Rutashubanyuma
JF-Expert Member
- Sep 24, 2010
- 219,470
- 911,174
- Thread starter
- #81
Rutashubanyuma hatuwezi kuingia kwenye kinyang'anyiro bila kujiandaa toka tupate uhuru mwaka 1961 Tanzania tumepoteza muda mwingi tukisaidi nchi zingine kupigania uhuru na kuzikomboa toka kwa watawala wabovu nchi kama Angola, Msumbiji, Zimbabwe, shelisheli, Uganda na Afrika ya Kusini wakati wenzetu wakenya toka uhuru wanashughulika na biashara wanajua umuhimu wa ardhi na wanaelimu ya masoko ya hisa toka mwaka 63 wakati watanzania tumeanza juzi maana muda mwingi pia tulikuwa kwenye siasa ya ujamaa na kujitegemea
Kawhiyo haitakuwa haki kutuunganisha na watu wenye uzoefu undercover ya kuwa nasi tutapata bidii hakuna kitu kama hicho inabidi watanzania wapate muda wa kujiandaa ili kuingia kwenye shirikisho kitendo cha kulazimisha Tanzania kuingia sasa hivi ni sawasawa na mwanafunzi wa darasa la nne umpeleke kufanya mtihani wa darasa la saba eti atajifunza mbele kwa mbele bila kuandaliwa ili afikie kiwango cha mwanafunzi wa darasa la saba au ni sawaswa na kupeleka timu ya Olyimpic kwenye mashindano kabla haijafikia kiwango eti itajiongeza mbele kwa mbele itaishia kuwa msindikizaji
Wenzetu nchi za ulaya zina jiandaa kwanza kabla ya kuingia European Union haziendi kichwa kichwa halafu katika EU kuna nchi viongozi zimeset standard ili mwanachama aweze kuingia ili wanachama wawe ni member wanaofanana. sasa sisi tutaunganaje na madikteta kama Museveni? Kibaki au Kagame lazima wawe na mifumo yenye kuheshimu katiba bila kubalidi term limit kwa mtu kama Museveni na Kenya waondoe dhana ya kuwa bila wakikuyu nchi haitawaliki pia Kagame kujifanya nabii wa Rwanda kuwa bila yeye hakuna Rwanda
hoja hizi ndizo zinatudanganya kabisa................................maendeleo ni kipimo cha ulinganishi...................unajilinganisha na nchi hii kuanzia mwaka 1961 amabyo GDP zilikuwa zinashahibiana?
Jibu ni South Korea ambayo leo...................GDP yake inaizidi hii ya TZ zaidi ya mara 400...................tafakari haya kwanza kabla ya kuwafuta wanasiasa uchwara wa nchi ambao hujivunia umasikini ili kuhalalaisha kitumbua chao ambacho hata hivyo kina mchanga...........