Msajili wa Vyama vya Siasa awataka CHADEMA kusitisha Mkutano wa Temeke kisa kutumia Viongozi wa Dini. Awaita kwenye kikao Julai 24, 2023

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,504
3,034
WhatsApp Image 2023-07-23 at 14.46.50.jpeg

WhatsApp Image 2023-07-23 at 14.46.51.jpeg


Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa tumepata taarifa kupitia vyombo vya habari ikiwemo mitandao ya kijamii kwamba, CHADEMA mmepanga kufanya mkutano wa hadhara tarehe 23 Julai 2023 katika Wilaya ya Temeke Dar-es salaam.

Taarifa hizo zinaonyesha kuwa, mmewaalika watu ambao siyo wanachama wen kuhudhuria mkutano huo. Miongoni mwa watu hao ni viongozi wa dini na taasisi nyingine ikiwemo Rais wa Chama cha Wanasheria cha Tanzania Bara (TLS).

Taarifa hizo zinaonyesha kuwa, katika mwaliko wenu CHADEMA mmewataja viongozi hao kwa majina na vyeo walivyonavyo katika taasisi zao na zinaonyesha viongozi hao wa dini wakiwa wamevaa nguo rasmi za taasisi zao za dini.

Hali hi siyo sawa, kwanza ni ukiukaji wa sheria za nchi zinazokataza vyama vya siasa kuwa na udini na kutumia dini kufikia malengo yake ya kisiasa. Pia ni ukiukaji wa sheria zinazokataza taasisi za dini kufanya shughuli za kisiasa.

Vilevile, hali hi inaweza kuleta mkanganyiko na sintofahamu kubwa katika jamii ya Watanzania na hata nje ya nchi, kwa watu kudhani kuwa, viongozi hao wa dini na taasisi ningine watakachoongea katika mkutano huo, ni msimamamo wa taasisi zao au hata wasipoongea, inaweza kuonekana kuwa, taasisi zao zinaunga mkono kilichoongewa katika mkutano huo, wakati taasisi za dini na hata TLS, zina wafuasi na wanachama wengi wenye mitazamo tofauti ya kisiasa. Hali hii inaweza kuhatarisha amani, utulivu, udugu na umoja wa Taifa letu. CHADEMA mnapaswa kuzingatia kuwa, nyie ndio mmepanga kufanya mkutano huo wa hadhara ili kunadi sera zenu, hivyo mkutano huo ni wa chama chenu siyo watu wengine.

Hivyo, Msajili wa Vyama vya Siasa akiwa ndiye mwenye jukumu la kusimamia utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa yenye masharti ya yanayokataza masuala hayo na akiwa ni mlezi wa vyama vya siasa, anawasihi CHADEMA msitishe mkutano huo a viongozi wen waku kufika Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa tarehe 24 Julai 2023 saa nne asubuhi kuonana naye, ili kuongea kuhusu suala hilo a masuala mengine ya utekelezaji wa Sheria ya Vyama vya Siasa.

Nashukuru kwa ushirikiano wenu.

Pia soma: KWELI - Ofisi ya Msajili yawasihi CHADEMA kusitisha Mkutano uliopangwa kufanyika Julai 23, 2023 huko Buriaga, Temeke
 
Safiii sana msajili, hiki ki NGO cha bwana mbowe kifutwe tu, futia kabisa usajili. Wakishupaza shingo wachapwe kipigo cha mbwa koko
Ni kweli, na vile ccm imeshapoteza mvuto, namna pekee ni kuifuta CDM ili ccm ipumue.
 
Ni kweli, na vile ccm imeshapoteza mvuto, namna pekee ni kuifuta CDM ili ccm ipumue.
CCM inapendwa haijawahi tokea. Cheki nyomi ya jana Arusha! CCM ni mziki mnene, ni chama la wote, kila sehemu ni CCM tu!
 
Nimeisoma hii barua nimeshangaa sana huyu Mbilikomo hana akili kabisa. Yeye hapo ana dini na anahudumia vyama vya siasa.
 
CCM inapendwa haijawahi tokea. Cheki nyomo ya jana Arusha! CCM ni mziki mnene, ni chama la wote, kila sehemu ni CCM tu!
Mtu mjinga kabisa ndio anaweza kuamini watu kujaa kwenye chama kilichopo madarakani miaka 60 kwa shuruti, wanahudhuria kwa ushawishi wa chama hicho. Nguvu za dola ndio huwezesha vyama vilivyoko madarakani kwa mabavu kujaza watu kwa shuruti ili kuhadaa umma kuwa wanakubalika. Unajidanganya kuwa unakubalika, kisha ikifika wakati wa uchaguzi unategemea uhayawani kutangazwa mshindi!
 
Back
Top Bottom