Kwa walioolewa: Ulikutaje Nyumba au Chumba chako uliporudi kutoka Safari ambayo ulienda peke yako bila Mwenza?

Mwaka Jana nilisafiri masika nkaenda kulima bush, basi nkakaa kama wiki mbili, Ile narudi usiku nimechoka balaa nikajitupa kitandani na viatu nkaanza kuota kama nipo mtoni naskia sauti za vyura, ila Ile sauti ikawa kama inatokea kichwani mwangu, dakika Moja nyingi nkakurupuka Kumbe frog yupo chini ya kitanda.

Yaani wenge lote la usingizi likakata nikawa najiuliza kaingilia wapi au ni wa kutumwa, nikagundua alipitia chini ya mlango palipokuwa na uwazi.

Sasa mawazo yakazidi kuwa kama kaingia chura, nyoka atashindwaje, nikatoka nikaenda lala Kwa mshkaji kesho yake nikafanya famigesheni huwezi amini Ili kuwa kama zoo ya wadudu maana walitoka wengine hata siwafahamu.
Hahahahah
 
Sifa ya mwanamme wa kweli ni ukiingia kwake ukute kuchafu na vitu viko disorganized.

Ukienda anakokaa mwanamme pekee yake ukakuta ni kusafi na kumepangiliwa vizuri ujue huyo si mwanamme kamili ni mwanamke mwenzio.
Acha matusi bro mi binafsi tangu mdogo nilikua nafundishwa usafi chumba changu lazima nifanyie usafi nguo situpitupi naweka kwenye utaratibu mzuri, hadi leo hii nimeondoka nyumban bado suala la usafi nazingatia japo sifanyi kila siku lakini vitu vyangu ghetto naweka kwenye mpangilio mzuri na nikiona vimekaa vibaya weekend lazima nifanye usafi

Kuwa mwanaume haiuhusiani na kuwa mchafu, uchafu ni tabia hata wanawake wapo wachafu kuliko hata wanaume
 
Uchafu na mimi ni mbalimbali,tatizo nililo nalo mimi ni kuto kupangilia vitu ndani ya nyumba.
Ugomvi na mke wangu hutokana na hili na hata uvaaji wangu asipokuwa karibu navaa nguo kwa maana tu ni safi,habari za kuzingatia rangi,kujitizama kwenye kioo hapo ni kulazimishwa tu.
 
Kuna ghetto niliomba hifadhi, jumla tulikuwa tunaishi watatu. Wenzangu wanaenda kazini saa mbili asubuhi wanatoka saa tisa alasiri. Mimi nilikuwa naondoka saa 12 asubuhi kurudi saa tano usiku na nakuwa nimechoka sana. Sasa ghetto lilikuwa chafu balaa na muda mwingi jamaa wapo tu free wanacheki filamu. Sasa kuna wakati maji ya mvua yaliingia ndani, walichofanya waliweka tofali kuelekea kwenye kitanda. Yale maji yalikaa mule ndani hadi yakakauka likabaki tope tu lililoganda. Hadi naondoka kwenye lile ghetto halikuwahi kufanyiwa usafi.
malegendary
 
Nilibahatika kumsindikiza dada mmoja kwake na mizigo yake akiwa amerudi safari. Sasa ile namsaidia kuiingiza vitu ndani, sebuleni nilichokiona ni hatari!

Kweli sisi wanaume ni wachafu ila yule jamaa noma, gamboot na tope zake ndani, soksi juu ya meza, chupa za soda chini ya meza, mabuibui, yaani sio mchezo.

Sasa hapo ni sebuleni, chumbani sijui kulikuwaje! Wanawake mna mchango.
Chumba!?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom