JohnShaaban
JF-Expert Member
- Aug 23, 2007
- 464
- 114
Waendeshaji wa Clouds ni opportunists:Jile79 said:Acha bwana vijana walisha nunuliwa kwa pesa za kutosha na ccm na mafisadi kwa hiyo wanatekeleza agizo la mkuu wao kusaga kwani ndiye aliyepewa mgawo ili vijana wafanye kazi za siasa kwenye clouds......nasikia kati ya wote kibonde ndiye alipewa mgawo mkubwa...............
1. sio watu wa kupigana pale haki yao inapopindishwa na watawala. Serikali ya CCM ilijua kuwa vijana wengi wanawasikiliza wakahakikisha leseni ya TV inawarudisha kwa mafisadi.
2. ni watu wa kuchumia tumbo, wenye tamaa ya vitu vya kupita; kumbuka issue dhidi ya Sugu.
3. wanapenda kuonekana wako juu sana mbele ya jamii, hivyo wako tayari kufanya lolote kwa kutegemea fadhila ya mtawala itayowakuza.
Binafsi nilipenda sana kusikiliza power-breaskfast na jahazi lakini tangu wameanza intentional biasness nimehachana nao ili nisighafilike. Kumbuka kabla hawajapa TV kila mtu alitamani wawe na TV-station tukijua wangekwenda sambamba na vyombo vya "National Media Group" uko Kenya, lakini laana inayowasumbua Watanzania wengi imeshawafika, a curse towards cheap means of earning (not making) money and hence superiority.
Tazama wasanii walivyohangaika kumnadi Kikwete hata nje ya kampeni as if wamepata mwokozi. Ni wachache sana waliotafakari kugundua jamaa anawatumia baada ya row na wafanyakazi. Sasa watulie watafakari nini walichopata maana mtu waliyemkampenia amesababisha/atasababisha hali ngumu kwa watu wa soko la bidhaa zao. Mwisho wa siku bidhaa zao zitachakachuliwa na hawataweza kuzuia hilo maana hakuna mwananchi atayeweza kukidhi gharama za bidhaa halisi.
Kalaghabao!