Bams
JF-Expert Member
- Oct 19, 2010
- 16,547
- 41,059
Kuna njia za msingi za kidemokrasia za kufikisha ujumbe ama kudai haki iliyokanywagwa. Na njia hizo ziluzodhahiri ni pamoja na:
1) Njia ya kwanza ni ya uwakilishi. Ndiyo maana tunachagua wawakilishi.
2) Njia ya pili ni ya wananchi wenyewe kufikisha ujumbe au kudai haki, pale inapoonekana uwakilishi umeshindwa, haufanyi kazi, umewasaliti unaowawakilisha, umepuuzwa au uwakilishi haupo.
Kwa yaliyotokea Tanzania mwaka 2020 ambapo uchaguzi ulivurugwa, Watanzania wamekosa wawakilishi halali:
1) Wagombea 75% kupitia CCM waliopendekezwa na wajumbe, majina yao yalikatwa na kupachikwa ya watu ambao hawakuchaguliwa na yeyote.
2) Zaidi ya 90% ya majina ya wagombea kutoka vyama vya upinzani, yalikatwa na Tume haramu ya Mahela, na wachache ambao majina yao yaliachwa, kura zao ziliporwa kwa kutumia ofisi haramu za wakurugenzi.
3) Wagombea haramu kupitia CCM ambao majina yao yalipachikwa na kikundi cha watu, wengi wao hawakupigiwa hata kura, bali wale wakurugenzi haramu waliwatangaza kuwa wamepita bila kupingwa.
4) Mahakama kuu ilitoa hukumu kuwa kuanzia Waziri Mkuu mpaka na wabunge wengine wote waliotangazwa kuwa wamepita bila kupingwa siyo wabunge halali.
Kutokana na ukweli huo, Watanzania kwa sasa hawana chombo chochote cha uwakilishi. Hivyo yale yote yanayowaumiza sana ni lazima wapaze sauti zao wenyewe kwa nguvu kwa sababu hawana mwakilishi. Na njia mojawapo halali kabisa ya kisheria, ya kupaza sauti ni WANANCHI WENYEWE KUJITOKEZA KUFIKISHA UJUMBE KWA WATAWALA.
Hivyo nawashauri wananchi wote siku ya tarehe 24, pamoja na hayo yaliyotajwa na CHADEMA, wananchi tubebe mabango yanayotaja madhira yote ambayo wananchi wanapitia.
HATUNA UWAKILISHI POPOTE, HIMA TUJIWAKILISHE WENYEWE KWA NJIA YA MAANDAMANO.
Lakini tutambue kuwa wale wanaokanyaga haki za wananchi wana vibaraka wao wanaotupiwa makombo. Hao watajaribu kutukatisha tamaa kwa sababu wao kazi yao usiku na mchana ni kuwapumbaza watu kwa kuwahadaa watawala kwa sifa kuwa mambo yote ni safi kabisa kwa wananchi kwa sababu sasa wanaishi kama malaika.
Taarifa za ndani, watawala wameamua kutowagusa waandamanaji alimradi yawe maandamano ya amani ili kupata credit kwenye jumuia ya kimataifa na kuonesha kuwa wamekuwa wakiwasikiliza wananchi bali CHADEMA ni wakorofi. Na mapendekezo mengi ya mswada yatafanyiwa kazi kudhihirisha hoja yao dhidi ya CHADEMA.