AirTanzania
JF-Expert Member
- Mar 17, 2011
- 1,139
- 1,035
Nimesikitishwa sana na Huduma zinazotolewa na bank za hapa nchini, huduma zao ni mbovu zisizojali wateja na wafanyakazi wa bank wanadharau utafikiri huduma hiyo ni ya bure kumbe unalipia all transaction na isitoshe pia kuwa mishahara yao inatokana na wateja kuweka au chukuwa pesa. Isitoshe ukiingia bank utamuona mfanyakazi wa bank anachezea kasimu kake kana kwamba wameajiriwa kuchezea simu. Ukiomba kukutana na Meneja ili utoe malalamiko utazungushwa na kuulizwa maswali utafikiri umekamatwa na polisi kwa kosa la kuua. Kwa nyie Mameneja na vibaraka wenu mnaofanyakazi za bank kuweni wastaarabu kwa kuwasiliza wateja. Ninavyojua mimi kuwa Bank hairuhusiwi kuzungumza na simu wala kuchezea simu ikiwa na maana kuwa kama mtu amekuja kuchukuwa pesa halafu kama unawaambia vibaka nje kuwa mtu amevaa ngu rangi hiyo amechukuwa kiasi hicho, kutumia simu Bank ni uhalifu hasa kama mfanyakazi wa ndani. Kwa kweli sifurahiwi na huduma zenu.