Toa maoni yako kwenye first draft ya Katiba, malengo, dira na muundo wa baraza la vijana Tanzania

Jun 10, 2014
30
5
Picture1.png

1.0 UTANGULIZI
Tulipopata uhuru 1961, hapakuwa na sera rasmi ilkiyokuwa inaelekeza nini kifanyike kwa ajili ya maendeleo ya vijana nchini. Takribani miongo mitatu ndipo Sera ya Vijana ikawa imepatikana, lakini Kwa kipindi hiki kirefu miongozo iliandaliwa na kutekelezwa na Serikali. Mwaka 1996 na 2007 serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali iliandaa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya vijana ambayo kwa ujumla wake ilizingatia mambo mengi ya msingi kwa maendeleo ya Vijana. Haki hizi ni pamoja na: Haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa na kujiendeleza, kushiriki na kushirikishwa katika mambo mbalimbali ya maendeleo ya vijana na jamii kwa ujumla wake. Haki zingine ni pamoja na kutobaguliwa, kuheshimiwa, haki ya kumiliki mali, kufanya kazi na kupokea matunda/ujira halali wa kazi aliyofanya pamoja na usawa mbele ya sheria.
Kwa ujumla Sera ilimhakikishia Kijana usawa mbele ya sheria, uhuru na nafasi ya kushiriki na kutumia uwezo wao na vipaji vyao katika shughuli za maendeleo kama uongozi, utamanduni, uzalishaji mali pamoja na kunufaika na huduma za jamii zilizopo katika maeneo yao kwa lengo la kuboresha maisha yao.
1:1 FASILI NA UFAFANUZI Chama cha siasa – Ni kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992. BAVITA – Baraza la Vijana Tanzania. Mwenyekiti – Kiongozi mkuu wa Baraza la vijana Tanzania. Katibu Mkuu – Kiongozi ntendaji mkuu wa Baraza la vijana Tanzania Uongozi wa chama cha siasa - Ni uongozi wa chama cha siasa kwa mujibu wa sheria sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992. Idara – Ni taasisi za kitendaji ndani ya Baraza la vijana Tanzania. Mkutano mkuu- chombo kikuu cha maamuzi katika mambo yote ya Baraza la vijana. Bodi – Ni chombo kinacho angalia kwa ukaribu utendaji wa kamati tendaji ya Baraza la vijana. Kamati tendaji Ni – chombo kikuu cha utendaji wa Baraza la vijana. KUANZISHWA KWA BARAZA LA VIJANA 1) Kutakuwa na Baraza ambalo; i) Litakuwa ni chombo chenye mamlaka, lakili yake, uwezo wa kushitaki na kushitakiwa. ii) Linaweza , katika kutekeleza malengo yake kununua, kumiliki, kutunza na kuuza mali yeyote iwe ni mali inayohamishika au isiyohamishika na inaweza kufunga mkataba na kufanya shughuli yeyote halali kwa mujibu wa sheria. iii) Linaweza kujiunga na mabaraza mengine ya vijana yanayofanana kimalengo ya kikanda au kimataifa. 8 MALENGO
Lengo kuu la Baraza La Vijana Tanzania ni kujenga mawasiliano na mahusiano mazuri kati ya Vijana na Vyombo vya Maamuzi kama Kamati za Maendeleo za Mtaa, Kijiji, Kata, Halmashauri ya Jiji na Bunge kupitia Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana. Baraza litawajengea Vijana moyo wa kujituma, Kuwajibika, kujiendeleza na kujiimarisha katika maeneo yote ya maendeleo ya Jamii na Taifa kwa ujumla. 1. Kuwezesha Vijana kujadili masuala yanayowahusu kama yalivyoelekezwa katika Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana na kutoa mapendekezo na ushauri kwenye vyombo vya Maamuzi. 2. Kutoa Elimu ya Ujasiriamali kwa Vijana ili kukabili changamoto za Ajira kwa Vijana kupitia Midahalo, Warsha, Makongamano na Semina mbalimbali. 3. Kuwajengea Vijana mshikamano wa Kitaifa katika kuleta muamko wa ushirikishwaji katika masuala yanayowahusu, kuwa na Sera bora, kutetea haki za Binadamu, Ulinzi na Usalama katika maeneo yao na Taifa kwa ujumla. 4. Kuwajenga vijana kuutambua utaifa wao hali ya umoja na mshikamano, kujiheshimu na kuifahamu kwa kina jamii kiuchumi halihalisi kiutamaduni na upeo wake.
5. Kufanya kazi kama jukwaa na kiungo wakilishi kwa masuala ya vijana katika Tanzania
6. Kuratibu mipango ya kuwajengea uwezo vijana ilikuwafanya wazalishaji katika jamii
7. Kuwezesha vijana kufikia ndoto zao kimaisha kisiasa, kiuchumi na kijamii kutokana na vipaji walivyojaliwa na Mungu.
8. Bazara kuwa kama mwamvuli wa kuwalinda vijana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika dunia ya utandawazi.
9. Kuwakilisha maslahi ya vijana ndani na nje ya nchi.

9 BARAZA LITAKUWA NA KAZI ZIFUATAZO
a. Kushauri na kushauriana na wizara katika masuala yote ya vijana na mipango ya maendeleo.
b. Kuwezesha upatikanaji wa haki za vijana kupanua wigo endelevu wamaendeleo ikijumuisha sera, kanuni, sheria, mambo ya kimsingi na mipango.
c. Kuwezesha na kuimalisha ushirikiano miongoni mwa jumuiya zilizosajiliwa za vijana kitaifa, kikanda na kimataifa.
d. Kuandaa, kusimamia na kuthaminiwa mipango iliyoanzishwa na vijana ambayo yanaweza kupimwa baadae na jumui ya vijana sambamba na mipango yaTaifa.
e. Kusaidia na kuwezesha vikundi vyenye maslahi na maendeleo ya vijana katika kuanzisha mafunzo kwa vijana na mipango ya maendeleo na utafiti ilikuunga mkono mipango iliyogunduliwa na vijana na kukuza utumiaji wake.
f. Kwakushirikiana na wizara kuandaa nyaraka mbalimbali na kueneza taaluma iliyopatikana na mifano ya matendo ya kuigawa yanayohusiana na mipango ya vijana.
g. Kuhamasisha na kusambaza asilimali katika kuunga mkono utekelezaji wa mipango ya vijanana kuimalisha uwezo vikundi au jumui ya /za vijana.
h. Kuanzisha, kuendesha na kusimamia miradi yenye faida katika kuunga mkono maendeleo ya vijana kama itakavyoonekana inafaa.
i. Kupanga na kuendesha mikutano, semina, workshop, kongamano, mafunzoyabaraza la vijana.
j. Kufanya kazi nyingine zakama ambavyo baraza litaona inafaa kufuatana na malengo yake.
9.0 Katika kuhakikisha kuwa baraza linafanya kazi zake kiufanisi kwa mujibu wa sheria hii baraza litakuwa na uwe zo wa;
a. Kuajiri watendaji wabaraza kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma au sheria nyingine yoyote inayohusiana na hayo.
b. Kuanziasha vitega uchumi au kuzishughulikia fedha ambazo bado hazijahitaji kimatumizi kwa dhamana na katika njia nyingine itakayoonekana inafaa na kubadilisha vitega uchumi hivyo.
c. Kisimamia, kuhakikisha usalama, kukodisha, kuweka rehani au kwa njia nyingine kuzifanyia kazi mali za baraza kwa mujibu wa sheria zilizopo na taratibu za nchi.
d. Kupokea michango au riba iwenifedha au mali nyingine kutoka kwa mtu au taasisi kwa ajili ya kuendeleza utekelezaji wa malengo yake isipokuwa pale ambapo mtu au taasisi hiyo wanajihusisha na malengo yaliyokinyume na sheria au yaliyokinyume na maadili.
e. Kutangaza kila baada yamuda umahili au maelezo mengine ambayo yataonekana ni muhimu kwa ajili yakuyatukuza malengo ya baraza.
f. Kudhibitisha na kuidhinisha mipango ya vijana.
Waziri anaehusika na vijana anaweza kutoa maelekezo na ushauri kwa baraza kuhusiana na utekelezaji wa kazi itakapotokea umuhimu wa maslahi ya vijana

9.1.5 DIRA YA BARAZA LA VIJANA NI
Kuwa na jamii ya Vijana wanaoishi kwa usawa na kuyafikia malengo yao na mahitaji yao ya msingi bila kubaguliwa 9.1.6 DHAMIRA YA BARAZA LA VIJANA Kuona Vijana wanafikia ndoto zao za kimaisha na kuwa na sauti ya pamoja katika kusaidia upatikanaji wa huduma za jamii kwa vijana. 9.1.7 UANACHAMA [UJUMBE] Ujumbe utakuwa wa wazi kwa Kijana yeyote bila kujali Kabila, Dini na usajili utakuwa ngazi ya mtaa au kijiji isipokuwa Asasi za vijana. Masharti na vigezo vya jumla vya Uanachama: v Awe na umri kuanzia miaka 15 hadi 35 v Apige vita Ukabila, Udini, Rushwa na Ubaguzi wowote v Asiwe kiongozi wa chama cha siasa ngazi yoyote v Awe Mzalendo, mtetezi wa Amani na Utaifa v Awe na akili timamu v Awe tayari kuitetea Katiba ya Baraza La Vijana Tanzania v 9.1.8 HAKI NA WAJIBU WA MJUMBE WA BARAZA LA VIJANA v Kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu madhumuni ya Baraza La Vijana Tanzania v Kutekeleza na kuielewa Katiba ya Baraza La Vijana Tanzania v Kutetea na kusimamia Haki na Amani popote awapo v Kujiepusha na vitendo vya ushabiki wa Vyama vya Siasa, Dini, Ukabila katika kutekeleza shughuli za baraza 9.1.9 KUACHA / KUKOMA KWA UANACHAMA Mwanachama ataacha Uanachama kwa: v Kujiondoa mwenyewe kwa hiari na kutoa taarifa kwa barua katika Ofisi za Baraza la vijana eneo husika v Kuondolewa kwa kukiuka Katiba ya Baraza La Vijana Tanzania v Kiongozi wa Baraza Kujihusisha na harakati za Vyama vya Siasa wakati bado ni Kiongozi wa Baraza La Vijana v Ubadhirifu wa mali au Fedha za Baraza La Vijana v Kifo v Endapo mwanachama atafikisha umri zaidi ya miaka 35. Kiongozi anayeacha Uanachama aidha kwa kufukuzwa, wizi au matumizi mabaya ya mali za Baraza La Vijana Tanzania atafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili kurudisha au kushtakiwa na kufungwa Jela. 9.2.0 HAKI ZA MWANACHAMA WA BARAZA LA VIJANA TANZANIA v Kushiriki vikao vya Baraza vinavyomuhusu na kutoa mawazo yake kwa uhuru na uwazi v Kujitetea, kusikilizwa na kukata rufaa anaposhitakiwa au kuchukua hatua za kinidhamu. 9.2.1 UONGOZI Baraza La Vijana Tanzania litaongozwa na Viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa. 9.2.2 SIFA MAHUSUSI ZA KILA KIONGOZI WA BARAZA v Elimu ya Msingi na kuendelea
v Umri kuanzia miaka 18 – 35
v Mwaminifu na mwadilifu
v Uwezo wa kutafsiri mambo yahusuyo sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana kwa ufasaha.

v Moyo wa kujituma na kujitolea kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa na ya Baraza La Vijana dhidi ya maslahi binafsi.
v Awe na historia ya kukubalika na uadilifu katika jamii, hii ina maanisha amekuwa mwanachama kwa muda wa kutosha ndani ya Baraza na kujijengea historia hiyo au tayari anayo sifa hiyo ndani ya jamii.
v Aonyeshe tabia na mwenendo wa uzalendo wa kupenda nchi yake na kuitetea.
v Awe na uzoefu katika masuala ya uongozi wa jumuiya mbalimbali katika jamii.
v Adhihirishe mapenzi yake na imani yake kwa Baraza na wanachama kwa juhudi na vitendo vyake kuendeleza kukuza Baraza
v Awe na msimamo wa kuaminika.
v Aonyeshe uzoefu wa kuwa tayari kushirikiana na wenzake na uzoefu wa kufanya kazi na vikudi mbalimbali ndani ya jamii.
v Kuwa na njia halali za mapato yake ya kujitosheleza kwani uongozi wa Baraza ni wa msingi wa kujitolea isipokuwa viongozi waajiliwa.
v Adhihirishe kuwa na nidhamu na utii kwa kutekeleza maagizo au maelekezo ya vikao vya Baraza na uongozi wa baraza.
v Akubali kukosoa na kukosolewa au kuelekezwa na awe tayari kujirekebisha.

9.2.3 MIIKO YA UONGOZI v Asiwe mtumishi wa chombo chochote cha dola. v Asiwe amewahi kushitakiwa au kuadhibiwa kwa makosa ya jinai v Asiwe kiongozi wa chama chochote cha siasa. 9.2.4 UENDESHAJI WA BARAZA Kutakuwa na: v Mkutano mkuu, v Kamati ya utendaji, v Idara za utendaji za Baraza la Vijana Tanzania, 9.2.5 MKUTANO MKUU
Ni chombo chenye maamuzi ya mwisho katika uendeshaji wa majukumu ya Barazaa ambayo ni:- v Kuchagua Viongozi wa Baraza la vijana Tanzania v Kuidhinisha uundwaji wa idala mpya za Baraza la vijana. v Kuandaa na kupitisha mikakati ya Baraza la vijana. v Kupokea na kupitia ripoti ya kila mwaka ya utendaji wa Baraza la vijana kutoka kamati Tendaji. v Kubadili au kurekebisha Katiba v Kupokea taarifa kutoka katika Kamati mbalimbali v Kuridhia majina ya wajumbe wa bodi ya baraza la vijana Tanzania v Kumwajibisha kiongozi yoyote ikiwa pamoja na kumvua uongozi kiongozi yoyote ndani ya Baraza kwa kukiuka misingi na kanuni za Baraza la vijana.
9.2.6 UENDESHAJI WA MKUTANO MKUU v Utafanyika mara moja kwa mwaka v Utaitishwa na Katibu Mkuu baada ya kushauriana na Mwenyekiti v Maamuzi ya kikao yatafikiwa iwapo zaidi ya 50% ya Wanachama watapiga kura za kukubali au kukataa v Utaongozwa na Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti, Mjumbe/Mwanachama atakayeteuliwa na Wanachama wakati wa mkutano ikiwa watajwa hapo juu hawatakuwepo kwa kutoa taarifa. v Unaweza kuitishwa wakati wowote kwa dharura,ikiwa aliyechaguliwa na mkutano huu amefariki,amejiudhuru au amefukuzwa n.k. utaitishwa ndani ya miezi mitatu [3] 9.2.7 KAMATI YA UTENDAJI Itaundwa na Katibu Mkuu, Wakuu wa Idara zote za Baraza na Mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Mwenyekiti kutoka kila Idara za Baraza La Vijana au Asasi za vijana. KAZI YA KAMATI ZA UTENDAJI: v Kusimamia shughuli za kila siku za Baraza La Vijana v Kuratibu shughuli zote za Wajumbe v Itasimamia uandikishaji wa Wajumbe v Itawawajibisha Wajumbe wanaokiuka Katiba ya Baraza v Itatoa ripoti maalum kuhusu semina, warsha na makongamano yaliyoendeshwa na Baraza kwenye mkutano mkuu wa baraza v Itasimamia matumizi na mapato kwa kushirikiana na Idara ya fedha na Utawala v Kuandaa na kufanikisha mikutanao na Wadau v Itakutana mara moja kwa mwezi 9.2.8 VIONGOZI Kutakuwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu. v Watachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Baraza La Vijana v Watakuwa madarakani kwa miaka minne [4], wanaweza kuchaguliwa tena lakini sio zaidi ya awamu mbili [2]. v Makamu Mwenyekiti ataendesha mikutano ikiwa Mwenyekiti hayupo v Mwenyekiti na Makamu ikiwa hawapo Baraza la Vijana litateua Mwenyekiti wa muda 9.2.9 MUUNDO WA BARAZA LA VIJANA TANZANIA

1. 9.2.9 Baraza la vijana ngazi ya kijiji au mtaa.
Baraza la vijana litaazia ngazi ya kijiji au mtaa ili kuwepo uwakilishi halisi wa vijana kuanzia ngazi ya chini kabisa.
a] Kila kijana ambaye ni raia wa Tanzania na ametimiza umri wa miaka 15 na ana umri chini ya miaka 35 na ni mkazi wa kijiji au mtaa atakuwa ana haki ya kusajiliwa kwenye daftari maalum la baraza la vijana la kijiji au mtaa.
b] Kiongozi wa chama cha siasa hatasajiliwa kama mwanachama katika daftari la baraza la vijana kwenye mtaa au kijiji.

8.2 Baraza la vijana ngazi ya kata.
a] Wajumbe wa mkutano mkuu baraza la vijana ngazi ya kata ni wajumbe wote waliosajiliwa katika daftari ngazi za mitaa au vijiji vya kata nzima.
b] Kutakuwa na viongozi wa baraza la vijana ngazi ya kata.
i. Mwenyekiti.
ii. Makamu mwenyekiti.
iii. Katibu.
iv. Mweka hazina.

9.3.0. Baraza la vijana ngazi ya wilaya.
a] Wajumbe wa mkutano mkuu wa baraza la vijana ngazi ya wilaya ni viongozi wote wa kata na wawakilishi wawili kwa usawa wa kijinsia kutoka kila kata na mwakilishi wa vijana kwenye halmashauri, viongozi wa dini
i. Mwakilishi kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya .
ii. Wawakilishi wawili wa walemavu.
iii. Kutakuwa na uwakilishi wa mjumbe mmoja kutoka kila wilaya kwenye halmashauri kwa utaratibu wa uchaguzi kwenye mkutano mkuu wa wilaya wa baraza la vijana

b] Kutakuwa na viongozi wa baraza la vijana ngazi ya wilaya.
iv. Mwenyekiti.
v. Makamu mwenyekiti.
vi. Katibu .
vii. Mweka hazina.

8.4 .Baraza la vijana ngazi yaTaifa.

a] Wajumbe wa baraza la vijana Taifa watakuwa wafuatao:

i. Wawakilishi wawili kutoka kila wilaya ambapo mwenyekiti wa wilaya atakuwa mjumbe kwa nafasi yake katiyawawakilishiwawili.
ii. Wawakilishi wawili kutoka jumuiya ya wanafunzi elimu ya juu. Mwenyekiti wajumuiya atakuwa mjumbe kwa nafasi yake.
iii. Wawakilishi 5 wa walemavu
iv. Wawakilishi wa asasi iliyosajiliwa na baraza la vijana kwa vigezo vilivyowekwa vya usajili waasasi kwenye baraza.
v. Uwakilishi viongozi wa dini
vi. Wawakilishi 2 kwenye bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
vii. Wawakilishi wawili kwa usawa wa kijinsia kutoka kila mkoa wa Zanzibar

b]Kutakuwa na viongozi wa baraza la vijana ngazi ya Taifa.
i. Mwenyekiti.
ii. Makamu mwenyekiti.
iii. Katibu. mkuu
iv. Wakuu wa idala.
v Idalaya sera na utafiti.
v Idala ya fedha za uchumi.
v Idala ya habari na elimu.
v Idala ya sheria na haki.

9.3.1 MWENYEKITI
Mwenyekiti atachaguliwa na mkutano mkuu na atakuwa madarakani kwa miaka minne [4]

KAZI ZA MWENYEKITI v Mwenyekiti ni msimamizi mkuu wa shughuli zote za uendeshaji wa Baraza La Vijana v Mwenyekiti wa vikao vyote vya mikutano ya Baraza v Mfafanuzi na msuluhishi mkuu wa migongano na migogoro na matatizo ya ndani ya Baraza La Vijana v Atakuwa Msemaji Mkuu wa Baraza la Vijana 9.3.2 MAKAMU MWENYEKITI Mwenyekiti wa baraza la vijana Zanzibar ndiye atakuwa makamu mwenyekiti wa Baraza la vijana Tanzania na atakuwa madarakani kwa miaka minne [4] KAZI ZA MAKAMU MWENYEKITI v Msaidizi wa Mwenyekiti v Atafanya kazi za Mwenyekiti iwapo Mwenyekiti hatakuwepo. 9.3.3 KATIBU MKUU Atakuwa Mtendaji mkuu wa Baraza La vijana Tanzania, atateuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na kumwapisha na atakaa madarakani kwa miaka minne [4] KAZI ZA KATIBU v Mtendaji na Mtekelezaji Mkuu wa shughuli zote zilizoamriwa na Baraza la Vijana Tanzania v Mtoaji na mtunzaji wa kumbukumbu zote zinazohusu Baraza la Vijana Tanzania v Muandaaji wa Mikutano yote baada ya kuandaa Agenda kwa kushauriana na Mwenyekiti v Msimamizi wa Idara zote ndani ya Baraza la vijana Tanzania v Mwajibikaji wa kwanza katika masuala yote yanayohusina na fedha au mali za Baraza 9.3.4 BARAZA LA VIJANA LITAKUWA NA IDARA. Ili kulifanya baraza linakuwa taasisi inayojishughulisha na masuala ya vijana kila siku na kutekeleza malengo ya baraza la vijana Tanzania litakuwa na idara za kitendaji: 9.3.5 IDARA YA FEDHA NA UCHUMI Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ambaye atateuliwa na mwenyekiti kwa kushauriana na Katibu Mkuu wa Baraza na atawajibika moja kwa moja kwa Katibu Mkuu wa baraza kwa shughuli zake za kila siku za Idara nzima. A) IDARA YA FEDHA NA UCHUMI ITAKUWA NA WAJUMBE WAFUATAO:
i) mkurugenzi wa idara. ii) Mweka hazina iii) Afisa mikopo kwa vijana iv) Afisa ujasiriamali kwa vijana KAZI ZA IDARA YA FEDHA NA UCHUMI
v Kutunza kumbukumbu zote za fedha zitokazo na kuingia katika akaunti za Baraza la Vijana v Kutoa taarifa za fedha kwa Kamati Tendaji v Kukusanya viingilio, ada na vyanzo vingine vya mapato au mali ya Baraza v Mtayarishaji wa maombi ya fedha yanayohitaji kuidhinishwa na waweka saini benki wa Baraza v Kushirikiana na Idara ya Sera na mipango kubuni mikakati itakayoingizia fedha Baraza v Kusimamia mambo yote yanayohusu ukusanyaji wa ada, michango na misaada kutoka kwa Wafadhili na Wahisani mbalimbali. v Kutoa na kusimamia mikopo kwa vijana v Kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana v Kutoa elimu ya mikopo na ulejeshaji kwa vijana v Kubuni vyanzo vipya vya mapato vya baraza. 9.3.6 IDARA YA SERA NA MIPANGO Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi wa Idara amabaye atateuliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Tanzania kwa kushauriana na Katibu Mkuu. Atawajibika moja kwa moja kwa Katibu mkuu wa baraza kwa shughuli zake za kila siku za uendeshaji wa Idara nzima. A) WAJUMBE WA IDARA WATAKUWA WAFUATAO. i) mkurugenzi wa idara ii) Afisa vijana masuala ya wanafunzi iii) Afisa vijana masuala ya wafanyakazi iv) Afisa vijana masuala ya michezo, sanaa na vipaji KAZI ZA IDARA YA SERA NA MIPANGO Ø Kutafuta na kuchambua Sera, Miswada na Tafiti mbalimbali zinazohusu masuala ya Vijana Ø Kubuni njia, mbinu au mikakati ya kuwasilisha matokeo ya uchambuzi wa Sera na Mapendekezo kwenye vyombo vya Maamuzi kwa ajili ya utekelezaji Ø Kushirikiana na Idara ya Fedha na Uchumi katika kubaini miradi ya fedha za Baraza Ø Kufanya utafiti juu ya masuala mbalimbali ya Vijana au changamoto zinazowakabili Nchini na kutoa mapendekezo juu ya utafiti husika kwa Serikali au Taasisi zinazohusika na kushughulika na Vijana Ø 9.3.7 IDARA YA HABARI NA ELIMU Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ambaye atateuliwa na Mwenyekiti kwa kushauriana na Katibu Mkuu wa Baraza Atawajibika moja kwa moja kwa Katibu Mkuu wa Baraza kwa shughuli zake za kila siku za Idara nzima. A) WAJUMMBE WA IDARA WATAKUWA WAFUATAO i) Mkurugenzi wa idara ii) Afisa habari iii) Afisa Elimu mtambuka na utamaduni iv) Afisa wa vijana masuala ya kiroho KAZI ZA IDARA YA HABARI NA ELIMU Ø kusambaza Sera, mipango na taarifa mbalimbali za masuala yanayohusu vijana Ø Idara inayohusika na masuala yote ya habari na taarifa ya Baraza la vijana Tanzania. Ø Kusambaza vipeperushi, majarida, magazine na viandikwa vingine vya Baraza Ø Kusambaza taarifa na Kuandaa Itifaki na matayarisho ya warsha, kongamano na mikutano mbalimbali ya Baraza Ø Kuandaa na kusambaza taarifa za utafiti na uchambuzi wa sera kwenye masuala yahusuyo Vijana kwa vijana wote Ø Kuunda na kusimamia utunzaji wa Maktaba ya Baraza 9.3.8 IDARA SHERIA NA HAKI Idara hii itaongozwa na mkurugenzi ambaye atateuliwa na mwenyekiti kwa kushauriana na katibu mkuu wa Baraza kwa kuzingatia sifa na taaruma za kuongoza idara akisaidiwa na wajumbe watakaoteuliwa. KAZI ZA IDARA YA SHERIA NA HAKI Kazi za idara ya sheria ni kushughulikia masuala yote kisheria ndani ya baraza kwa vijana na kusimamia mikataba ya baraza la vijana. 10 9.3.9 BODI YA BARAZA LA VIJANA TANZANIA § Itaundwa na Wajumbe wasiozidi kumi na wasiopungua sita na ndio chombo cha pili kwa maamuzi baada ya Mkutano Mkuu § Itakaa kila baada ya miezi mitatu [3] na itaongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ambaye atachaguliwa na Wajumbe wa Bodi kutoka miongoni mwao
§ Mwenyekiti wa Baraza atakuwa Katibu wa Bodi na Katibu Mkuu wa Baraza atakuwa Mjumbe wa Bodi kwa wadhifa wake lakini hatakuwa na haki ya kupiga kura kwenye maamuzi ya Bodi.
KAZI ZA BODI YA BARAZA LA VIJANA TANZANIA
§ Kujadili Ajenda zilizopendekezwa na Kamati tendaji kabla ya kuzipeleka kwenye Mkutano Mkuu wa baraza La Vijana § Kupitia Utendaji wa Baraza la Vijana Tanzania § Kuitisha na kuthibitisha majina ya Wanachama wapya kila mwaka 9.4 .0 TAASISI SHIRIKI
9.4.1 – (1) Taasisi zinazoongozwa na vijana,kikundi au taasisi za vijana ,zenye
a) Nia na malengo ya kuendeleza ustawi wa vijana na
b) Kuendana na malengo ya sharia hii,vitakuwa huru kujiunga kama vyama shiriki
(2) Taasisi ya vijana ambayo inataka kujiunga kama tasisi shiriki chini ya kifungu cha 9.4(I) itatakiwa:-
a) Iwe katika ngazi ya Taifa na iwe na uwakilishi angalau katika mikoa kumi ya Tanzania bara
b) Kuambatanisha idadi ya wanachama wake waliosajiriwa na mfumo wa uongozi wake;
c) Uanachama uwe wazi kwa watanzania wote bila kujali rangi zao,makabila ,jinsia au dini.
d) Kuwakilisha kwa katibu mkuu maombi ya kujiunga katika fomu maalum na kwa utaratibu uliowekwa na kuambatanisha katiba,Kanuni,sharia nyingine za kimataifa zinazotumia kama zipo pamoja na mpoango wake wa kazi.
(3) Baada ya kupokea maombi yaliyotajwa katika kifungu cha 9.4(2)kamati tendaji itayapitia na kutoa mapendekezo kwa bodi.
(4) Baada ya kuzingatia yaliyo wasilishwa pamoja na mapendekezo ya kamati tendaji kwa mujibu wa kifungu cha 9.4(30 Bodi inaweza kuidhinisha au kutupilia mbali maombi yaliyowasilishwa
(5) Endapo bodi itajiridhisha kwamba
a) Katiba ya taasisi au kikundikilichowasilisha maombi,kanuni na sharia nyingine zake ni nakala halisi na hazipingani na sharia hii;
b) Kwa kuona usajili wake wanachama wa mwombaji wanaomba kwa nia njema na kwa manufaa ya uanachama na kikundi au taasisi.
c) Uanachama wa kikundi kinachoomba uko wazi kwa watanzania wote bila kujali rangi,kabila,jinsia au dini, na
d) Bodi itaidhinisha maombi yaliyowasilishwa na kukiandikisha taasisi au kikundi kama kikundi shiriki,baada ya kulipa ada ya kiingilio na ada ya uanachama kama itakayokuwa imepangwa kwa ajili hiyo.
(6) Endapo kikundi shiriki kitafanya marekebisho katika katiba kanuni au Sheria nyingine inayoongoza taasisi au kikundi hicho, kikundi hicho kitatakiwa kuwasilisha marekebisho hayo mapema itakavyowezekana kwa katibu Mkuu ili kuweza kusajili mabadiliko hayo
(7) Taasisi au kikundi shiriki baada ya kuandikishwa na baraza kama mshiriki kinaweza kupata ruzuku kutoka Baraza
(8) Baraza litatunza kumbukumbu na uandikishwaji wa mshiriki.
(9) Kumbukumbu zinazotajwa katika kifungu cha 9..4(8) zitakuwa wazi kwa ajili ya kukaguliwa na mtu yeyote katika ofisi ya baraza bila gharama yeyote,kwa utaratibu utakaowekwa na kamati tendaji
9.5.1 - (1) Kila mshiriki anayepokea ruzuku kutoka baraza atatakiwa kuwasilisha kwa baraza, si zaidi ya miezi sita baada ya mwaka wao wa fedha –
a) Taarifa ya shughuli katika kipindi hicho cha mwakawa fedha;na
b) Ripoti ya ukaguzi inayonyesha mapato na matumizi kwa mwaka huo wa fedha.
(2) Kila taasisi shiriki inayokea ruzuku toka kwa Baraza itatakiwa kuwasilisha,kabla ya kuisha kwa mwaka wa fedha taarifa ya matumizi ya ruzuku hiyo, makadilio ya mapato na matumizi kwa kipindi cha mwaka unaofuata pamoja na mpango kazi.
(3) Endapo katibu Mkuu ataona kwamba makadilio yaliyowasilishwa kwa mjibu wa kifungu kidogo cha (2) hayana maslahi kwa mjibu wa sharia hii,atapeleka taarifa kwenye bodi
(4) Endapo taarifa itatolewa kwa bodi kwa mujibu wa kifungu cha 9.5(3) bodi,baada ya kusikiliza utetezi wa kikundi shiriki,inaweza kukitaka kikundi hicho kuyafanyia marekebisho makadirio hayo.
VIFUNGU VINAVYOHU MFUKO WA BARAZA LA VIJANA
9.5.6.-(1) Kutakuwa na mfuko utakaojulikana kwa jina la mfuko wa maendeleo ya vijana na malengo yake ni kugharamia shughuli za baraza la vijana la Taifa mipango ya baraza na kutekeleza miradi ya vijana na kwa ajili ya maendeleo ya vijana
(2) Fedha za Mfuko zitatokana na-
a) Fedha itakayotafutwa na vijana kutoka katika vyanzo vyake vya mapato kama vile mauzo ya bidhaa zake,au fedga zitakazopatikana kutokana mipango yake au huduma ambayo vijana wataitoa
b) Faida itakayo patikana kutokana na uwekezaji utakaofanywa na baraza
c) Michango au misaada itakoyopokelewa na baraza kutoka sehemu mbalimbali kwa uhakiki wa waziri anayehusika na
d) Fedha halali itayopokelewa kutoka vyanzo vingine
(3) Mfuko utaratibiwa na kusimamiwa na kamati tendaji kwa kuzingatia makadilio ya mapato na matumizi yanayoandaliwa na kamati tendaji na kupitishwa na waziri kwa kuzingatia mahitaji ya kila mwaka wafedha wa baraza.
(4) Hakuna matumizi yatakayofanyika kutoka kwenye mfuko wa baraza isipokuwa kwa kufuata masharti ya kifungu cha 9.5.6(3)
(5) Kamati tendaji itafungua na kutunza akaunti ya Benki itakayokuwa na jina la mfuko katika taasisi ya benki au katika tasisi ya kifedha iliyosajiliwa kujishughulisha na masuala ya kiffedha kwa mujibu wa sharia zinazoongoza taasisi za fedha kwa Tanzania.
a) Akaunti hiyo itatumikakwa kutunzia fedha zote za baraza zilizopokelewa kwa niaba ya baraza na kwa manufaa ya baraza kwa mujibu wa sharia hii na sharia nyingine.
b) Akaunti hii itatumika kufanya malipo ya-
i. Matumizi yote yanayousiana na utendaji kazi wa baraza
ii. Kiasi chochote ambacho mfuko huu unapaswa kulipa kwa mujibu wa sharia hii
c) Hakutokuwa na fedha itakayotolewa isipokuwa tu kwa njia ya hundi au njia nyingine rasmi kama itakavyotakiwa sahihi na mtu au watu waliodhinishwa na kamati tendaji
(6) Kamati tendaji ,katika namna ambayo itaidhinishwa na waziri inaweza kuwekeza kiasi kinachotoka kwenye mfuko kilchowekwa benki ambacho hakihitajiki kwa matumizi ya karibuni
(7) Kamati tendaji kwa kuzungatia maombi yatakayo wasilishwa kwake au kwa kuanzisha yenyewe kama itakavyoamua inaweza kutoa msaada wa kifedha kutoka katika mfuko wa baraza la vijana kwa mtu yeyote, klabu ya vijana muunganiko wa vijana au utaratibu ulioko katika kifungu cha 9.5.6(1)
(8) Kwa ajili ya kutoa fedhakama ilivyoainishwa katika kifungu cha 9.5.6(7) kamati tendaji inaweza kuhitaji kutoka kwa mlengwa.
a) Vielelezo na taarifa kama ambavyo kamati tendaji itaitaji au
b) Vitabu,vielelezo,nyaraka,maelezo na kumbukumbu kulingana na jinsi ambavyo kamati tendaji itahitaji
(9) Kamati tendaji inaweza ikahitaji kutoka kwa mlengwa wa msaada wa kifedha chini ya 9.5.6(7) kutoa-
a) Taarifa na vielelezo
b) Vielelezo,maelezo au kumbukumbu kuhusiana na fedha ambazo kamati tendaji itampatia au kama kamati tendaji itakavyoamua.
(10) Kiasi chochote ambacho kitakuwa hakijatumika ndani ya mfuko kufikia mwisho wa mwaka wa fedha wa baraza itachukuliwa kuwa ni fedha za mwaka ujao wa fedha.
9.5.7.-(1) Mwaka wa fedha wa baraza utaanza kila tarehe 1Julai na utaisha tarehe 31Julai ya kila mwaka
(2) Kamati tendaji itawajibika kutunza nyaraka zinazohusiana na hesabu na taarifa za fedha zinazohusiana na shughuli za baraza ili kuliwezesha muda wowote,kuwasilisha taarifa za malipo na manunuzi ya baraza
(3) Mapema kadiri itakavyowezekana kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha ila siyo zaidi ya kipindi cha miezi mitatu .kamati tendaji
a) Itawajibika kuandaa-
i. Taarifa ya fedha inayohusu mwaka huo wa fedha;na
ii. Kutoa taarifa juu ya maendeleo na shughuli za baraza kwa kipindi hicho cha mwaka huo
b) Itawasilisha taarifa za mahesabu na taarifa za fedha kwa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa ajiri ya ukaguzi
(4) Mkakuzi mkuu wa hesabu wa hesabu za serikali baada ya kufanya ukaguzi atatoa hati,na taarifaa ya ukaguzi ,kwa mujibu wa sharia na kanuni za ukaguzi na sharia hii,ambayo itaasilishwa kwa waziri kwa ajili ya kuwasilishwa bungeni na nakala ya ripoti hiyo itapelekwa kwa kamati tendaji
9.5.8.-(1) Fedha iliyotengwa kwa ajili ya mfuko itatumiwa na baraza kulingana na matakwa yaliyoidhinishwa katika kifungu cha9.5.6(3) na kutumika pia katika
a) Mipango,miradi na shughuli nyingine za baraza
b) Kazi za kamati tendaji na

c) Utawala wa mfuko
(2) Kiasi chochote cha fedha kitakachokuwa kimetolewa na benki kwa matakwa ya kifungu 9.5.6(1)au mali ya baraza kama itakavyokuwa imeoneshwa itatmika kama ilivyokusudiwa na matarajio ya matumizi hayo yataoneshwa

9.5.9.(a) Kutakuwana siku itakayojulikana kama siku ya taifa ya vijana ambayo itatanguliwa na juma la Taifa la Vijana
c) Siku na juma la Taifa la vijana linalotajwa kwenye kifungu 9.5.9(a) litaamuliwa na Baraza na itaidhinishwakama itakavyopangwa na Baraza
9.6.0.-(1) Waziri,kwa kushauriwa na kamati tendaji,anawezakutangeneza kanuni zinazohusiana na-
(a) Fomu ya maombi,vyeti vya uandikishaji unaofanywa,kutolewa au kutunzwa kwa mujibu wa
(b) Jambo lolote ambalo waziri anatakiwa au anaruhusiwa kufanya kwa mujibu wa sharia hii
(c) Jambo lolote ambalo ni muhumu ili kufanikisha malengo ya sharia hii kufanya kazi
(2) Kanuni zitakazotengenezwa chini ya kifungu cha 9.6.0(1) zinaweza kutaja adhabu ya kuzikiuka.
(3) Kamati tendaji kwa idhini ya waziri inaweza kutengeneza taratibu zinazousiana na:-
(a) Maswala ya wafanyakazi
(b) Mpangilio na utunzaji wa vitabu vya hesabu na utawala wa mfuko wa baraza
(c) Utaratibu wa uchaguzi utakaofanywa na mkutano mkuu na mifumo tawala
(d) Uchaguzi na mwenendo wa taasisi au vikundi shiriki kwa baraza na taratibu za kuwasilisha
Taarifa

(e) Namna na utamaduni ambavyo siku na juma la vijana la Taifa litazingatiwa na kuadhimishwa.
9.1.6 MALIPO YA VIONGOZI § Uongozi na wadhifa wowote atakaopewa Mjumbe wa Baraza la Vijana kuanzia ngazi ya wilaya kushuka chini. Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, mweka hazina na uwakilishi mwingine ni kazi ya kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya Vijana isipokuwa katibu wa wilaya atakuwa mwajiliwa wa baraza § Hivyo Wajumbe wataamua kwa kujadiliana uwezekano wa kuwapa posho kulingana na uwezo wa rasilimali za Baraza kwa kuangalia umuhimu wa kazi zinazofanyika na mazingira ya kazi hizo.
9.1.7 WAWEKA SAINI WA JUVITA KATIKA BENKI 1. Katibu Mkuu atakuwa mmoja wa waweka saini 2. Mkuu wa Idara ya fedha na uchumi 3. Mwanachama/Mjumbe mmoja atakaechaguliwa katika Mkutano Mkuu wa baraza la vijana. 9.1.8 TARATIBU ZA KUTATUA MIGOGORO NDANI YA BARAZA Kutakuwa na Kamati ya muda ya kuratibu shughuli za kutatua migogoro. Kamati itaongozwa na Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti. Kutakuwa na taratibu katika kuchukua hatua za kinidhamu kwa Mwanachama yoyote atakaekiuka Katiba na kuleta mgogoro ndani ya Baraza Kabla ya Mwanachama hajachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kuonywa, kuachishwa Uanachama kwa muda ama kufukuzwa kabisa uanachama, atakuwa na haki ya: a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili [2] baada ya kujulishwa. b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao husika c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao wiki mbili [2] baada ya kusikilizwa. d) Mwanachama aliyewahi kufukuzwa ama kuachishwa uanachama anaweza kuomba kurejea kwa maandishi kupitia ngazi iliyomfukuza akieleza sababu za marekebisho yake na kutaka kurejea. e) Kiongozi yoyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashtaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashtaka hayo kwa maandishi. f) Kiongozi mwenye mashtaka, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujitetea bayana mbele ya kikako cha Mamlaka ya Nidhamu.
g) Kiongozi atakayeadhibiwa atapewa taarifa ya msingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumuwezesha kupata nafasi ya kukata rufaa ikibidi.
h) Mwadhibiwa atakayeamua kukata rufaa atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini [30] baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu. i) Baada ya kutoa uamuzi, Kikao husika kitaandaa taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha mwenendo huo kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza baada ya kupitia kwenye Bodi ya Baraza la vijana Tanzania 9.1.9 TARATIBU ZA UCHAGUZI WA NAFASI ZA UONGOZI 1) Kamati Tendaji ndio chombo kinachoainisha ratiba ya uchaguzi ndani ya Bazara, ratiba itaonyesha pia tarehe ya kuwasilisha rufani 2) Ratiba ya uchaguzi ndani ya Baraza itatolewa siyo chini ya miezi sita [6] kabla ya uhai wa kamati tendaji ya uongozi inayomaliza muda wake. 3) Kamati tendaji itaiwasilisha ratiba ya uchaguzi kwenye bodi ya Baraza ili kuipa nafasi bodi ya Baraza kuunda kamati ya uchaguzi ya watu watano (5) ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia uchaguzi tu na baada ya uchaguzi kuisha nayo itavunjika.
4) Mwenyekiti na katibu wa kamati ya uchaguzi watachaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe na wajumbe wenyewe. 5) Wagombea watajaza fomu za maombi ambazo zitatayarishwa na kamati tendaji fomu hizi zitalenga kupata taarifa kamili ya mwombaji ili kuviwezesha vikao vya uteuzi kumwelewa kumtathimini mgombea. 6) Mwanachama yoyote hataruhusiwa kugombea nafasi zaidi ya moja na atakuwa na kadi yake wakati atakaposhiriki kwenye vikao vya Baraza kwa ajili ya kuhakiki uhalali wa uanachama wake.
7) Wanaoomba nafasi za ukuu wa idara watapaswa kujaza fomu maalum zitakazotayarishwa na kuzifikisha kwa katibu mkuu naye atawasilisha fomu zote kwa mwenyekiti atakapofanya uteuzi wa wakuu hao kwa taratibu zitakazokubaliwa na Baraza. 8) Upigaji wa kura utakuwa wa siri na karatasi maalum zitatumika kwa shughuli hiyo.
9) Matokeo yatatangazwa baada ya uchaguzi kukamilika. 10) Mgombea yeyote asiyeridhika na matokeo ya uchaguzi ataruhusiwa kuwasilisha malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa nafasi aliyogombea kwa Kamati ya Rufaa.
9.1.10 KAMATI YA RUFAA 1) Itakuwa na Wajumbe watano [5] ambao watachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Baraza. 2) Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Rufaa watachaguliwa kutoka miongoni mwa Wajumbe na Wajumbe mwenyewe kwa kupigiana kura.
3) Itakuwa na jukumu la kupokea, kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya rufaa ya uchaguzi itakayokuwa imewasilishwa kwenye Kamati hiyo. 4) Kamati ya Rufaa ndio itakuwa yenye maamuzi ya mwisho kwenye masuala yanayohusu uchaguzi.
9.6.6 MAREKEBISHO YA KATIBA 1) Mapendekezo juu ya mabadiliko yoyote ya Katiba yatafanywa na Kamati tendaji kwa kuwasilishwa kwenye Bodi na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Baraza la vijana. 2) Katiba hii inaweza kubadilishwa na Mkutano Mkuu wa Baraza la vijana baada ya theluthi mbili ya Wajumbe kukubali mabadiliko hayo ya Katiba 3) Mkutano Mkuu ndio wenye maamuzi ya juu ya kubadili Katiba hii 4) Kutakuwa na kanuni zitakazoendana na Katiba ya Baraza la vijana pale ambapo patatokea utatanishi Katiba ndio itatawala.
5) Kamati tendaji itakuwa na uhuru wa kuzifanyia marekebisho kanuni za Baraza la vijana ili kuendana na wakati. 9.6.7 KUVUNJWA KWA BARAZA LA VIJANA TANZANIA Ø Baraza La Vijana Tanzania litavunjwa rasmi endapo robo tatu ya Wajumbe wote watakaohudhuria Mkutano Mkuu wa Baraza la vijana ulioitishwa kwa madhumuni kwa madhumuni ya kuvunjwa kwa Baraza la vijana watapitisha hoja hiyo. Mkutano huo utatangaza rasmi kuvunjwa kwa Baraza la vijana na kusimamisha shughuli zote za Baraza la vijana. Ø Wajumbe wote wataacha kushiriki shughuli za Baraza la vijana Tanzania Ø Katika tukio la kuvunjwa kwa Baraza la vijana, Bodi ya wadhamini itahodhi mali za Baraza la vijana kwa lengo la kulipa madeni yote ya Baraza la vijana kama yatakuwepo. Baada ya kulipa madeni yote, Mali za Baraza la vijana zitakazobakia zitakabidhiwa kwa wizara inayohusika na masuala ya vijana Tanzania.
NOTE: FAHAMI MASTAWILI
fahamijuma@yahoo.com
0717262629
 
1.0 UTANGULIZI
Tulipopata uhuru 1961, hapakuwa na sera rasmi ilkiyokuwa inaelekeza nini kifanyike kwa ajili ya maendeleo ya vijana nchini. Takribani miongo mitatu ndipo Sera ya Vijana ikawa imepatikana, lakini Kwa kipindi hiki kirefu miongozo iliandaliwa na kutekelezwa na Serikali. Mwaka 1996 na 2007 serikali kwa kushirikiana na Wadau mbalimbali iliandaa Sera ya Taifa ya Maendeleo ya vijana ambayo kwa ujumla wake ilizingatia mambo mengi ya msingi kwa maendeleo ya Vijana. Haki hizi ni pamoja na: Haki ya kuishi, kulindwa, kuendelezwa na kujiendeleza, kushiriki na kushirikishwa katika mambo mbalimbali ya maendeleo ya vijana na jamii kwa ujumla wake. Haki zingine ni pamoja na kutobaguliwa, kuheshimiwa, haki ya kumiliki mali, kufanya kazi na kupokea matunda/ujira halali wa kazi aliyofanya pamoja na usawa mbele ya sheria.
Kwa ujumla Sera ilimhakikishia Kijana usawa mbele ya sheria, uhuru na nafasi ya kushiriki na kutumia uwezo wao na vipaji vyao katika shughuli za maendeleo kama uongozi, utamanduni, uzalishaji mali pamoja na kunufaika na huduma za jamii zilizopo katika maeneo yao kwa lengo la kuboresha maisha yao.

1:1 FASILI NA UFAFANUZI Chama cha siasa – Ni kwa mujibu wa sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992. BAVITA – Baraza la Vijana Tanzania. Mwenyekiti – Kiongozi mkuu wa Baraza la vijana Tanzania. Katibu Mkuu – Kiongozi ntendaji mkuu wa Baraza la vijana Tanzania Uongozi wa chama cha siasa - Ni uongozi wa chama cha siasa kwa mujibu wa sheria sheria ya vyama vya siasa ya mwaka 1992. Idara – Ni taasisi za kitendaji ndani ya Baraza la vijana Tanzania. Mkutano mkuu- chombo kikuu cha maamuzi katika mambo yote ya Baraza la vijana. Bodi – Ni chombo kinacho angalia kwa ukaribu utendaji wa kamati tendaji ya Baraza la vijana. Kamati tendaji Ni – chombo kikuu cha utendaji wa Baraza la vijana.

KUANZISHWA KWA BARAZA LA VIJANA

1)
Kutakuwa na Baraza ambalo;

i) Litakuwa ni chombo chenye mamlaka, lakili yake, uwezo wa kushitaki na kushitakiwa.

ii) Linaweza , katika kutekeleza malengo yake kununua, kumiliki, kutunza na kuuza mali yeyote iwe ni mali inayohamishika au isiyohamishika na inaweza kufunga mkataba na kufanya shughuli yeyote halali kwa mujibu wa sheria.

iii)
Linaweza kujiunga na mabaraza mengine ya vijana yanayofanana kimalengo ya kikanda au kimataifa.

8 MALENGO
Lengo kuu la Baraza La Vijana Tanzania ni kujenga mawasiliano na mahusiano mazuri kati ya Vijana na Vyombo vya Maamuzi kama Kamati za Maendeleo za Mtaa, Kijiji, Kata, Halmashauri ya Jiji na Bunge kupitia Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana. Baraza litawajengea Vijana moyo wa kujituma, Kuwajibika, kujiendeleza na kujiimarisha katika maeneo yote ya maendeleo ya Jamii na Taifa kwa ujumla.

1. Kuwezesha Vijana kujadili masuala yanayowahusu kama yalivyoelekezwa katika Sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana na kutoa mapendekezo na ushauri kwenye vyombo vya Maamuzi.

2. Kutoa Elimu ya Ujasiriamali kwa Vijana ili kukabili changamoto za Ajira kwa Vijana kupitia Midahalo, Warsha, Makongamano na Semina mbalimbali.

3. Kuwajengea Vijana mshikamano wa Kitaifa katika kuleta muamko wa ushirikishwaji katika masuala yanayowahusu, kuwa na Sera bora, kutetea haki za Binadamu, Ulinzi na Usalama katika maeneo yao na Taifa kwa ujumla.

4. Kuwajenga vijana kuutambua utaifa wao hali ya umoja na mshikamano, kujiheshimu na kuifahamu kwa kina jamii kiuchumi halihalisi kiutamaduni na upeo wake.

5. Kufanya kazi kama jukwaa na kiungo wakilishi kwa masuala ya vijana katika Tanzania

6. Kuratibu mipango ya kuwajengea uwezo vijana ilikuwafanya wazalishaji katika jamii

7. Kuwezesha vijana kufikia ndoto zao kimaisha kisiasa, kiuchumi na kijamii kutokana na vipaji walivyojaliwa na Mungu.

8. Bazara kuwa kama mwamvuli wa kuwalinda vijana na mabadiliko ya sayansi na teknolojia katika dunia ya utandawazi.

9. Kuwakilisha maslahi ya vijana ndani na nje ya nchi.

9 BARAZA LITAKUWA NA KAZI ZIFUATAZO
a. Kushauri na kushauriana na wizara katika masuala yote ya vijana na mipango ya maendeleo.
b. Kuwezesha upatikanaji wa haki za vijana kupanua wigo endelevu wamaendeleo ikijumuisha sera, kanuni, sheria, mambo ya kimsingi na mipango.
c. Kuwezesha na kuimalisha ushirikiano miongoni mwa jumuiya zilizosajiliwa za vijana kitaifa, kikanda na kimataifa.
d. Kuandaa, kusimamia na kuthaminiwa mipango iliyoanzishwa na vijana ambayo yanaweza kupimwa baadae na jumui ya vijana sambamba na mipango yaTaifa.
e. Kusaidia na kuwezesha vikundi vyenye maslahi na maendeleo ya vijana katika kuanzisha mafunzo kwa vijana na mipango ya maendeleo na utafiti ilikuunga mkono mipango iliyogunduliwa na vijana na kukuza utumiaji wake.
f. Kwakushirikiana na wizara kuandaa nyaraka mbalimbali na kueneza taaluma iliyopatikana na mifano ya matendo ya kuigawa yanayohusiana na mipango ya vijana.
g. Kuhamasisha na kusambaza asilimali katika kuunga mkono utekelezaji wa mipango ya vijanana kuimalisha uwezo vikundi au jumui ya /za vijana.
h. Kuanzisha, kuendesha na kusimamia miradi yenye faida katika kuunga mkono maendeleo ya vijana kama itakavyoonekana inafaa.
i. Kupanga na kuendesha mikutano, semina, workshop, kongamano, mafunzoyabaraza la vijana.
j. Kufanya kazi nyingine zakama ambavyo baraza litaona inafaa kufuatana na malengo yake.

9.0 Katika kuhakikisha kuwa baraza linafanya kazi zake kiufanisi kwa mujibu wa sheria hii baraza litakuwa na uwe zo wa;

a. Kuajiri watendaji wabaraza kwa mujibu wa sheria ya utumishi wa umma au sheria nyingine yoyote inayohusiana na hayo.
b. Kuanziasha vitega uchumi au kuzishughulikia fedha ambazo bado hazijahitaji kimatumizi kwa dhamana na katika njia nyingine itakayoonekana inafaa na kubadilisha vitega uchumi hivyo.
c. Kisimamia, kuhakikisha usalama, kukodisha, kuweka rehani au kwa njia nyingine kuzifanyia kazi mali za baraza kwa mujibu wa sheria zilizopo na taratibu za nchi.
d. Kupokea michango au riba iwenifedha au mali nyingine kutoka kwa mtu au taasisi kwa ajili ya kuendeleza utekelezaji wa malengo yake isipokuwa pale ambapo mtu au taasisi hiyo wanajihusisha na malengo yaliyokinyume na sheria au yaliyokinyume na maadili.
e. Kutangaza kila baada yamuda umahili au maelezo mengine ambayo yataonekana ni muhimu kwa ajili yakuyatukuza malengo ya baraza.
f. Kudhibitisha na kuidhinisha mipango ya vijana.
Waziri anaehusika na vijana anaweza kutoa maelekezo na ushauri kwa baraza kuhusiana na utekelezaji wa kazi itakapotokea umuhimu wa maslahi ya vijana

9.1.5 DIRA YA BARAZA LA VIJANA NI

Kuwa na jamii ya Vijana wanaoishi kwa usawa na kuyafikia malengo yao na mahitaji yao ya msingi bila kubaguliwa

9.1.6 DHAMIRA YA BARAZA LA VIJANA

Kuona Vijana wanafikia ndoto zao za kimaisha na kuwa na sauti ya pamoja katika kusaidia upatikanaji wa huduma za jamii kwa vijana.

9.1.7 UANACHAMA [UJUMBE]

Ujumbe utakuwa wa wazi kwa Kijana yeyote bila kujali Kabila, Dini na usajili utakuwa ngazi ya mtaa au kijiji isipokuwa Asasi za vijana. Masharti na vigezo vya jumla vya Uanachama:

v
Awe na umri kuanzia miaka 15 hadi 35
v Apige vita Ukabila, Udini, Rushwa na Ubaguzi wowote
v Asiwe kiongozi wa chama cha siasa ngazi yoyote
v Awe Mzalendo, mtetezi wa Amani na Utaifa v Awe na akili timamu
v Awe tayari kuitetea Katiba ya Baraza La Vijana Tanzania

v
9.1.8 HAKI NA WAJIBU WA MJUMBE WA BARAZA LA VIJANA

v Kuwa na uelewa wa kutosha kuhusu madhumuni ya Baraza La Vijana Tanzania

v Kutekeleza na kuielewa Katiba ya Baraza La Vijana Tanzania
v Kutetea na kusimamia Haki na Amani popote awapo
v Kujiepusha na vitendo vya ushabiki wa Vyama vya Siasa, Dini, Ukabila katika kutekeleza shughuli za baraza

9.1.9 KUACHA / KUKOMA KWA UANACHAMA

Mwanachama ataacha Uanachama kwa:
v Kujiondoa mwenyewe kwa hiari na kutoa taarifa kwa barua katika Ofisi za Baraza la vijana eneo husika
v Kuondolewa kwa kukiuka Katiba ya Baraza La Vijana Tanzania
v
Kiongozi wa Baraza Kujihusisha na harakati za Vyama vya Siasa wakati bado ni Kiongozi wa Baraza La Vijana
v Ubadhirifu wa mali au Fedha za Baraza La Vijana
v Kifo
v Endapo mwanachama atafikisha umri zaidi ya miaka 35.

Kiongozi anayeacha Uanachama aidha kwa kufukuzwa, wizi au matumizi mabaya ya mali za Baraza La Vijana Tanzania atafikishwa kwenye vyombo vya sheria ili kurudisha au kushtakiwa na kufungwa Jela.

9.2.0
HAKI ZA MWANACHAMA WA BARAZA LA VIJANA TANZANIA

v Kushiriki vikao vya Baraza vinavyomuhusu na kutoa mawazo yake kwa uhuru na uwazi
v Kujitetea, kusikilizwa na kukata rufaa anaposhitakiwa au kuchukua hatua za kinidhamu.

9.2.1
UONGOZI Baraza La Vijana Tanzania litaongozwa na Viongozi wa kuchaguliwa na kuteuliwa.

9.2.2
SIFA MAHUSUSI ZA KILA KIONGOZI WA BARAZA

v Elimu ya Msingi na kuendelea
v Umri kuanzia miaka 18 – 35
v Mwaminifu na mwadilifu
v Uwezo wa kutafsiri mambo yahusuyo sera ya Taifa ya Maendeleo ya Vijana kwa ufasaha.

v Moyo wa kujituma na kujitolea kwa kuweka mbele maslahi ya Taifa na ya Baraza La Vijana dhidi ya maslahi binafsi.
v Awe na historia ya kukubalika na uadilifu katika jamii, hii ina maanisha amekuwa mwanachama kwa muda wa kutosha ndani ya Baraza na kujijengea historia hiyo au tayari anayo sifa hiyo ndani ya jamii.
v Aonyeshe tabia na mwenendo wa uzalendo wa kupenda nchi yake na kuitetea.
v Awe na uzoefu katika masuala ya uongozi wa jumuiya mbalimbali katika jamii.
v Adhihirishe mapenzi yake na imani yake kwa Baraza na wanachama kwa juhudi na vitendo vyake kuendeleza kukuza Baraza
v Awe na msimamo wa kuaminika.
v Aonyeshe uzoefu wa kuwa tayari kushirikiana na wenzake na uzoefu wa kufanya kazi na vikudi mbalimbali ndani ya jamii.
v Kuwa na njia halali za mapato yake ya kujitosheleza kwani uongozi wa Baraza ni wa msingi wa kujitolea isipokuwa viongozi waajiliwa.
v Adhihirishe kuwa na nidhamu na utii kwa kutekeleza maagizo au maelekezo ya vikao vya Baraza na uongozi wa baraza.
v Akubali kukosoa na kukosolewa au kuelekezwa na awe tayari kujirekebisha.

9.2.3 MIIKO YA UONGOZI

v Asiwe mtumishi wa chombo chochote cha dola.
v
Asiwe amewahi kushitakiwa au kuadhibiwa kwa makosa ya jinai v Asiwe kiongozi wa chama chochote cha siasa.

9.2.4 UENDESHAJI WA BARAZA

Kutakuwa na: v Mkutano mkuu,
v Kamati ya utendaji,
v Idara za utendaji za Baraza la Vijana Tanzania,

9.2.5 MKUTANO MKUU
Ni chombo chenye maamuzi ya mwisho katika uendeshaji wa majukumu ya Barazaa ambayo ni:-
v Kuchagua Viongozi wa Baraza la vijana Tanzania
v Kuidhinisha uundwaji wa idala mpya za Baraza la vijana.
v Kuandaa na kupitisha mikakati ya Baraza la vijana.
v
Kupokea na kupitia ripoti ya kila mwaka ya utendaji wa Baraza la vijana kutoka kamati Tendaji.
v Kubadili au kurekebisha Katiba
v Kupokea taarifa kutoka katika Kamati mbalimbali v Kuridhia majina ya wajumbe wa bodi ya baraza la vijana Tanzania
v
Kumwajibisha kiongozi yoyote ikiwa pamoja na kumvua uongozi kiongozi yoyote ndani ya Baraza kwa kukiuka misingi na kanuni za Baraza la vijana.

9.2.6 UENDESHAJI WA MKUTANO MKUU

v Utafanyika mara moja kwa mwaka
v Utaitishwa na Katibu Mkuu baada ya kushauriana na Mwenyekiti
v Maamuzi ya kikao yatafikiwa iwapo zaidi ya 50% ya Wanachama watapiga kura za kukubali au kukataa
v Utaongozwa na Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti, Mjumbe/Mwanachama atakayeteuliwa na Wanachama wakati wa mkutano ikiwa watajwa hapo juu hawatakuwepo kwa kutoa taarifa.
v Unaweza kuitishwa wakati wowote kwa dharura,ikiwa aliyechaguliwa na mkutano huu amefariki,amejiudhuru au amefukuzwa n.k. utaitishwa ndani ya miezi mitatu [3]

9.2.7 KAMATI YA UTENDAJI
Itaundwa na Katibu Mkuu, Wakuu wa Idara zote za Baraza na Mjumbe mmoja atakayeteuliwa na Mwenyekiti kutoka kila Idara za Baraza La Vijana au Asasi za vijana.

KAZI YA KAMATI ZA UTENDAJI:

v Kusimamia shughuli za kila siku za Baraza La vijana
Kuratibu shughuli zote za Wajumbe
v Itasimamia uandikishaji wa Wajumbe
v
Itawawajibisha Wajumbe wanaokiuka Katiba ya Baraza
v Itatoa ripoti maalum kuhusu semina, warsha na makongamano yaliyoendeshwa na Baraza kwenye mkutano mkuu wa baraza v Itasimamia matumizi na mapato kwa kushirikiana na Idara ya fedha na Utawala v Kuandaa na kufanikisha mikutanao na Wadau v Itakutana mara moja kwa mwezi
9.2.8 VIONGOZI
Kutakuwa na Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, Katibu Mkuu.
v Watachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Baraza La Vijana
v Watakuwa madarakani kwa miaka minne [4], wanaweza kuchaguliwa tena lakini sio zaidi ya awamu mbili [2].
v Makamu Mwenyekiti ataendesha mikutano ikiwa Mwenyekiti hayupo
v Mwenyekiti na Makamu ikiwa hawapo Baraza la Vijana litateua Mwenyekiti wa muda

9.2.9 MUUNDO WA BARAZA LA VIJANA TANZANIA

1. 9.2.9 Baraza la vijana ngazi ya kijiji au mtaa.
Baraza la vijana litaazia ngazi ya kijiji au mtaa ili kuwepo uwakilishi halisi wa vijana kuanzia ngazi ya chini kabisa.

a] Kila kijana ambaye ni raia wa Tanzania na ametimiza umri wa miaka 15 na ana umri chini ya miaka 35 na ni mkazi wa kijiji au mtaa atakuwa ana haki ya kusajiliwa kwenye daftari maalum la baraza la vijana la kijiji au mtaa.
b] Kiongozi wa chama cha siasa hatasajiliwa kama mwanachama katika daftari la baraza la vijana kwenye mtaa au kijiji.

8.2 Baraza la vijana ngazi ya kata.
a] Wajumbe wa mkutano mkuu baraza la vijana ngazi ya kata ni wajumbe wote waliosajiliwa katika daftari ngazi za mitaa au vijiji vya kata nzima.
b] Kutakuwa na viongozi wa baraza la vijana ngazi ya kata.
i. Mwenyekiti.
ii. Makamu mwenyekiti.
iii. Katibu.
iv. Mweka hazina.

9.3.0. Baraza la vijana ngazi ya wilaya.
a] Wajumbe wa mkutano mkuu wa baraza la vijana ngazi ya wilaya ni viongozi wote wa kata na wawakilishi wawili kwa usawa wa kijinsia kutoka kila kata na mwakilishi wa vijana kwenye halmashauri, viongozi wa dini
i. Mwakilishi kutoka ofisi ya mkuu wa wilaya .
ii. Wawakilishi wawili wa walemavu.
iii. Kutakuwa na uwakilishi wa mjumbe mmoja kutoka kila wilaya kwenye halmashauri kwa utaratibu wa uchaguzi kwenye mkutano mkuu wa wilaya wa baraza la vijana

b] Kutakuwa na viongozi wa baraza la vijana ngazi ya wilaya.
iv. Mwenyekiti.
v. Makamu mwenyekiti.
vi. Katibu .
vii. Mweka hazina.

8.4 .Baraza la vijana ngazi yaTaifa.

a] Wajumbe wa baraza la vijana Taifa watakuwa wafuatao:

i. Wawakilishi wawili kutoka kila wilaya ambapo mwenyekiti wa wilaya atakuwa mjumbe kwa nafasi yake katiyawawakilishiwawili.
ii. Wawakilishi wawili kutoka jumuiya ya wanafunzi elimu ya juu. Mwenyekiti wajumuiya atakuwa mjumbe kwa nafasi yake.
iii. Wawakilishi 5 wa walemavu
iv. Wawakilishi wa asasi iliyosajiliwa na baraza la vijana kwa vigezo vilivyowekwa vya usajili waasasi kwenye baraza.
v. Uwakilishi viongozi wa dini
vi. Wawakilishi 2 kwenye bunge la jamuhuri ya muungano wa Tanzania.
vii. Wawakilishi wawili kwa usawa wa kijinsia kutoka kila mkoa wa Zanzibar

b]Kutakuwa na viongozi wa baraza la vijana ngazi ya Taifa.
i. Mwenyekiti.
ii. Makamu mwenyekiti.
iii. Katibu. mkuu
iv. Wakuu wa idala.
v Idalaya sera na utafiti.
v Idala ya fedha za uchumi.
v Idala ya habari na elimu.
v Idala ya sheria na haki.

9.3.1 MWENYEKITI
Mwenyekiti atachaguliwa na mkutano mkuu na atakuwa madarakani kwa miaka minne [4]

KAZI ZA MWENYEKITI

v Mwenyekiti ni msimamizi mkuu wa shughuli zote za uendeshaji wa Baraza La Vijana
v
Mwenyekiti wa vikao vyote vya mikutano ya Baraza
v
Mfafanuzi na msuluhishi mkuu wa migongano na migogoro na matatizo ya ndani ya Baraza La Vijana
v
Atakuwa Msemaji Mkuu wa Baraza la Vijana

9.3.2 MAKAMU MWENYEKITI
Mwenyekiti wa baraza la vijana Zanzibar ndiye atakuwa makamu mwenyekiti wa Baraza la vijana Tanzania na atakuwa madarakani kwa miaka minne [4]
KAZI ZA MAKAMU MWENYEKITI

v Msaidizi wa Mwenyekiti v Atafanya kazi za Mwenyekiti iwapo Mwenyekiti hatakuwepo.

9.3.3 KATIBU MKUU

Atakuwa Mtendaji mkuu wa Baraza La vijana Tanzania, atateuliwa na Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania na kumwapisha na atakaa madarakani kwa miaka minne
[4]
KAZI ZA KATIBU
v Mtendaji na Mtekelezaji Mkuu wa shughuli zote zilizoamriwa na Baraza la Vijana Tanzania
v Mtoaji na mtunzaji wa kumbukumbu zote zinazohusu Baraza la Vijana Tanzania
v Muandaaji wa Mikutano yote baada ya kuandaa Agenda kwa kushauriana na Mwenyekiti
v Msimamizi wa Idara zote ndani ya Baraza la vijana Tanzania
v Mwajibikaji wa kwanza katika masuala yote yanayohusina na fedha au mali za Baraza

9.3.4 BARAZA LA VIJANA LITAKUWA NA IDARA.

Ili kulifanya baraza linakuwa taasisi inayojishughulisha na masuala ya vijana kila siku na kutekeleza malengo ya baraza la vijana Tanzania litakuwa na idara za kitendaji:

9.3.5
IDARA YA FEDHA NA UCHUMI

Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ambaye atateuliwa na mwenyekiti kwa kushauriana na Katibu Mkuu wa Baraza na atawajibika moja kwa moja kwa Katibu Mkuu wa baraza kwa shughuli zake za kila siku za Idara nzima.

A) IDARA YA FEDHA NA UCHUMI ITAKUWA NA WAJUMBE WAFUATAO:
i) mkurugenzi wa idara.
ii)
Mweka hazina
iii) Afisa mikopo kwa vijana
iv) Afisa ujasiriamali kwa vijana

KAZI ZA IDARA YA FEDHA NA UCHUMI

v Kutunza kumbukumbu zote za fedha zitokazo na kuingia katika akaunti za Baraza la Vijana
v Kutoa taarifa za fedha kwa Kamati Tendaji
v Kukusanya viingilio, ada na vyanzo vingine vya mapato au mali ya Baraza
v Mtayarishaji wa maombi ya fedha yanayohitaji kuidhinishwa na waweka saini benki wa Baraza
v Kushirikiana na Idara ya Sera na mipango kubuni mikakati itakayoingizia fedha Baraza
v Kusimamia mambo yote yanayohusu ukusanyaji wa ada, michango na misaada kutoka kwa Wafadhili na Wahisani mbalimbali.
v Kutoa na kusimamia mikopo kwa vijana
v Kutoa elimu ya ujasiriamali kwa vijana
v Kutoa elimu ya mikopo na ulejeshaji kwa vijana
v Kubuni vyanzo vipya vya mapato vya baraza.

9.3.6
IDARA YA SERA NA MIPANGO

Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi wa Idara amabaye atateuliwa na Mwenyekiti wa Baraza la Vijana Tanzania kwa kushauriana na Katibu Mkuu.
Atawajibika moja kwa moja kwa Katibu mkuu wa baraza kwa shughuli zake za kila siku za uendeshaji wa Idara nzima.

A) WAJUMBE WA IDARA WATAKUWA WAFUATAO.

i) mkurugenzi wa idara
ii) Afisa vijana masuala ya wanafunzi
iii) Afisa vijana masuala ya wafanyakazi
iv)
Afisa vijana masuala ya michezo, sanaa na vipaji

KAZI ZA IDARA YA SERA NA MIPANGO

Ø Kutafuta na kuchambua Sera, Miswada na Tafiti mbalimbali zinazohusu masuala ya Vijana
Ø Kubuni njia, mbinu au mikakati ya kuwasilisha matokeo ya uchambuzi wa Sera na Mapendekezo kwenye vyombo vya Maamuzi kwa ajili ya utekelezaji
Ø Kushirikiana na Idara ya Fedha na Uchumi katika kubaini miradi ya fedha za Baraza
Ø Kufanya utafiti juu ya masuala mbalimbali ya Vijana au changamoto zinazowakabili Nchini na kutoa mapendekezo juu ya utafiti husika kwa Serikali au Taasisi zinazohusika na kushughulika na Vijana

Ø 9.3.7 IDARA YA HABARI NA ELIMU

Idara hii itaongozwa na Mkurugenzi wa Idara ambaye atateuliwa na Mwenyekiti kwa kushauriana na Katibu Mkuu wa Baraza Atawajibika moja kwa moja kwa Katibu Mkuu wa Baraza kwa shughuli zake za kila siku za Idara nzima.

A) WAJUMMBE WA IDARA WATAKUWA WAFUATAO

i) Mkurugenzi wa idara
ii) Afisa habari
iii) Afisa Elimu mtambuka na utamaduni
iv) Afisa wa vijana masuala ya kiroho

KAZI ZA IDARA YA HABARI NA ELIMU

Ø kusambaza Sera, mipango na taarifa mbalimbali za masuala yanayohusu vijana
Ø Idara inayohusika na masuala yote ya habari na taarifa ya Baraza la vijana Tanzania.
Ø Kusambaza vipeperushi, majarida, magazine na viandikwa vingine vya Baraza
Ø Kusambaza taarifa na Kuandaa Itifaki na matayarisho ya warsha, kongamano na mikutano mbalimbali ya Baraza
Ø Kuandaa na kusambaza taarifa za utafiti na uchambuzi wa sera kwenye masuala yahusuyo Vijana kwa vijana wote
Ø Kuunda na kusimamia utunzaji wa Maktaba ya Baraza

9.3.8 IDARA SHERIA NA HAKI

Idara hii itaongozwa na mkurugenzi ambaye atateuliwa na mwenyekiti kwa kushauriana na katibu mkuu wa Baraza kwa kuzingatia sifa na taaruma za kuongoza idara akisaidiwa na wajumbe watakaoteuliwa.

KAZI ZA IDARA YA SHERIA NA HAKI

Kazi za idara ya sheria ni kushughulikia masuala yote kisheria ndani ya baraza kwa vijana na kusimamia mikataba ya baraza la vijana.

10 9.3.9 BODI YA BARAZA LA VIJANA TANZANIA

§ Itaundwa na Wajumbe wasiozidi kumi na wasiopungua sita na ndio chombo cha pili kwa maamuzi baada ya Mkutano Mkuu
§ Itakaa kila baada ya miezi mitatu [3] na itaongozwa na Mwenyekiti wa Bodi ambaye atachaguliwa na Wajumbe wa Bodi kutoka miongoni mwao
§ Mwenyekiti wa Baraza atakuwa Katibu wa Bodi na Katibu Mkuu wa Baraza atakuwa Mjumbe wa Bodi kwa wadhifa wake lakini hatakuwa na haki ya kupiga kura kwenye maamuzi ya Bodi.

KAZI ZA BODI YA BARAZA LA VIJANA TANZANIA

§ Kujadili Ajenda zilizopendekezwa na Kamati tendaji kabla ya kuzipeleka kwenye Mkutano Mkuu wa baraza La Vijana § Kupitia Utendaji wa Baraza la Vijana Tanzania
§ Kuitisha na kuthibitisha majina ya Wanachama wapya kila mwaka

9.4 .0 TAASISI SHIRIKI

9.4.1 – (1) Taasisi zinazoongozwa na vijana,kikundi au taasisi za vijana ,zenye
a) Nia na malengo ya kuendeleza ustawi wa vijana na
b) Kuendana na malengo ya sharia hii,vitakuwa huru kujiunga kama vyama shiriki
(2) Taasisi ya vijana ambayo inataka kujiunga kama tasisi shiriki chini ya kifungu cha 9.4(I) itatakiwa:-
a) Iwe katika ngazi ya Taifa na iwe na uwakilishi angalau katika mikoa kumi ya Tanzania bara
b) Kuambatanisha idadi ya wanachama wake waliosajiriwa na mfumo wa uongozi wake;
c) Uanachama uwe wazi kwa watanzania wote bila kujali rangi zao,makabila ,jinsia au dini.
d) Kuwakilisha kwa katibu mkuu maombi ya kujiunga katika fomu maalum na kwa utaratibu uliowekwa na kuambatanisha katiba,Kanuni,sharia nyingine za kimataifa zinazotumia kama zipo pamoja na mpoango wake wa kazi.
(3) Baada ya kupokea maombi yaliyotajwa katika kifungu cha 9.4(2)kamati tendaji itayapitia na kutoa mapendekezo kwa bodi.
(4) Baada ya kuzingatia yaliyo wasilishwa pamoja na mapendekezo ya kamati tendaji kwa mujibu wa kifungu cha 9.4(30 Bodi inaweza kuidhinisha au kutupilia mbali maombi yaliyowasilishwa
(5) Endapo bodi itajiridhisha kwamba
a) Katiba ya taasisi au kikundikilichowasilisha maombi,kanuni na sharia nyingine zake ni nakala halisi na hazipingani na sharia hii;
b) Kwa kuona usajili wake wanachama wa mwombaji wanaomba kwa nia njema na kwa manufaa ya uanachama na kikundi au taasisi.
c) Uanachama wa kikundi kinachoomba uko wazi kwa watanzania wote bila kujali rangi,kabila,jinsia au dini, na
d) Bodi itaidhinisha maombi yaliyowasilishwa na kukiandikisha taasisi au kikundi kama kikundi shiriki,baada ya kulipa ada ya kiingilio na ada ya uanachama kama itakayokuwa imepangwa kwa ajili hiyo.
(6) Endapo kikundi shiriki kitafanya marekebisho katika katiba kanuni au Sheria nyingine inayoongoza taasisi au kikundi hicho, kikundi hicho kitatakiwa kuwasilisha marekebisho hayo mapema itakavyowezekana kwa katibu Mkuu ili kuweza kusajili mabadiliko hayo
(7) Taasisi au kikundi shiriki baada ya kuandikishwa na baraza kama mshiriki kinaweza kupata ruzuku kutoka Baraza
(8) Baraza litatunza kumbukumbu na uandikishwaji wa mshiriki.
(9) Kumbukumbu zinazotajwa katika kifungu cha 9..4(8) zitakuwa wazi kwa ajili ya kukaguliwa na mtu yeyote katika ofisi ya baraza bila gharama yeyote,kwa utaratibu utakaowekwa na kamati tendaji

9.5.1 - (1) Kila mshiriki anayepokea ruzuku kutoka baraza atatakiwa kuwasilisha kwa baraza, si zaidi ya miezi sita baada ya mwaka wao wa fedha –
a) Taarifa ya shughuli katika kipindi hicho cha mwakawa fedha;na
b) Ripoti ya ukaguzi inayonyesha mapato na matumizi kwa mwaka huo wa fedha.
(2) Kila taasisi shiriki inayokea ruzuku toka kwa Baraza itatakiwa kuwasilisha,kabla ya kuisha kwa mwaka wa fedha taarifa ya matumizi ya ruzuku hiyo, makadilio ya mapato na matumizi kwa kipindi cha mwaka unaofuata pamoja na mpango kazi.
(3) Endapo katibu Mkuu ataona kwamba makadilio yaliyowasilishwa kwa mjibu wa kifungu kidogo cha (2) hayana maslahi kwa mjibu wa sharia hii,atapeleka taarifa kwenye bodi
(4) Endapo taarifa itatolewa kwa bodi kwa mujibu wa kifungu cha 9.5(3) bodi,baada ya kusikiliza utetezi wa kikundi shiriki,inaweza kukitaka kikundi hicho kuyafanyia marekebisho makadirio hayo.

VIFUNGU VINAVYOHU MFUKO WA BARAZA LA VIJANA

9.5.6.-(1) Kutakuwa na mfuko utakaojulikana kwa jina la mfuko wa maendeleo ya vijana na malengo yake ni kugharamia shughuli za baraza la vijana la Taifa mipango ya baraza na kutekeleza miradi ya vijana na kwa ajili ya maendeleo ya vijana
(2) Fedha za Mfuko zitatokana na-
a) Fedha itakayotafutwa na vijana kutoka katika vyanzo vyake vya mapato kama vile mauzo ya bidhaa zake,au fedga zitakazopatikana kutokana mipango yake au huduma ambayo vijana wataitoa
b) Faida itakayo patikana kutokana na uwekezaji utakaofanywa na baraza
c) Michango au misaada itakoyopokelewa na baraza kutoka sehemu mbalimbali kwa uhakiki wa waziri anayehusika na
d) Fedha halali itayopokelewa kutoka vyanzo vingine
(3) Mfuko utaratibiwa na kusimamiwa na kamati tendaji kwa kuzingatia makadilio ya mapato na matumizi yanayoandaliwa na kamati tendaji na kupitishwa na waziri kwa kuzingatia mahitaji ya kila mwaka wafedha wa baraza.
(4) Hakuna matumizi yatakayofanyika kutoka kwenye mfuko wa baraza isipokuwa kwa kufuata masharti ya kifungu cha 9.5.6(3)
(5) Kamati tendaji itafungua na kutunza akaunti ya Benki itakayokuwa na jina la mfuko katika taasisi ya benki au katika tasisi ya kifedha iliyosajiliwa kujishughulisha na masuala ya kiffedha kwa mujibu wa sharia zinazoongoza taasisi za fedha kwa Tanzania.
a) Akaunti hiyo itatumikakwa kutunzia fedha zote za baraza zilizopokelewa kwa niaba ya baraza na kwa manufaa ya baraza kwa mujibu wa sharia hii na sharia nyingine.
b) Akaunti hii itatumika kufanya malipo ya-
i. Matumizi yote yanayousiana na utendaji kazi wa baraza
ii. Kiasi chochote ambacho mfuko huu unapaswa kulipa kwa mujibu wa sharia hii
c) Hakutokuwa na fedha itakayotolewa isipokuwa tu kwa njia ya hundi au njia nyingine rasmi kama itakavyotakiwa sahihi na mtu au watu waliodhinishwa na kamati tendaji
(6) Kamati tendaji ,katika namna ambayo itaidhinishwa na waziri inaweza kuwekeza kiasi kinachotoka kwenye mfuko kilchowekwa benki ambacho hakihitajiki kwa matumizi ya karibuni
(7) Kamati tendaji kwa kuzungatia maombi yatakayo wasilishwa kwake au kwa kuanzisha yenyewe kama itakavyoamua inaweza kutoa msaada wa kifedha kutoka katika mfuko wa baraza la vijana kwa mtu yeyote, klabu ya vijana muunganiko wa vijana au utaratibu ulioko katika kifungu cha 9.5.6(1)
(8) Kwa ajili ya kutoa fedhakama ilivyoainishwa katika kifungu cha 9.5.6(7) kamati tendaji inaweza kuhitaji kutoka kwa mlengwa.
a) Vielelezo na taarifa kama ambavyo kamati tendaji itaitaji au
b) Vitabu,vielelezo,nyaraka,maelezo na kumbukumbu kulingana na jinsi ambavyo kamati tendaji itahitaji
(9) Kamati tendaji inaweza ikahitaji kutoka kwa mlengwa wa msaada wa kifedha chini ya 9.5.6(7) kutoa-
a) Taarifa na vielelezo
b) Vielelezo,maelezo au kumbukumbu kuhusiana na fedha ambazo kamati tendaji itampatia au kama kamati tendaji itakavyoamua.
(10) Kiasi chochote ambacho kitakuwa hakijatumika ndani ya mfuko kufikia mwisho wa mwaka wa fedha wa baraza itachukuliwa kuwa ni fedha za mwaka ujao wa fedha.

9.5.7.-(1) Mwaka wa fedha wa baraza utaanza kila tarehe 1Julai na utaisha tarehe 31Julai ya kila mwaka
(2) Kamati tendaji itawajibika kutunza nyaraka zinazohusiana na hesabu na taarifa za fedha zinazohusiana na shughuli za baraza ili kuliwezesha muda wowote,kuwasilisha taarifa za malipo na manunuzi ya baraza
(3) Mapema kadiri itakavyowezekana kabla ya mwisho wa mwaka wa fedha ila siyo zaidi ya kipindi cha miezi mitatu .kamati tendaji
a) Itawajibika kuandaa-
i. Taarifa ya fedha inayohusu mwaka huo wa fedha;na
ii. Kutoa taarifa juu ya maendeleo na shughuli za baraza kwa kipindi hicho cha mwaka huo
b) Itawasilisha taarifa za mahesabu na taarifa za fedha kwa mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali kwa ajiri ya ukaguzi
(4) Mkakuzi mkuu wa hesabu wa hesabu za serikali baada ya kufanya ukaguzi atatoa hati,na taarifaa ya ukaguzi ,kwa mujibu wa sharia na kanuni za ukaguzi na sharia hii,ambayo itaasilishwa kwa waziri kwa ajili ya kuwasilishwa bungeni na nakala ya ripoti hiyo itapelekwa kwa kamati tendaji

9.5.8.-(1) Fedha iliyotengwa kwa ajili ya mfuko itatumiwa na baraza kulingana na matakwa yaliyoidhinishwa katika kifungu cha9.5.6(3) na kutumika pia katika
a) Mipango,miradi na shughuli nyingine za baraza
b) Kazi za kamati tendaji na

c) Utawala wa mfuko
(2) Kiasi chochote cha fedha kitakachokuwa kimetolewa na benki kwa matakwa ya kifungu 9.5.6(1)au mali ya baraza kama itakavyokuwa imeoneshwa itatmika kama ilivyokusudiwa na matarajio ya matumizi hayo yataoneshwa

9.5.9.(a) Kutakuwana siku itakayojulikana kama siku ya taifa ya vijana ambayo itatanguliwa na juma la Taifa la Vijana
c) Siku na juma la Taifa la vijana linalotajwa kwenye kifungu 9.5.9(a) litaamuliwa na Baraza na itaidhinishwakama itakavyopangwa na Baraza

9.6.0.-(1) Waziri,kwa kushauriwa na kamati tendaji,anawezakutangeneza kanuni zinazohusiana na-
(a) Fomu ya maombi,vyeti vya uandikishaji unaofanywa,kutolewa au kutunzwa kwa mujibu wa
(b) Jambo lolote ambalo waziri anatakiwa au anaruhusiwa kufanya kwa mujibu wa sharia hii
(c) Jambo lolote ambalo ni muhumu ili kufanikisha malengo ya sharia hii kufanya kazi
(2) Kanuni zitakazotengenezwa chini ya kifungu cha 9.6.0(1) zinaweza kutaja adhabu ya kuzikiuka.
(3) Kamati tendaji kwa idhini ya waziri inaweza kutengeneza taratibu zinazousiana na:-
(a) Maswala ya wafanyakazi
(b) Mpangilio na utunzaji wa vitabu vya hesabu na utawala wa mfuko wa baraza
(c) Utaratibu wa uchaguzi utakaofanywa na mkutano mkuu na mifumo tawala
(d) Uchaguzi na mwenendo wa taasisi au vikundi shiriki kwa baraza na taratibu za kuwasilisha
Taarifa

(e) Namna na utamaduni ambavyo siku na juma la vijana la Taifa litazingatiwa na kuadhimishwa.

9.1.6 MALIPO YA VIONGOZI

§ Uongozi na wadhifa wowote atakaopewa Mjumbe wa Baraza la Vijana kuanzia ngazi ya wilaya kushuka chini. Mwenyekiti, Makamu Mwenyekiti, mweka hazina na uwakilishi mwingine ni kazi ya kujitolea kwa ajili ya maendeleo ya Vijana isipokuwa katibu wa wilaya atakuwa mwajiliwa wa baraza
§ Hivyo Wajumbe wataamua kwa kujadiliana uwezekano wa kuwapa posho kulingana na uwezo wa rasilimali za Baraza kwa kuangalia umuhimu wa kazi zinazofanyika na mazingira ya kazi hizo.

9.1.7 WAWEKA SAINI WA BARAZA LA VIJANA KATIKA BENKI

1.
Katibu Mkuu atakuwa mmoja wa waweka saini
2. Mkuu wa Idara ya fedha na uchumi
3. Mwanachama/Mjumbe mmoja atakaechaguliwa katika Mkutano Mkuu wa baraza la vijana.

9.1.8 TARATIBU ZA KUTATUA MIGOGORO NDANI YA BARAZA

Kutakuwa na Kamati ya muda ya kuratibu shughuli za kutatua migogoro. Kamati itaongozwa na Mwenyekiti au Makamu Mwenyekiti. Kutakuwa na taratibu katika kuchukua hatua za kinidhamu kwa Mwanachama yoyote atakaekiuka Katiba na kuleta mgogoro ndani ya Baraza Kabla ya Mwanachama hajachukuliwa hatua za kinidhamu ikiwemo kuonywa, kuachishwa Uanachama kwa muda ama kufukuzwa kabisa uanachama, atakuwa na haki ya:

a) Kujulishwa makosa yake kwa maandishi na kutakiwa kutoa majibu katika muda usiopungua wiki mbili [2] baada ya kujulishwa.
b) Kupewa nafasi ya kujitetea mbele ya kikao husika
c) Mwanachama atajulishwa kwa maandishi uamuzi wa kikao wiki mbili [2] baada ya kusikilizwa.
d) Mwanachama aliyewahi kufukuzwa ama kuachishwa uanachama anaweza kuomba kurejea kwa maandishi kupitia ngazi iliyomfukuza akieleza sababu za marekebisho yake na kutaka kurejea.
e) Kiongozi yoyote hatachukuliwa hatua za kinidhamu bila kwanza kupewa mashtaka kwa maandishi na mamlaka husika na kupewa nafasi ya kujibu mashtaka hayo kwa maandishi.
f) Kiongozi mwenye mashtaka, zaidi ya utetezi wa maandishi, atapewa nafasi ya kujitetea bayana mbele ya kikako cha Mamlaka ya Nidhamu.
g) Kiongozi atakayeadhibiwa atapewa taarifa ya msingi ya maamuzi ya mamlaka ya nidhamu ili kumuwezesha kupata nafasi ya kukata rufaa ikibidi.
h) Mwadhibiwa atakayeamua kukata rufaa atatakiwa kufanya hivyo katika muda wa siku thelathini [30] baada ya kuarifiwa uamuzi wa adhabu.
i) Baada ya kutoa uamuzi, Kikao husika kitaandaa taarifa kamili ya mwenendo wa shauri na kuwasilisha mwenendo huo kwenye Mkutano Mkuu wa Baraza baada ya kupitia kwenye Bodi ya Baraza la vijana Tanzania

9.1.9 TARATIBU ZA UCHAGUZI WA NAFASI ZA UONGOZI

1) Kamati Tendaji ndio chombo kinachoainisha ratiba ya uchaguzi ndani ya Bazara, ratiba itaonyesha pia tarehe ya kuwasilisha rufani 2) Ratiba ya uchaguzi ndani ya Baraza itatolewa siyo chini ya miezi sita [6] kabla ya uhai wa kamati tendaji ya uongozi inayomaliza muda wake.
3)
Kamati tendaji itaiwasilisha ratiba ya uchaguzi kwenye bodi ya Baraza ili kuipa nafasi bodi ya Baraza kuunda kamati ya uchaguzi ya watu watano
(5) ambayo itakuwa na jukumu la kusimamia uchaguzi tu na baada ya uchaguzi kuisha nayo itavunjika.

4) Mwenyekiti na katibu wa kamati ya uchaguzi watachaguliwa kutoka miongoni mwa wajumbe na wajumbe wenyewe. 5) Wagombea watajaza fomu za maombi ambazo zitatayarishwa na kamati tendaji fomu hizi zitalenga kupata taarifa kamili ya mwombaji ili kuviwezesha vikao vya uteuzi kumwelewa kumtathimini mgombea.
6) Mwanachama yoyote hataruhusiwa kugombea nafasi zaidi ya moja na atakuwa na kadi yake wakati atakaposhiriki kwenye vikao vya Baraza kwa ajili ya kuhakiki uhalali wa uanachama wake.
7) Wanaoomba nafasi za ukuu wa idara watapaswa kujaza fomu maalum zitakazotayarishwa na kuzifikisha kwa katibu mkuu naye atawasilisha fomu zote kwa mwenyekiti atakapofanya uteuzi wa wakuu hao kwa taratibu zitakazokubaliwa na Baraza. 8) Upigaji wa kura utakuwa wa siri na karatasi maalum zitatumika kwa shughuli hiyo.
9) Matokeo yatatangazwa baada ya uchaguzi kukamilika. 10) Mgombea yeyote asiyeridhika na matokeo ya uchaguzi ataruhusiwa kuwasilisha malalamiko ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa nafasi aliyogombea kwa Kamati ya Rufaa.

9.1.10
KAMATI YA RUFAA

1)Itakuwa na Wajumbe watano [5] ambao watachaguliwa na Mkutano Mkuu wa Baraza.
2)
Mwenyekiti na Katibu wa Kamati ya Rufaa watachaguliwa kutoka miongoni mwa Wajumbe na Wajumbe mwenyewe kwa kupigiana kura.
3) Itakuwa na jukumu la kupokea, kusikiliza na kutoa maamuzi juu ya rufaa ya uchaguzi itakayokuwa imewasilishwa kwenye Kamati hiyo.
4) Kamati ya Rufaa ndio itakuwa yenye maamuzi ya mwisho kwenye masuala yanayohusu uchaguzi.

9.6.6 MAREKEBISHO YA KATIBA

1) Mapendekezo juu ya mabadiliko yoyote ya Katiba yatafanywa na Kamati tendaji kwa kuwasilishwa kwenye Bodi na kuidhinishwa na Mkutano Mkuu wa Baraza la vijana.
2) Katiba hii inaweza kubadilishwa na Mkutano Mkuu wa Baraza la vijana baada ya theluthi mbili ya Wajumbe kukubali mabadiliko hayo ya Katiba
3) Mkutano Mkuu ndio wenye maamuzi ya juu ya kubadili Katiba hii
4) Kutakuwa na kanuni zitakazoendana na Katiba ya Baraza la vijana pale ambapo patatokea utatanishi Katiba ndio itatawala.
5) Kamati tendaji itakuwa na uhuru wa kuzifanyia marekebisho kanuni za Baraza la vijana ili kuendana na wakati.

9.6.7 KUVUNJWA KWA BARAZA LA VIJANA TANZANIA

Ø Baraza La Vijana Tanzania litavunjwa rasmi endapo robo tatu ya Wajumbe wote watakaohudhuria Mkutano Mkuu wa Baraza la vijana ulioitishwa kwa madhumuni kwa madhumuni ya kuvunjwa kwa Baraza la vijana watapitisha hoja hiyo. Mkutano huo utatangaza rasmi kuvunjwa kwa Baraza la vijana na kusimamisha shughuli zote za Baraza la vijana.

Ø Wajumbe wote wataacha kushiriki shughuli za Baraza la vijana Tanzania
Ø Katika tukio la kuvunjwa kwa Baraza la vijana, Bodi ya wadhamini itahodhi mali za Baraza la vijana kwa lengo la kulipa madeni yote ya Baraza la vijana kama yatakuwepo.

Baada ya kulipa madeni yote, Mali za Baraza la vijana zitakazobakia zitakabidhiwa kwa wizara inayohusika na masuala ya vijana Tanzania.

NOTE: FAHAMI MASTAWILI
fahamijuma@yahoo.com
0717262629
 
Rasimu ya mwizi kama Chenge mzee wa ufisadi aliyekithiri kwangu ni takataka na sitothubutu kulithamini kwa namna yoyote ile. Katiba iliyopatikana kimabavu kama ya Sitta ni takataka la chooni!! Ninasubiri nilipate nilichome hadharani kufikisha ujumbe!
 
Hivi ni nani aliyetoa mamlaka kuanza kuandaliwa kwa katiba na muongozo wa baraza la vijana?
 
fahami matsawily naomba nitangulize maoni yangu ya awali pia badae ntarudi kutoa mengine.

Kuhusu sifa za kijana kuwa kiongozi hii rasimu inasema lazima kijana awe na uzoefu wa kuongoza asasi mbalimbali za kijamii, alafu pia hapohapo rasimu imesema kwamba sifa ya kijana ni lazima awe na umri kuanzia 18, sasa huyu kijana mwenye miaka 18 huo uzoefu atakuwa ameupatia wapi au ndo kusema tunarudi kule kule kwenye mambo ambayo vijana tunayalalamikia siku zote juu ya vigezo vinavyomnyima kijana fursa!

Pia rasimu inasema kiongozi au mjumbe wa baraza la vijana hatakiwi kujihusisha na harakati za kisiasa, sasa neno HARAKATI lina maana kubwa sana na hii naogopa baraza hili litawanyima fursa vijana ambao ni member wa vyama vya siasa ila a angependa kujiunga na baraza hili.

Pia rasimu inasema mtu atakayefukuzwa na baraza la vijana kwa kujihusisha na harakati za kisiasa atapelekwa mahakamani mmmh? I doubt sheria hizi zitakimbiza wengi.
 
Last edited by a moderator:
Pia hapo kwenye upande wa malipo, kuna tatizo, viongozi wa wilaya kushuka ngazi za chini watatikiwa wajitolee tu na hakuna malipo yeyote, suala hili litazidi kuwagawa viongozi, mfumo mbovu sijui kwanini umekuwa sugu, hata kwenye vyama vya siasa vyote, serkali yenyewe hakuna mkazo wa kuwapa motisha viongozi wa ngazi za chini kwa kisingizio cha kipato kidogo, sasa kwanini hata hicho kidogo wasigawanishwe na viongozi wa ngazi za chini?
 
Nishapita ujanani

Ndugu Yangu shardcole sifa za kuwa kiongozi ni general qualification kuanzia ngazi ya kata hadi Taifa uzoefu wa kiungozi may be kwenye masuala ya vijana itategemea na ngazi unayoomba kugombea mfano ya Taifa na suala la umri pia sio lahisi Kijana mwenye umri miaka 18 kushinda nafasi ya uwenyekiti Taifa kutokana na ushindani lakini demokrasia inampa Uhuru wa kushiriki kugombea nafasi yoyote kwa hiyo hapo kuna haki ya kidemokrasia na ushindani wa kidemokrasia.
suala kushiriki kutoa maoni mchakato wa suala la baraza la vijana kila Kijana ana wajibu wa kushiriki na kutoa maoni yake kwa Uhuru.

Na bunge LA januari mswaada utasomwa bungeni kwa mala ya pili.
 
Na kuhusu malipo ya viongozi ngazi za chini ya wilaya ni kutokana uwezo wa kifedha wa baraza lenyewe ila kutakuwepo posho kulingana na majukumu watakoyopewa huko lakini wao hawatakuwa waajiliwa
 
Back
Top Bottom