Kwa nini baadhi ya magazeti yanatumika kupotosha wananchi????????????

VEDASTUS

Member
Aug 25, 2010
7
0
Nimekuwa msomaji wa magazeti mbalimbali nhini hasa yale yanayoandika habari za makala. nilichokuja kubaini ni kwamba baadhi ya magazeti hayo yaliibuka mwaka jana na yamekuwa yakipambwa na vichwa vya habari ambavyo vimekuwa vikiwashambulia wabunge flani wa CCM walioluwa wakipiga kelele bungeni kukemea ufisadi. magazeti hayo yalianza kampeni za kuwachafua wabunge hao tokea mwaka jana na kuonesha kwamba wabunge hao kamwe hawatarudi bungeni eti wananchi majimboni mwao wamewachoka. magazeti hayo yalikwenda mbali zaidi kwa kuwataja wapinzani wa wabunge hao ndani ya CCM na ambao eti wangewaangusha wabunge hao kwenye kura za maoni ndani ya CCM kuanzi kule Kyela kwa Mwkyembe, Simanjiro kwa Sendeka Same Mashariki kwa Kilango, Kahama kwa Lembeli hadi kwa akina Mpendazoe, Kimaro, Selelii na hata Spika Sitta.
Cha kushangaza wabunge hao wengi wao wamepeta tena wengine hawana wapinzani. Swali ni hili; 'hivi magazeti haya yanafanya kazi kwa maslahi ya nani? waandishi na wahariri wa magazeti haya hawaoni madhara ya ufisadi wa mikataba mikubwa mikubwa inavyo ligahrimu taifa? hatima ya upotoshaji huo ni nini? jamani changieni. moja ya magazeti hayo ni "tazama tanzania na ndg yake mkakati" je wanataka kutuambia kwamba mkakati wao ni kuiangusha tanzania kwa kuwashambulia makamanda wa vita dhidi ya ufisadi na kuwainua wafanyabiashara ambao lengo la kwenda bungeni ni kulinda maslahi yao ya kibiashara?
Je tuamini kwamba magazeti haya yanafadhiliwa na wale walioguswa na tuuma hizo ili kuwasafisha?

WADAU TOENI MAONI YENU.
 
Hahaha Veda kwani we mgeni hapa Tanzania, ina maana kweli kweli kabisa hujui wamiliki wa haya magazeti, kaka kuna msemo unasema " hata kama hujui kusoma , basi tazama picha tu unaweza elewa nini kinaendelea". Magazeti uyasemayo yalianzishwa kwa maslahi ya Ole EL, RZ, AC, NK na their allies!
 
Kinachoniuma ni kwamba watanzania walio wengi hawawezi kuchambua pumba na mchele! yaani ni wahcache wanaoelewa kuwa kuna magazeti yanatumiwa na watu kisiasa zaidi
 
Kinachoniuma ni kwamba watanzania walio wengi hawawezi kuchambua pumba na mchele! yaani ni wahcache wanaoelewa kuwa kuna magazeti yanatumiwa na watu kisiasa zaidi

Maybe you are wrong on this one, fanya research japo is not scientific kila ukiona kijana muuza magazeti muulize madazeti gani yana soko na yapi ni ya kudoda, you will get the answer!
 
Kinachoniuma ni kwamba watanzania walio wengi hawawezi kuchambua pumba na mchele! yaani ni wahcache wanaoelewa kuwa kuna magazeti yanatumiwa na watu kisiasa zaidi

si kweli Mkuu, kuna magazeti hayakai kabisa sokoni, ni kitu adimu mno (Tdaima, Mwanahalis, RaiaMwema na hata Mwananchi), Ipp walikuwa nao wako juu lakini kadri muda unavyoenda anafanana na Rai tu

Mkuu Watanzania sio Mabwege tena
 
mungu nisamehe kwa hilo,ila namchukia mengi na kila kitu chake kwa kushindwa kutumia vyombo vyake kulikomboa taifa zaidi ya kujikomba kwa ccm
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom