Kwa walioolewa: Ulikutaje Nyumba au Chumba chako uliporudi kutoka Safari ambayo ulienda peke yako bila Mwenza?

Mwaka Jana nlisafiri masika nkaenda kulima bush,basi nkakaa kama wiki mbili,Ile narudi usiku mechoka balaa nkajitupa kitandani na viatu nkaanza kuota kama nipo mtoni naskia sauti za vyura,ila Ile sauti ikawa kama inatokea kichwani mwangu,dakika Moja nyingi nkakurupuka Kumbe frog yupo chini ya kitanda.
Yaani wenge lote la usingizi likakata nkawa najiuliza kaingilia wapi au niwa kutumwa,nikagundua alipitia chini ya mlango palipokuwa na uwazi.
Sasa mawazo yakazidi kuwa kama kaingia chura ,nyoka atashindwaje,nikatoka nkaenda lala Kwa mshkaji kesho yake nikafanya famigesheni huwezi amini Ili kuwa kama zoo ya wadudu maana walitoka wengine hata siwafahamu.
Moral of the story unaogopa chura,ila nyie wakaka wa siku hizi😁😁😁😁
 
Kuna kijana ukuta wa chumba chake uliachia kwa nyuma usawa wa kitanda kutokana na mvua kunyesha.... mwenyewe alikuwa mihangaikoni......

Yaani kulikuuwa na chupa za mikojo kama zote......aisee kuna watu ni wachafu......

Nyumba imezungushiwa ukuta lakini anaogopa kutoka nje usiku.......
 
Mimi huwa nakuta shuka analotandika kitandani limefungwa pande zote ili lisichomoke. Kwahiyo akilala akiamka hamna haja ya kutandika.

Vingine navikuta kama vilivyo, hagusi kitu zaidi ya anapokaa aangalie TV. Hapiki hata chai hadi mbwa anawanunulia chakula.
 
Nilibahatika kumsindikiza dada mmoja kwake na mizigo yake akiwa amerudi safari. Sasa ile namsaidia kuiingiza vitu ndani, sebuleni nilichokiona ni hatari!

Kweli sisi wanaume ni wachafu ila yule jamaa noma, gamboot na tope zake ndani, soksi juu ya meza, chupa za soda chini ya meza, mabuibui, yaani sio mchezo.

Sasa hapo ni sebuleni, chumbani sijui kulikuwaje! Wanawake mna mchango.
Duh mm nguo huwa navalia sebuleni hadi zinaisha
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom