Kwa leo acheni tu niwape heshima zao wanawake wote:

matokeo yanakuwa
husband_and_wife_quarrel.png
mpaka ifikie hapa nishachapa lapa zamani mnoooooo au naenda kumshitaki kwa mshenga kwann hataki kunipa haki yangu
 
ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza, anasononeka, unambembeleza anakuelewa anakusamehe halafu anasahau na anaendelea kukupenda!!!
...
UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka na kulia sana. Anakuchukia lakini baadaye anakusamehe. Halafu analea mtoto uliyemzaa nje kwa upendo. Kama ni kuchukiwa atachukiwa mtoto, si wewe uliyefanya umalaya!

UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA MTUNGI:Anakuwa na hofu kwa kuhofia usalama wako,Ukirudi anafurahi, Anakukaribisha vizuri, anakuandalia chakula, unagoma kula. Anahifadhi chakula alichokuandalia bila manung'uniko.
...
UNAAMKA ASUBUHI NA MAHANGOVER: Anakuandalia staftahi,supu n.k. (saa nyingine unagoma kutumia staftahi yake unakimbilia baa kwenda kunywa Supu na kuzimua. Wala halalamiki!

CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi wako, unataka huduma. Unamrukia, hufanyi maandalizi yoyote unamuumiza.Ukishamaliza bila kujali kama mwenzako naye karidhika unageukia pembeni na kuanza kukoroma.
Anavumilia ili akuridhishe. Na kesho yake tena inaweza tokea hii; hana kinyongo!

UNAJIANDAA KWENDA KIBARUANI: Unaamka,Unakuta tayari kakuandalia viwalo, suruwali imenyooshwa kama ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya maana! Nguo ulizovua jana zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa usafi!
Ulichomuudhi jana keshasahau na kukusamehe! anakutakia kazi njema kwa pendo!!!

UNAMPA UJAUZITO: Anauthamini, anautunza anajifungua kwa uchungu, mtoto anakuachia wewe umpe jina, la kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi kukuzalia mtoto mwingine na mwingine tena!

Na mengine meeeeengi sana wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE, WANAVUMILIA,WANAENDELEA KUWAPENDA!

Kwa leo acheni tu niwape
heshima zao wanawake wote:

LOVE WOMEN!

GOD BLESS WOMEN!!!!!!"
Aminata; Mimi nadhani umeelezea habari za wanawake wa zamani enzi hizo, siku hizi umfanyie nani mambo hayo?! sana sana wanaume ndio wamegeuziwa kibao na ukijaribu kulalamika unaambiwa mlitutesa sana miaka hiyo sasa tumeelimika. Haki sawa kwa wote!
 
Ndio huo usaidizi ambao Mungu aliwaumbia kwa ajili ya wanaume....!na bado,watatumika sana coz ndio wajibu wao kutumika katika mengi kama ulivyoainisha hapa!.....Poleeeeeeeee samaki pole,.........Offside trick waliimba
 
Ndio huo usaidizi ambao Mungu aliwaumbia kwa ajili ya wanaume....!na bado,watatumika sana coz ndio wajibu wao kutumika katika mengi kama ulivyoainisha hapa!.....Poleeeeeeeee samaki pole,.........Offside trick waliimba
umenikumbusha uo wimbo poleeeeeeee samaki poleeeeeeeee loh!
 
Mtawafanyia hvyo wasio na alternative ya maisha (magoli kipa) hakuna mwanamke mwenye maisha yake na pesa zake anayejiamin indepentend atavumilia huo upuziii wenu kwa ushauri wa bure wanaume wenye ujinga huo tafuten wajinga wenzenu.
 
Mtawafanyia hvyo wasio na alternative ya maisha (magoli kipa) hakuna mwanamke mwenye maisha yake na pesa zake anayejiamin indepentend atavumilia huo upuziii wenu kwa ushauri wa bure wanaume wenye ujinga huo tafuten wajinga wenzenu.

acha kuwaza kama 2011.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom