Kwa kauli hii tu waTZ wangekuwa makini kikwete asingefaa kuwa hata M/kiti wa kijiji

Gosbertgoodluck

JF-Expert Member
Mar 3, 2008
2,855
401
WanaJF,

Mnakumbuka ile kauli maarufu ya jk kwamba hafahamu kwa nini nchi yake ni maskini?!? Kwa mawazo yangu watanzania tungekuwa makini angalau kidogo, kauli hii ingem-disqualify kikwete kiasi cha kutofaa kuwa hata M'kiti wa serikali kijiji.
 
Ooohhh yes, kiongozi gani wa nchi asiyejua hata sababu ya nchi kuwa maskini!!!!!! Sasa yupo ikulu kufanya nini kama siyo kupoteza muda tu!!!!! Angegombea uenyekiti wa mtaa wetu wala asingepata.
 
Ukiwa kiongozi unatakiwa uwe na falsafa yako na maono yako.

Kama kiongozi hajui matatizo ya anaowaongoza basi pasi shaka kila njia inafaa kwake.

Nyerere aliazimia kujenga umoja wa kitaifa na kwa sehemu alifanikiwa.
Mwinyi aliazimia kufungua milango ya uchumi na alifanikiwa ingawa hata mainzi yaliingia. Serikali ikawa maskini ingawa wananchi wanaweka pesa kwenye soksi.
Mkapa aliazimia kukuza uchumi mkuu na serikali kweli ikawa na mapesa kibao hata ya kununua rada, jet, epa, meremeta, reserve ya kufa mtu n.k. Hapa serikali tajiri wananchi wanalia Ukapa.

Our very own presidaa akaambiwa na kina EL aje na kauli mbiu ya maisha bora kwa kila mtanzania. Miaka mitano down the road, maisha yangu hayajabadilika. Serikali haina pesa na wananchi hatuna pesa cha msingi BORA MAISHA.

Mkuu wa nchi anasema anataka tumkumbuke kwamba alitutoa hapa mpaka hapa. A very general statement as usual.

Uzuri/Ubaya ni kwamba iwe tulimchagua ama hatukumchagua anabaki kuwa Presidaa wetu, tutakoma!
 
Back
Top Bottom