Ujasiri wa Mwanamke

Rural Swagga

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
1,579
1,081
ANAKUFUMANIA: Analia, ananyamaza,
anasononeka, unambembeleza
anakuelewa anakusamehe halafu
anasahau na anaendelea kukupenda!!!
... UNAZAA NJE YA NDOA: Anasononeka
na kulia sana. Anakuchukia lakini
baadaye anakusamehe. Halafu analea
mtoto uliyemzaa nje kwa upendo.
Kama ni kuchukiwa atachukiwa mtoto,
si wewe uliyefanya umalaya! UNARUDI USIKU WA MANANE UKIWA
MTUNGI:Anakuwa na hofu kwa kuhofia
usala...ma wako,Ukirudi anafurahi,
Anakukaribisha vizuri, anakuandalia
chakula, unagoma kula. Anahifadhi
chakula alichokuandalia bila manung'uniko. UNAAMKA ASUBUHI NA
MAHANGOVER:
Anakuandalia staftahi,supu n.k. (saa
nyingine unagoma kutumia staftahi
yake unakimbilia baa kwenda kunywa
Supu na kuzimua. Wala halalamiki! CHAKULA CHA USIKU: Ushapiga mtungi
wako, unataka huduma. Unamrukia,
hufanyi maandalizi yoyote
unamuumiza.Ukishamaliza bila kujali
kama mwenzako naye karidhika
unageukia pembeni na kuanza kukoroma. Anavumilia ili akuridhishe.
Na kesho
yake tena inaweza tokea hii; hana
kinyongo! UNAJIANDAA KWENDA
KIBARUANI:
Unaamka,Unakuta tayari kakuandalia viwalo, suruwali imenyooshwa kama
ya askari trafiki, shati limepigwa pasi ya
maana! Nguo ulizovua jana
zimeshalowekwa tayari kwa kufanyiwa
usafi!
Ulichomuudhi jana keshasahau na kukusamehe! anakutakia kazi njema
kwa pendo!!! UNAMPA UJAUZITO:
Anauthamini,
anautunza anajifungua kwa uchungu,
mtoto anakuachia wewe umpe jina, la
kwake halimo kabisa kwenye majina atakayotumia mtoto! Na pamoja na
uchungu wa kuzaa, bado yuko radhi
kukuzalia mtoto mwingine na
mwingine tena! Na mengine meeeeengi
sana
wanafanyiwa hawa watu lakini WANASAMEHE,
WANAVUMILIA,WANAENDELEA
KUTUPENDA! Kwa leo acheni tu walau tuwape
heshima zao wanawake wote: LOVE
WOMEN! GOD BLESS WOMEN!!!!!!"

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom