Ghosryder
JF-Expert Member
- Jul 6, 2014
- 10,316
- 4,301
Kama tujuavyo, waislam wa nchi hii wamekuwa wakitumika sana katika chaguzi za nchi hii, wamekuwa wakitumiwa na CCM kupitia Bakwata. Waislam walitumiwa katika uchaguzi wa Igunga baada ya kuambiwa mkuu wa wilaya kavuliwa Hijab na CHADEMA, Bakwata kama kawaida yao wakatoa tamko la kulaani CHADEMA, lakini baadae ikagundulika huyo mama hakuwa na Hijab, pia imani yake haijulikani vizuri.
Mwaka 2005 hadi 2010, Waislam waliahhidiwa kuwa watapewa Mahakama ya kadhi, mahakama ya kadhi ilikuwa kwenye ajenda ya CCM ili wawavutie waislam wapigie kura CCM, ingawa CCM wenyewe walijua kuwa ni mbinu tu ya kuwavuta Waislam na wala hakuna dhamira ya dhati.
Mwaka 2010 katika uchaguzi mkuu, kupitia misikiti ya Bakwata, Mashekhe walizunguka nchi nzima kuipigia debe CCM kwa lengo kwamba watapata Mahakama ya Kadhi. Waislam kwa mara nyingine wakamiminika kwenda kupigia kura CCM kwa wingi wakidhani watapata Mahakama ya Kadhi, lakini hadi leo kupitia Bunge Maalum la Katiba, Mahakama ya kadhi imeendelea kuwa kitendawili, hivyo Waislam kama kawaida yao wakatumika.
Mwaka huu 2015 kuna uchaguzi mkuu, CCM wamebuni mkakati mpya wa kuwatumia Waislam kama kawaida waendelee kuwa mtaji wao. Baada ya kuona UKAWA wameungana, na Dr Slaa kuwa na ushawishi mkubwa kwa sasa, CCM kwa kutumia vijana wao mitandaoni, wametengeneza picha zinazomuonesha Dr. Slaa akiwa katika vazi la Upadre, kazi ambayo aliachana nayo na kujiunga na CCM, na baadae CHADEMA. Kwa sasa ukitembelea social media nyingi tayari picha hizo zilitengenezwa kwa Computer zimesambaa, lengo kubwa ni kuwafanya Waislam watumike kwa mara nyingine tena.
Ngoja tuone kama Tena mwaka huu Waislam watakuwa mtaji wa CCM kupitia ahadi hewa na propaganda
Kwanini wewe una chuki sana na waislamu? kweli chadema ni chaguo la shetani.