Sanctus Mtsimbe
R I P
- Jul 14, 2008
- 1,820
- 1,031
Huu siyo wakati wa maazimio japokuwa wazo la TPN ni zuri. Mimi nafikiri watanzania tunahitaji kujikita zaidi ktk utekelezaji wa maazimio lukuki yaliyo kwisha tolewa miaka ya nyuma na yamewekwa kapuni.
Kwa mfano, suala la ku-review mikataba ya madini ambayo imesainiwa wakati wa mwinyi na mkapa linahitaji utekelezaji lakini shangaa kwamba kila mtu yuko kimya.
Kuwa na tume huru ya uchaguzi inayo shirikisha vyama vyote vya siasa, hili nalo linahitaji utekelezaji tu, je wasomi tumefanya nini ktk hili?? au tunaona ni sawa??
Mzalendo Magezi;
Kila issue ambayo kutakuwa na ushahidi wa kutosha na kuna sheria inaruhusu yatafanyiwa kazi. pale ambapo sheria hairuhusu, njia mbadala za kuleta mabadiliko zitatumika.
Kinachotakiwa ni wote kuunganisha nguvu, si wengine wanatenda wengine wako nje wanaangalia. Let us all be part of changes.