Kwa nini tusichapishe hela mpya?

Kwa nchi zenye uchumi tete kama Tanzania, ni mbinu ya gavana ku control dafu mtaani. However I doubt kwani kughushi pesa kupo duniani kote na hatujasikia Marekani au UK wakibadilisha noti. Pesa yaweza kubadilishwa gradually. Kama kweli wanataka ku control pesa feki
1. kila mfanyabiashara awe na mashine za kude tect noti bandia
2 wanapochapisha hizo noti basi apewe mkandarasi mwenye kujua kazi yake sio noti inatoka leo kesho ukiiona haifai tena. na watumie modern technology.
Hivi kweli porofesa mzima wa uchumi anabadilisha pesa eti kuzuia noti za kughushi!!!! I dont think so. angetoa another financial and economical stands kwa zoezi hilo.
 
I am learning a lot!
 
Zakumi,

Okay, lets reverse the fortunes. What if Jamhuri and BOT would guarantee a 5% interest into a savings account for anyone who would open an account with a bank during the exercise than taking out a Bulungutu la shilingi kwa shilingi?

Hiyo inakubalika. Lakini swali lina baki palepale. Je hao wateja wataendelea kuweka pesa zao benki au baada ya muda fulani watarudi katika hali yao ya kawaida.

Ikiwa nia ni kubadilisha pesa hili ni kuondoa pesa za kugushi mara moja, It doesnt really matter how they approach it. Kwa sababu baada ya muda mfupi, pesa zote za kugushi zitakuwa zimeondoka mitaani. Na kama kulikuwa kuna negavite impacts za pesa za kugushi kama vile mfumuko wa bei, basi kwa kipindi fulani zoezi hilo litasaidia.
 
Kwa nchi zenye uchumi tete kama Tanzania, ni mbinu ya gavana ku control dafu mtaani. However I doubt kwani kughushi pesa kupo duniani kote na hatujasikia Marekani au UK wakibadilisha noti. Pesa yaweza kubadilishwa gradually. Kama kweli wanataka ku control pesa feki
1. kila mfanyabiashara awe na mashine za kude tect noti bandia
2 wanapochapisha hizo noti basi apewe mkandarasi mwenye kujua kazi yake sio noti inatoka leo kesho ukiiona haifai tena. na watumie modern technology.
Hivi kweli porofesa mzima wa uchumi anabadilisha pesa eti kuzuia noti za kughushi!!!! I dont think so. angetoa another financial and economical stands kwa zoezi hilo.

Maarifa:

Mimi sina financial and economical stands kuwatetea. Lakini kuchapisha pesa kumetumika na nchi mbalimbali kwa sababu tofauti.

Kwanza zoezi la kuchapisha pesa ni zoezi linaloendelea kwa nchi nyingi kwa sababu pesa zinazeeka. Hivyo pesa zinazozeeka ni lazima ziondolewe kwenye circulation.

Kuwa na mashine ya ku-detect ni gharama vilevile. Je wamachinga nao wanatakiwa kuwa na detectors?

Sina uhakika lakini nafikiri hata noti za sasa ni superior kuliko noti bandia. Matatizo yanayokuja ni kuwa watumiaji wengi wana kiwango kidogo cha elimu au hawaelewi kutofautisha noti bandia na halali. Na kuongeza matatizo, sehemu kubwa ya transactions za kila siku zinafanyika kwa cash.
 
Date::3/16/2009

Noti mpya za Sh2,000 kuanza kutumika karibuni

Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi​
SHEHENA ya noti mpya za Sh2,000 inatarajiwa kuingia nchini wakati wowote na kuanza kutumika, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilisema jana.

Kwa mujibu wa gavana wa BoT, Profesa Benno Ndulu noti hizo zitaingizwa kwa njia maalumu (tunayo), ambayo alisita kuitaja kwa sababu za usalama.

Akizungumzia mchakato huo, Gavana Ndulu alisema tayari kila hatua muhimu zimekwishamalizika.

"Zitaingizwa nchini wakati wowote, lakini kwa sababu za kiusalama si vizuri kutaja ni njia gani," alisema Profesa Ndulu.

"Kazi kubwa ya BoT ni kutunza noti, huwa zinatengenezwa sehemu fulani kisha tunaletewa."

Awali fedha za Tanzania zilikuwa zikichapishwa na kampuni ya Thomas de la Rue, ambayo imeshamaliza mkataba wake baada ya kuchapisha noti za Tanzania kwa kipindi cha miaka saba.

Awali, Prof Ndulu alikiri kuwa wanatarajia kufanya mabadiliko makubwa kwenye fedha za sasa, ingawa hakutaja mabadiliko hayo wala aina ya fedha ambazo zingebadilishwa. Baadaye alibainisha kuwa wataanzia na noti za Sh2,000.

Mpango wa mabadiliko hayo unalenga katika kuondoa saini ya maofisa wawili wa juu wa BoT. Noti za sasa zina saini ya gavana wa zamani wa benki hiyo, Daudi Bilali, ambaye amefariki, na Waziri wa Fedha, Basil Mramba, ambaye amefunguliwa mashtaka ya kutumia vibaya madaraka yake.

Kwa mujibu wa Gavana Ndulu hadi sasa maandalizi ya kupokea noti hizo na kuziingiza katika mzunguko yamekuwa yakienda vizuri.

Profesa Ndulu aliongeza kwamba mfumo mzima wa mzunguuko wa fedha uko katika uangalizi maalumu tayari kwa mabadiliko.

Katika hatua nyingine, Profesa Ndulu amesema kampuni ya Lazad ya Ufaransa ambao inajukumu la kukagua deni halisi la Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) itasaini mkataba wa kazi wakati wowote.

Profesa Ndulu alisema Lazad, ambayo ilipaswa kusaini mkataba huo muda mfupi tu baada ya mkutano kati ya Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) na mawaziri wa fedha na magavana wa nchi za Afrika uliofanyika mapema mwezi huu jijini Dar es salaam, iko tayari kwa kazi hiyo.
 
Date::3/16/2009

Noti mpya za Sh2,000 kuanza kutumika karibuni

Na Ramadhan Semtawa
Mwananchi​
SHEHENA ya noti mpya za Sh2,000 inatarajiwa kuingia nchini wakati wowote na kuanza kutumika, Benki Kuu ya Tanzania (BoT) ilisema jana.

Awali, Prof Ndulu alikiri kuwa wanatarajia kufanya mabadiliko makubwa kwenye fedha za sasa, ingawa hakutaja mabadiliko hayo wala aina ya fedha ambazo zingebadilishwa. Baadaye alibainisha kuwa wataanzia na noti za Sh2,000.

Mpango wa mabadiliko hayo unalenga katika kuondoa saini ya maofisa wawili wa juu wa BoT. Noti za sasa zina saini ya gavana wa zamani wa benki hiyo, Daudi Bilali, ambaye amefariki, na Waziri wa Fedha, Basil Mramba, ambaye amefunguliwa mashtaka ya kutumia vibaya madaraka yake.

Profesa Ndulu alisema Lazad, ambayo ilipaswa kusaini mkataba huo muda mfupi tu baada ya mkutano kati ya Shirika la Kimataifa la Fedha (IMF) na mawaziri wa fedha na magavana wa nchi za Afrika uliofanyika mapema mwezi huu jijini Dar es salaam, iko tayari kwa kazi hiyo.

Naomba kuuliza wana JF, sote tunajua kuwa Mramba anatuhumiwa kwa ufisadi/kutotumia vizuri madaraka yake. Vilevile tunatambua kuwa Dr. Daudi Balalli alishafariki. Je hizi ni sababu za musingi kubadilisha noti kwa lengo la kubadili sahihi za wahusika hawa?????, Natambua swala la kuchapisha noti linahitaji pesa nyingi tu na Tanzania si kisiwa katika kipindi hiki cha economic meltdown. Naombeni msaada hapa.
 
mm naona hawakufanya vibaya ukizingatia zoezi lenyewe linakwenda hatua kwa hatua, halafu mabadiliko kama haya ni ya kawaida kwa mabenki kila baada ya kipindi fulani, hata kama kusinge kuwa na sababu hizo zilizotajwa, kwani mara ngapi bot imebadili sarafu zake kwa sababu tofauti na hizo, kuhusu timing ni kweli lakini mipango hiyo ilikuwapo kabla hali ya uchumi wa dunia haujapata msukosuko
 
Junius, nafahamu utaratibu wa ubadilishaji sarafu/noti. Tatizo langu ni sababu yamsingi iliyotolewa na Gavana wetu. Hilo ndio tatizo langu.
 
Kuna tetesi kuwa hizo noti zina picha ya Mkapa. Tafadhali niondeeni hofu hii -- maana kama ni hivyo, bila shaka lengo si kuondoa tu hizo sahihi, sababu ambayo ni ya kipuuzi kupindukia, bali ni kujaribu kumsafisha Mkapa kwa ufisadi wote aliousimamia katika awamu yake, hasa katika kipindi chake cha pili.
 
Back
Top Bottom