Kwa Umafia huu mkubwa wa FA ya Mbeya, Ihefu FC wakisaidiwa na Watu wa Simba SC 'Unbeaten Record' ingeisha tu leo

Kwa hyo hakuna sheria ya jezi???hv we jamaa unajua nini kwenye soka??sasa kwanini kuna jezi ya home na ya away??bora uwe unapiga kimya tu muda mwingine
Achana na hilo Pumbavu ( Pang'ang'a ) Mkuu sawa? Ukiona namdharau sana Mtu hapa JamiiForums jua pia kuwa ni Mental Case ( Mwendawazimu ) kama huyu malantu
 
Mzee wa kutunga stori (mzee wa propaganda) siku hizi mchezo wa mpira umekuwa watu wakiamka wanajiamulia tu. Endelea kudanganya wehu wenzio
Mbona hata 'Aliyekuzaa' nae ni Mwehu kama ulivyoniita Mimi na wala hushangai?
 
Umeandika kama vile unawasimulia watoto zako ambao hawatumii akili kufikiria.

1) ishu ya kubadilika kwa uwanja haiwezi kutokea Yanga wasijue kwasababu kisheria ni kwamba kunapotokea mabadiliko ya uwanja basi inatakiwa timu ijulishwe masaa 24 kabla na sio ishu ya uwanja tu bali mabadiliko yoyote ikiwemo hata muda wa mchezo. Hivyo laiti kama Yanga wangekuwa hawalijui hilo basi walikuwa na haki ya kuugomea mchezo.

2) kwenye mchezo wa mpira wa mguu kuna kitu kinaitwa pre match. Na hufanyika siku moja kabla ya mchezo, hapa ndipo kila tumu inawasilisha rangi ya jezi atakayoitumia katika mchezo husika ambapo mwenyeji ndiye anayepewa kipaumbele cha aina ya jezi kisha timu mgeni ndiye anayepaswa kuangalia rangi ya tofauti na ya mwenyeji.

Stori yako ya kusema yanga wamestukiziwa siku ya mechi kuhusu uwanja na jezi, kawadanganye wasiojua taratibu za mchezo wa soka

Sent from my Redmi Note 9 Pro using JamiiForums mobile app
Hua anawachota mandezi wenzake
 
Kwa hyo hakuna sheria ya jezi???hv we jamaa unajua nini kwenye soka??sasa kwanini kuna jezi ya home na ya away??bora uwe unapiga kimya tu muda mwingine
Yanga kamfunga Simba akiwa na jezi ipi? Karne hii bado una amini vitu vya kijinga hivyo?
 
Kwa Kawaida Makomandoo wa Yanga SC na hasa Mganga wao Hatari hupenda Kutangulia (Kuwahi) Mkoa ambao Yanga SC inacheza kisha wanaanza Kuufanyia Umafia na Uchawi (Ndumba) Uwanja ambao Utachezewa.

Hivyo basi baada ya FA ya Mkoa wa Mbeya (hasa Kiongozi wao Mmoja mwana Simba SC) Kugundua Janja ya Yanga SC (hasa Kiushirikina) kwa kuamini Mechi itachezewa Uwanja wa Sokoine haraka sana Mkakati mpya ulisukwa kwa Kushirikiana na Viongozi wa Ihefu FC na wale wa Simba SC ambao umefanikiwa kwa 100%

Wakiwa Wasiri kabisa FA ya Mbeya walijua kuwa Mechi haitocheza Sokoine ambako Yanga SC waliamini ungechezewa hapo hivyo kama Kawaida yao wakaanza Kuroga pasipokujua kuwa Wanaroga mahala ambako Mechi haitochezwa.

Huku Wao Yanga SC wakiroga Uwanja wa Sokoine wenzao wa Ihefu FC kwa Kushirikiana na K? Watu (Mafia) wa Simba SC (Walioko Kazini sasa kwa Michezo Michafu ili Kuipunguza Kasi Yanga SC) nao (Ihefu FC) wakawa Wanauroga vilivyo Uwanja wa Highland Estate ambao umechezewa huo Mchezo leo.

Baada ya Mkakati huu Kukamilika iliwabidi Ihefu FC na Viongozi wa FA ya Mbeya kwa Kusaidiwa na Mafia wa Simba SC ilitafutwa Mbinu mpya ya Kuwamaliza Yanga SC Kisaikolojia kwa kulenga kile Kitu ambacho huwa kinawapa Nguvu ambacho ni Matumizi ya Jezi yao Nyeusi iliyofanyiwa Ndumba Kali na Mganga wao Hatari na Kulazimisha iwe inavaliwa hiyo hiyo tu kwani nyinginezo hasa ya Njano waliyoivaa Leo ina Nuksi na hawaipendi ila hawana jinsi.

Na kweli mapema kabisa Jana Mchana Yanga SC (bila ya Kutegemea) waliambiwa na FA ya Mbeya kuwa Mechi yao ya leo dhidi ya Ihefu FC itachezewa Uwanja wa Highland Estate na siyo Sokoine ambako ndiko walikuwa Wameroga sana (tena kwa Kukufuru kabisa) hali iliyowavunja kabisa Nguvu na Kuchanganyikiwa na inasemekana hata Mganga wao (Yanga SC) alishawaambia kuwa Mechi ya leo 95% wanafungwa na 5% ndiyo za Kushinda au kutoka Sare.

Baada ya FA ya Mbeya jana Kuwamaliza Yanga SC juu ya Uwanja utakaotumika leo Asubuhi Taarifa ikatoka TFF kwenda FA ya Mbeya kuwataka Yanga SC wasiitumie Jezi yao Nyeusi (ambayo Yanga SC ndiyo wanaiamini kuwa ina Bahati Kwao na Mganga wao ameshaifanyia Ndumba sana) na Kuzingatia Kanuni za Ligi hali ambayo iliwashtua zaidi Yanga SC na kujua kuwa leo wamepatikana na kuingia Mtegoni ambako wakaishia kupata Kipigo kutoka kwa Timu dhaifu ya Ihefu FC.

Kipigo leo kilikuwa hakiepukiki kabisa.

Cc: Fundi mahiri wa ujenzi
Habari ya kipuuzi hi i ni ajabu pia Kama watu wataicomment na kuiamini Kama umeweza kupata taarifa hizi Leo ulishindwaje kuzipata tango mwaka mzima na usher Tanga wakiwa bila kufungwa ? Non sence
 
Habari ya kipuuzi hi i ni ajabu pia Kama watu wataicomment na kuiamini Kama umeweza kupata taarifa hizi Leo ulishindwaje kuzipata tango mwaka mzima na usher Tanga wakiwa bila kufungwa ? Non sence
Hauna Akili acha kunipotezea muda!!
 
Sasa kama mnajua mnaweza kumfunga simba na jezi hizo mbona hamtaki kuvaa mpaka mnakiuka sheria za bodi ya ligi?
umesikia wapi hio habari,? anyway endelea na jamaa yako Genta akujaze uongo
 
JF imekua ya kipuuzi sana siku hizi, watu wameigeuza fb, majukwaa tuliyokua tunapata taarifa serious na reliable siku hizi yamejaa story za kizushi hazina logic, hazina ushahidi.
Unazungumzia kubadili uwanja huoneshi kanuni zinavyosema, unahusisha mambo ya Jezi huoanishi na kanuni. Na watu walivyo wa ajabu nao wanaamini tu.Ingekua kule kwingine tungesema mtu anaandika il kutafuta followers, sasa humu JF unatafuta followers wakusaidie nini zaidi ya ujuha tu.
Pathetic.
 
JF imekua ya kipuuzi sana siku hizi, watu wameigeuza fb, majukwaa tuliyokua tunapata taarifa serious na reliable siku hizi yamejaa story za kizushi hazina logic, hazina ushahidi.
Unazungumzia kubadili uwanja huoneshi kanuni zinavyosema, unahusisha mambo ya Jezi huoanishi na kanuni. Na watu walivyo wa ajabu nao wanaamini tu.Ingekua kule kwingine tungesema mtu anaandika il kutafuta followers, sasa humu JF unatafuta followers wakusaidie nini zaidi ya ujuha tu.
Pathetic.
Rubbish and Nonsensical.
 
Back
Top Bottom