Kwa NEC hii mpya, CCM inakwenda kufa - Dr. Slaa

Anachofanya Dr Slaa ni kuziba shimo la panya kwa mkate wa nyama.
Mkuu Ritz
Dr. Slaa amekuwa msemaji wa CCM? Mwambieni amalize ngoma yake hii yetu haiwezi!
Chama
Gongo la mboto DSM
 
Ukimpiga swala mshale mkimbilie.....usianze kupiga vigelegele...

Ni kweli Mzee, lakini Slaa alipaswa kulijua hilo. Hawa wanasiasa waliotoka CCM wakati mwingine hawana dhamira ya kweli na wako tayari kuiamusha CCM wakati ikita roho. wengine waweza kuwa ni double agent. Time will tell
 
slaa1.jpg

Dr Slaa

Adai ni kwa kuwapitisha watuhumiwa wa ufisadi kugombea

na Sitta Tumma, Mwanza


KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibroad Slaa, amemvaa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Jakaya Kikwete, akisema amekitengenezea kaburi la kukizika rasmi chama chake kwa kuruhusu watuhumiwa wakubwa wa ufisadi kugombea nyadhifa mablimbali.
Dk. Slaa alisema uteuzi wa wagombea ndani ya CCM uliomalizika juzi umeonyesha wazi kwamba sasa chama hicho kinatumbukia kwenye dimbwi kubwa na pana lisiloweza kukitoa tena.
Akizungumza na Tanzania Daima jijini Mwanza, alikojichimbia kuhakikisha mchakato wa uchaguzi wa mameya wa jiji hilo unakwenda vizuri leo, Dk. Slaa alisema dhamira ya kweli dhidi ya CCM katika kuwaweka vijana kwenye uongozi ili kukinusuru chama hicho imezimika baada ya Kikwete kuruhusu watuhumiwa wa ufisadi na wakongwe kugombea uongozi.
“Katika hili la uteuzi wa CCM, nangojea taratibu zao zikamilike. Tulitegemea CCM muda huu ni wa kujisafisha, lakini imeshindwa kufanya hivyo. Mimi simung’unyi maneno kuhusu watuhumiwa wa ufisadi.
Mfano (anataja) ni fisadi wa fedha za rada. Mimi hapa nilishapeleka ushahidi hadi wa akaunti namba ya benki yake kwa DPP (Mkurugenzi wa Mashtaka Nchini), alisema.
Alisema inashangaza kuona katika utetezi wa CCM, mtuhumiwa huyo amepatiwa nafasi licha ya kushindwa kueleza wazi fedha nyingi kwenye akaunti hiyo ya Uswisi alizipataje.
“Mtuhumiwa mkubwa kama huyu wa ufisadi eti leo CCM inampitisha awe mgombea. Kweli? Sioni dhamira ya CCM kupambana na vitendo vya kifisadi. Na hata dhamira ya vijana haipo bali imejitumbukiza kwenye dimbwi ambalo kamwe hakitatoka humo,” alisisitiza.
Kuhusu Lowassa na tuhuma zake za ufisadi wa kampuni ya kufua umeme wa dharura wa Richmond zilizosababisha kujiuzulu uwaziri mkuu mwaka 2008, Dk. Slaa alisema kiongozi huyo alilazimika kujiuzulu kama sehemu ya kuwajibika, lakini ameshindwa hadi leo kumtaja mhusika hasa wa kampuni hiyo.
Alisema kama kweli Lowassa alisingiziwa katika tuhuma hizo, alipaswa kuwaeleza Watanzania nani anayehusika na ufisadi huo wa Richmond ambayo ilishindwa kuzalisha umeme licha ya kutumia mamilioni ya fedha za umma.
Kuhusu wanachama wa CCM ambao majina yao yamekatwa na NEC, Dk. Slaa alisema milango iko wazi CHADEMA kwa wale wasio mafisadi kujiunga ili kukielekeza chama hicho kushika dola mwaka 2015.
Alisema CHADEMA ni chama makini huenda kuliko vyama vingine, hivyo hakiwezi kupokea wanachama kutoka CCM wanaotuhumiwa kwa ufisadi, vinginevyo kitafunga milango na mapazia yake.
“Unajua, kuna watu wanaojulikana kwa ufisadi. Pia wapo wasafi wanaoomba kujiunga na CHADEMA, hivyo watu safi hawana tatizo kujiunga na CHADEMA kwa ajili ya kuunganisha nguvu kwenda kuongoza dola mwaka 2015,” alisema Dk. Slaa.
Mnyukano wa umeya
uchaguzi wa mameya wa wilaya mbili za Nyamagana na Ilemela jijini Mwanza, unatarajiwa kufanyika leo huku mnyukano mkali ukiwa katika halmashauri ya Nyamagana kutokana na CCM na CHADEMA kuwa na idadi sawa ya viti vya madiwani na hivyo kutegemea kura za CUF ziamue mshindi.
Katika Halmashauri ya Ilemela, CHADEMA ina uhakika wa asilimia mia moja kutokana na kuwa na madiwani wengi kuzidi wenzao wa CCM huku mikakati yao ikilenga kuwashirikisha CUF ili waitwae pia Nyamagana.
Uchaguzi huo unafanyika baada ya Halmashauri ya Jiji la Mwanza kugawanywa na hivyo kuzaa halmashauri hizo mbili. Lakini pia Halmashauri ya Jiji la Mwanza kwa sasa muda kadhaa haikuwa na Meya baada ya Baraza la Madiwani kumvua wadhifa huo, Jackson Manyerere (CHADEMA).
Baada ya meya kuenguliwa, kulizuka mtafaruku ndani ya CHADEMA jijini hapa ambao ulisababisha madiwani wawili kutimuliwa uanachama kwa kile kilichodaiwa ni usaliti wa kuanzisha hoja ya kumtosa kiongozi huyo.
Hivyo kutokana na CHADEMA kutokuwa na madiwani hao, inaingia kwenye uchaguzi wa leo ikiwa na madiwani sita na mbunge Ezekiel Wenje katika wilaya ya Nyamagana wakati wenzao CCM wana madiwani saba na CUF wawili.
Kwa mnyukano huo ni dhahiri kuwa CHADEMA na CCM watakuwa wamefungana kwa kura na hivyo kuhitaji huruma ya madiwani wa CUF ili upande mmoja uibuke kidedea.
Taarifa za uhakika kutoka jijini hapa ni kwamba CHADEMA wamefanya mazungumzo ya kushirikiana na CUF kwa kuwaachia nafasi ya Naibu Meya ambayo itagombewa na diwani wao wa kata ya Mirongo, Daud Mukama.
Kwa halmashauri ya Ilemela CHADEMA wana uhakika wa kuibuka kidedea kutokana na kuwa na madiwani wanane na mbunge Highness Kiwia huku wenzao wa CCM wakiwa na madiwani sita na CUF ina mbunge wa Viti Maalum, Mkiwa Kimwanga.
Kamati za utendaji za CHADEMA katika wilaya hizo zimefanya vikao tofauti kwa kushirikiana na kamati za madiwani na kukamilisha mchakato wa kupata wagombea wao.
Kwa mujibu wa ofisa habari wa CHADEMA, Tumaini Makene, kamati ya utendaji ya wilaya pamoja na madiwani wa Nyamagana walimteua aliyekuwa Naibu Meya kabla, Diwani wa Kata ya Maina, Charles Chibara, kuwa mgombea wa umeya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza.
Kwa upande wa Ilemela, kikao cha kamati ya utendaji pamoja na madiwani walimteua Diwani wa Kata ya Nyamanoro, Abubakar Kapera, kuwa mgombea wa umeya Halmashauri ya Manispaa ya Ilemela.
Kikao hicho cha Ilemela, pia kilimteua Diwani wa Kirumba, Danny Kahungu, kuwa mgombea wa nafasi ya Naibu Meya halmashauri hiyo wakati kamati ya utendaji ya Nyamagana imekubali kumwachia kugombea nafasi ya Naibu Meya wa Halmashauri ya Jiji la Mwanza, Diwani wa Mirongo, Daudi Mkama (CUF).
Wao CCM wamemteua Diwani ya Kata ya Mkolani, Stanslaus Mabula, kugombea nafasi ya umeya katika halmashauri ya jiji la Mwanza huku diwani wa kata ya Igogo, John Minja, akigombea unaibu meya na Ilemela wagombea ni Renatus Kalunga na naibu wake Sarah Ng’hwanu.


 
Tanzanians, listen up. The only way to fet rid of these crooks is to assassinate them. Mnajua wanaishi wapi, wanakula wapi nk. Msisubiri chama, mahakama nk.
 
siyo huyo mzee tu ata mimi nauchukia ufisadi kuliko kitu chochote dunia. kwahiyo anachofanya huyo mzee hakosei, ni watanzania wengi sana tunalia kila siku kuhusu ufisadi na hicho ndiyo pekee kitakacho iuwa CCM. wakiiba kura kama kawaida yao tuna wapiga mawe kama vibaka. tumeisha wachoka sana

Hahaha mkuu umenifanya nicheke sana. Mi nilikua najiuliza mbona hatukuanza tangia 2010 maana nilishaanda viroba vya mawe teh teh.
 
Haya mambo ya kusem nimeshauriwa vibaya au ameshauriwa vibaya si kweli.kwnini usijishauri vivuri mwenyewe? kwanini mtu uwe na akili za kushikiwa?unaona huu ni moto na halafu unaambiwa huo ni mchanga nawe unakubali ukiungua unalalamika eti sikushuriwa............ utajiju
 
JK hataki aonekane mbaya kwa akina Lowasa pia anaogopa kuonekana mbaya kwa jamii. Kwa hiyo anachofanya hapa, ni kuwaweka pamoja Nape na akina Lowasa, halafu ampe Ukatibu mkuu Nape ili Nape awashughulikie (japo hii itakuwa ngumu!) Ili isionekane ni yeye ndiye aliyewashughulikia!
Halafu anaitwa RAIS. Hata ujumbe wa nyumba kumi ni ZERO huyu. UOGA, KUJIPENDEKEZA, UNAFIKI huo sio uongozi ni UCHAWI
 
Huyu mzee hana sera ingine zaidi ya ufisadi? analia sana.....aseme mengine...hawa ni watuhumiwa sio mafisadi.....tumechoshwa na sera zake za ufisadi ufisadi....


Kwako wewe neno ufisadi siju unalitathimini vipi na unaliangalia kwa mapana gani. Kama ni kwa mtazamo mfupi/mdogo/weak utaona ufisadi kama swala dogo. Tunaposema ufisadi, Dr. anaposema ufisadi maana yake ni: Mfumo wa rushwa unaokwamisha maendeleo ya nchi hii katika kila sector e.g ni ufisadi unasababisha huduma za afya kuwa duni, elimu duni, maslahi kwa wafanyakazi wa umma kuwa duni, nishati isiyokuwa ya uhakika mjini na vijijini. Ni ufisadi ndo unaosababisha haki kupatikana kwa shida. Ni ufisadi unasababisha watanzania kunywa matope badala ya maji safi na salama, ni ufisadi ndo unaofanya CCM kuendelea kuwapumbaza watanzania kwamba CCM ndo mmiliki wa nchi hii.

Sasa kuna nini zaidi ya kupamabana nacho zaidi ya ufisadi hapa nchini? Wewe Gamaba Vipi?
 
Ufisadi ndio ulioifikisha hii nch tajiri namna hii mahali tulipo, ni mungu tu anaweza kuturehemu na mabadiliko ya kweli ktk utawala na siasa. Dr. Slaa niko nyuma yako kabisa. We need changes basi!!!!
 
Chadema badala mjikite kwenye mambo yenu mnaongelea mambo NEC mnasahau Meya wa Nyamagana Mwanza kashindwa na CCM.
 
Acha kupiga mayowe, mkuu tupo kupanga safu Ya ushindi, Dr Slaa ongeza vikosi na tupige mbizi zaidi kuibukia 2015.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
Kwako wewe neno ufisadi siju unalitathimini vipi na unaliangalia kwa mapana gani. Kama ni kwa mtazamo mfupi/mdogo/weak utaona ufisadi kama swala dogo. Tunaposema ufisadi, Dr. anaposema ufisadi maana yake ni: Mfumo wa rushwa unaokwamisha maendeleo ya nchi hii katika kila sector e.g ni ufisadi unasababisha huduma za afya kuwa duni, elimu duni, maslahi kwa wafanyakazi wa umma kuwa duni, nishati isiyokuwa ya uhakika mjini na vijijini. Ni ufisadi ndo unaosababisha haki kupatikana kwa shida. Ni ufisadi unasababisha watanzania kunywa matope badala ya maji safi na salama, ni ufisadi ndo unaofanya CCM kuendelea kuwapumbaza watanzania kwamba CCM ndo mmiliki wa nchi hii.

Sasa kuna nini zaidi ya kupamabana nacho zaidi ya ufisadi hapa nchini? Wewe Gamaba Vipi?

Wewe sio fisadi? Kama tafsiri ya ufisadi hata wewe ni fisadi...tukianza kuangalia mapato yako na kukwambia weka kweney spreedsheet utakuwa fisadi ata one time....hakuna aliye msafi...Dr anaogopa safu ile ambayo yeye anaita fisadi...kwa sera zake za 2010 hazina mzuka tena kama mmoja wao atakuwa mgombea urais...kwani itabidi atafute sera ingine ya kupambana nao....

Na mtu kama lowasa na chenge wamemnyamazia Dr. na anafahamu hilo siku wakiamua kumchokonoa dr. hataonekana majukwaani kabisa...
 
Huyu mzee hana sera ingine zaidi ya ufisadi? analia sana.....aseme mengine...hawa ni watuhumiwa sio mafisadi.....tumechoshwa na sera zake za ufisadi ufisadi....

Lazima, Kwa sababu ufisadi ndio mzizi na shina la matatizo yote ya nchi yetu kwa sasa. Ukosefu wa maji, dawa mahospitalini, shule duni, n.k. ni kwa sababu ya ufisadi. Unataka aongee nini tena zaidi ya kuongelea mzizi na shina la tatizo?
 
hakuna CCM bila mafisadi na hakuna Mafisadi bila CCM nawote watakufa pamoja........mimi nakichanga walo niwe na shotgun na risasi 1000 before October 2015
 
Kiongozi wa Upinzani Nchini Na Katibu Mkuu wa chama kikuu cha upinzani nchini-CHADEMA Dr Wilbroad Slaa amesema ameshangazwa na uamuzi wa CCM kupitisha majina ya watuhumia wakuu wa ufisadi nchini kugombea nafasi mbalimbali ndani ya chama hicho ukiwemo ujumbe wa Halmashauri kuu ya Taifa CCM-NEC.

Kiongozi huyo machachari nchini amesema hayo yote yamefanywa na CCM licha ya kelele za wananchi kote nchini kulaani ufisadi uliofanywa na watu hao na pia CCM kuizika kauli yake ya kujivua Gamba na kuwaondoa watuhumiwa wa ufisadi.

Hata hivyo Dr Slaa amesema hiyo ni furaha kubwa kwake na chama chake kwani kwa hali hiyo CCM imejizika yenyewe kwani wananchi kamwe hawawezi kukubali kuongozwa tena na chama kinachokumbatia ufisadi kwa viwango hivyo.

Source: Nipashe na Tanzania Daima.



Mie ninacho shindwa kumuelewa huyu mzee nikusema maneno matupu pasipo matendo, km Ana ushahidi na uko wazi kwa nn asiwasiliane na wana sheria akawa peleka hao watuhumiwa wa ufisadi mahakamani? Kuna saidia nn kusema tu kila siku bila actions? Slaa unajishushia hadhi kwa ngonjera zako
 
Back
Top Bottom