Mzee Mwinyi, Mkapa, Kikwete na Hayati Magufuli, walisifiwa, walikosolewa! Haki ya kusifu/kupongeza iende sambamba na haki ya kukosoa!

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
50,504
113,618
Wanabodi,

Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa huja na makala zangu za " Kwa Maslahi ya Taifa". Makala ya leo ni kuhusu moja ya haki muhimu sana ndani ya katiba, kwenye Ibara ya 18, iitwayo haki ya uhuru wa kutoa maoni, "freedom of expression" ni haki inayotolewa na katiba yetu lakini kufuatia kushambuliwa kila kona kwa Dr. Bashiru, kutokana na kutoa nawazo yake ya ukosoaji, naona kuna watu wanataka kuingilia haki hii muhimu na kujimilikisha wao kwa kuingilia uhuru wa maoni wa watu wengine na hata kuwapangia ni maoni gani watoe!. Yaani wenye haki ni wanaosifu tuu na kupongeza, lakini ukikosoa, inakuwa nongwa kama anavyoshukiwa Dr. Bashiru!

Kwa vile wengi humu ni madogo, sisi kaka zenu tuna wajibu wa kuwaelimisha ya nyuma, toka enzi za Mzee Rukhsa, Ben, JK na JPM, wote walisifiwa na walikosolewa!. Ile haki ya Freedom of Expression provided na katiba yetu, yenye haki ya kusifu na kupongeza, inapaswa kwenda sambamba na haki ya kukosoa!. Hivyo kuna watu wanataka haki ya Mama ni asifiwe tuu na apongezwe tuu, lakini akikosolewa ni kosa, ni dhambi!.

Naomba tukumbushane tuu uhuru wa kutoa maoni yaani freedom of expression ni haki ya maoni huru ya kila mtu, wa kusifu na kupongeza wawe huru na wa kukosoa pia wawe huru, haki yao iheshimiwe, mtu akitoa mawazo yake kuhusu jambo lolote, hata kama hukubaliani nalo, mawazo yake yaheshimiwe!.

Bandiko hili ni kufuatia ukosoaji uliofanywa na Dr. Bashiru, watu wanamshukia kila kona, utadhani amemkufuru Mungu!, kumbe ni ametoa tuu mawazo yake na maoni yake, hata kama haukubaliani naye, heshimu mawazo yake, kama unatofautiana, pangua hoja zake, hoja kwa hoja na sio kwa viroja vya kumshambulia yeye binafsi. Hoja zake zijibiwe au zipingwe kwa hoja!

Ukimuondoa Rais Nyerere, marais wengine wote waliofuatia, walisifiwa na walikosolewa hadharani, kama Ilivyokuwa kwa Rais Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Rais Samia, wote wanasifiwa nav wanakosolewa na hakuna ubaya wowote na ukosoaji sii dhambi, sii kosa!

Freedom of expression ya haki ya kumpongeza rais, inakwenda sambamba na haki ya kumkosoa rais, hivyo ukosoaji wa Dr. Bashiru, naomba uheshimiwe!

Ukosoaji Enzi za Nyerere
Kwa vile mimi ni mtu wa mastori mastori ya kimepanda kikashuka, naomba wale wa short and clear muishie hapa na ku jump kwenye cònclusion, wale wa mastori stori, tuendeleeni
Hii katiba yetu ya mwaka 1977, haikuwa na vipengele vya haki za binaadamu hivyo enzi za Nyerere ukosoaji ulikuwa ni tatizo!.

Mwaka 1980 Mzee wangu Mzee Andrew Mayalla, (RIP) ni miongoni mwa watu waliosaini petition ya James Mapapala kupinga mfumo wa chama kimoja!, enzi hizo nchi yetu ilikuwa na sheria ya presidential preventive detention order, ambapo mtu ukihisiwa ni hatari kwa usalama wa taifa, rais anaisaini tuu hiyo order, mtu unahifadhiwa mahala salama indefinately bila kufikishwa mahakamani!. Watu 59 walisaini petition hiyo na wate walisombwa!. Baada ya kusombwa, walihojiwa, wengine wakaachiwa, ( kuna baadhi ya kazi watu huwa hawastaafu!). Hivyo Nyerere hakupingwa!. Hili pia liliwahi kuwakuta kina Bibi Titi Mohamedi, Lifa Chipaka, Michael Kamaliza enzi za TANU, Kasanga Tumbo, Joseph Kasela Bantu na Tumtemeke Sanga, ukimkosoa, Mwalimu au kuisosoa serikali, ulikuwa unahifadhiwa mahali salama, ukitoka huko, unakuwa umechakaa!, umenyoroka ni mwendo wa, heshima na adabu!.

Hata hivyo, Mwalimu Nyerere kabla hajang'atuka madarakani, 1984 ile Bill of Rights kutoka kwenye The Universal Declaration of Human Rights, ndio ikaingizwa ndani ya katiba yetu kwa marekebisho ya katiba na kuanza kutumika mwezi May, 1985.

Enzi za Mwinyi, ndipo watu tulianza kukohoa, na kuna wakati Mzee Punch wa Chuo Kikuu alifikia kumkeli rais Mwinyi na wanafunzi wa chuo kikuu kina Bazigiza, kabinti Sikitiko Kapile na wengine kupanda pale Revolution Squire na kutukana hadi Mwinyi akakifunga Chuo Kikuu.

Mmoja wa Wakosoaji wakuu wa serikali na Bunge alikuja kuwa ni Mwalimu Nyerere mwenyewe!, Bungeni kuliibuka kundi la G-55 likiongozwa na Njelu Kasaka, kina Jenerali Ulimwengu, likaidai serikali ya Tanganyika, Bunge likapitisha, Mwalimu, enzi hizo Chama ndio kinashika hatamu, kiliitishwa kikao cha chama ambacho wabunge ni members, wabunge wale waligombezwa kama watoto, G 55 ilisambaratishwa, Waziri Mkuu akiwa JS Malecela, alipigwa chini!. Ukosoji wa Mwalimu ulihamia kwa rais Mwinyi hadi akamtungia vitabu, Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Kitabu cha Nyufa!, hakukutokea mburumatata wowote waliomshambulia Mwalimu!, na Mwinyi kwa uungwana, alijinyamazia, hakuwahi kujibu chochote!. Tunamuomba Rais Samia, kweli hili la Dr. Bashiru, afuate uungwana wa rais Ali Hassan Mwinyi, asijibu lolote, asisikilize hizo kelele za hao mburumatata wanaomshambulia Dr. Bashiru, hatapungukiwa na kitu!

Enzi za Mkapa tayari nchi yetu ilikuwa kwenye mfumo wa vyama vingi, ukosoaji ukawa sio kosa.

Mimi niliingia newsroom ile 1990-1995 nikiwa RTD, hivyo sikushiriki ukosoaji wowote.

1995 nikahamia DTV na kuendesha kipindi cha "Mada Moto" kuhusu uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi, Mada Moto producer ni Beatrix Mugishagwe akishirikiana na Wolfgang Baraniek na baada ya uchaguzi niliendesha kipindi cha "Kiti Moto" produced by Masai Studio, huko ni ukosoaji mwanzo mwisho!. Kuna viongozi walukuwa wakialikwa Kiti Moto, wanakimbia!

Mwaka 2005, JK akatinga ikulu mwaka 2006 Jamiiforums ikaanzishwa hapo ndio ukosoaji ukafika peak!, na hata mimi nilitomasa tomasa hapa na pale! Mapungufu ya Kikwete: Constructive Criticisim!

2014 hata kabla JPM hajawa rais, humu jf nilipandisha bandiko hili, Elections 2015 - Mgombea wa Urais Kwa tiketi ya CCM, 2015 "Could Be" John Pombe Magufuli na tangu alipoingia, mpaka alipoitwa humu jf, usifiaji, ukosoaji ni bandika bandua!.
Mimi tuu mwenyewe nilibandika mabandiko zaidi ya 25 kukosoa na zaidi ya 25 kusifu!. Kati ya wakosoaji wa Rais Magufuli na Serikali yake, na wasifiaji nani wanamsaidia zaidi? Ijue nafasi ya JamiiForums

Ukosoaji wa JPM ulivuka mipaka kwa lugha ambazo sio za staha, tukajaribu kusaidia saidia Wito Kwa wana JamiiForums kuhusu ukosoaji wa Rais Magufuli

Pia from time to time tukawa tunakumbushana humu,
Hadi Mungu alipomchukua mja wake hadi leo ukosoaji wa JPM humu jf unaendelea.

Ndipo akaingia Rais Samia, kama kawa
sisi watu wa mbali kwa mbali, Samia nae tulianza nae mbali...
The same applies to urais wa Samia, hakuna mtu yoyote alijua kuwa kuna siku rais wa JMT anaweza kufa akiwa madarakani!, hivyo siku zote Makamo wa rais alikuwa anateuliwa tuu bila kumhesabia anaweza kuja kuwa rais wa JMT kwasababu hakuna aliyewahi kufikiri rais wetu anaweza kufa!.

Hivyo naamini hata wakati Samia ni Makamo wa JPM, hakuwahi kuwaza kuwa kuna siku JPM anaweza kuitwa kwa Baba yake na yeye kuwa rais wa JMT!, hivyo ilivyotokea JPM akaitwa Baba yake na Samia kawa rais, watu wote wanajua imetokea tuu, ni mipango ya Mungu, lakini hakuna watu wanaojua kumbe kuna watu, walitoa kauli zenye nguvu ya kuumba, waliomuomba Mungu, wakamuumbia urais wa JMT ili Samia awe rais na kweli Mungu akasikia hivyo kauli hizo zikamuumbia Samia urais, hivyo usikute hata Samia mwenyewe anajihesabu amekuwa rais wa JMT kwa kudra tuu za Mwenyeenzi Mungu, kumbe hajui sio kudra tuu, kuna watu waliomba, na wakapewa!.

Kwanza anza kuangalia ni lini watu walianza kumspot Mama Samia, mimi nilimspot 2010 New Cabinet: Baadhi ya Majina ni Haya Hapa!.
Wanabodi,
Bado niko hapa mjini Dodoma, nikijivinjari katika viwanja vya Bunge kwa haya na yale.

Japo mpaka sasa kitendawili cha Waziri Mkuu bado hakijatenguliwa, nimeonelea niwatajie baadhi ya majina mapya kwenye new cabinet.

2. Mwingine ni Samia Suluhu Hassan.
Huyu mama ni very powerful in Zanzibar na miongoni mwa wanawake wachache wa shoka kutoka Zanzibar. Ni Mjumbe wa CC na NEC wa CCM.
Very high profile woman from Zanzibar, baada ya kuhudumu kwa miaka 10 kwenye Baraza la Wawakilishi, sasa ameingia Bunge la JMT, atapewa important portfolio kumuandaa ama kuwa rais wa Zanzibar kisha kuja bara, au kuwa VP 2015.
Pasco
Bandiko hili ni la 2010, angalia hiyo 2010 tulisema nini kumhusu Samia, na nini kilikuja kutokea... mkiambiwa baadhi ya kauli zinaumba, mjue ni kweli kauli huumba!.

Kisha 2015 Siku ya Wanawake Duniani: Je, tuna Wanawake wenye sifa za Presidential Material?
Kauli Umba ya kuunda VP mwananke kwa Tanzania
Kufuatia kilio cha muda mrefu cha wanawake kunyimwa fursa, je ni kweli tunao wanawake wenye sifa na uwezo wa kutupeleka kwenye 50/50?. Hebu na tuanzie na wanawake wenye sifa za urais, je tunao?

Hebu tuwakumbuke the top ten female politicians in Tanzania, na nafasi wanazoshika! Je, wamefikaje hapo, kwa kupanda wenyewe, au wamebebwa ndipo wakafika hapo? Je, wana sifa za urais?
  1. Top No.1 ni Mhe. Samia Suluhu Hassan.
    Huyu mama ni very powerful in Zanzibar na miongoni mwa wanawake wachache wa shoka kutoka Zanzibar. Ni Mjumbe wa CC na NEC wa CCM.
    Very high profile woman from Zanzibar, baada ya kuhudumu kwa miaka 10 kwenye Baraza la Wawakilishi, ameingia Bunge la JMT for 5 years sasa ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamo wa Rais. Ndiye alikuwa Makamo Mwenyekiti wa Bunge la Katiba. Huyu ni presidential material, sasa ni kumuandaa kwanza kuwa rais wa Zanzibar kwa kumpumzisha Dr. Shein kipindi chake cha pili, kisha 2020 aje urais wa Muungano, ili hili ifanyike, itabidi, CCM iachane na ule utaratibu wake wa two terms za urais, kwasababu kusubiria 2025, kwa huyu mama itakuwa too little too late, age itakuwa imemtupa mkono.
Natoa wito kwa wanawake, kama ni kweli mna uwezo, jitokezeni kwenye urais, ili hata msiposimamishwa, angalau 2015, tuwe na makamo rais mwanamke, au Waziri Mkuu Mwanamke!

Paskali.
Tanzania ilipata VP, mwanamke kwa mara ya kwanza, baada ya uchaguzi wa 2015, kuna wengi wanadhani ilijitokea tuu, Tanzania kuwa na VP mwanamke!, hawajui kuwa huo u VP wa mwanamke, kuna watu wenye kauli zenye powers za kuumba, walitoa kauli za kutaka tupate VP mwanamke, toka Machi 8, 2015!.

Then Siku ya Wanawake Duniani: VP Samia Suluhu: "Womanly, Genuine, Humble, Simple na Down To Earth!”
kiukweli huyu ni mwanamke wa kupigiwa mfano, mtanisamehe sina maneno ya Kiswahili ya kujitosheleza kumuelezea, she is just so womanly, so genuine, so simple, very humble na down to earth!, ana a very rare charisma, which is very hard to find kwa viongozi wetu wengi wa kisasa.

She is just everything a woman needs to be!. Ingekuwa ni amri yangu ningetaka wanawake wenye uongozi, madaraka na mamlaka waige mfano wa Mwanamke huyu and to be honest I wish if Mungu angemua, huyu mama ndio akawa, then amini usiamini tutakuwa na Tanzania nzuri 100 times kuliko Tanzania hii tulionayo sasa!.

Ingekuwa ni amri yangu, ningemwambia tuu naniliu aamue 2020 asigombee his second term, na badala yake, ampishe ili awe huyu mama!.

Mungu ambariki sana Mama Samia na kuwabariki wanawake wote leo siku ya Wanawake Duniani.

Paskali
Hii ni kauli umba ya kumuumbia mtu urais wa JMT.

na hili "Watu waachwe Huru kuujadili Muungano"- VP, Samia Suluhu Hassan. Huyu mama anaongea vizuri kwa Unyenyekevu mpaka raha. Huchoki kumsikiliza
Angalia kwa makini hii kauli umba hapa iliumba nini?
Makamo wa Rais wa JMT, Mhe. Samia Suluhu Hassan anauzungumzia Muungano, kiukweli huyu Mama Samia anauzumguza vizuri muungano huku akiongea kwa heshima, taratibu, kwa utulivu na unyenyekevu, na anaongea vizuri mpaka raha, na kwa wale wenzangu na mimi wenye udhaifu na macho fulani, kiukweli Mwenyenzi Mungu amemjaalia macho mashaalah, huchoki kumsikiliza, utatamani aendelee tuu kuongea na kipindi kisiishe!.

Kwa hoja za muungano Mama Samia alizoshusha, ningekuwa ni uwezo wangu, ningeshauri October 2020, Mama Samia ndiye ampokee Dr. Shein kule Zanzibar, ili 2025, aje ampokee Magufuli, maana kwa maoni yangu, kwa uongeaji huu, huyu mama ndiye Mzanzibari pekee anayekubalika kuweza kuchagulika kuwa rais wa JMT kutokea Zanzibar, vinginevyo Wazanzibari wausahau kabisa urais wa Muungano, wao mwisho wao ni umakamo wa rais pekee.

Kwa hoja kama hizi za huyu mama Samia, kama age sio issue sana, si huyu mama atatufaa sana 2025 au tuwashauri kwa vile Magufuli analamika sana kuhusu urais, mara ni mateso, mara ni kazi ngumu, mara ni mzigo mzito, tumshauri rais Magufuli, kwa vile Samia anatosha sana, hivyo tumpunguzie mateso, hana haja ya kuendelea na mateso, mzigo mzito na kazi ngumu ya urais, na hata kama ni wale tausi au wanyama wa Magogoni, au yale majabali ya Chamwino, tutamjengea Chato na kumuomba bora apumzike tuu mapema, na kumpisha Mama Samia ndio amalizie ngwe yake iliyobakia?.

Paskali
Hapa kuna mtu ameumbiwa urais wa JMT kwa kauli tuu!.

Naamini kama JPM angesoma hapa, halafu akaamua tangu ile ile ,2020 angempisha Samia, you never know...

Tukawasisitiza watu humu kuwa Rais Samia na yeye ni binadamu, sio malaika!, Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Hivyo kama ilivyo kwenye haki ya kupiga kura, inakwenda sambamba na haki ya kupigiwa kura, vivyo hivyo kwenye haki ya kusifu na kumpongeza rais Samia, haki hiyo ya kumpongeza, inakwenda sambamba na haki ya kumkosoa rais Samia, mkosoaji asishambuliwe yeye, ishambuliwe hoja yake!.

Wapongezaji wa Mama kwa jinsi anavyoupiga mwingi wana haki ya kusifu na kupongeza, ila wanapotokea watu ma critiki, wanaopinga Mama kuupiga mwingi, wapongezaji wasijimilikishe haki za wengine kumkosoa Mama Samia, hivyo kuwashukia wakosoaji as if ni wamemkufuru Mungu kama sasa Dr. Bashiru anavyoshukiwa kama mwewe anavyo sarandia kunyakuwa kifaranga cha kuku!.

Hitimisho
Wanaosifu wasifu kwa hoja, ni haki yao kusifu, lakini pia, wanao kosoa, wakosoe kwa hoja kwa kutumia ukosoaji wa contructive criticism, ukosoaji wenye nia njema ya kujenga, kwa kutumia lugha ya staha na amini usiamini, unaweza kukuta, wanaomkosoa Rais Mama Samia, ndio wanao msaidia kuliko wanaomsifu!.

Wasalaam

Paskali
 
Tatizo sio kukosoa unadhani haya matamshi yangetoka toka mwanachama wa chama chochote cha upinzani ingekuwa hoja? ungetuwaambia labda hao kina Mkapa, JK na JPM kama walikosolewa na wana CCM au watu wa serikalini.

Waliomkosoa JPM na yaliyowakuta tunayajuwa na Bashiru ndio alikuwa mbele kuwahoji kwenye vikao au kasahahu? JK alitukanwa sana tu lakini wapinzani tuambie nani alitoka ndani ya CCM akamtukana kiongozi wake akabaki salama.

Hata Mbowe anatukanwa lakini tuambie nani katika Chadema aliwahi kumkosoa kiongozi wake akabaki salama. Ukosoaji mzuri kama unaona sikubaliani na chama changu unakaa pembeni sio uko ndani ya system halafu unamtukana kiongozi wako.

Chama ina vikao vyao vya kukosoana na haya aliongea mwenyewe BASHIRU.
 
Tatizo sio kukosoa unadhani haya matamshi yangetoka toka mwanachama wa chama chochote cha upinzani ingekuwa hoja? ungetuwaambia labda hao kina Mkapa, JK na JPM kama walikosolewa na wana CCM au watu wa serikalini. Waliomkosoa JPM na yaliyowakuta tunayajuwa na Bashiru ndio alikuwa mbele kuwahoji kwenye vikao au kasahahu? JK alitukanwa sana tu lakini wapinzani tuambie nani alitoka ndani ya CCM akamtukana kiongozi wake akabaki salama. Hata Mbowe anatukanwa lakini tuambie nani katika Chadema aliwahi kumkosoa kiongozi wake akabaki salama. Ukosoaji mzuri kama unaona sikubaliani na chama changu unakaa pembeni sio uko ndani ya system halafu unamtukana kiongozi wako. Chama ina vikao vyao vya kukosoana na haya aliongea mwenyewe BASHIRU.
Unakumbuka hoja za HUSSEIN BASHE kwa usalama wa Taifa kabla hajawa waziri
 
"Akili kubwa hujadili hoja ,akili ya Kati hujadili matukio na akili ya chini hujadili watu"Socrates

Ni bora watu hasa walio ndani ya chama Cha mapinduzi wajikite kujibu hoja za Dr Bashiru kwa kutumia lugha Safi na staha kuliko vijembe na kejeli ambazo kimsingi hazina tija kwa taifa na chama.

Tumekuwa taifa la ajabu Sana kwa kuwa na tabia ya kumshambulia mleta hoja badala ya hoja hata mzee kikwete kasha wahi sema "hoja ya mtu haupingwi rungu" pamoja na jaji mstaafu jaji warioba amesisitiza Bashiru ajibiwe kwa hoja, sitaki kuamini chama Cha mapinduzi hakina watu makini wa kujibu hoja za Dr Bashiru.

"Kukatwa kwa kisu ni tofauti na kukatwa kwa ulimi"
 
tatizo walisifiwa na kukoselewa na watu gani?

Nadhani mwezi/miezi imepita kuna msimamizi wa mhimili alijitokeza akawaambia wanajamii yeyote atakayemkosoa mheshimiwa raisi, awe CCM ama chama kingine wasimwache hata kidogo, wahakikishe wanadeal nae perpendicular

Wengi wa wakosoaji wakiwa nje ya chama tawala huwa ndani ya dakika/saa/siku kadhaa huishia kupatwa na madhila mabaya kama sing-bad the sailor ni vigumu sana kuukubali ukweli katika zama hizi na kutetea uongo
bora ukosoaji uendelee ndani ya chamaa
 
Hata mahakamani mtu anaweza fungwa maisha au kuachiliwa huru kama "motive" imejukikana.....

Huwezi sema ni freedom of speech wakati motive ya mhusika inajulikana.......motive ndo inafanya MTU anapoongea ionekane ni Busara au majungu ...motive...Motive ya Bashiru ni kuendeleza demokrasia?ambayo akiikanyaga alipokuwa na power?au kushambulia kundi moja ili kundi lake lipate mileage?

Ujinga ni kutokujua...lakini upumbavu ni kujua na kukataa kitu kiko wazi kabisa
 
Mpaka sasa hakuna hata mmoja kati ya wanao mshambulia Bashiru ambae anaweza kuonyesha kosalake katika hotuba yake.

Wote wanamshambulia kwa mambo ya kipuuzi tu, yani wanamshambulia kwa mambo binafsi na sio kwa hojazake za kupinga kusifiasifia.

Kifupi wanachuki binafsi to na wengi wanajipendekeza Ili waonekane wanampenda mkuu,Ili ugali uendelee.

Tumefika pabaya sana.
Watu wanajitoa akili kupambana na ukweli kwasababu ya ulafi wa madaraka.
 
Wanaomkosa Bashiru wapo sahihi na Bashiru yupo sahivi sababu wote ni wasaka fursa hakuna ambaye yupo ajili ya wananchi au nchi, Bashiru alihusika na mauji sn enzi ya dikteta
 
Hata mahakamani mtu anaweza fungwa maisha au kuachiliwa huru kama "motive" imejukikana.....

Huwezi sema ni freedom of speech wakati motive ya mhusika inajulikana.......motive ndo inafanya MTU anapoongea ionekane ni Busara au majungu ...motive...Motive ya Bashiru ni kuendeleza demokrasia?ambayo akiikanyaga alipokuwa na power?au kushambulia kundi moja ili kundi lake lipate mileage?

Ujinga ni kutokujua...lakini upumbavu ni kujua na kukataa kitu kiko wazi kabisa
Bashiru na wana CCM wenzake ni mashetani tupu
 
"baada ya uchaguzi niliendesha kipindi cha "Kiti Moto" produced by Masai Studio, huko ni ukosoaji mwanzo mwisho!. Kuna viongozi walukuwa wakialikwa Kiti Moto, wanakimbia!."

Daaaah Mkuu leo ndio umenifumbua macho. Kumbe aka ya ile nyama yetu maarufu, chanzo ni hapa.

Nyama ya Nguruwe aka Kitimoto aka Pascal Mayalla.

Sent from my SM-A715F using JamiiForums mobile app
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa huja na makala zangu za " Kwa Maslahi ya Taifa". Makala ya leo ni kuhusu moja ya haki muhimu sana ndani ya katiba, kwenye Ibara ya 18, iitwayo haki ya uhuru wa kutoa maoni, "freedom of expression" ni haki inayotolewa na katiba yetu lakini kufuatia kushambuliwa kila kona kwa Dr. Bashiru, kutokana na kutoa nawazo yake ya ukosoaji, naona kuna watu wanataka kuingilia haki hii muhimu na kujimilikisha wao kwa kuingilia uhuru wa maoni wa watu wengine na hata kuwapangia ni maoni gani watoe!. Yaani wenye haki ni wanaosifu tuu na kupongeza, lakini ukikosoa, inakuwa nongwa kama anavyoshukiwa Dr. Bashiru!.

Kwa vile wengi humu ni madogo, sisi kaka zenu tuna wajibu wa kuwaelimisha ya nyuma, toka enzi za Mzee Rukhsa, Ben, JK na JPM, wote walisifiwa na walikosolewa!. Ile haki ya Freedom of Expression provided na katiba yetu, yenye haki ya kusifu na kupongeza, inapaswa kwenda sambamba na haki ya kukosoa!. Hivyo kuna watu wanataka haki ya Mama ni asifiwe tuu na apongezwe tuu, lakini akikosolewa ni kosa, ni dhambi!.

Naomba tukumbushane tuu uhuru wa kutoa maoni yaani freedom of expression ni haki ya maoni huru ya kila mtu, wa kusifu na kupongeza wawe huru na wa kukosoa pia wawe huru, haki yao iheshimiwe, mtu akitoa mawazo yake kuhusu jambo lolote, hata kama hukubaliani nalo, mawazo yake yaheshimiwe!.

Bandiko hili ni kufuatia ukosoaji uliofanywa na Dr. Bashiru, watu wanamshukia kila kona, utadhani amemkufuru Mungu!, kumbe ni ametoa tuu mawazo yake na maoni yake, hata kama haukubaliani naye, heshimu mawazo yake, kama unatofautiana, pangua hoja zake, hoja kwa hoja na sio kwa viroja vya kumshambulia yeye binafsi. Hoja zake zijibiwe au zipingwe kwa hoja!.

Ukimuondoa Rais Nyerere, marais wengine wote waliofuatia, walisifiwa na walikosolewa hadharani, kama Ilivyokuwa kwa Rais Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Rais Samia, wote wanasifiwa nav wanakosolewa na hakuna ubaya wowote na ukosoaji sii dhambi, sii kosa!.

Freedom of expression ya haki ya kumpongeza rais, inakwenda sambamba na haki ya kumkosoa rais, hivyo ukosoaji wa Dr. Bashiru, naomba uheshimiwe!.

Ukosoaji Enzi za Nyerere
Mwaka 1980 Mzee wangu Mzee Andrew Mayalla, (RIP) ni miongoni mwa watu waliosaini petition ya James Mapapala kupinga mfumo wa chama kimoja!, enzi hizo nchi yetu ilikuwa na sheria ya presidential preventive detention order, ambapo mtu ukihisiwa ni hatari kwa usalama wa taifa, rais anaisaini tuu hiyo order, mtu unahifadhiwa mahala salama indefinately bila kufikishwa mahakamani!. Watu 59 walisaini petition hiyo na wate walisombwa!. Baada ya kusombwa, walihojiwa, wengine wakaachiwa, ( kuna baadhi ya kazi watu huwa hawastaafu!). Hivyo Nyerere hakupingwa!. Hili pia liliwahi kuwakuta kina Bibi Titi Mohamedi, Lifa Chipaka, Michael Kamaliza enzi za TANU, Kasanga Tumbo, Joseph Kasela Bantu na Tumtemeke Sanga, ukimkosoa, Mwalimu au kuisosoa serikali, ulikuwa unahifadhiwa mahali salama, ukitoka huko, unakuwa umechakaa!, umenyoroka ni mwendo wa, heshima na adabu!.

Enzi za Mwinyi, mkosoaji Mkuu alikuja kuwa ni Mwalimu mwenyewe!, mpaka akamtungia vitabu, Uongozi Wetu na Hatima ya Tanzania, Kitabu cha Nyufa!.

Enzi za Mkapa tayari nchi yetu ilikuwa kwenye mfumo wa vyama vingi, ukosoaji ukawa sio kosa.

Mimi niliingia newsroom ile 1990-1995 nikiwa RTD, hivyo sikushiriki ukosoaji wowote.

1995 nikahamia DTV na kuendesha kipindi cha "Mada Moto" kuhusu uchaguzi mkuu wa kwanza wa vyama vingi, Mada Moto producer ni Beatrix Mugishagwe akishirikiana na Wolfgang Baraniek na baada ya uchaguzi niliendesha kipindi cha "Kiti Moto" produced by Masai Studio, huko ni ukosoaji mwanzo mwisho!. Kuna viongozi walukuwa wakialikwa Kiti Moto, wanakimbia!.

Mwaka 2005, JK akatinga ikulu mwaka 2006 Jamiiforums ikaanzishwa hapo ndio ukosoaji ukafika peak!, na hata mimi nilitomasa tomasa hapa na pale!.

2014 hata kabla JPM hajawa rais, humu jf nilipandisha bandiko hili, na tangu alipoingia, mpaka alipoitwa humu jf, usifiaji, ukosoaji no bandika bandua!.
Mimi tuu mwenyewe nilibandika mabandiko zaidi ya 25 kukosoa na zaidi ya 25 kusifu!.

Ukosoaji wa JPM ulivuka mipaka kwa lugha ambazo sio za staha, tukajaribu kusaidia saidia.

Pia from time to time tukawa tunakumbushana humu,
Hadi Mungu alipomchukua mja wake hadi leo ukosoaji wa JPM humu jf unaendelea.

Ndipo akaingia Rais Samia, kama kawa sisi watu wa mbali kwa mbali, Samia nae tulianza nae mbali...

Tukawasisitiza watu humu kuwa Rais Samia na yeye ni binadamu, sio malaika!,

Hivyo kama ilivyo kwenye haki ya kupiga kura, inakwenda sambamba na haki ya kupigiwa kura, vivyo hivyo kwenye haki ya kumpongeza rais Samia, haki hiyo ya kumpongeza, inakwenda sambamba na haki ya kumkosoa.

Wapongezaji wa Mama anavyoupiga mwingi wana haki ya kupongeza, ila wanapotokea watu wanaopinga Mama kuupiga mwingi, wasijimilikishe haki za wengine kumkosoa Mama Samia, hivyo kuwashukia wakosoaji as if ni wamemkufuru Mungu kama sasa Dr. Bashiru anavyoshukiwa kama mwewe anavyo sarandia kunyakuwa kifaranga cha kuku!.

Hitimisho
Wanaosifu wasifu kwa hoja, ni haki yao kusifu, lakini pia, wanao kosoa, wakosoe kwa hoja kwa kutumia ukosoaji wa contructive criticism, ukosoaji wenye nia njema ya kujenga, kwa kutumia lugha ya staha na amini usiamini, unaweza kukuta, wanaomkosoa Samia, ndio wanao msaidia kuliko wanaomsifu!.
Wasalaam

Paskali
Nawe mbona mgumu kuelewa, tumesema Bashiru alichokisema kiko sahihi kwa kiwango cha juu sana. Tatizo haya anayoyakemea aliyafanya yeye wakati wa magufuli kwa vile alikuwa anakula mlo wake, and therefore ni mnafiki. Siyo kuwa anataka advancement ya wakulima, anawatetea wakulima, never, ni kwa vile amepokwa madaraka aliyorundikiwa na magufuli!
Once a traitor, always a traitor. It only takes true repentance and a turn -around to regain public Trust! by Maria sarurungi
 
Wanabodi,
Kama kawaida yangu, kila nipatapo fursa huja na makala zangu za " Kwa Maslahi ya Taifa". Makala ya leo ni kuhusu moja ya haki muhimu sana ndani ya katiba, kwenye Ibara ya 18, iitwayo haki ya uhuru wa kutoa maoni, "freedom of expression" ni haki inayotolewa na katiba yetu lakini kufuatia kushambuliwa kila kona kwa Dr. Bashiru, kutokana na kutoa nawazo yake ya ukosoaji, naona kuna watu wanataka kuingilia haki hii muhimu na kujimilikisha wao kwa kuingilia uhuru wa maoni wa watu wengine na hata kuwapangia ni maoni gani watoe!. Yaani wenye haki ni wanaosifu tuu na kupongeza, lakini ukikosoa, inakuwa nongwa kama anavyoshukiwa Dr. Bashiru!.

Kwa vile wengi humu ni madogo, sisi kaka zenu tuna wajibu wa kuwaelimisha ya nyuma, toka enzi za Mzee Rukhsa, Ben, JK na JPM, wote walisifiwa na walikosolewa!. Ile haki ya Freedom of Expression provided na katiba yetu, yenye haki ya kusifu na kupongeza, inapaswa kwenda sambamba na haki ya kukosoa!. Hivyo kuna watu wanataka haki ya Mama ni asifiwe tuu na apongezwe tuu, lakini akikosolewa ni kosa, ni dhambi!.

Naomba tukumbushane tuu uhuru wa kutoa maoni yaani freedom of expression ni haki ya maoni huru ya kila mtu, wa kusifu na kupongeza wawe huru na wa kukosoa pia wawe huru, haki yao iheshimiwe, mtu akitoa mawazo yake kuhusu jambo lolote, hata kama hukubaliani nalo, mawazo yake yaheshimiwe!.

Bandiko hili ni kufuatia ukosoaji uliofanywa na Dr. Bashiru, watu wanamshukia kila kona, utadhani amemkufuru Mungu!, kumbe ni ametoa tuu mawazo yake na maoni yake, hata kama haukubaliani naye, heshimu mawazo yake, kama unatofautiana, pangua hoja zake, hoja kwa hoja na sio kwa viroja vya kumshambulia yeye binafsi. Hoja zake zijibiwe au zipingwe kwa hoja!.

Ukimuondoa Rais Nyerere, marais wengine wote waliofuatia, walisifiwa na walikosolewa hadharani, kama Ilivyokuwa kwa Rais Mwinyi, Mkapa, Kikwete, Magufuli na sasa Rais Samia, wote wanasifiwa nav wanakosolewa na hakuna ubaya wowote na ukosoaji sii dhambi, sii kosa!.

Freedom of expression ya haki ya kumpongeza rais, inakwenda sambamba na haki ya kumkosoa rais, hivyo ukosoaji wa Dr. Bashiru, naomba uheshimiwe!.

Ukosoaji Enzi za Nyerere
Kwa vile mimi ni mtu wa mastori mastori ya kimepanda kikashuka, naomba wale wa short and clear muishie hapa na ku jump kwenye cònclusion, wale wa mastori stori, tuendeleeni

Tukawasisitiza watu humu kuwa Rais Samia na yeye ni binadamu, sio malaika!, Rais Samia, sio malaika ni binadamu anaweza kukosea. Tusimlaumu, kumshutumu na kumponda kwa makosa ya kukoseshwa. Tumvumilie tumpe muda

Hivyo kama ilivyo kwenye haki ya kupiga kura, inakwenda sambamba na haki ya kupigiwa kura, vivyo hivyo kwenye haki ya kusifu na kumpongeza rais Samia, haki hiyo ya kumpongeza, inakwenda sambamba na haki ya kumkosoa rais Samia, mkosoaji asishambuliwe yeye, ishambuliwe hoja yake!.

Wapongezaji wa Mama kwa jinsi anavyoupiga mwingi wana haki ya kusifu na kupongeza, ila wanapotokea watu ma critiki, wanaopinga Mama kuupiga mwingi, wapongezaji wasijimilikishe haki za wengine kumkosoa Mama Samia, hivyo kuwashukia wakosoaji as if ni wamemkufuru Mungu kama sasa Dr. Bashiru anavyoshukiwa kama mwewe anavyo sarandia kunyakuwa kifaranga cha kuku!.

Hitimisho
Wanaosifu wasifu kwa hoja, ni haki yao kusifu, lakini pia, wanao kosoa, wakosoe kwa hoja kwa kutumia ukosoaji wa contructive criticism, ukosoaji wenye nia njema ya kujenga, kwa kutumia lugha ya staha na amini usiamini, unaweza kukuta, wanaomkosoa Rais Mama Samia, ndio wanao msaidia kuliko wanaomsifu!.

Wasalaam

Paskali
Paskali mbona sikuelewi, wewe unakataa Chadema wasijieleze na wewe huyohuyo unataka uhuru wa kujieleza uwepo! Unajipa upopo huku ukiwa mwanasheria.
 
Back
Top Bottom