Kibenje KK
JF-Expert Member
- May 28, 2016
- 267
- 380
Hii ni Moja ya biashara nzuri mnonahitahitaji kuanzisha biashara ya juis za matunda,naomba msaada wa mchanganuo na location nzuri
.
Unaweza Kuanza kwa kutembeza mitaani au Kwenye maofisi, anza na dumu 2 zenye ladha tofauti, kuna mtu atataka umchanganyie, mwengine atapenda moja zaidi.
.
Pia jitahidi iwe na ubaridi vizuri maana ndio inayopendwa zaidi. .
.
Pia hakikisha usiuze juice iliyolala ili kuepusha mtu kuumwa tumbo.
MAMBO YA KUZINGATIA.
USAFI
Usafi binafsi kwako muuzaji, usafi wa vyombo na mahali unapoandalia juice.
.
SOKO
Soko ni Kubwa, mtaani, masokoni, kwenye maofisi, kwenye Migahawa na shughuli mbalimbali.
BEI
Tengeneza za kuanzia Tsh 500_5000 na zaidi ukijenga jina
MAHITAJI
Blender heavy duty ni zuri zaidi na litadumu, package nzuri, mirija, fridge, maji masafi, chujio, vyombo vinginevyo
TENGENEZA JUICE PENDWA
Juice pendwa ni Maembe, maparachichi, Passion, Ukwaju, Ubuyu, Rosella, juice ya Tende, juice pendwa ya miwa na Smoothies
CONSISTENCY (Usiache)
Fanya kwa muendelezo Mpaka ujenge jina.
.
PANUA SOKO, FANYA KWA UKUBWA.
Usiogope kuomba tenda kwenye Migahawa ya kuwa muuzaji wa juice. Migahawa mingi hawatengenezi juice, wewe nenda waombe kuuza juice kwa wateja wanaonujua chakula.
.
TENGENEZA JUICE KWA ODA.
.
Kwenye sherehe zote omba nafasi ya kutengeneza juice, iwe ni kipaimara au harusi omba nafasi. Kama sherehe ni kubwa omba wakulipe Advance kwanza.
.
Hii ni biashara nzuri unayoweza kuanza sasa na kuanza na kuanza kutengeneza faida.
.
Unatamani kujifunza kuhusu hii biashara kiundani? Kuna vitabu vya jinsi ya kutengeneza aina mbalimbali za juice, mbinu, mauzo na masoko.
........
Mawazo mbalimbali ya biashara pitia page yangu ya instagram ya @kelvinkibenje utashukuru