Andrew Kisaka, amesema Mamlaka hiyo itawachukulia hatua baadhi ya Watangazaji wanaosoma magazeti kwa mbwembwe

GENTAMYCINE

JF-Expert Member
Jul 13, 2013
56,646
109,034
Meneja wa Huduma za Utangazaji wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Andrew Kisaka, amesema Mamlaka hiyo itawachukulia hatua baadhi ya Watangazaji wanaosoma magazeti kwa mbwembwe huku wakiongezea baadhi ya vitu visivyotakiwa wakati wa usomaji.

Chanzo: millardayo

GENTAMYCINE nawapongeza sana kwa hatua hii japo pia mmechelewa sana kuitoa kutokana na Upuuzi huu mkubwa uliokuwepo.

Hata hivyo kuonyesha kuwa TCRA hamheshimiki na Mliowaonya ( yaani ni Nyoka wa Kibisa ) ni kwamba Asubuhi hii hii katika Kipindi cha Joto la Asubuhi cha EFM Radio Mtangazaji mwenye Upuuzi huu mlioukataza Masanja Mkandamizaji ( Emanuel Mgaya ) kaendelea na Utaratibu huu japo Kiuwoga Uwoga.
 
vichwa vya habari vina fasihi ndani yako utakvyosoma na kuelewa wewe tofauti na mimi

ok watachukuliwa hatua kwa sheria ipi? unakuta kichwa cha habari kimeandikwa 'TAFITI, kucheka kunatibu ugonjwa wa moyo' wanasoma wanaanza kucheka hapo tatizo liko wapi??
We unaona baba levo anajua maana ya fasihi,mtu serious na anayejua kazi yake hawezi kuleta mzaa kwenye serious news,pumbavu zao
 
huyo afisa wa tcra kasoma wapi masuala ya habari? Hebu asikwamishe ladha ya usikilizaji wa kusoma magazeti. Mambo ya habari zaidi hutawaliwa na ubunifu na utashi wa mtu katika kufanya presentation ya taarifa. Huyo afisa anakurupuka tu
 
kwani wapo chama gani na wanasifia chama gani?.wangekuwa sio ccm hapo leo ilishakwisha ila n i ccm na kila jambo ni mama ilo limekwisha
 
Kusoma kwa mbwembe tumeanza kusoma tangu tukiwa shule za msingi, kule sekondari tulikuwa tunawasoma akina okonkwo na ikemefuna kwa mbwembwe mbele ya mwalimu wa english literature, tena tulikuwa tunasoma kwa mbwembwe kwa lafudhi ya american englishi, slang
 
Siasa tu. Kwa sheria ipi . Kila mtu anataka tu publicity
Mfano.
"Auawa na kukatwa sehwmu za siri"
Hapa inaweza kusomwa kwa sauti mbili au zaidi tofauti
1. Sauti ya mshangao . Iweje sehemu za siri zikatwe!
2. Sauti ya masikitiko
Wasomaji hawa utawashitaki kwa kosa lipi? Kushangaa au kusikitika?
 
Mahubiri yenyewe tu ukileta u serious waumini wanasinzia na kulala usingizi hutasikilizwa lazima ulete mbwembwe waumini wawe active kukusikiliza. Ukiwa mwalimu kama huna mbwembwe somo halitaeleweka utaishia kunong'ona na ubao na kuacha wanafunzi hoi hawaelewi ulichofundisha. Hotuba zenye mbwmbwe ndizo husikilizwa zaidi, wajumbe hawasinzii.
 
Mahubiri yenyewe tu ukileta u serious waumini wanasinzia na kulala usingizi hutasikilizwa lazima ulete mbwembwe waumini wawe active kukusikiliza. Ukiwa mwalimu kama huna mbwembwe somo halitaeleweka utaishia kunong'ona na ubao na kuacha wanafunzi hoi hawaelewi ulichofundisha. Hotuba zenye mbwmbwe ndizo husikilizwa zaidi, wajumbe hawasinzii.
Mahubiri hayahitaji mbwembwe. Shindana na nguvu za shibe zinazoleta usingizi. Kisha kazia mahubiri

Halafu waliointroduce kuweka viti makanisani hawaendi mbinguni
 
Back
Top Bottom