Kwanini Banks za Tanzania hazitumii "Mobile Phone Signal Jammers" badala ya kusumbuka kuwaambia wateja wasiongee na simu ili kupambana na wahalifu?

Infantry Soldier

JF-Expert Member
Feb 18, 2012
15,893
16,317
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa JamiiForums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

Ninaomba ufafanuzi kutoka kwa wataalamu wa ICT pamoja na Telecommunications.

Kwanini Banks za Tanzania hazitumii "Short-range Cellphone Signal Jammers" badala ya kusumbuka kuwaambia wateja wasiongee na simu wawapo eneo lile la kazi ili kupambana na ujambazi?

IMG_20191123_111415_665.jpg

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana nimeona katika dunia hii ya science and technology kuna haja gani ya mtumishi wa bank kumfuata mteja na kumuambia ya kwamba haruhusiwi kuongea na simu awapo eneo lile la bank kwa sababu za usalama ilhali kuna vifaa maalum kwa ajili ya shughuli hiyo.

Kuna kisa kimoja cha mtumishi wa bank moja hapa Tanzania alikuwa anawasiliana na majambazi kila ambapo mteja akiwa ametoka kuchukua kiasi kikubwa sana cha pesa.

Watu walikuwa wakitoa kuchukua pesa let's say 10 millions anashangaa pikipiki inasimama mbele yake kisha ananyooshewa pistol na kuambiwa akabidhi bahasha au pochi ya pesa ili asiuawe.

Baada ya matukio kadhaa ya namna ile ikaja ikagundulika ya kuwa taarifa zilikuwa zinatoka kwa moja ya wahudumu wa bank ile tena ni mwana mama na alikuwa akitoa description zote za mteja mlengwa kuanzia mavazi yake, rangi, kimo mpaka jinsia.

Mbona katika misafara ya baadhi ya viongozi tunaona Mobile Phone Signals zikiwa jammed for a short range of diameter kwa muda, kwanini inashindikana kufanyika kwa taasisi nyeti kama hizi za fedha?

OUR MOTTO: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO
 
Shikamooni wakubwa zangu wote wa hapa jamiiforums. Mimi mdogo wenu Infantry Soldier nipo mzima kabisa wa afya. Thanks to God the Almighty.

NINAOMBA UFAFANUZI KUTOKA KWA WATAALAM WA ICT PAMOJA NA TELECOMMUNICATIONS.

Kwanini Banks za Tanzania hazitumii "Short-range Cellphone Signal Jammers" badala ya kusumbuka kuwaambia wateja wasiongee na simu wawapo eneo lile la kazi ili kupambana na ujambazi?

View attachment 1270023

Nimeamua kuuliza hivi kwa maana nimeona katika dunia hii ya science and technology kuna haja gani ya mtumishi wa bank kumfuata mteja na kumuambia ya kwamba haruhusiwi kuongea na simu awapo eneo lile la bank kwa sababu za usalama ilhali kuna vifaa maalum kwa ajili ya shughuli hiyo.

Mbona katika misafara ya baadhi ya viongozi tunaona Mobile Phone Signals zikiwa jammed for a short range of diameter kwa muda, kwanini inashindikana kufanyika kwa taasisi nyeti kama hizi za fedha?

NINAOMBA UFAFANUZI KUTOKA KWA WATAALAM WA ICT PAMOJA NA TELECOMMUNICATIONS.

OUR MOTTO: KUWA MZALENDO IPENDE TANZANIA. USTAWI WA NCHI YETU UNAANZA NA WEWE. TIMIZA WAJIBU WAKO IPASAVYO
Hutaki wafanyakazi watumie whatsapp
 
Kwa kuongea na simu tuu ziibiwe sinaweza kuja nimevaa earphone utajuaje kaa naongea au nasikiliza mziki jambaz gani huyo mjinga atakuwa kill mda ananyanyua simu kupiga SA ataonekana teknolojia inaenda Kasi mtu anaweza kuja amevaa mawani tuu hyo hyo inawapa picha washikaji zake hyo hyo anazungumza nao wewe upo kwenye ule ulimwengu wa kipindi kile Cha pkipki Aina ya Baja hazitakiwi bank
 
Watu hawazuiwi kuongea na simu benki ili kupambana na ujambazi bali ili kupunguza kelele.Fahamu pia kwamba wafanyakazi wa benki hutumia simu kuwasiliana na wateja wao au wafanyakazi wenzao sehemu nyingine.
 
Watu hawazuiwi kuongea na simu benki ili kupambana na ujambazi bali ili kupunguza kelele.
Kuna kisa kimoja cha mtumishi wa bank moja hapa Tanzania alikuwa anawasiliana na majambazi kila ambapo mteja akiwa ametoka kuchukua kiasi kikubwa sana cha pesa. Watu walikuwa wakitoa kuchukua pesa let's say 10 millions anashangaa pikipiki inasimama mbele yake kisha ananyooshewa pistol na kuambiwa akabidhi bahasha au pochi ya pesa ili asiuawe.

Back
Top Bottom