Kwanini JK hakubaliki ndani ya EAC?

baadhi ya wanaJf ni raia wa nchi za kigeni ambao wanataka kutumia jukwaa hili kuonyesha kwamba Jk au Tanzania haikubaliki katika Jumuia EA
 
ni lazima ifahamike kuwa Tanzania katika EA itahakikisha kwamba kwanza maslahi yake na watu wake yanalindwa
 
Tanzania itafanya kosa kubwa kama itataka kusifiwa na EA kuwa pawe na uingiaji na ukaazi kiholela wa raia wa EA. hata Uingereza ilikataa kuachana na sarafu yake ya pound kwenda EURO na wote tunayaona sasa baada ya kuporomoka kwa EURO na nchi nyingine ziliheshimu uamuzi wa Uingereza. Lakini nchi tunazotaka kuungana nazo haziheshimu uamuzi wetu.
 
Rutashubanyuma ndo yale yale ya kina hypokite kanimbe aka Joseph kabila wanataka kujenga the HIMA EMPIRE kwenye maziwa makuu
 
Kwa hili naomba nimpongeze Jk maana Wakenya wametuacha mbali katika nyanja mbalimbali ikiwemo elimu,Hatuitaji kufanya haraka juu ya uundwaji wa shirika la EAC tujipange kwanza.
 
baadhi ya wanaJf ni raia wa nchi za kigeni ambao wanataka kutumia jukwaa hili kuonyesha kwamba Jk au Tanzania haikubaliki katika Jumuia EA

Jibu hoja badala ya kushambulia mleta thread. Siyo siri kwamba kutokuja kwa wakuu wa nchi za EAC ktk mahadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika kunaonyesha wenzetu wamechoshwa na ubabaishaji wa watawala wetu! Ombwe la uongozi ktk serikali ya awamu ya 4 limeishavuka mipaka,sasa na majirani zetu wametustukia. Niliwahi uliza huko nyuma kwamba watendaji wetu serikalini na waziri walikuwa wapi mpaka dakika ya mwisho ya sherehe ya utiaji sahihi ndipo wanagundua kwamba kuna vipengele ktk haviko sawa! Kwa mtu yeyote makini huo ulikuwa ni uzembe.
 
Dogo, ukichemka unakula kona kimya kimya.

Umeingia na gia ya Miaka 50 ya Uhuru imegonga mwamba.

Ukaja na udini ukapiga chini.

Bado unaendelea kuzuga na ngonjera mpya.

Hivi hujishtukii tu.

Ulipaswa kujua kuwa choo ulichoingia sicho. Hatimaye watu wameshaijua vema sura yako halisi.

Watu wanajua hizo nyingine mwembwembwe tu lakini ajenda yako ni ARDHI yetu.

Kwa hilo Watanzania wooote tunasema NO!

Kama ni Jumuiya naife!!
 
Jibu hoja badala ya kushambulia mleta thread. Siyo siri kwamba kutokuja kwa wakuu wa nchi za EAC ktk mahadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika kunaonyesha wenzetu wamechoshwa na ubabaishaji wa watawala wetu! Ombwe la uongozi ktk serikali ya awamu ya 4 limeishavuka mipaka,sasa na majirani zetu wametustukia. Niliwahi uliza huko nyuma kwamba watendaji wetu serikalini na waziri walikuwa wapi mpaka dakika ya mwisho ya sherehe ya utiaji sahihi ndipo wanagundua kwamba kuna vipengele ktk haviko sawa! Kwa mtu yeyote makini huo ulikuwa ni uzembe.

Mbona hakuna rais yeyote wa EAC aliyehudhuria Kenya's Jamhuri day juzi?:eyebrows:
 
ni tanzania ndio haitakiwi east afrika kwa sababu ya msimamo wake imara wa kutetea rasilimali zake hasa ardhi.pili nchi zote wanachama wa east af.hazina amani na usalama wa kutoSha.tz haiwezi kuingia huko kichwa kichwa.kikwete haamui km yeye bali ni msimamo wa nchi.tuache kupotoSha ukweli
 
Mtu aliyeenda shule anaona jambo kwa sura mbili: Jk akifanya vizuri msifu akikosea mlaumu. Usiwe kipofu wa kumlaumu tuuuuu. Tz ndiyo yenye ardhi wenzetu hawana. Kenya hupati hata pa kuzikia !
 
kwanza koma kabisa wazururaji wewe na watusi wenzio ambao mmedandia nchi yetu na sasa mnataka kutumia wema wetu uliopitiliza kutaka kumiliki ardhi yetu. then kabla ya kuongea upuuzi wako kafanye research kupata details za umilikaji wa ardhi unaozungumziwa EAC na pia kwa mwekezaji. Tanzania tuna sehemu kubwa ya ardhi yenye rutuba na pia kwa matumizi mbalimbali so hawa jamaa wanaitamani sana coz tumeshindwa kuitumia.but hiyo sio sababu ya kuwakabidhi wao,tuko tayari kuwaachia wajukuu zetu urithi kulliko kuwanufaisha wasiotuhusu.hatutakubali kamwe tuibiwe kila kitu!afta ol we kinakuuma nini sisi kukataa ardhi yetu isiamuliwe matumizi na wengine?kama inakukera kajinyonge!
 
Jibu hoja badala ya kushambulia mleta thread. Siyo siri kwamba kutokuja kwa wakuu wa nchi za EAC ktk mahadhimisho ya miaka 50 ya uhuru wa Tanganyika kunaonyesha wenzetu wamechoshwa na ubabaishaji wa watawala wetu! Ombwe la uongozi ktk serikali ya awamu ya 4 limeishavuka mipaka,sasa na majirani zetu wametustukia. Niliwahi uliza huko nyuma kwamba watendaji wetu serikalini na waziri walikuwa wapi mpaka dakika ya mwisho ya sherehe ya utiaji sahihi ndipo wanagundua kwamba kuna vipengele ktk haviko sawa! Kwa mtu yeyote makini huo ulikuwa ni uzembe.
Kama wamechoshwa na sie dawa ni kuendelea na jumuiya yao. Kususia sherehe hakuwasaidii maana kwetu sie EAC ni ajenda ya wakenya kujaribu kutatua matatizo yake kwa mgongo wa TZ. Sherehe zenyewe zilikuwa za ccm wala hazikuwa za watanzania lakini ishu ya ardhi na ulinzi ni ya watanzania, na kwa hilo kikwete anafanya maamuzi mazuri ya kwanza tangu aingie madarakani! Hongera kikwete!
 
huyo timbilu ni mtutsi aliye hamia hapa Tanzania kwa hyo michango yake ni kutetea Rwanda 2.
 
Katika hili naungana na JK na Sitta kuliangalia kwa macho mawaili.
Nyerere alipotaka muungano wa EAC Kenya ilikataa na KIbaki alipiga kura akiwa mbunge kukataa hilo. Nyerere alipoanzisha juhudi za EAC Kenya wakaiua kwa vile Tanzania na Uganda ni tegemezi.

Baada ya vituko vyote hivyo Kenya wanataka muungano leo hii jioni, hivi hujiulizi ina maana Kibaki amekuwa na akili baada ya miaka 50!

Kinachoongelewa ni ardhi tu na sio miundo mbinu, elimu au afya, jiulize ni kwanini. Angalia population ya Rwanda, Kenya na Uganda halafu fikiria miaka 20 ijayo itakuwaje.
Kwanini wasiilaumu Tanzania kwa miundo mbinu au elimu ila suala la ardhi tu!!!

Tanzania imesema kama wanaona wanaweza kwenda peke yao basi na waende. Kenya na Rwanda wameanza na wala Tanzania haijalalmika. Kwanini wasubiri kama wanaweza kuungana wao. Wanasubiri nini?

Uganda na Kenya waligombea kisiwa cha KM 1, halafu unataka Tanzania iachie kila kitu. Kama wao wanataka ardhi iwe ya jumuiya kwanini walifikia mahali pa kutangaza vita kwa KM 1 tu. Fikiria kwanza na tanguliza busara Rutashu..

Mwisho, EU ina matatizo makubwa sana leo na wanafikiria kila nchi kurudi katika sarafu yake n.k. Wameanza miaka 50 iliyopita na bado wana matatizo sasa sisi wa miaka 10 tukurupuke tu.

Hili la muungano lina interest zao vinginevyo wangekomalia uchumi, soko la pamoja, elimu na afya. Wao wamekomalia suala moja tu ardhi. Kwa hili lazima Watanzania tuwe macho kwasababu tumeshaonja shubiri ya mwaka 1977. Mimi niliyaona kwa macho yangu. Kama si Mchina na mataifa rafiki nchi ilikwama kabisa.
 
Back
Top Bottom