Mjomba Fujo
JF-Expert Member
- Oct 27, 2012
- 2,322
- 5,946
Kiukweli nasikitishwa na huduma za kibenki kwa ujumla, kwa bank za hapa TZ.
Unaweza kwenda bank na shida ndogo na ya kawaida ila mlolongo unakua mrefu usio na maana wala tija yoyote.
Nilikua na shida ya majina kwenye kadi yangu ya nmb, majina yalichanganywa la kati na la mwisho hivyo ishu ilikua ni kuyapanga tu.
Kimbembe kinaanza:
1. Kadi imezuiliwa siwezi kufanya chochote mpaka nikaboreshe taarifa, kwenda bank wanataka nida, nida nimewapa wanasema inabidi kwenda kwa wanasheria nianze mchakato wa deed poll.
Kwa mwanasheria nikaenda tumeahauriana kwakua jina halibadiliki ni arrangement tu ya majina inafanyika hivyo hamna haja ya kuandaa deed poll, afidavit tu itatosha.
Kweli nikaandaliwa nikaenda nayo tawi la nmb, kufika, huko nao kwanza mmoja wa staff akaniambia inatakaiwa deed poll mwingine akajitokeza akasema affidavit inatosha, wakawa wanabishana, namimi ikabidi nitie utetezi kwamba jina halibadiliki, bali ni arrangement tu ya jina la la kati na la mwisho haya hapo nikafanikiwa tukaendelea na mchakato.
Wakataka kadi y nida nikawapa,
Chakushangaza naanza kuulizwa nimelaliza shule ya msingi mwaka gani, mara jina la kati la mama yako.
Maswali nilijibu ila nikawa najiuliza huu mlolongo wote wa nini, wana verify kitu gani, na kwenye nida kuna picha yangu.
Hilo likaisha
Kwenye kujaza form wakaniambia sign haifanani, ukawa mlolongo mwingine naambiwa nikale kiapo tena kwa mwanasheria cha kubadili signature, ikabidi nirudi tena kutolewa upepo na wakili yule, nikaandaliwa kiapo na kurudi nacho bank, kazi ikaanza upya.
Kiukweli zoezi lilikwisha ila shida yangu haikutatuka, nikaanza kufatilia tena napigwa danadana nenda kule nenda huku, kila mtu hajui nani wakunisaidia, nikaana kabisa nikija kutoa pesa zangu hii kadi naitupilia mbali.
Nikaja kwenda siku za mbele nikafanikiwa kutatua ila card ikawa bado na shida, hivyo nikatakiwa kuomba kadi mpya, mlolongo wake sasa mrefu balaa.
Kiukweli nimeshangaa mbona Equity bank hawana ukiritimba kiasi hichi.
Nimebaki nashangaa, nmb nimeambiwa kadi inatoka baada ya siku 10, ila equity bank nikienda siku moja naondoka na kadi yangu.
Kingine cha kunishangaza equity naenda na nida nawapatia siulizwi mambo ya shule ya msingi wala rangi ya nyumba yetu.
Cha mwisho, niliwahi kupata changamoto ya signature equity pia kwamba haifanani lakini yule mtu alinipa ushirikiano akaniambia irekebishe ifanane na hii kiukweli nilifungua ac muda mrefu na muda mwingine sign zinaweza chechemea ila nilipata ushirikiano na kingine equity wanatumia biometric verification, kwa maana unaweka dole gumba kwenye finger print scanner, sasa bank kubwa kama nmb wanashindwaje kujiongeza kuendana na mazingira ya sasa.
Nimeapa kamwe sintaweka pesa zangu huku kwasababu shida yoyote itakayojitokeza mlolongo ni mrefu sana.
Nmb mjirekebishe.
Kitu kidogo mlolongo mrefu sana.
Nawapongeza equity bank na bank nyingine zote ambazo zinaendana na wakati.
Nmb muda mwingi wafanyakazi wenu wanajaza maform, na kujaza taarifa kwenye computer utasema wana calculate mabomu ya nuclear mtu dk 15 ana click mouse anajaza taarifa.