Kwa mara nyingine Waislam kutumika tena kama mtaji wa CCM 2015

Kama tujuavyo, waislam wa nchi hii wamekuwa wakitumika sana katika chaguzi za nchi hii, wamekuwa wakitumiwa na CCM kupitia Bakwata. Waislam walitumiwa katika uchaguzi wa Igunga baada ya kuambiwa mkuu wa wilaya kavuliwa Hijab na CHADEMA, Bakwata kama kawaida yao wakatoa tamko la kulaani CHADEMA, lakini baadae ikagundulika huyo mama hakuwa na Hijab, pia imani yake haijulikani vizuri.

Mwaka 2005 hadi 2010, Waislam waliahhidiwa kuwa watapewa Mahakama ya kadhi, mahakama ya kadhi ilikuwa kwenye ajenda ya CCM ili wawavutie waislam wapigie kura CCM, ingawa CCM wenyewe walijua kuwa ni mbinu tu ya kuwavuta Waislam na wala hakuna dhamira ya dhati.

Mwaka 2010 katika uchaguzi mkuu, kupitia misikiti ya Bakwata, Mashekhe walizunguka nchi nzima kuipigia debe CCM kwa lengo kwamba watapata Mahakama ya Kadhi. Waislam kwa mara nyingine wakamiminika kwenda kupigia kura CCM kwa wingi wakidhani watapata Mahakama ya Kadhi, lakini hadi leo kupitia Bunge Maalum la Katiba, Mahakama ya kadhi imeendelea kuwa kitendawili, hivyo Waislam kama kawaida yao wakatumika.

Mwaka huu 2015 kuna uchaguzi mkuu, CCM wamebuni mkakati mpya wa kuwatumia Waislam kama kawaida waendelee kuwa mtaji wao. Baada ya kuona UKAWA wameungana, na Dr Slaa kuwa na ushawishi mkubwa kwa sasa, CCM kwa kutumia vijana wao mitandaoni, wametengeneza picha zinazomuonesha Dr. Slaa akiwa katika vazi la Upadre, kazi ambayo aliachana nayo na kujiunga na CCM, na baadae CHADEMA. Kwa sasa ukitembelea social media nyingi tayari picha hizo zilitengenezwa kwa Computer zimesambaa, lengo kubwa ni kuwafanya Waislam watumike kwa mara nyingine tena.

Ngoja tuone kama Tena mwaka huu Waislam watakuwa mtaji wa CCM kupitia ahadi hewa na propaganda

Kwanini wewe una chuki sana na waislamu? kweli chadema ni chaguo la shetani.
 
hee jamaa kaaacha upadri kwa hiyo hataki kuitwa padri kwikwikwi nyerere aliacha ualimu lakini mpaka kufa kwake aliitwa MWALIMU

Mbona Jakaya Mrisho Kikwete ni Luteni lakini mnamwita Professor?...Au unasumbuliwa na tatizo la selective memory?
 
BAKWATA inajulikana kuwa ni kigango cha Kanisa Katoliki jimbo la CCM ... Hakuna Mwislam mwenye kujitambua anaweza kuifagilia BAKWATA hata siku moja! Iko wapi mali za iliyokuwa East Africa Muslim Welfare Society? Nyakati zile kulikuwa na muamko mkubwa wa maendeleo! Chuo alichokizindua JKN hakikuendelezwa baada ya kuzalishwa BAKWATA... Itoshe kusema kuwa ADUI mkubwa wa Waislam wa Tanzania ni CCM na BAKWATA ...
Kama tujuavyo, waislam wa nchi hii wamekuwa wakitumika sana katika chaguzi za nchi hii, wamekuwa wakitumiwa na CCM kupitia Bakwata. Waislam walitumiwa katika uchaguzi wa Igunga baada ya kuambiwa mkuu wa wilaya kavuliwa Hijab na CHADEMA, Bakwata kama kawaida yao wakatoa tamko la kulaani CHADEMA, lakini baadae ikagundulika huyo mama hakuwa na Hijab, pia imani yake haijulikani vizuri.

Mwaka 2005 hadi 2010, Waislam waliahhidiwa kuwa watapewa Mahakama ya kadhi, mahakama ya kadhi ilikuwa kwenye ajenda ya CCM ili wawavutie waislam wapigie kura CCM, ingawa CCM wenyewe walijua kuwa ni mbinu tu ya kuwavuta Waislam na wala hakuna dhamira ya dhati.

Mwaka 2010 katika uchaguzi mkuu, kupitia misikiti ya Bakwata, Mashekhe walizunguka nchi nzima kuipigia debe CCM kwa lengo kwamba watapata Mahakama ya Kadhi. Waislam kwa mara nyingine wakamiminika kwenda kupigia kura CCM kwa wingi wakidhani watapata Mahakama ya Kadhi, lakini hadi leo kupitia Bunge Maalum la Katiba, Mahakama ya kadhi imeendelea kuwa kitendawili, hivyo Waislam kama kawaida yao wakatumika.

Mwaka huu 2015 kuna uchaguzi mkuu, CCM wamebuni mkakati mpya wa kuwatumia Waislam kama kawaida waendelee kuwa mtaji wao. Baada ya kuona UKAWA wameungana, na Dr Slaa kuwa na ushawishi mkubwa kwa sasa, CCM kwa kutumia vijana wao mitandaoni, wametengeneza picha zinazomuonesha Dr. Slaa akiwa katika vazi la Upadre, kazi ambayo aliachana nayo na kujiunga na CCM, na baadae CHADEMA. Kwa sasa ukitembelea social media nyingi tayari picha hizo zilitengenezwa kwa Computer zimesambaa, lengo kubwa ni kuwafanya Waislam watumike kwa mara nyingine tena.

Ngoja tuone kama Tena mwaka huu Waislam watakuwa mtaji wa CCM kupitia ahadi hewa na propaganda

Mimi sipendi mambo haya ya Udini atakaekuja na hayo simptatii kura yangu. Kumbukeni hili ni Taifa lenye watu waliochanganyikana sana tu. Wakristo na waislamu wameoana wengi tu tuna ndugu tena wa karibu kutoka dini nyingine sasa mnataka kusema nini humu? yeyote alieegamia ukristo ama uislam mm simpendi maan anchi yetu haina hayo mambo. Kiongozi yeyote kwa namna yeyote akiweka hili swala mbele itakula kwake mazima. KAMWE MTU HATASHIKA DOLA KWA KUENEZA CHUKI ZA UDINI.
 
Wakristo na waislamu sasa ni kitu kimoja ndani ya UKAWA;
Wakulima na wafugaji sasa ni kitu kimoja ndani ya UKAWA;
Watanganyika na Wazanzibari sasa ni kitu kimoja ndani ya UKAWA;
Makabila yote Tanzania sasa ni kitu kimoja ndani ya UKAWA.

Ni muda muafaka sasa wa UKAWA kuchukua hatamu za uongozi wa nchi yetu - Hongera sana wana mapinduzi wa kweli kuanzisha umoja huu wa dhati kutukomboa sisi wanyonge tunaonyanyasika ndani ya nchi yetu.

AAAH... HAPA UMEMALIZA YOTE MPAKA AM HAPPY, Good
 
Wajinga ndio waliwao!!!! Mbinu zitakazotumika ni zile zile za kuwadanganya na kama kawa watadanganyika!!!!...... Chezea ile kitu ya "to keep doing same things in the same way...... Expecting a different result!!!!"

Sent from my iPhone using JamiiForums app
 
....nahitaji kuona sera mpya,aina mpya ya uongozi na Tanzania ni mpya...mimi kazi yangu ni moja tu kuikataa CCM na vibaraka wake wote kwa kuwapigia wagombea wa ukawa kura zote basi.

Mkuu chukua 5
 
Ivi wakristo mmesahau jinsi mlivyo sambaza waraka kanisani 2010? kikwete angefanyaje kama si kuwakimbilia waislam wenzie? na bado mliahidi 2015 slaa atagombea tena mkawashawishi vijana wa shule wajiunge na chadema.Na kama kawaida nasisi tutatoa tamko letu kuelekea uchaguzi kama mbwai mbwai nyi si mnasema mpo wengi tz tutaonana sasa.

Hilo tamko lako ni la kupambana na yupi katika UKAWA? Teh teh teh teh teh
 
Waislam zamu yenu imepita, miaka 10 imeenda bure chini ya Kikwete hamjaongeza hata Chuo kikuu kimoja zaidi ya kile aliwasaidia Mkapa. Mwaka huu hata asipokuwa Slaa but LAZIMA raisi ajaye awe mkristo. Kama mmenuna kuleni kitimoto kupunguza hasira. Je suis Charlie

Jamani haya mambo ya kushupalia dini za kigeni mpaka unatokwa povu na.kuchukua.slogan ya kuwabeza imani ya wengine ndio yanaleta shida duniani we ni mmoja wapo.
 
Ivi wakristo mmesahau jinsi mlivyo sambaza waraka kanisani 2010? kikwete angefanyaje kama si kuwakimbilia waislam wenzie? na bado mliahidi 2015 slaa atagombea tena mkawashawishi vijana wa shule wajiunge na chadema.Na kama kawaida nasisi tutatoa tamko letu kuelekea uchaguzi kama mbwai mbwai nyi si mnasema mpo wengi tz tutaonana sasa.

Kinachoongelewa hapa ni kwamba Waislamu ni wepesi sana kudanganyika na kutumika.Wakristo wanasimamia wanachoamini na hawawezi kutumika kirahisi.Angalia hata wewe ni shahidi maana unasema mtatoa Waraka baada ya kuona Wakristo wametoa.Yaleyale ya Mahakama ya Kadhi,Hamuwezi kuianzisha bila Msaada wa Wakristo.(Kumbuka; kuiweka kwenye Katiba ni ili iwe inajadiliwa na Watanzania wote na kupangiwa Bajeti Bungeni)
 
Mkuu asante sana kwa kunikumbusha ile habari ya mkuu wa wilaya ya igunga , unajua bhana yule mama alivaa mtandio wa kawaida sana , kama ile mitandio wanayovaa mabinti kwenye vigodoro huku kwetu mwembeyanga ! Ni uzushi mtupu kudai alivaa hijab .
 
Ukweli utabakia vilevile slaa achukui nchi hii sababu wenyewe ndo mmejiaribia kitendo cha kusambaza waraka kanisani mbona msikitini hamkuleta?

Watanzania wanachohitaji kwa sasa sio kuona Slaa anachukua Nchi bali CCM inaondoka Madarakani.
 
Nimejifunza yafuatayo:
1. Baadhi ya waumini wa dini ya kiislam wanaamini kwamba kuna watu wanaopiga kura kama waislam, ukweli ni kwamba wananchi wengi wamejikuta kwenye siasa za makundi na mara nyingi baada ya kura wanagundua kuwa watu walio katika makundi haya wapo kulinda maslahi yao binafsi.

2. Kuna baadhi ya waumini wa kiislam wanaoamini kwamba wanaweza kutumia kura yao - kupata wanayoyataka, na mtizamo huu ndio ambao wengi wetu wangeutumia kubadilisha mifumo na kupata taasisi imara, kubadili maisha yetu na mustakabali wa chi yetu.

3. Hili suala la waislam kuwekwa sokoni na kununuliwa kura zao kama bidhaa - hii shughuli ni kubwa.
 
Ikiwa CHADEMA inalitumia Kanisa na Wakristo kwanini CCM isitumie wanachama wake wote bila kujali itikadi zao za kiimani?

Lukuvi alipoenda kuongea uoga wake wa Uislam kuhusu Zanzibar alienda kuongelea hayo kwa Waislam?

Chadema mlivyoswagwa na Lipumba kutoka BMK alichokiongea hapo kulikuwa nini kama si kutumia hilo hilo la Waislam? Na mkakubaliana nae, au umesahau?

Au ndiyo kisa cha nyani haoni tundule?
Mimi ni Mwislamu, lakini hapa bibie FaizaFoxy umeongea kwa mihemuko tu! Wala hueleweki!!! Topic inahusu jinsi CCM wanavyotudanganya sisi waislamu ili wafanikishe mambo yao. Sasa wewe unakuja na uharo gani hapa tena?
 
Wewe unadanganywa na chadema huko, hao toka lini wakawa marafiki na Waislam? Imekula kwako.
 
Back
Top Bottom