Kwa vile ni Mwenyekiti wa CCM, unawajibika kwa hao vijana 46

Wadau, amani iwe kwenu.

Kumeibuka mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kumuomba Rais Magufuli kuwafikiria, kuwapongeza na kuwawezesha vijana 46 waliokuwa mitandaoni kukitetea chama. Naamini kuwa Kikwete alikuwa na dhamira njema ya kutambua mchango wa kila mmoja wetu alioutoa wakato wa mapambano ya kutwaa Dola. Naamini pia kuwa chama kilikuwa na mikakati imara ya kuhakikisha kuwa inashinda uchaguzi huo na miongoni mwa mikakati hiyo ni kuwa na vijana wa kushinda kwenye mitandao baada ya kubaini kuwa media zote zimenunuliwa na mafisadi.

Pamoja na hayo, binafsi naamini kuwa vijana hao 46 wapo chini ya chama. Kwa maana nyingine ni kwamba Mwenyekiti wa CCM ndiye anayewajibika kuwapongeza vijana hao na kuweka mikakati ya kuwawezesha ili wajipange upya kwa ajili ya 2020. Hata hivyo, hakika najisikia huzuni kubwa sana kuona Mwenyekiti wangu akitamka maneno hayo hadharani. Mikakati hiyo ilikuwa ya kichama na kitendo cha kutamka hadharani maana yake ni kwamba unadisclose mbinu za ushindi ambazo hazikupaswa kuwafikia maadui.

Nakubaliana na Maneno yako Mwenyekiti wangu kuwa Mwisho wa uchaguzi wa 2015 ni mwanzo wa uchaguzi wa 2020. Pia naamini kuwa mbinu zilizosaidia ushindi wa 2015 hazitatumika uchaguzi wa 2020 kwa vile CCM ina mbinu zaidi ya 200. Hata hivyo, wajibu wa kukitetea chama ni wa kila mwanachama. Inashangaza kuona Mwenyekiti ukiwaona vijana 46 tu ndio wanaostahili kupongezwa ilhali wapo vijana wengi hususan Wasanii ambao waliacha kazi zao na kuzunguka nchi nzima kukitetea chama mpaka wengine wakapachikwa majina mabaya yakiwemo WASALITI, WAPINGA MABADILIKO, WANATUMIKA KAMA CONDOM nk. Hawa umechukua hatua gani ya kuwapongeza?

Kutokana na kauli hiyo ya Kikwete na jinsi mjadala unavyoenda humu JF, hakika ninapata wasiwasi juu ya dhamira ya Januari Makamba. Ni vema tukajua hao vijana 46 aliwapataje? Je aliwaahidi nini? Mchango wao ulikuwaje mpaka Mwenyekiti wa Chama ashinikizwe kumuomba Rais awatambue vijana hao? Je wakati wa kuwaajiri vijana hao mlitangaza uwepo wa nafasi hizo kwenye Media? Kama mlifanya kimya kimya, iweje sasa mambo hayo yawe hadharani? Kuna tatizo gani limejitokeza?

Mambo haya ya kupongezana na kukwezana ndiyo yaliyowaponza Wapinzani. Mathalan, kule CHADEMA, kuna vijana kama akina Yeriko Nyerere, Michael Aweda, Marehemu Mohamed Mtoi, Henry Kilewo, Ben Saanane nk ambao walijifanya watetezi wakubwa wa chama kumbe walikuwa na malengo yao. Matokeo yake, waliojitokea kwa dhati kama akina Nusrat Hanje wamejikuta wakitupwa hata kwenye nafasi za viti maalum. Hizo ndo siasa za upinzani. CCM tunaamini kuwa kujitolea kwa ajili ya chama ni wajibu wa kila mwanachama na si mtu anafanya hivyo ili apate chochote au awe mtu fulani baada ya ushindi. Kama dhamira ya hao vijana ilikuwa wale shavu, hakika hawafai kuwa Makomredi. Watu wa aina hiyo ni rahisi kurubunika kama ilivyotokea kwa akina MUSSA ALLAN, MINYOO, FUNZA, MAMNDENYI, ASSADSYRIA3 na wengineo ambao wa sasa wamegeuka kuwa wapambe wa upinzani baada ya kununuliwa na fisadi Lowasa.

Narudia tena kusema kuwa kama dhamira ya vijana hao ni kutaka wapongezwe na hatimaye wateuliwe kuwa watu fulani au waajiriwe Serikalini, hakika hawafai kuwa wana CCM. Wafia chama tupo na tupo wengi sasa kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Tunafanya kazi 24 Hours na hatulipwi ujira wowote. Tunafanya hivyo kwa mapenzi yetu huku tukiamini kuwa ushindi wa CCM ndiyo faraja yetu. Kama ni lazima wapongezwe, basi nakuomba Mwenyekiti wangu timiza wajibu wako kwa vile utaendelea kuwa Menyekiti wa chama chetu hadi 2017
Mbona unaweweseka lizaboni,si tayari raisi kashaambiwa awakumbuke subir mrejesho basi, punguza kujiforward basi
 
Mkuu, yaani kama uliingia kwenye mtima wangu. Umeandika mambo ya msingi sana
Huu ndio ukweli wetu kama kweli tunaipenda Ccm. Kupongeza baadhi ya watu kwa kuwa wamekipigania Chama ni kutaka kuwagawa vijana ambao walijitokeza zaidi kuliko Hiyo Idadi ambayo inaonyeshwa kutengenezwa na mtu. Ufahari wetu uendelee kusimama na kuhakikisha kuwa tunakipigania chama bila kujali pongezi wala Malipo. Jk nadhani ameteleza katika kile alichokisema au wale waliomfikishia Hiyo habari ndio wamempotosha. Magufuli anaongoza Watanzania Wote bila kujali itikadi zao, pesa inazotumia Serikali ni pesa ya wananchi, kumwambia Rais Magufuli awawezeshe ni kosa lakini kama angekuwa yeye kama mwenyekiti wa chama basi lisingekuwa tatizo
 
Nilitimiza wajibu wangu kama mwanachama. Nitaendelea kufanya hivyo
WANACHAMA Wa CHAMA Chochote Cha Siasa Au Cha Upatu, Lazima Wana Wawe Na KATIBA, SHERIA, KANUNI Na TARATIBU Zao Walizojiwekea Na Walizokubaliana Kuzifuata!!! SIJUI Kama Ww Ni MWANACHAMA Wa CCM, Ambaye Unamiliki KADI Ya Uanachama!! MAANA Kama Ni MWANACHAMA Kweli, Lazima Ungekuwa UNAFAHAMU Kuwa Kuna Taratibu Za KUTOA MALALAMIKO, MAONI Na KUKOSOA Uteuzi, Uchaguzi, Matumizi, Kuhoji Na Utendaji Wa Baadhi Ya Viongozi Wako, Kwa Mujibu Wa KATIBA, SHERIA, MIONGONI, KANUNI, TARATIBU Na ZILE AHADI ZA MWANACHAMA!! KAMA CCM Leo Unaweza Kumpinga M/kiti Wao Wa TAIFA, Mitandaoni!!!! KWELI Napata Shaka UTARATIBU Huo MPYA Mliojiwekea!!!! BUT KWA IMANI NA NINAVYOJUA KATIBA, SHERIA, KANUNI, TARATIBU NA MIONGOZO YA VYAMA Na Zile Ahadi Za Utii Wa MWANACHAMA!! WW Na Wenzako Sio Wanachama Wa CCM, Bali Ni Mashabiki Tu Wa Kawaida!! ILA Mnataka Kulazimisha Kujulikana Na KULIPWA POSHO, Au FADHIRA KAMA AKINA AMON MPANJU!!
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Kumeibuka mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kumuomba Rais Magufuli kuwafikiria, kuwapongeza na kuwawezesha vijana 46 waliokuwa mitandaoni kukitetea chama. Naamini kuwa Kikwete alikuwa na dhamira njema ya kutambua mchango wa kila mmoja wetu alioutoa wakato wa mapambano ya kutwaa Dola. Naamini pia kuwa chama kilikuwa na mikakati imara ya kuhakikisha kuwa inashinda uchaguzi huo na miongoni mwa mikakati hiyo ni kuwa na vijana wa kushinda kwenye mitandao baada ya kubaini kuwa media zote zimenunuliwa na mafisadi.

Pamoja na hayo, binafsi naamini kuwa vijana hao 46 wapo chini ya chama. Kwa maana nyingine ni kwamba Mwenyekiti wa CCM ndiye anayewajibika kuwapongeza vijana hao na kuweka mikakati ya kuwawezesha ili wajipange upya kwa ajili ya 2020. Hata hivyo, hakika najisikia huzuni kubwa sana kuona Mwenyekiti wangu akitamka maneno hayo hadharani. Mikakati hiyo ilikuwa ya kichama na kitendo cha kutamka hadharani maana yake ni kwamba unadisclose mbinu za ushindi ambazo hazikupaswa kuwafikia maadui.

Nakubaliana na Maneno yako Mwenyekiti wangu kuwa Mwisho wa uchaguzi wa 2015 ni mwanzo wa uchaguzi wa 2020. Pia naamini kuwa mbinu zilizosaidia ushindi wa 2015 hazitatumika uchaguzi wa 2020 kwa vile CCM ina mbinu zaidi ya 200. Hata hivyo, wajibu wa kukitetea chama ni wa kila mwanachama. Inashangaza kuona Mwenyekiti ukiwaona vijana 46 tu ndio wanaostahili kupongezwa ilhali wapo vijana wengi hususan Wasanii ambao waliacha kazi zao na kuzunguka nchi nzima kukitetea chama mpaka wengine wakapachikwa majina mabaya yakiwemo WASALITI, WAPINGA MABADILIKO, WANATUMIKA KAMA CONDOM nk. Hawa umechukua hatua gani ya kuwapongeza?

Kutokana na kauli hiyo ya Kikwete na jinsi mjadala unavyoenda humu JF, hakika ninapata wasiwasi juu ya dhamira ya Januari Makamba. Ni vema tukajua hao vijana 46 aliwapataje? Je aliwaahidi nini? Mchango wao ulikuwaje mpaka Mwenyekiti wa Chama ashinikizwe kumuomba Rais awatambue vijana hao? Je wakati wa kuwaajiri vijana hao mlitangaza uwepo wa nafasi hizo kwenye Media? Kama mlifanya kimya kimya, iweje sasa mambo hayo yawe hadharani? Kuna tatizo gani limejitokeza?

Mambo haya ya kupongezana na kukwezana ndiyo yaliyowaponza Wapinzani. Mathalan, kule CHADEMA, kuna vijana kama akina Yeriko Nyerere, Michael Aweda, Marehemu Mohamed Mtoi, Henry Kilewo, Ben Saanane nk ambao walijifanya watetezi wakubwa wa chama kumbe walikuwa na malengo yao. Matokeo yake, waliojitokea kwa dhati kama akina Nusrat Hanje wamejikuta wakitupwa hata kwenye nafasi za viti maalum. Hizo ndo siasa za upinzani. CCM tunaamini kuwa kujitolea kwa ajili ya chama ni wajibu wa kila mwanachama na si mtu anafanya hivyo ili apate chochote au awe mtu fulani baada ya ushindi. Kama dhamira ya hao vijana ilikuwa wale shavu, hakika hawafai kuwa Makomredi. Watu wa aina hiyo ni rahisi kurubunika kama ilivyotokea kwa akina MUSSA ALLAN, MINYOO, FUNZA, MAMNDENYI, ASSADSYRIA3 na wengineo ambao wa sasa wamegeuka kuwa wapambe wa upinzani baada ya kununuliwa na fisadi Lowasa.

Narudia tena kusema kuwa kama dhamira ya vijana hao ni kutaka wapongezwe na hatimaye wateuliwe kuwa watu fulani au waajiriwe Serikalini, hakika hawafai kuwa wana CCM. Wafia chama tupo na tupo wengi sasa kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Tunafanya kazi 24 Hours na hatulipwi ujira wowote. Tunafanya hivyo kwa mapenzi yetu huku tukiamini kuwa ushindi wa CCM ndiyo faraja yetu. Kama ni lazima wapongezwe, basi nakuomba Mwenyekiti wangu timiza wajibu wako kwa vile utaendelea kuwa Menyekiti wa chama chetu hadi 2017

In short Lizabon,kwa akili yangu ya KIUTU UZIMA Mwenyekiti wenue anamwambia JPM kwamba asipige kelele sana hakushinda kwa haki.Pili Anatuonyesha kama yeye ndiye aliyemweka MAGUFULI na lazima wapatie hao 46 nafasi za serikali either ukuu wa wilaya au ukuu wa mikoa.Kwa maantiki kwamba waliopo 46 lazima waondoke au kwenye nafasi za kazi za serikali kuna watu wanachama wa UPINZANI kwa hiyo hao 46 lazima wapewe nafasi hizo na wengine wafagiwe kwa kisingizio cha kupasua majipu.

Haiingii akilini JK ambaye amemaliza CHUO kikuu akaongea ujinga huo.Thinking capacity yake ni 0.

Hivyo basi Lizabon usisiikitike kwa maana Mwenyekiti wako hapo ndipo mwisho wa kufikiri kwake.
 
"Wafia chama tupo na tupo wengi sasa kuliko ilivyokuwa huko nyuma.................."

Duh! sasa unalalamika nini? si uendelee kukifiaa chama

Acha kulalama kama una mapenzi na chama
 
Kwa kuwahadaa wtz eti mnazo mbinu za kikampeni kushinda hamjambo nani asiyejua mbinu zenu za tume na vyombo ya hela...huu uliopita mlipigwa mbaya ila niyaleyale ya zanzbar! hadanganywi mtu hapa.......wtz wa leo sio wale wa mwalimu....tupo macho tunaona kila kitu!!TUNATAKA TUME HURU YA UCHAGUZI AMBAYO ITALINDA AMANI YA NCHI YETU!!HII YA SASA NI MOJA YA MATAWI YA FCCM
Tulipigwa mbaya na nani? Na fisadi? Toka lini fisadi akashinda?
 
Hahahahah...kumbe haya matakataka kina Lizaboni yalikuwa yanakuja kwa shift hapa yakibadilishana ID......Nyambaaf kabisa
 
Hapana Mkuu. Mimi si katika hao vijana 46 wa Makamba
Sasa nyie mlosahaulika ni vijana wa Nape au nyie hamna kiongozi wenu, jikusanyeni mjulikane bwana msijifanyie tu mambo wakati makao makuu hawana taarifa zenu mtakosa vingi
 
Mkuu, kazi zangu ni biashara ya vifaa vya kielectronic na ujenzi. Nina maduka hapa Songea Mjini ambayo inanipa kipato kikubwa. Nimeajiri vijana wengi wa kazi na weledi kwenye kazi hizo. Ninapopata mwanya najitahidi kutimiza wajibu wangu kama mwanachama
Ngoja tupite TRA tuangalie acc yako
 
Kwa mara ya kwanza Lizaboni nimekupa like, Kikwete alishazoea mambo ya kubebana angekuwa ndiye raisi saa hii hao vijana wangepewa ukuu wa wilaya na mkoa. Magufuli hacheki na Kima
 
Ahsante sana dada Prishaz. Hakika nilijisikia aibu sana wakati Kikwete akiongea yale pale Namfua
 
Eti hawakulala masaa 24, wanapokezana shift kama wataalamu wa afya au walinzi!?

Kuna thread iliwahi kuletwa humu, ikionyesha picha vijana wamekaa kwenye room na laptop ikiwa na caption "Ccm Masaki IT," nikapuuzia, kumbe M/kiti kafunguka rasmi.

Aliyewapa jina la MISUKULE hakukosea kabisa. Nadhani mnaijua sifa yao.
 
Back
Top Bottom