Kwanini huolewi? Au una kasoro?

Da Pretty

JF-Expert Member
Dec 9, 2010
3,060
1,147
Habari wanajamvi.
Kwa kweli hilo swali huwa linanisononesha sana.
Nina umri wa miaka 30, sijaolewa, sina mchumba wala mpenzi yapata mwaka na miezi kadhaa sasa.
Mdogo wangu anayenifuatia ana miaka 27 aliolewa akiwa na miaka 24 na ana watoto wawili sasa.
Familia yangu na jamii inayonizunguka hainielewi na mara nyingi nakutana na hilo swali
"Mbona wenzako wanaolewa wewe huolewi, au una tatizo?"
Kiukweli hua napata ugumu sana kujibu hilo swali kwa sababu sina cha kuwajibu.
Labda ningesema nina tatizo au kasoro lakini kati ya niliowahi kuwa nao kimahusiano hakuna alieoa hadi sasa japo wote walinizidi umri na kuna wawili walikua na watoto tayari na mpaka sasa hawajaoa.
Hivi kwa jamii yetu mwanamke kutoolewa ni kasoro?
Maana kuna rafiki yangu naye anapata usumbufu kama wangu kutoka kwa familia yake.
Vipi kama mwanaume ninayempata yeye hana wazo la kuoa nifanyeje?
Na wanaume huwa wanaulizwa na kuonekana wana matatizo kama wanawake?
 
Pole kwa changamoto unazo kutana nazo. Ni kweli baadhi ya wana jamii wanatabia ya kuwa nyoshea vidole wasichana ambao bado hawajaingia kwenye ndoa kwa sababu wana jamii hao hawana uelewa mpana juu ya maamuzi binafsi ya mtu kuingia kwenye ndoa. Hii tabia inasababisha baadhi ya wasichana kuingia kwenye ndoa ili kuiridhisha jamii inayo wazunguka lakini si ajabu hana furaha yoyote ndani ya hiyo ndoa. Maisha yako na furaha yako ipo mikononi mwako, usikubali jamii iendeshe maisha yako kama ni kuolewa wewe muombe mungu unayemuamini utampata unayempenda atakuoa. Ndoa ni taasisi yenye changamoto nyingi sana hivyo inahitaji umpate mtu unayempenda na anayekupenda vinginevyo changamoto zake zinaweza kugharimu maisha yako.
 
Habari wanajamvi.
Kwa kweli hilo swali huwa linanisononesha sana.
Nina umri wa miaka 30, sijaolewa, sina mchumba wala mpenzi yapata mwaka na miezi kadhaa sasa.
Mdogo wangu anayenifuatia ana miaka 27 aliolewa akiwa na miaka 24 na ana watoto wawili sasa.
Familia yangu na jamii inayonizunguka hainielewi na mara nyingi nakutana na hilo swali
"Mbona wenzako wanaolewa wewe huolewi, au una tatizo?"
Kiukweli hua napata ugumu sana kujibu hilo swali kwa sababu sina cha kuwajibu.
Labda ningesema nina tatizo au kasoro lakini kati ya niliowahi kuwa nao kimahusiano hakuna alieoa hadi sasa japo wote walinizidi umri na kuna wawili walikua na watoto tayari na mpaka sasa hawajaoa.
Hivi kwa jamii yetu mwanamke kutoolewa ni kasoro?
Maana kuna rafiki yangu naye anapata usumbufu kama wangu kutoka kwa familia yake.
Vipi kama mwanaume ninayempata yeye hana wazo la kuoa nifanyeje?
Na wanaume huwa wanaulizwa na kuonekana wana matatizo kama wanawake?
Nlijua unataka kutoa msaada ili wasiolewa sasa waolewe!
Suala la kuolewa ni bahati wala si kasoro.
Maana najua kasoro zipo nyingi...lakini watu wenye bahati zao hawaangaliwi...wao ni kupeta tu!
Pia pole saba kwa hilo tatizo...hapo umeshajiharibu mwenyewe kisaikolojia.
NiPM.
 
Mume/Mke uchaguliwa na mungu kwani na walio olewa au kuoa hawakuoa walioanza nao au wale waliowapenda zaidi lakini kwa mipangoya mungu walijikuta waliowapenda wamewaacha kwingine nawalikoenda wakajikuta wamekuwa na mahusiano yasiyokuwa rasimi na baadae yakawa rasimi!!hivyo kuolewa/kuoa nimipango ya mungu!!
 
Kuolewa sio issue sana ila kwa jamii yetu eti usipoolewa may una matatizo sio kweli bana.

Pole ila usijali watu wanaolewa na 40yrs wala isikutishe my dear
 
Pole sana mama wala usijali sana kuolewa ni kwa wakati na bahati tu inategemea, hasa kama umeamua mwenyewe. Usikilize moyo wako tu wala si maneno ya watu!
 
Wewe bint ucjinyanyapae, binafsi sion tatizo lolote, age yangu ni 30 (mwanaume) cjaoa na cna mchumba, ingawa maswali kama hayo huwa naulizwa, na huwa nawajibu kuwa cjaamua kuoa, jiamini utapata chaguo lako. Angalizo: ucjaribu! nasema tena usijaribu kuingia ktk ndoa kwa ajili ya kuiridhisha jamii inayokuzunguka!
 
Siku zote sioni kama kuolewa ni bahati au kasoro.
Kuolewa ni maamuzi + muda.
Muda ukifika utaolewa kama utaamua.
Ukiamua kuolewa wakati muda hauruhusu hutoolewa.
Usihofu da pretty, utaolewa hata kama utakuwa m bibi.
 
Habari wanajamvi.
Kwa kweli hilo swali huwa linanisononesha sana.
Nina umri wa miaka 30, sijaolewa, sina mchumba wala mpenzi yapata mwaka na miezi kadhaa sasa.
Mdogo wangu anayenifuatia ana miaka 27 aliolewa akiwa na miaka 24 na ana watoto wawili sasa.
Familia yangu na jamii inayonizunguka hainielewi na mara nyingi nakutana na hilo swali
"Mbona wenzako wanaolewa wewe huolewi, au una tatizo?"
Kiukweli hua napata ugumu sana kujibu hilo swali kwa sababu sina cha kuwajibu.
Labda ningesema nina tatizo au kasoro lakini kati ya niliowahi kuwa nao kimahusiano hakuna alieoa hadi sasa japo wote walinizidi umri na kuna wawili walikua na watoto tayari na mpaka sasa hawajaoa.
Hivi kwa jamii yetu mwanamke kutoolewa ni kasoro?
Maana kuna rafiki yangu naye anapata usumbufu kama wangu kutoka kwa familia yake.
Vipi kama mwanaume ninayempata yeye hana wazo la kuoa nifanyeje?
Na wanaume huwa wanaulizwa na kuonekana wana matatizo kama wanawake?
Pole Sis' kwa hizo changamoto kutoka ktk jamii zetu za kiafrika,kwa kukusaidia jibu hapo kwenye red,wambie "BADO NIPO NIPO KWANZA"
then life is goes on.
 
Kuolewa hakuna umri maarumu, panga mambo yako kama kawaida huku ukiendelea kumuomba Mungu akupe Mwenza mwema, naamini Mungu atakupa mwenza muda ukifika.
 
Nlijua unataka kutoa msaada ili wasiolewa sasa waolewe!
Suala la kuolewa ni bahati wala si kasoro.
Maana najua kasoro zipo nyingi...lakini watu wenye bahati zao hawaangaliwi...wao ni kupeta tu!
Pia pole saba kwa hilo tatizo...hapo umeshajiharibu mwenyewe kisaikolojia.
NiPM.
Unaonaje ukimPM wewe ?
 
Pole Da Pretty. Ila hizi social pressures ni ngumu sana kuzi ignore hasa zinapotoka kwa watu wako wa karibu!
 
Wewe bint ucjinyanyapae, binafsi sion tatizo lolote, age yangu ni 30 (mwanaume) cjaoa na cna mchumba, ingawa maswali kama hayo huwa naulizwa, na huwa nawajibu kuwa cjaamua kuoa, jiamini utapata chaguo lako. Angalizo: ucjaribu! nasema tena usijaribu kuingia ktk ndoa kwa ajili ya kuiridhisha jamii inayokuzunguka!

Sijinyanyapai na mara nyingi huwa nafurahia maisha yangu, tatizo pale wapoanza maswali yao, mbaya zaidi ni watu wangu tena ninaowaheshimu sana hasa mama zangu.
Hudhani ninavyoishi nakosea sana kama kutoka na marafiki zangu hivyo hutaka niachane na marafiki kwa kudhan nazua waoaji kunifata.
 
Nlijua unataka kutoa msaada ili wasiolewa sasa waolewe!
Suala la kuolewa ni bahati wala si kasoro.
Maana najua kasoro zipo nyingi...lakini watu wenye bahati zao hawaangaliwi...wao ni kupeta tu!
Pia pole saba kwa hilo tatizo...hapo umeshajiharibu mwenyewe kisaikolojia.
NiPM.

Inawezekana kweli nimejiharibu kisaikolojia (lakini bila kujua)
Hilo ni swali linalonikera kulisikia ndio maana nimeliweka hapo juu labda kwa kupitia sana hii post nitalizoea.
 
Pole Da Pretty. Ila hizi social pressures ni ngumu sana kuzi ignore hasa zinapotoka kwa watu wako wa karibu!
Kweli SMU,
Fikiria mama yangu mazi ananiuliza tena ujue haiishii hapo, na mawaidha kibao.
Najitahidi kuongea ila inafikia nanyamaza tu.
 
Dada angu pole sana kwa mawazo mabaya ulojiwekea na unawaza sana sababu wewe mwenyewe unapenda upate mchumba uolewe lakini inakuwa sivyo, embu jiulize maswali kwanza kwa nini unaokuwa nao hawakukuuliza swali hilo? pengine kuna kitu kinawakwaza bila ya wewe mwenyewe kujua, relax kila kitu kitakuja chenyewe wakati ukifika wala usiumie roho kuona mdogo wako alishaolewa, pia siku hizi kutaka kusoma kwanza wasichana wengi wamejikuta wana madegree kibao then wanatafuta wachumba wa kuwaoa miaka inakuwa imeenda sana mwishoni unajikuta kwenye situation ambayo unajiona umechelewa. mimi naona umri wako bado upo freshutapata tu mchumba
 
Sijinyanyapai na mara nyingi huwa nafurahia maisha yangu, tatizo pale wapoanza maswali yao, mbaya zaidi ni watu wangu tena ninaowaheshimu sana hasa mama zangu.
Hudhani ninavyoishi nakosea sana kama kutoka na marafiki zangu hivyo hutaka niachane na marafiki kwa kudhan nazua waoaji kunifata.
Miaka 2 ilopita mamangu mzaz alicctiza sana nioe mpaka akapendekeza kumchumbia bint m1 huko kijijin kwe2, nikamwambia acfanye jambo hilo mpaka hapo ntakapo mwambia, nashukuru naye had sasa hajarudia kuliongelea tena.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom