ccm , huku halmashauri iliongozwa na chadema kwa karibu 100% , jambo hili liliwakasirisha watawala waoga wasio na hoja.

Taarifa za kidunia zinadokeza kwamba Tunduma ndio Jimbo la Tanzania lililoteswa kuliko yote na uongozi wa kidikteta wa awamu ya 5 , likifuatiwa na Jimbo la Hai , Hakuna kiongozi wa Chadema Tunduma ambaye hakuwahi kukamatwa na Polisi , mamia ya viongozi wa Chadema wametekwa, wameteswa , wamesweka rumande , wamefungwa kwa kesi za uongo za kubambikwa na wengine wameuawa.

Taarifa zingine zinadai kwamba kulitengwa bajeti maalum kwa vyombo vya usalama kwa ajili ya kuishughulikia Chadema Tunduma , wanausalama walisombwa kutoka Dar na kwingineko ili kuishughulikia Chadema na wanachama wake ( vyombo vya habari vya Tanzania vilijua lakini viliufyata)

Mstahiki Meya Mwafongo na viongozi wengine zaidi ya 100 waliwekwa jela kwa miaka mingi kwa kesi za uongo kutokana na udikteta wa awamu ya 5.

Sasa hatimaye leo Chadema na Kamati kuu yake wameingia Tunduma kwa kishindo.

Nashauri kabla ya Mkutano kuanza kuwe na Ukimya wa Dk 5 za kuomboleza waliouawa , kuteswa na kufungwa kwa kusingiziwa.

Usiondoke JF kwa taarifa za Uhakika

==============
UPDATES :

Hatimaye Msafara wa Chadema waingia Tunduma , Mapokezi yake haelezeki wala hayaandikiki , Umati ni mkubwa mno !

Picha na video zake zitakujia hivi punde , kama wewe ni mwanaccm na labda una shinikizo la damu usiangalie uzi huu


View attachment 2528636
View attachment 2528712View attachment 2528714View attachment 2528713
 
Hatuangalii wachangiaji , tunaangalia viewers
Kamanda muhangaikaji uko vizuri dada.
Wewe si umedai kuwa mada hizi zipo bored, sasa nini kimekuleta humu kwenye mada hii?, ndio maana mimi nikakuita wewe ni mpumbavu na hili sio tusi ila ni ugonjwa uliokua nao
kwa iyo ndio unajiona smart kuniita mimi mpumbavu ok you win what else unataka sema au kuita hata ivyo huwezi
kuninyamazisha wewe kabwela chapa lapa.
 
nimejaribu kukukumbusha tu kwamba kwenye uzi wowote , angalia waliousoma , siyo wachangiaji , lengo letu ni kuwafikia watu wengi zaidi
Mbona nimekuelewa dada Ery ukumbusho ni muhimu kwa wanaoamini, but u need to stop capping.
 
Back
Top Bottom