Kwa vile ni Mwenyekiti wa CCM, unawajibika kwa hao vijana 46

Teeeeeeeeh teeeeeeeeh teeeeeeeeeh, naona ndio unatoka kuning'inizwa,pole na hapo bado utaisoma mwaka huu ndiobutaacha kucheza na watu
Naendelea kukuuliza swali la asubuhi. Unaendelea kucomment ukiwa umekumbatiwa na wanaume wangapi? Swali hili tangu asubuhi halijapata jawabu
 
Mkuu Lizaboni hili suala kwa kweli ni tete.

Yaani umenikumbusha kwenye Ma group ya whatsup nk jinsi ambavyo watu walikuwa wananuniana kisa mmoja UKAWA mwingine CCM. Ugomvi tumeshuhudia hata makanisani, maofisini, kwenye ndoa, wana ndg nk watu wengine wamepigwa kwa ajili ya CCM!!! Leo nani anawakumbuka???

This time chama kimepiganiwa na watu wengi mno na wengine ni UKAWA. Wewe mwenyewe tathmini Ma grp ya whatsup, fb nk yalivyokuwa ya moto. Mimi nadhani Mhe. Makamba amekosea.

Kama ni vi katuni kila mwenye uwezo Wa kuchora alichora, wengine wasioweza kuchora walipiga picha za magazetini na kurusha kwenye mitandao mradi kujibu hoja za UKAWA na kuitetea CCM.

Kuna mama lishe na wanawake huku MITAANI walikuwa wanazunguka nyumba kwa nyumba na hawakupewa hata nauli.

KWANZA KAMPENI ZA MWAKA HUU ZILIKUWA NGUMU MNO; HELA WALISHIKA WATU WACHACHE NA WENGINE NDIO HAO WANADAI FADHILA KWA DR. JPM

Uchaguzi UMEISHA tupige kazi jamani. Watu Wa kukumbukwa ni wengi mnoooooo!!!!! Naamini kila mtu alifanya kwa raha zake. Pia hiyo itavunja moyo wapambanaji ambao mpaka sasa wako live!!!

Kupambana JF sio mchezo!!!! Na wana JF kwaribu 98% hawako kwenye list????? Mh!!!!!

Queen Esther
Wewe ni mnafki mkubwa sana... Jana humu ulileta uzi wa kuorodhesha vijana ili mupeleke huko Lumumba mkapongezwe, leo unakuja na story nyingine... CCM acheni unafki, au mnawaonea wivu hao vijana 46?? Wacheni wapongezwe nyie endeleeni kula vumbi humu JF... Mnaambiwa CCM ina wenyewe kila siku ila hamuelewi. Mfurahie tu hizo buku 7 zinawatosha..
 
Huu ndio ukweli wetu kama kweli tunaipenda Ccm. Kupongeza baadhi ya watu kwa kuwa wamekipigania Chama ni kutaka kuwagawa vijana ambao walijitokeza zaidi kuliko Hiyo Idadi ambayo inaonyeshwa kutengenezwa na mtu. Ufahari wetu uendelee kusimama na kuhakikisha kuwa tunakipigania chama bila kujali pongezi wala Malipo. Jk nadhani ameteleza katika kile alichokisema au wale waliomfikishia Hiyo habari ndio wamempotosha. Magufuli anaongoza Watanzania Wote bila kujali itikadi zao, pesa inazotumia Serikali ni pesa ya wananchi, kumwambia Rais Magufuli awawezeshe ni kosa lakini kama angekuwa yeye kama mwenyekiti wa chama basi lisingekuwa tatizo
acha kubishana na wenye chama.. wenye chama wanajua fika vijana wa huko CCM wako kimaslahi..
 
Mkuu, kazi zangu ni biashara ya vifaa vya kielectronic na ujenzi. Nina maduka hapa Songea Mjini ambayo inanipa kipato kikubwa. Nimeajiri vijana wengi wa kazi na weledi kwenye kazi hizo. Ninapopata mwanya najitahidi kutimiza wajibu wangu kama mwanachama
wafanyabiashara wengi tunajua ni wezi wakubwa na mmeliibia taifa hili vya kutosha. Na mko chamani ili mambo yenu yaende vizuri. Hamlipi kodi hata kidogo, biashara nyingi za magendo. Acheni wizi tujenge taifa.
 
Yaani sioni kama hata kuna impact yoyotw mliyoisababisha. Kama kuna mbinu iliyofanikiwa mitandaoni basi ni moja tu ambayo ilikua ni kuondoa threads na comments za watu fulani hapa JF.
Nje ya hapo mnajitekenya tu.
Na kilichowapeni ushindi ni Lubuva and the company, hakuna kingine.
 
Ahsante sana Queen Esther kwa bandiko lako hili. Hakika uzi huu umetiwa nguvu na lile bandiko lako la juzi. Hakika ulieleza vizuri sana. Nami nikaona nitoe maoni yangu humu ili kuunga mkono hoja zako. Nasema ahsante sana na tuendelee kuwa wakweli daima

wewe na queen mnajichanganya sana kwakweli... mara nazitaka mbichi hizi, mara sizitaki mbichi hizi, na watu wanawasoma vizuri tu... ni huzuni sana aisee.

mzee MM kakaa kimyaaaa...
 
Hapa sasa ndio nimeona ni Kwa nini office za serikali zina wafanya kazi vihiyo kumbe ni fadhila ndio ndio zinazotuletea shida hizi
 
Mkuu nipo ktk kurasa moja na ww,
wala viwavi wa IT masaki wameanza kulalama.

ili hawa vijana 46 wa ccm wafanye hiyo kazi yao ilibidi polisi wavamie na kuwateka vijana zaidi ya 100 wa UKAWA waliokuwa wanafanya the same job, sasa wala viwavi wametupwa kama kamasi imebaki story hapo Lumumba.
Mkuu nipo kurasa moja na wewe,vijana waliozungumziwa na jk ni wale waliokuwa kwenye tallying center zao,aliamua tu kumung'unya maneno na kikosi kingine kiligawanyiwa majukum ya kushambulia mitandao,ote tu mashahidi jinsi mashambulizi dhidi ya JF yalivyokithiri usiku wa kuamkia tarehe 26
 
Huu ndio ukweli wetu kama kweli tunaipenda Ccm. Kupongeza baadhi ya watu kwa kuwa wamekipigania Chama ni kutaka kuwagawa vijana ambao walijitokeza zaidi kuliko Hiyo Idadi ambayo inaonyeshwa kutengenezwa na mtu. Ufahari wetu uendelee kusimama na kuhakikisha kuwa tunakipigania chama bila kujali pongezi wala Malipo. Jk nadhani ameteleza katika kile alichokisema au wale waliomfikishia Hiyo habari ndio wamempotosha. Magufuli anaongoza Watanzania Wote bila kujali itikadi zao, pesa inazotumia Serikali ni pesa ya wananchi, kumwambia Rais Magufuli awawezeshe ni kosa lakini kama angekuwa yeye kama mwenyekiti wa chama basi lisingekuwa tatizo

eti katereza, eti wasaidizi wake wamempotosha... kwa hiyo sera za kulipana fadhila na kukumbukana jk hazijui? dah!!!! kwanini mnapata shida hivyo kusimamia ukweli???
 
eti katereza, eti wasaidizi wake wamempotosha... kwa hiyo sera za kulipana fadhila na kukumbukana jk hazijui? dah!!!! kwanini mnapata shida hivyo kusimamia ukweli???
ukweli upi unaouzungumzia hapa? Kama ni kulipa fadhila ni jukumu la chama sio Serikali..
 
ukweli upi unaouzungumzia hapa? Kama ni kulipa fadhila ni jukumu la chama sio Serikali..

kwa hiyo 'alitereza' kumwambia magufuli awalipe fadhila vijana wa ccm waliomwezesha kushika dola...ilhali akijua yeye ni mwenyenyekiti wa chama!!? alijisahau kabisa kwamba yeye ndio mwenyekiti wa chama...
 
Wadau, amani iwe kwenu.

Kumeibuka mjadala mzito kwenye mitandao ya kijamii baada ya Mwenyekiti wa CCM, Jakaya Kikwete kumuomba Rais Magufuli kuwafikiria, kuwapongeza na kuwawezesha vijana 46 waliokuwa mitandaoni kukitetea chama. Naamini kuwa Kikwete alikuwa na dhamira njema ya kutambua mchango wa kila mmoja wetu alioutoa wakato wa mapambano ya kutwaa Dola. Naamini pia kuwa chama kilikuwa na mikakati imara ya kuhakikisha kuwa inashinda uchaguzi huo na miongoni mwa mikakati hiyo ni kuwa na vijana wa kushinda kwenye mitandao baada ya kubaini kuwa media zote zimenunuliwa na mafisadi.

Pamoja na hayo, binafsi naamini kuwa vijana hao 46 wapo chini ya chama. Kwa maana nyingine ni kwamba Mwenyekiti wa CCM ndiye anayewajibika kuwapongeza vijana hao na kuweka mikakati ya kuwawezesha ili wajipange upya kwa ajili ya 2020. Hata hivyo, hakika najisikia huzuni kubwa sana kuona Mwenyekiti wangu akitamka maneno hayo hadharani. Mikakati hiyo ilikuwa ya kichama na kitendo cha kutamka hadharani maana yake ni kwamba unadisclose mbinu za ushindi ambazo hazikupaswa kuwafikia maadui.

Nakubaliana na Maneno yako Mwenyekiti wangu kuwa Mwisho wa uchaguzi wa 2015 ni mwanzo wa uchaguzi wa 2020. Pia naamini kuwa mbinu zilizosaidia ushindi wa 2015 hazitatumika uchaguzi wa 2020 kwa vile CCM ina mbinu zaidi ya 200. Hata hivyo, wajibu wa kukitetea chama ni wa kila mwanachama. Inashangaza kuona Mwenyekiti ukiwaona vijana 46 tu ndio wanaostahili kupongezwa ilhali wapo vijana wengi hususan Wasanii ambao waliacha kazi zao na kuzunguka nchi nzima kukitetea chama mpaka wengine wakapachikwa majina mabaya yakiwemo WASALITI, WAPINGA MABADILIKO, WANATUMIKA KAMA CONDOM nk. Hawa umechukua hatua gani ya kuwapongeza?

Kutokana na kauli hiyo ya Kikwete na jinsi mjadala unavyoenda humu JF, hakika ninapata wasiwasi juu ya dhamira ya Januari Makamba. Ni vema tukajua hao vijana 46 aliwapataje? Je aliwaahidi nini? Mchango wao ulikuwaje mpaka Mwenyekiti wa Chama ashinikizwe kumuomba Rais awatambue vijana hao? Je wakati wa kuwaajiri vijana hao mlitangaza uwepo wa nafasi hizo kwenye Media? Kama mlifanya kimya kimya, iweje sasa mambo hayo yawe hadharani? Kuna tatizo gani limejitokeza?

Mambo haya ya kupongezana na kukwezana ndiyo yaliyowaponza Wapinzani. Mathalan, kule CHADEMA, kuna vijana kama akina Yeriko Nyerere, Michael Aweda, Marehemu Mohamed Mtoi, Henry Kilewo, Ben Saanane nk ambao walijifanya watetezi wakubwa wa chama kumbe walikuwa na malengo yao. Matokeo yake, waliojitokea kwa dhati kama akina Nusrat Hanje wamejikuta wakitupwa hata kwenye nafasi za viti maalum. Hizo ndo siasa za upinzani. CCM tunaamini kuwa kujitolea kwa ajili ya chama ni wajibu wa kila mwanachama na si mtu anafanya hivyo ili apate chochote au awe mtu fulani baada ya ushindi. Kama dhamira ya hao vijana ilikuwa wale shavu, hakika hawafai kuwa Makomredi. Watu wa aina hiyo ni rahisi kurubunika kama ilivyotokea kwa akina MUSSA ALLAN, MINYOO, FUNZA, MAMNDENYI, ASSADSYRIA3 na wengineo ambao wa sasa wamegeuka kuwa wapambe wa upinzani baada ya kununuliwa na fisadi Lowasa.

Narudia tena kusema kuwa kama dhamira ya vijana hao ni kutaka wapongezwe na hatimaye wateuliwe kuwa watu fulani au waajiriwe Serikalini, hakika hawafai kuwa wana CCM. Wafia chama tupo na tupo wengi sasa kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Tunafanya kazi 24 Hours na hatulipwi ujira wowote. Tunafanya hivyo kwa mapenzi yetu huku tukiamini kuwa ushindi wa CCM ndiyo faraja yetu. Kama ni lazima wapongezwe, basi nakuomba Mwenyekiti wangu timiza wajibu wako kwa vile utaendelea kuwa Menyekiti wa chama chetu hadi 2017
Fisadi si kikwete nawe umenunuliwa
 
Back
Top Bottom