LNG Project: Njooni tujadili unadhani kwanini mradi wa gesi ya LNG unachelewa na nini chakufanya ili utekelezwe kwa wakati

Meneja Wa Makampuni

JF-Expert Member
Jul 7, 2020
6,329
8,247
MJADALA HURU WA KITAIFA KUHUSU MRADI WA GESI ASILIA MIMINIKA (LNG) MWAKA 2024

SEKTA NDOGO YA MAFUTA NA GESI

Mabibi na mabwana, wanasiasa, wafanya biashara, wajasiliamali, wanazuoni, wataalam wa fedha, wataalam wa uchumi, wahasibu, walimu, madaktari, wataalam wa mafuta na gesi, wataalam wengine wote na wananchi wote watanzania, habari za wakati huu wakuu wangu.

Wakuu wangu nipo chini ya miguu yenu. Nikiwaomba mje hapa tujadiliane kwa kina juu ya mradi wetu wa LNG.

AGENDA ZETU
AGENDA 1:
Kwanini mradi wa LNG unachelewa kuanza?

AGENDA 2: Tufanye nini ili utekelezaji wake uanze kwa wakati?

OMBI: Sisi kama watanzania wapenda maendeleo njooni tujadili badala ya kuweka akili zetu kwenye kujadili Simba na Yanga njooni hapa tujadili kwa kina.

ANGALIZO
ANGALIZO WACHANGIAJI MSIJE MKACHANGANYA LNG na LPG au CNG.

LNG = LIQUIFIED NATURAL GAS, gesi asilia miminika, hii haijawahi kuzalishwa Tanzania wala haijawahi kuletwa. Hii inahitaji fedha nyingi sana ili kuwekeza. Na hii ili upikie lazima uirudishe tena katika hali ya gesi na kuiingiza kwenye bomba hadi jikoni.

LPG = LIQUIFIED PETROLEUM GAS, gesi ya petroli miminika, hii ipo tunaipikia kila siku majumbani ikiwa kwenye mitungi. Hii uwekezaji wake hauhitaji fedha nyingi. Mtu yeyote anaweza kuwekeza tu. Kuna magari mengine yanatumia gesi hii pia.

CNG = COMPRESSED NATURAL GAS, ges asilia iliyo shindiliwa, hii wakuu wangu inatumika kwenye magari tu, huwezi pikia hii. Wale wote waliofunga mfumo wa gesi kwenye magari yao ndio wanatumia gesi hii.

Sisi tunacho zungumzia hapa ni LNG.

Wakuu mtanisamehe kwa kuwashitukiza katika kikao hichi cha dharura. Nimeleta mjadala huu baada ya kushituliwa na hii habari.

US cautions Tanzania on LNG project delays

The United States this week warned Tanzania of a likely exodus of investors in its long-anticipated, multimillion-dollar liquified natural gas project if it continues to be bogged down by delays over negotiation technicalities.

US Deputy Assistant Secretary of State Joy Basu told The EastAfrican in Dar es Salaam this week that companies such as Exxon Mobil that have been pushing the deal with Tanzanian authorities had reached a point where they were now “willing to walk away.”

“There is LNG in lots of places around the world now, and for Tanzania the window for this particular investment is closing fast. Such windows do not remain open forever,” said Ms Basu whose portfolio in the Joe Biden administration includes overseeing economic and regional affairs in Sub-Saharan Africa.

Kwa kifupi naomba nieleze LNG nini.

LNG (Gesi kimiminika)
Gesi miminika (kwa Kiingereza: liquefied natural gas; kifupi: LNG) ni gesi asilia katika hali ya kiowevu au miminika.
Ni dutu safi isiyo na rangi na isiyo na sumu, inayotengenezwa kwa kupoza gesi asilia hadi nyuzi joto -162ºC hadi kiwango ambacho inakuwa kimiminika.
Mchakato huo hurahisisha usafirishaji wenye ufanisi wa gesi asilia kwa kutumia barabara (malori) au bahari (meli). Sababu kuu ya kupoza gesi ni, gesi miminika ina ujazo mdogo mara 600 kuliko gesi asilia ikiwa katika hali ya kawaida.

600px-Methanier_aspher_LNGRIVERS.jpg

Meli za kubeba gesi miminika mara nyingi hutambuliwa kutokana na matanki ya mviringo

Asilimia kubwa ya gesi asilia hutoka kwenye chanzo na kusafirishwa kwa njia ya bomba baada ya kuisafisha hadi kufikia hali ya methani safi kiasi. Pasipo mabomba ni muhimu kupunguza ujazo wa gesi hii ili kuisafirisha ama kwa meli au kwa malori.
Ujengaji wa mitambo ya gesi miminika unahitaji mtaji mkubwa na yenye madeni makubwa. Lakini wakati gesi miminika ina gharama kiasi kuizalisha, maendeleo ya teknolojia yanapunguza gharama hizo zinazotokana na kuifanya kimiminika na kuirudisha tena katika hali yake ya gesi asilia.
Chapisho la BP World Energy Outlook lilitabiri mnamo mwaka 2012 kwamba biashara ya gesi miminika itakua kwa haraka maradufu kama ulivyokua haraka uzalishaji wa gesi asilia duniani, yaani kwa kiwango cha asilimia 4.4 kwa mwaka.

Mradi wa LNG Tanzania

Tanzania imegundua kiwango kikubwa cha gesi asilia katika ukanda wa pwani ya Lindi na Mtwara. Amana hii ya gesi inajulikana kama “gesi ya kina kirefu cha bahari” kwakua gesi hii inapatikana zaidi ya kilomita 100 kutoka pwani kwenye kina cha maji hadi kilomita 2.5.

Kutokana na kiasi hiki cha gesi kilichogunduliwa, Tanzania itaweza kuitumia gesi hii kwa miaka 500 kulingana na viwango vya sasa vya matumizi. Hii inamaanisha kuna gesi ya kutosha kwa nchi kuzalisha umeme sasa na ziada kwa siku za mbeleni, upanuzi wa matumizi ya gesi viwandani kwenye viwanda vya saruji, bia, plastiki, vigae, glasi, chuma na viwanda vingine vinavyotumia nishati ya juu pamoja na uwezekano wa kuuza gesi asilia katika nchi jirani utaifanya Tanzania kuwa kitivo cha nishati ya gesi katika ukanda huu wa nchi za Africa Mashariki.

Hivyo basi, kutokana na hichi kiasi kikubwa cha gesi, kuna fursa kubwa sana kwa Tanzania kuuza gesi yake kwenye masoko makubwa ulimwenguni na halikadhalika kujipatia kipato ambacho kitasaidia katika ukuaji wa kiuchumi na kufanikisha shughuli nyingine za kimaendeleo nchini. Nchi nyingine nyingi ulimwenguni zimetumia rasilimali zao kwa njia kama hizi katika kukuza ustawi na maendeleo ya watu wao kwa muda mrefu.

Screenshot_20240303_201448_Word.jpg

Kielelezo na 1: Muktasari wa mradi wa gesi na uchakataji wa gesi (LNG) Tanzania

Mpaka sasa,wawekezaji wa gesi ya kina kirefu baharini wamekua wakifanya kazi kushirikiana na Shirika la Maendeleo ya Petroli Tanzania (TPDC) kwa niaba ya serikali na takribani kiasi cha Trilioni 9 za kitanzania (sawa na dola za Kimarekani Billioni 4) zimekwisha wekezwa na wawekezaji wakuu katika sekta hii kwenye shughuli za utafiti na utathminishaji gesi. Lakini, ili Tanzania iweze kutumia vizuri fursa hii na kuiendeleza zaidi sekta ya gesi nchini, kuchuma mapato makubwa yatokanayo na usafirishaji na uuzaji wa gesi kwenye masoko ya kimataifa yenye kulipa zaidi, uwekezaji mkubwa zaidi unahitajika kujenga vituo katika maji ya kina kirefu baharini ambavyo vitawezesha kuleta gesi nchi kavu kwa ajili ya kusindika gesi tayari kwa matumizi ya ndani na nje ya nchi. Uwekezaji huu unahitaji kiasi kikubwa cha fedha utakaogharimu matrilioni ya fedha za Kitanzania (mabilioni ya dola za Kimarekani). Hivyo basi, kama ilivyo kwenye ujenzi wa makazi makubwa, inahitajika wapangaji wakuu na pia uhakika kwenye mapato ya msingi yatakayomthibitishia mwekezaji. Kwa mantinki hiyo soko la gesi la kimataifa litasimama kama “mteja mkuu” kwa kuendeleza na kukuza zaidi soko la gesi la ndani ya nchi wakati huohuo ikizalisha mapato mengi ya ushuru ambayo yanaweza kutumika katika kukuza uchumi wa Tanzania.

Ili kuweza kusafirisha na kuuza gesi kwenye soko la kimataifa na haswa masoko yaliyoko katika bara la Asia ambayo hutoa bei ya juu zaidi, gesi hupoozwa chini ya nyuzi joto -162C na kugeuka kuwa katika hali ya kimiminika (hivyo kuwa gesi iliochakatwa ijulikanayo kama LNG). Gesi inapobadilika na kuwa katika hali ya kimiminika inasinyaa takribani mara 600, sawa na kufanya mpira wa miguu upundue ukubwa kuwa sawa na golori. Kwa njia hii gesi inachukua nafasi ndogo zaidi na kuruhusu urahisi wa kusafirisha gesi hiyo kwa njia ya meli maalum kwenda masoko ya kimataifa katika nchi kama India, China, Japani na Korea.

Sifa za uendelezaji wa shughuli za utafutaji na uzalishaji wa gesi hii iliyoko katikati ya bahari hauna tofauti na miradi mingine mikubwa ikiwemo, uwekezaji mkubwa wa kifedha, ugumu wa kuizalisha kwa maana ya teknolojia husika, matokeo chanya na ya kudumu katika uchumi na upatinanaji wa ajira katika jamii.

Mradi huu utakua ndio mradi mkubwa kuliko yote iliyowahi kutokea nchini, ukilinganisha na miradi mingine mikubwa ambayo iko kwenye mchakato ama tayari imeshakamilika. Tanzania iko kwenye safari ya kufikia azma yake ya kuwa kitovu cha viwanda cha Africa Mashariki.

Hivyo basi, maendeleo haya yatatumika kama kichocheo muhimu katika kusaidia kufanikisha malengo na mikakati ya kuendeleza sekta ya viwanda nchini kwa kuchangia kiasi kikubwa cha mapato serikalini pamoja na kutoa faida nyingi za muda mrefu kwa Tanzania (angalia kielelezo na.2).

Baadhi ya mifano ya faida zitakazotokana na mradi ni:
• Upatikanaji wa ajira: Mradi huu utatengeneza na kutoa ajira za moja kwa moja kwa watanzania makumi kwa maelfu pamoja na kutoa fursa za kibiashara kwa makampuni ya wazawa yatakayotoa bidhaa na huduma mbalimbali kwenye mradi katika kipindi cha uendelezaji, ujenzi na hatua za utendaji wa mradi.
• Ukuaji wa viwanda: Uendelezaji wa shughuli za utafutaji na uzalishaji gesi ya kina kirefu baharini utazalisha gesi nyingi zaidi ambayo itaweza kutumika katika nchi hii kwa matumizi mbalimbali ikiwemo kufua umeme, kama njia mojawapo ya kuongeza upatikanaji wa umeme katika nchi nzima pamoja na kusambaza gesi katika viwanda mbalimbali ambavyo vinatumia gesi katika shughuli zake kwa mfano aluminiamu, viwanda vya nguo, viwanda vya karatasi, viwanda vya mafuta ya kula,vinywaji vya kaboni, viwanda vya unga na vingine vingi vinavyotegemea na kuhitaji umeme wa uhakika na salama.
• Ongezeko la mapato: Serikali itajizalishia mapato makubwa kila mwaka na hivyo kusaidia wananchi wa Tanzania katika shughuli za kimaendeleo nchini.

Screenshot_20240303_202000_Word.jpg

Kielelezo na 2. Manufaa ya gesi na Maendeleo ya LNG kwa Tanzania

2. Jinsi Tanzania inaweza kuhimili ushindani katika soko la kimataifa la LNG
Gesi ambayo haitauzwa kwenye soko la ndani, itasafirishwa kwenda kwenye soko la kimataifa la LNG. Kwa hivyo basi, mradi wa Tanzania LNG utakua unashindana na miradi mingine kama huu ulimwengu mzima na gesi ya Tanzania lazima iwe na bei shindanishi dhidi ya miradi mingine inayoshindana nayo katika soko la dunia. Huu mchoro hapa chini unaonyesha ushindani kwa Tanzania kwenye soko la LNG ulimwenguni na jinsi mataifa mengine yanayouza LNG katika soko la nje yanavyoshindana kwenye soko moja.

Screenshot_20240303_202211_Word.jpg

Kielelezo na 3: Soko la dunia la LNG – mchoro huu unaonyesha uhalisia wa ushindani katika soko la dunia la LNG

Licha ya mazingira ya sasa ya bei ya mafuta kuwa chini ambayo pia inatarajiwa kuendelea kuwa hivyo kwa mnamo kipindi kifupi kijacho, walakini kunaweza kuwa na soko lenye faida kubwa kwa Tanzania LNG ikiwapo tu mradi huu utaendelezwa kwa ushindani na kwa kuwa mahitaji ya LNG bado yanatarajiwa kukua katika miaka 20 ijayo. Kwa kipindi kirefu kijacho, ukuaji katika sekta hii unatazamiwa kukua kwa asilimia nne (4%) kila mwaka. Mahitaji yanatarajiwa kuzidi upatikanaji wa gesi ndani ya miaka kumi ijayo, ambayo itafungua upenyo kwa gesi ya Tanzania kuweza kuingia kwenye soko hili la LNG duniani.

Kwa kuongezea, sasa ni wakati wa Tanzania kuendeleza rasilimali hizi, kwani tunapotazama muda mrefu ujao masoko ya dunia yataweza kuhamia zaidi kwenye nishati mbadala hivyo kusababisa rasilimali ya hidrokaboni (mafuta & gesi) kupoteza thamani yake kwa kiasi fulani. Japokua hili linategemewa baada ya miongo mingi kutoka sasa, miradi ya LNG inachukua muda mrefu kuendelezwa na inazalisha kwa miongo mingi pia, hivyo basi hichi ndicho kipindi muafaka kwa mradi huu kuendelezwa ili iweze kukidhi mahitaji pamoja na kukamata fursa hii iliyoelezwa hapo juu.

Kichocheo cha mahitaji haya ni ongezeko la watu,mahitaji ya hewa safi kupitia kupunguza chembe chembe pamoja na hewa chafu ya dioksidi kaboni (CO2) na kushuka kwa uzalishaji wa ndani wa gesi kwenye nchi nyingi. Soko la Asia ambalo linatoa bei kubwa kuliko zote kwenye manunuzi ya gesi litachukua zaidi ya asilimia sabini (70%) ya mahitaji mapya ya gesi. Ukaribu wa Tanzania katika masoko haya unaiweka gesi ya Tanzania katika nafasi nzuri ya ushindani dhidi ya washindani wengine.

Gesi asilia ina sifa kuu ya kuwa na kiwango cha chini cha Kaboni na pia uchafuzi wa mazingira ni wa hali ya chini ukilinganisha na mafuta na makaa ya mawe na pia wepesi wa usafirishaji wa LNG katika masafa marefu unaifanya gesi hii kuwa chanzo bora zaidi cha nishati yenye kaboni ya kiwango cha chini kwa siku za mbeleni. Gesi asilia ya Tanzania ina maudhui ya chini kabisa ya CO2 ikilinganishwa na miradi mingine ambayo inashindana nayo.

Sifa hii itaipa gesi ya Tanzania nafasi ya juu kabisa ya ushindani ikishindanishwa kwa kipimo cha kiasi cha CO2. Mradi huu unauwezo wa kuwa na alama ya chini kabisa ya CO2 dhidi ya mradi wowote mpya wa LNG ambao unaendelea kwa sasa, haswa ikiwa vyanzo vya nishati mbadala kama jua na umeme wa maji vimejumuishwa kwenye muundo wa mradi huu.

Kwa kuzingatia yaliyoainishwa hapo juu, unaweza kuhitimisha kwa kusema Tanzania ina fursa nzuri ya kuhamasisha ukuaji wa uchumi na kupata faida kupitia kusafirisha LNG katika soko la ulimwengu. Ili kuwezesha fursa endelevu kuna mambo makuu mawili muhimu ambayo Tanzania inabidi itilie maanani:

Kuwezesha gesi ya Tanzania kuwa na bei shindani dhidi ya wazalishaji wengine kwenye soko la LNG duniani – serikali inapaswa kufanya kazi kwa karibu na TPDC na wawekezaji kuendeleza mradi wa LNG wenye ufanisi zaidi na wa gharama nafuu ambao utawezesha Tanzania LNG kuwa na bei shindani dhidi ya kile ambacho ushindani unaweza toa kama ilivyoainishwa kwenye kielelezo hapo chini. Bei ya LNG ya Tanzania kwenye soko la kimataifa inatokana na vitu viwili ambavyo ni gharama za uzalishaji na faida inayogawanywa kati ya serikali (kwa njia ya kodi na mgawanyo wa uzalishaji) na wawekezaji. Inapasa serikali na wawekezaji kufanya kazi bega kwa bega kufanikisha LNG yenye ushindani wa juu katika soko dhidi ya miradi kama ile itokayo Marekani,Qatar na Msumbiji ambazo zina gharama za chini sana za uzalishaji kutokana na uwingi wa gesi na mifumo bora ya mgawanyo wa mapato yenye ushindani mkubwa.

Screenshot_20240303_222458_Word.jpg

Kielelezo na 4: Njia za kuwezesha gesi ya Tanzania kuwa na bei shindani dhidi ya wazalishaji wengine duniani

• Kuanzisha na kuimarisha mfumo wa udhibiti na kuufanya uwe wa kudumu na wenye kutabirika – Miradi ya LNG ni ya uwekezaji wa muda mrefu ambayo inadumu kwa miongo kadhaa. Hivyo basi kuwahakikishia wawekezaji uhakika wa uwekezaji wao nchini ni jambo muhimu sana. Hii inahusisha kuwa na makubaliano ya kisheria ambayo yanaheshimiwa katika kipindi chote cha mkataba na njia stahiki za kusuluhisha mifarakano baina ya wadau ambayo inafata kanuni za kimataifa zilizowekwa katika usuluhishaji.
 
Wakuu wangu nipo chini ya miguu yenu.

Nikiwaomba mje hapa tujadiliane kwa kina juu ya mradi wetu wa LNG.

Kwanini mradi unachelewa?

Tufanye nini ili utekelezaji wake uanze kwa wakati?

Sisi kama watanzania njooni tujadili badala ya kuweka akili zetu kwenye Yanga na Simba njooni hapa.
Nani kakuambia kuwa mradi unachelewa?
 
Miradi ambayo wazungu hawapendi kuisikia kwenye nchi za Dunia ya tatu:
1. Energy and power
2. Agriculture
3. Space exploration
4. Practical education .
Watatumia mabilioni ya Dola kuhonga wanasiasa Ili tu mambo yasiende.
Africa tunahitaji mfumo mwingine wa kiutawala achana na huu wa wazungu. Zaidi ya miaka 70 sanduku la kupigia kura limeshindwa kubadiri Hali ya mambo zaidi ya kuzalisha wanasiasa matajiri huku wananchi wengi wakidondokea kwenye Lindi la umasikini wakutupwa.
 
Hili nalo lipo lakini wazungu hawahawa wameendelea kuendeleza miradi ya gesi na mafuta katika nchi za Afrika. Hapo Mozambique tayari kuna mradi wa LNG, miradi yetu ya gesi huko Mtwara, haya hapo Uganda.
 
Wakuu wangu nipo chini ya miguu yenu.

Nikiwaomba mje hapa tujadiliane kwa kina juu ya mradi wetu wa LNG.

Kwanini mradi unachelewa?

Tufanye nini ili utekelezaji wake uanze kwa wakati?

Sisi kama watanzania njooni tujadili badala ya kuweka akili zetu kwenye Yanga na Simba njooni hapa.
Mkuu Meneja Wa Makampuni , kwanza asante sana kwa
kwa mjadala huu wenye maslahi kwa taifa. Kabla sijachangia, naomba kwanza unitembelee hapa Gesi asili: Is it "day light robbery?" Watanzania tunaibiwa mchana kweupe! hivyo kinachochelewesha ni kuzuia tisiibiwe!.
P
 
Miradi ambayo wazungu hawapendi kuisikia kwenye nchi za Dunia ya tatu:
1. Energy and power
2. Agriculture
3. Space exploration
4. Practical education .
Watatumia mabilioni ya Dola kuhonga wanasiasa Ili tu mambo yasiende.
Africa tunahitaji mfumo mwingine wa kiutawala achana na huu wa wazungu. Zaidi ya miaka 70 sanduku la kupigia kura limeshindwa kubadiri Hali ya mambo zaidi ya kuzalisha wanasiasa matajiri huku wananchi wengi wakidondokea kwenye Lindi la umasikini wakutupwa.
Na bado
Sasa wazee wanaokufa wameandaa watoto wao ambao ndio mawaziri sasa
Na wao hawafichi wanaonyesha mpaka watoto wao wanasoma chekechea kwa malipo kiasi gani
Na pia tumaambiwa ni Chipukizi wa CCM ingali bado wadogo sana
Nchi hii kuna koo zimefanya mali yao binafsi
Gas wala nini wao ndio wanaamua
 
Haya sio kweli tujikite kwenye mambo ya msingi sio kuwasema viongozi. Tujadili mkataba unasemaje, na terms zikoje, stake ilikua ngapi? na Nk.
 
Hili nalo lipo lakini wazungu hawahawa wameendelea kuendeleza miradi ya gesi na mafuta katika nchi za Afrika. Hapo Mozambique tayari kuna mradi wa LNG, miradi yetu ya gesi huko Mtwara, haya hapo Uganda.
Jaribu kufanya survey maeneo ambayo hao wazungu uone kama wanachokifanya kinalingana na hari ya maisha ya wananchi wa eneo husika.
 
Hili nalo lipo lakini wazungu hawahawa wameendelea kuendeleza miradi ya gesi na mafuta katika nchi za Afrika. Hapo Mozambique tayari kuna mradi wa LNG, miradi yetu ya gesi huko Mtwara, haya hapo Uganda.
Embu tafuta mikataba iliyoingiwa na hao wazungu hapa Africa, utagundua ni ya hovyo sana na ni vile tu haiwekwi wazi wananchi wakaona..
 
Mining, Oil and gas ili iweze kukunufaisha ni either utafute technolojia uchimbe mwenyewe au uweke mzigo mezani mgawane shares.

Kama Oil and gas investment yake ni gharama basi tungeanza wenyewe kuchimba hata madini kama dhahabu nk na hii gas tuwe part ya exploration kwa kuweka budget na kuattach TPDC chini ya wazawa ili wajenge uzoefu.
 
Liwe somo kuwapa vilaza kama hakina Makamba sensitive sectors. Yeye na kampuni yake hakina Zitto wanachukulia $42 billion ni hela ya mzaha kuirudisha.

Wakitoka hapo wanaongea ujinga wa local contents sijui tutakuwa tunauza kuku mia ngapi kwa siku etc with nonsense.

Muulize sasa hiyo $42 billion ina justy specification za plant au akupe breakdown cost, hawana hayo majibu; ukiwaona sasa wanavyokaa na wawekezaji hayo mapozi yao utadhani watu wa maana wakati atawajui hela yenyewe inarudi vipi.

My guess Tanzania itakuwa imestuka $42 billion ni inflated costs ya mradi. Sehemu kubwa ya hiyo hela itaenda kwa ‘Subsea 7’ kampuni ambayo ni joint venture ya marekani na Norway ni specialised engineering firm ya offshore construction na kutandaza pipes, nyingine inaenda kutoa biashara ya steel kwa makampuni ya Norway ambayo yapo mengi huko kwao na mfaidika mwingine ni LNG construction firm ambayo itakuwa ya kimarekani tu na yenyewe.

Hapo ukidadavua utakuta 90% ya hizo $42 billion zinafaida kwenye uchumi wao wana kila sababu ya ku inflate hizo costs.

Bado sasa hesabu za kurudisha hizo hela ni pasua kichwa na kama sehemu kubwa ya investment ni mkopo with interest ya 6% tu ni shida. Mradi ukianza hela ya investment inatoka kwanza kwenye faida regardless ya hali ya soko (sometimes production is high, sometimes is low). Kuna kanuni zake hapo, if global demand is low kurudisha deni unaweza kujikuta unazalisha na upati chochote zaidi ya kulipa deni tu.

Haya sio mambo ya kukurupuka ni very technical inataka uelewa mpana wa maswala ya finance, oil and gas industry, global politics, etc. Sio mambo ya kukurupuka na kusikiliza ropo ropo za mtu kama Zitto au January ambao uelewa wao wa hayo mambo ni mdogo mno kwa kuwasikiliza.
 
Na bado
Sasa wazee wanaokufa wameandaa watoto wao ambao ndio mawaziri sasa
Na wao hawafichi wanaonyesha mpaka watoto wao wanasoma chekechea kwa malipo kiasi gani
Na pia tumaambiwa ni Chipukizi wa CCM ingali bado wadogo sana
Nchi hii kuna koo zimefanya mali yao binafsi
Gas wala nini wao ndio wanaamua
Peleka na wewe wanao wakawe chipukizi,acha kulia kijinga,huko shuleni CCM hawakuja kutaka mjiunge nao!?..mlijiunga au ndiyo mliona upuuzi kuvaa sare za njano na kijani!?
 
Liwe somo kuwapa vilaza kama hakina Makamba sensitive sectors. Yeye na kampuni yake hakina Zitto wanachukulia $42 billion ni hela ya mzaha kuirudisha.

Wakitoka hapo wanaongea ujinga wa local contents sijui tutakuwa tunauza kuku mia ngapi kwa siku etc with nonsense.

Muulize sasa hiyo $42 billion ina justy specification za plant au akupe breakdown cost, hawana hayo majibu; ukiwaona sasa wanavyokaa na wawekezaji hayo mapozi yao utadhani watu wa maana wakati atawajui hela yenyewe inarudi vipi.

My guess Tanzania itakuwa imestuka $42 billion ni inflated price ya mradi na faida kubwa ya hiyo hela itaenda kwa ‘Subsea 7’ kampuni ambayo ni joint venture ya marekani na Norway ni specialised engineering firm ya onshore construction na kutandaza pipes, hela inaenda kutoa biashara ya steel kwa makampuni ya Norway na LNG construction firm ambayo itakuwa ya kimarekani tu.

Hapo ukidadavua utakuta 90% ya hizo $42 billion zinafaida kwenye uchumi wao.

Bado sasa hesabu za kurudisha hizo hela ni pasua kichwa na kama sehemu kubwa ya hizo ni mkopo with interest ya 6% tu ni shida, mradi ukianza hela ya investment inatoka kwanza kwenye faida regardless ya hali ya soko (sometimes production is high, sometimes is low). Kuna kanuni zake hapo, if global demand is low kurudisha deni unaweza kujikuta unazalisha na upati chochote zaidi ya kulipa deni.

Haya sio mambo ya kukurupuka ni very technical inataka uelewa mpana wa maswala ya finance, oil and gas industry, global politics na sio kusikiliza ropo ropo za mtu kama Zitto au January ambao uelewa wao hayo mambo ni mdogo mno kwa kuwasikiliza.
Asante sanaa mkuu ,hakuna cha kuongeza hapa ,message sent loud and clear🙏🙏🙏
 
Liwe somo kuwapa vilaza kama hakina Makamba sensitive sectors. Yeye na kampuni yake hakina Zitto wanachukulia $42 billion ni hela ya mzaha kuirudisha.

Wakitoka hapo wanaongea ujinga wa local contents sijui tutakuwa tunauza kuku mia ngapi kwa siku etc with nonsense.

Muulize sasa hiyo $42 billion ina justy specification za plant au akupe breakdown cost, hawana hayo majibu; ukiwaona sasa wanavyokaa na wawekezaji hayo mapozi yao utadhani watu wa maana wakati atawajui hela yenyewe inarudi vipi.

My guess Tanzania itakuwa imestuka $42 billion ni inflated costs ya mradi. Sehemu kubwa ya hiyo hela itaenda kwa ‘Subsea 7’ kampuni ambayo ni joint venture ya marekani na Norway ni specialised engineering firm ya onshore construction na kutandaza pipes, nyingine inaenda kutoa biashara ya steel kwa makampuni ya Norway ambayo yapo mengi huko kwa kwao na mfaidika mwingine ni LNG construction firm ambayo itakuwa ya kimarekani tu na yenyewe.

Hapo ukidadavua utakuta 90% ya hizo $42 billion zinafaida kwenye uchumi wao wana kila sababu ya ku inflate hizo costs.

Bado sasa hesabu za kurudisha hizo hela ni pasua kichwa na kama sehemu kubwa ya investment ni mkopo with interest ya 6% tu ni shida. Mradi ukianza hela ya investment inatoka kwanza kwenye faida regardless ya hali ya soko (sometimes production is high, sometimes is low). Kuna kanuni zake hapo, if global demand is low kurudisha deni unaweza kujikuta unazalisha na upati chochote zaidi ya kulipa deni tu.

Haya sio mambo ya kukurupuka ni very technical inataka uelewa mpana wa maswala ya finance, oil and gas industry, global politics, etc. Sio mambo ya kukurupuka na kusikiliza ropo ropo za mtu kama Zitto au January ambao uelewa wao wa hayo mambo ni mdogo mno kwa kuwasikiliza.
Wewe kuandika tu kiswahili huwezi,halafu unawadhihaki akina zitto...plus una poor knowledge ya mega projects investments
 
Wewe kuandika tu kiswahili huwezi,halafu unawadhihaki akina zitto...plus una poor knowledge ya mega projects investments
Mimi nimeeleza kwanini uelewa wao ni mdogo, sasa ili kuonyesha mimi ndio zwazwa ungetuambia ni kiasi gani cha hizo $42 billion dollar zinaingia kwenye mzunguko wa Tanzania.

Au tupe break down cost ya mradi ku justify $42 billion ambayo inakwenda kuwa kwenye top 3 ya LNG plants (bado hapo miradi kama hii ina desturi ya kuongezeka kwa gharama mbeleni).

We unadhani $42 billion unapewa tu, halafu hujui hata kiasi gani hapo ni mkopo wala interst za mkopo na madhara yake kwenye kurudisha.

Unachofukiria wewe local content ohoo tutajenga wazungu watapanga, sijui Mtwara kutachangamka etc with petty issues za mradi.
 
Back
Top Bottom