Da Pretty
JF-Expert Member
- Dec 9, 2010
- 3,059
- 1,148
Habari wanajamvi.
Kwa kweli hilo swali huwa linanisononesha sana.
Nina umri wa miaka 30, sijaolewa, sina mchumba wala mpenzi yapata mwaka na miezi kadhaa sasa.
Mdogo wangu anayenifuatia ana miaka 27 aliolewa akiwa na miaka 24 na ana watoto wawili sasa.
Familia yangu na jamii inayonizunguka hainielewi na mara nyingi nakutana na hilo swali
"Mbona wenzako wanaolewa wewe huolewi, au una tatizo?"
Kiukweli hua napata ugumu sana kujibu hilo swali kwa sababu sina cha kuwajibu.
Labda ningesema nina tatizo au kasoro lakini kati ya niliowahi kuwa nao kimahusiano hakuna alieoa hadi sasa japo wote walinizidi umri na kuna wawili walikua na watoto tayari na mpaka sasa hawajaoa.
Hivi kwa jamii yetu mwanamke kutoolewa ni kasoro?
Maana kuna rafiki yangu naye anapata usumbufu kama wangu kutoka kwa familia yake.
Vipi kama mwanaume ninayempata yeye hana wazo la kuoa nifanyeje?
Na wanaume huwa wanaulizwa na kuonekana wana matatizo kama wanawake?