j_h_kirigini
Senior Member
- Dec 31, 2015
- 131
- 56
Habari za muda huu wanajamvi. Naenda moja kwa moja kwenye mada..
Mpaka hivi leo matumizi ya saa janja za mkono (smart watch) yameongezeka sana hapa nchini na maeneo mengine duniani, hali hii imetokana na kuongezeka kwa uelewa juu ya teknolojia inavyoweza kusaidia kwenye maisha ya kila siku.
Lengo la kuandika uzi huu hasa ni kuleta mbele yenu jambo hili linalohusu Kutokuwepo/Kuzuiliwa kwa huduma muhimu nchini zitokanazo na hizi saa janja hasa katika kufuatilia mienendo ya Afya.
Pamoja na kuwepo saa janja nyingi zenye uwezo, nitatumia saa janja za kampuni zinazojulikana za Apple (yaani apple watch) na Samsung (yaani galaxy watch) kutokana na kuwa na ukaribu wa usahihi wa matokeo ya vipimo kulinganisha na matokeo ya vipimo vya vifaa tiba halisi.
APPLE WATCH (saa janja ya kampuni ya Apple)
Huduma za kufuatilia mienendo ya afya zilizozuiliwa kutumika hapa nchini ni kupima Pressure (shinikizo la damu), ECG (electrocardiography), AFib (atrial fibrillation) history na Irregular heart rhythm notifications.
GALAXY WATCH (saa janja ya kampuni ya Samsung)
Huduma za kufuatilia mienendo ya afya zilizozuiliwa kutumika hapa nchini ni kupima Pressure ya damu na ECG. Na hii ni kutokana na kuzuiliwa kwa matumizi ya Application ya Health Monitor kwenye simu za Samsung.
Pamoja na kuzuiliwa kwa huduma tajwa kuna huduma nyingine nyingi zinafanya kazi kwenye saa hizi janja hasa za kampuni tajwa hapo juu. Huduma kama kupima level ya oxygen, stress, activities tracking ya mazoezi mbalimbali, calories, sleep tracking, nk..
MASWALI
Je swala hili limeshazungumzwa sehemu yoyote hapa nchini?
Je ni kwanini huduma hizi zimezuiliwa kutumika hapa nchini ingawa Nchi nyingi duniani wameruhusu matumizi ya huduma hizi? Kama kuna sababu za kitaabibu zilizowahi kutolewa na wasimamizi katika sekta hii mfano. TMDA (msimamizi wa vifaa tiba nchini) naomba tuzifahamu kwa faida ya wengi hapa jukwaani
Nawasilisha..