Haiwezekani kwa EAC kuwa na sarafu moja bila ya kuwa na shirikisho la kisiasa kwanza

Lycaon pictus

JF-Expert Member
Jan 31, 2021
7,235
12,750
Naona kuna habari za EAC kuwa na sarafu moja. Kwa mipango ya EAC leo hii tayari tulitakiwa kuwa na sarafu moja. Lakini kiukweli ni ngumu sana kuwa na sarafu moja bila ya kuwa na shirikisho la kisiasa. Jambo hilo limewatesa na linazidi kuwatesa Umoja wa Ulaya.

Nchi huwa zinashindana kibiashara na huwa kuna zenye surplus na deficit katika biashara. Kutengeneza sarafu moja bila ya nchi hizi kutokuwa chini ya shirikisho moja la kisiasa ni kutengeneza losers na winners. Matokeo yake ni shirikisho lenyewe kucollapse.

Masuala ya kifedha, hasa masuala ya inflation, interest rates nk nk huamuliwa kisiasa. Kuwa na sarafu moja bila kuunganisha maamuzi yanayoiendesha sarafu hiyo ni kukaribisha matatizo. Wanasiasa hawako tayari kupokonywa mamlaka ya kucontrol pesa. So jambo la kwanza ni kuunganisha mamlaka ya kisiasa. Bila ya hivyo tutakuwa tu tunasogeza mbele tarehe ya kuanzisha common currency ya EAC.

Jambo la muhimu ambalo EAC inatakiwa kupambania sana ni shirikisho la kisiasa. Ukiisha kuwa na shirikisho la kisiasa mengine yote ni mtelezo tu.
 
Ni bora tuungane kiuchumi ZAIDI kuliko hata KISIASA.

Tuwe na Sarafu moja Paspoti Moja na Free Movement of People and Goods.

Baada ya hapo mambo mengine ni Rahisi kufikiwa.

Na hatimae AFRIKA MOKO From Atlantic to Indian Oceans From Cape Town to Alexandria.
 
Kupata shirikisho la kisiasa huku baadhi ya members,wakiwa katika mkwamo wa vita ni jambo ambalo sio bora.Vema kupata amani ya kudumu then,ndo mchakato wa sarafu moja na shirikisho moja la siasa ufuate.
Walifanya makosa kuingiza watu wenye migogoro. Tukiwa vilevile nchi tatu enzi hizo tulitakiwa kuunda shirikisho la kisiasa lenye serikali yenye mamlaka. Lakini tunaweza bado kuliunda hata sasa na likatatua hizi changamoto. Ila huwezi kuwa na sarafu moja bila shirikisho la kisiasa. Hiyo sarafu itaanguka kesho asubuhi.
 
Ni bora tuungane kiuchumi ZAIDI kuliko hata KISIASA.

Tuwe na Sarafu moja Paspoti Moja na Free Movement of People and Goods.

Baada ya hapo mambo mengine ni Rahisi kufikiwa.

Na hatimae AFRIKA MOKO From Atlantic to Indian Oceans From Cape Town to Alexandria.
Hayo masuala ya free market na sarafu huamuliwa na wanasiasa kisiasa. Ndiyo maana kuna kufungiana mipaka. Lakini sote tukawa chini ya shirikisho moja hayo mambo yataenda wepesi sana.

Kwame Nkrumah alikuwa sahihi sana kutaka tuharakishe shirikisho la kisiasa kuliko Nyerere aliyeleta visingizio kwamba tuungane polepole kikanda kwa miungano ya kiuchumi. Matokeo yake hadi leo tunazidi kugawanyika.
 
Sawa, shirikisho la kisiasa ni sawa.lakini ni kwa asilimia chache sana.kitu kikubwa muhimu ni SERA ZA KODI.

Kuna nchi wanachama bado changa sana. Hata mapato yao bado chini sana ukilinganisha na zingine.hivyo bado zinalelewa tu.

Hivyo wataweza kupata mtaji wa kuanzisha hiyo sarafu lakini kuikuza itakua ngumu kwasababu, kuna nchi wanachama hawajua hata vilivyomo kwenye umoja huo.

Lakini hata hizo nchi wanachama zilizoendelea kidogo bado hazina uzalendo kila mmoja anavutia kwake.anajiangalia binafsi na watu wake tu, kiajila na kibiashara.
 
Hii Jumuia ya EAC Ina imbalance kubwa ya mambo mengi... masitumie hizi akili zenu za kuku za kuvukia barabara kufanya conclusions.

Haya mambo ya Economic/Financial and political Integration kwa Sasa Bado sana.
 
Back
Top Bottom