Nyambala
JF-Expert Member
- Oct 10, 2007
- 4,465
- 1,170
- Thread starter
- #21
Nchi kama nchi inaweza kuzuia fedha yake isianguke thamani yake kwa njia kama hiyo ama kwa serikali kukataa kuishusha thamani kwa maelekezo ya WB au IMF.. Tanzania iliwahi kufanya hivyo katika utawala wa Nyerere. Na hata awamu ya Mwinyi kuingia madarakani alikubaliana na masharti yao na thamani ikashuka kadili vyombo hivyo vya fedha vilivyotaka.
Katika Nchi za Tiger miaka ya Mwishoni wa Tisini uchumi katika kanda hiyo ulishuka sana, baadhi ya nchi walikubali kushusha thamani ya pesa zao. Malaysia iligoma na kuifix fedha yao. Hali hii ilidumu kwa muda na hata baada ya uchumi wa nchi hizo kurudi kwenye hali yake, ringgit iliachiwa na ikashuka thamani.
Mkuu unachanganya mambo ile ya kina nyerere na mzee ruksa au hizo tigers na hata china sasa hivi inaitwa pegging. Kuna aina 2 za kuthamanisha hela yako kupeg au kuacha market iamue. Kupeg ndio kama vile unavyosema 1USD ni say sh10 regardless of market inasemaje. Hata huo mfano niliompa SteveD kuhusu Zimbabwe ni kwamba wao wamepegi 1USD kuwa Zim$30,000 lakini market haiko hivyo, market ndio iko kwenye masextrillioni au makwadrillioni.
Tukirudi bongo hela yetu sasa sisi inafloat tofauti na zamani ndio maana exchange rate inaweza kubadilika hata mara kumi kwa siku. Mkuu kibunango hili suala si zito kama unavyolifikiria it is just a language well unajua inafanyikaje, leo unaanzisha kitu say inaitwa tanzanian dollar TZD na unaitengenezea utaratibu kwamba 1TZD ni sawa na shilingi elfu moja, halafu unaondoa shillingi sokoni unabaki na TZD. Tht is how it is done Mozambique too did it, Zimbabwe , Uganda, Germany, Hungary, The old republics of Yugoslavia etc.
Tatizo tu hapa linakuwa kwenye inflation maana let's say sasa si 1USD ni shillingi 1250 baada ya miaka 2 labda itakuwa ini shillingi 2000 basi hata hiyo TZD inakuwa 2. Huoni kama inapendeza hiyo mkuu????