Nimekuwa msomaji wa magazeti mbalimbali nhini hasa yale yanayoandika habari za makala. nilichokuja kubaini ni kwamba baadhi ya magazeti hayo yaliibuka mwaka jana na yamekuwa yakipambwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa vikiwashambulia wabunge flani wa CCM walioluwa wakipiga kelele bungeni kukemea ufisadi. magazeti hayo yalianza kampeni za kuwachafua wabunge hao tokea mwaka jana na kuonesha kwamba wabunge hao kamwe hawatarudi bungeni eti wananchi majimboni mwao wamewachoka. magazeti hayo yalikwenda mbali zaidi kwa kuwataja wapinzani wa wabunge hao ndani ya CCM na ambao eti wangewaangusha wabunge hao kwenye kura za maoni ndani ya CCM kuanzi kule Kyela kwa Mwkyembe, Simanjiro kwa Sendeka Same Mashariki kwa Kilango, Kahama kwa Lembeli hadi kwa akina Mpendazoe, Kimaro, Selelii na hata Spika Sitta.
Cha kushangaza wabunge hao wengi wao wamepeta tena wengine hawana wapinzani. Swali ni hili; 'hivi magazeti haya yanafanya kazi kwa maslahi ya nani? waandishi na wahariri wa magazeti haya hawaoni madhara ya ufisadi wa mikataba mikubwa mikubwa inavyo ligahrimu taifa? hatima ya upotoshaji huo ni nini? jamani changieni. moja ya magazeti hayo ni "tazama tanzania na ndg yake mkakati" je wanataka kutuambia kwamba mkakati wao ni kuiangusha tanzania kwa kuwashambulia makamanda wa vita dhidi ya ufisadi na kuwainua wafanyabiashara ambao lengo la kwenda bungeni ni kulinda maslahi yao ya kibiashara?
Je tuamini kwamba magazeti haya yanafadhiliwa na wale walioguswa na tuuma hizo ili kuwasafisha?
WADAU TOENI MAONI YENU.