Katibu mwenezi wa CCM ndugu Paul Makonda anazinguka nchi nzima akiwa kwenye msafara mkubwa wenye magari mengi ya kifahari na ving’ora utadhani yeye ni kati ya wale viongozi wa juu kabisa wa nchi hii yaani rais, makamu wa rais au waziri mkuu.
Msafara wa Makonda wakati mwingine ni mkubwa kuliko wa waziri mkuu au hata rais!
Makonda akifika aendako watendaji wote wa serkali kama wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi wa mikoa na wilaya., maengineer, na hata mawaziri wanapaswa kuwepo tayari kujibu maswali.
Linaloshangaza ni kwa Makonda kuwaamrisha hao wakuu wa mikoa na mawaziri au hata waziri mkuu kama vile yeye ndiye rais wa nchi!
Utaratibu huu mbovu unaashiria nini?
Inaonekana mama Samia anataka kufanya siasa za Magufuli ila:
Pengine haziwezi,
Hazipendi lakini anajua zitamsaidia,
Au anataka kukwepa lawama zinazotokana na siasa hizo. Kwa ujumla jambo hili linaashiria udhaifu mkubwa wa kiuongozi wa rais Samia na utayari wake kufanya lolote ili mradi mambo yamwendee sawa.
Ukweli ni kwamba viongozi na wananchi wengi wanaghafilishwa na mambo haya ila hawana la kufanya.
Kupitia CCM wananchi wanaendelea kupoteza fedha nyingi na kulishwa maigizo ya kisiasa bila wao kujitambua vizuri wala kupata faida yoyote!