Zanzibar-ASP
JF-Expert Member
- Nov 28, 2013
- 10,431
- 36,063
Embu tuweke ushabiki pembeni, sasa tujadili hili.
Ni kweli rais wetu mpendwa mama Samia ameoneka kwenye msiba wa malkia wa Uingereza akiwa ndani ya basi, na picha mnato ikionyesha kama hakupenda kupigwa ile picha, yaani hakuwa comfortable kivileee!
Sasa kwa namna tulivyozoea kuona akiwa ziara za ndani hapa Tanzania Rais Samia huwa na msururu wa magari ya kifahari, akisindikizwa na helkopita huku shughuli zote za kijamii zikisimama kwenye mazingira ya barabara kwa muda wa saa kadhaa ili kupisha tu msafara wa rais kwa kigezo cha kiusalama. Kwa namna yoyote tukio la kupandishwa basi rais Samia haliwezi kupita bila kujadiliwa. Ni lazima tu tutalijadili tu.
Kama kupandishwa kule basi ulikuwa ni utaratibu wa wenyeji wake huko Uingereza, je Rais Samia alikubaliana nao au alilazimishwa?
Katika mazingira yale, rais wetu alikuwa salama kiasi gani?
Wakati rais Samia yuko kwenye basi, walinzi wake walikuwa wapi?
Mbona kuna marais wengine (sio kutoka Afrika) walikuwa kwenye magari binafsi na misafara maalum, vipi rais Samia ashindwe kupewa msafara wake ikiwa anataka hayo?