Kuunguruma kwa kongamano la Wanataaluma Dar: Moto wayaka!

Huu siyo wakati wa maazimio japokuwa wazo la TPN ni zuri. Mimi nafikiri watanzania tunahitaji kujikita zaidi ktk utekelezaji wa maazimio lukuki yaliyo kwisha tolewa miaka ya nyuma na yamewekwa kapuni.

Kwa mfano, suala la ku-review mikataba ya madini ambayo imesainiwa wakati wa mwinyi na mkapa linahitaji utekelezaji lakini shangaa kwamba kila mtu yuko kimya.

Kuwa na tume huru ya uchaguzi inayo shirikisha vyama vyote vya siasa, hili nalo linahitaji utekelezaji tu, je wasomi tumefanya nini ktk hili?? au tunaona ni sawa??

Mzalendo Magezi;

Kila issue ambayo kutakuwa na ushahidi wa kutosha na kuna sheria inaruhusu yatafanyiwa kazi. pale ambapo sheria hairuhusu, njia mbadala za kuleta mabadiliko zitatumika.

Kinachotakiwa ni wote kuunganisha nguvu, si wengine wanatenda wengine wako nje wanaangalia. Let us all be part of changes.
 
Nadhani wakicheza karata zao vizuri wanaweza kujiwekea miongoni mwa makundi ya mabadiliko. Hata hivyo ni lazima waoneshe kuwa wako tayari kulipa gharama ya mabadiliko wanayoyataka.

Nahisi unaweza kumaanisha kuwa tuwe tayari kuloose tulivyonavyo katika harakati hizi au kusumbuliwa kwa sababu au visingizio tofauti uli kuachana na jambo hili.

Labda tusaidie kufafanua kwa kina na ikiwezekana mkakati wa kuepukana na hilo. Ila ninachojua waliofika hakika Wamechoka, wamechoka, wamechoka na walikuwa tayari kukabiliana na changamoto.
 
Sasa wewe angalia mada zenyewe tu, kitu kimoja kimenyumbulishwa seven ways kujaza empty space, inaonyesha hawa watu hata hawana cha kuchangia above abstraction layer.

Halafu maswala muhimu kabisa wanaogopa kuyagusa.

Mbona katika abstraction layer tuna makabrasha kibao yamejaa policies nzuri tu, tatizo utendaji.

Ndiyo maana Julius anakupa hood philosophy ya "show me better than you can tell me"

Mzalendo; unaweza ukatuambia Mkakati Mbadala unaoweza kutoa? (Assume TPN is wrong).
 
Naona hii habari pia inaongelea suala hili hili kwenye chombo kingine cha wasomi.
Maliasili haziwezi kuinua uchumi bila kuimarishwa-Mkapa
Imeandikwa na Na Mwandishi Wetu; Tarehe: 18th December 2009






RAIS Mstaafu Benjamin Mkapa, amesema japokuwa Tanzania ina utajiri mkubwa wa maliasili yakiwemo madini, bado utajiri huo hauwezi kuinua uchumi wa nchi hiyo hadi pale itakapojidhatiti katika kuimarisha maeneo yanayogusa sekta husika za maliasili hizo.

Akifungua Mkutano Mkuu wa Taasisi ya Uhandisi na Teknolojia unaogusa uhandisi wa madini, jana Dar es Salaam, Mkapa alisema Tanzania imekuwa ikizungumzia kila kukicha suala la umasikini wa wananchi wake huku pia ukweli ukifahamika kuwa nchi hiyo imebarikiwa kwa utajiri wa rasilimali hasa zile za asili.

"Kwa sasa vipo vikwazo vingi na sababu nyingi zinazochangia maliasili isiwe chanzo kikubwa cha maendeleo ya uchumi wetu; kwa mfano Azimio la Arusha limekuwa likijadili sana juu ya maendeleo kupitia ujamaa kwa bahati mbaya katika maudhui ya azimio hilo, maadili ya uongozi ndio yamepewa kipaumbele," alisema Mkapa.

Alisema ili kufikia malengo ni lazima kutimiza masharti manne ambayo yatagusa watu, ardhi, sera nzuri na uongozi bora ambapo kwa upande wa watu ni lazima wawe na elimu bora. "Kumbuka wahenga walisema Kuku mjinga alilala na njaa akiwa juu ya gunia la mahindi," alisema Mkapa.

Mkapa alisema Watanzania lazima wawe na ubunifu na elimu ya kutosha kuwandaa kutumia ujuzi wao huo katika kazi za kujenga taifa ikiwemo kutumia taaluma walizonazo, kutafuta na kuhakikisha wanafanikisha malengo yao kwa faida ya nchi yao.

Alisema pia suala la mtaji linapaswa kupewa umuhimu hasa katika sekta ya madini inayohitaji uwekezaji mkubwa ili kutoa matokeo mazuri tofauti na sasa ambapo teknolojia inayotumika ni ndogo na hivyo kufanya kazi hiyo kuwa na tija kidogo kwa taifa.

Naye Makamu Mwenyekiti wa Taasisi ya Uhandisi na sehemu ya Wahandisi wa Madini, Assah Mwaipopo, alisema lengo la mkutano huo namna ya kukiamsha chama cha wahandisi wa madini ambacho pamoja na kuwepo, lakini utendaji wake ulikuwa hafifu.
 
Hapo kwenye bold ndipo penye mtihani kwa hawa Wasomi/ Wanataaluma.

Kama Keil alivyosema hapa tatizo letu lipo kwenye siasa...hatuna siasa safi yenye kutoa viongozi wasafi. Turekebishe hilo...haya mengine yote itakuwa mteremko kuyarekebisha.

Mzalendo;

Unaweza ukashauri mbinu ya Kurekebisha hilo ni ipi na mkakati wa utekelezaji ni upi?
 
Constructive criticism ni nini? Umesema constructive criticism inambidi critic "awe na better perspective in comparable" hii sentensi haijasimama, inaelea elea tu.

Ndicho tunachofanya, nimesema kama kweli wako serious na the bigger picture Tanzania hawaonyeshi hivyo kwa mujibu wa maada zao, maada zao zinatuambia square root ya 64 ni 128, wakati tunajua square root ya 64 ni ndogo kuliko 64, hata kama hatuna jibu sahihi, tushaanza kupata the right direction, kwamba ili kuipata square root ya 64 itabidi tuangalie kuanzia 64 kwenda chini, sio juu.Hii ni step nzuri tu. Sasa utasemaje hatuna constructive criticism kwa sababu hatuna majibu?

Kwa hiyo si sawa kusema kama critics hawana jibu wasi criticise wakati criticism hata kama haina jibu kamili inaweza ku improve method ya kupata jibu.

Mzalendo Bluray;

Nakusoma na nadhani Critism zako zinasaidia kutupa changamoto. Sijui kama mada ulizisoma vizuri na kupata muda wa kuleflect.

Hata havyo njia mbadala unayoweza kuwa nayo ya WAPI TUNGEANZIA bila kukutana inakaribishwa.
 
Hizi ndizo criticism za mtindo wa akina Galileo,Einstein na Copernicus..????

Kuna tatizo gani kujadili haya..

Asante Mkuu umeziorodhesha mada:

1. Namna gani Wataalamu Wanavyoweza Kusaidia Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa katika Kujenga Uchumi Imara

2. Ni Vipi Wanataaluma Wanaweza Kusaidia Watanzania wa Kawaida Waweze Kushiriki Katika Ujenzi wa Uchumi wa Taifa na Kuboresha Maisha Yao

3. Jinsi Wanataaluma Wanavyoweza Kukabiliana na Changamoto katika Kuleta Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa, Kielimu, Kijamii, nk.

4. Namna Gani Wanataaluma Waliopo Nje ya Nchi Wanaweza Kushiriki Kuleta Maendeleo Nchini

5. Wanataaluma na Dira ya Maendeleo ya Taifa Letu: Tukotoka; Tulipo, Tunakokwenda: Changamoto na Ufumbuzi

6. Je, Ni Wakati Gani Mwafaka Wanataaluma Walazimike Kuchukuka Hatua za Kuleta Mabadiliko Na kwa Vipi?

7. Ni Mikakati Gani Watumie Wanataaluma Kupeana Habari na Taarifa Za Uhakika na kwa Muda Muafaka

Bado sifahamu kwa nini kuna baadhi wanafikiri mada hizo si za msingi na muhimu. Tunasubiri watoe mada mbadala ili tuzitumie siku za usoni.

Ukiangalia mada nyingi hapo utaona ni za kimikakati na Kiutendaji. Agenda namba 6, si kitu cha kuchezea.

Tunasubiri kupata agenda Mbadala kama zipo.
 
Wana taaluma ni nani hao? Mafundi mchundo wamo? Wauguzi wamo? Wapishi wamo? Na kwa nini tuwasikilize? Wana nini kipya? Na nini kinakipa hiki chama cha TPN na hao watakaohudhuria haki ya kuwazungumzia wana taaluma wote? Mimi naona tunaongeza msululu wa vyama, vyombo ambavyo kwa kweli havitakuwa na maslahi yeyote kwa mwananchi wa kawaida.

Amandla..........
 
Hakuna kipya hapa maana walishazibwa midomo wakati ule wa tamasha la Nyerere na kelele zao za bure labda watu wengine ndio waseme
 
Sanctus Mtsimbe said:
Asante Mkuu umeziorodhesha mada:

1. Namna gani Wataalamu Wanavyoweza Kusaidia Kuweka Vipaumbele vya Kitaifa katika Kujenga Uchumi Imara
Mr Mtsimbe,kama nimekupata unamaanisha kwamba ni kwa jinsi gani wataalam wanaweza kusaidia kuwepo na uzingatiwaji wa National interests katika kujenga uchumi?If the intepretation is correct,then we have a problem,kwasababu hata mafisadi na wao si wataalam?nikisema mafisadi namaanisha wale wataalam/wanasiasa wasiojali National interest na matokeao yake ndio uchumi tulio nao wa kuuza rasilimali na mwishowe kujulikana kama "shamba la bibi"
Kwahiyo solution hapo ni wataalam wasio mafisadi wakae pamoja wawaondoe wataalam mafisadi ngoma ianze upya maybe we can do something for the sake of the coming generation.

Sanctus Mtsimbe said:
2. Ni Vipi Wanataaluma Wanaweza Kusaidia Watanzania wa Kawaida Waweze Kushiriki Katika Ujenzi wa Uchumi wa Taifa na Kuboresha Maisha Yao
Kimsingi hoja yangu ya mwanzo iiliyokuwa ikijibu hoja yako namba 1,inaendana na hoja angu ya pili yenye malengo ya kuijibu hoja yako namba 2.

Kwanza hatuwezi kusaidia watanzania wa kawaida kama wataalam wa hoja yangu ya mwanzo "mafisadi" wataendelea kuwa na influence kwenye maamuzi muhimu yanayohusiana na National interest na uchumi wa Taifa kwa ujumla.

Kuwaondoa viongozi wanaowalaghai wananchi kuwa wanayaboresha maisha yao kwa pilao,kanda2 na kanga,badala yake kuwa na viongozi wenye kuzingatia kuwa uongozi ni dhamana,na wasiowatumia wataalam wachache kulifisadi Taifa,badala yake wautumie utaalam wao kuwasaidia wananchi kupata maendeleo both kisiasa,kijamii na kiuchumi,viongozi wasiokuwa wabinafsi na wasiokuwa na mawazo kama ya kuku ya kutizama hapo chini tu na kula wadudu na huku wana mabawa.

Sanctus Mtsimbe said:
3. Jinsi Wanataaluma Wanavyoweza Kukabiliana na Changamoto katika Kuleta Maendeleo ya Kiuchumi, Kisiasa, Kielimu, Kijamii, nk.
Ujumbe wangu mmoja kwenu wanataaluma wenye mwamko wa kutaka kuleta mabadiliko ni kwamba,kwa muda mrefu nimeona mkidhani kuwa vita dhidi ya ufisadi itakuwa successfull through some sort of grassroot movement,it is easy to conclude that,hata mimi nilikuwa nikidhani hivyo before,hata hivyo that itself is not enough,it is not the fundamental way to deal with the matter,lakini ukiangalia kwa makini,uki utacle ufisadi in a grassroot kind of movement,utakuwa ni sawa na kudeal na rushwa ndogo ndogo,na hivyo kuzidi kutoa a long leash kwa vigogo wa rushwa kubwa kubwa zinazogusa maslahi ya Taifa moja kwa moja,na viongozi wetu wanautumia udhaifu huo.Hii issue ni a top down movement,otherwise we're stuck,ama "screwed" kama alivyosema MKJJ,wale ambao tunawish watatuondoa kwenye ufisadi ndio hao hao wanaofanya ufisadi.

Kwenye jamii yetu,kwa wananchi wa kawaida mtu kupata mafanikio hata kama ni kwa ufisadi bado anaonekana shujaa flani,sasa ukitaka mentality kama hiyo ife,ni wale watuhumiwa wa rushwa kubwa kubwa ambao jamii ndiyo inalook upon as reole models wafanywe kuwa mfano,na hapo kila mtu apate kujua kuwa uongozi ni dhamana na si nafasi ya kufanya ufisadi,Nyundo ipigwe juu na impact iende hadi chini.Pia kuzingatia mawazo ya kitaalam zaidi ya kukumbatia siasa na wanasiasa wanapowatumia wataalam hao hao kuona ni kwanamna gani watawalaghai wananchi ili waendelee kubaki madarakani.

Kwahiyo changamoto yangu ni kwamba,kwenye utatu wa siasa jamii na uchumi,in regard to the situation that we're in,wapi pa kuanzia?binafsi naamini kama hakuna siasa safi basi the rest is nothing.

Sanctus Mtsimbe said:
4. Namna Gani Wanataaluma Waliopo Nje ya Nchi Wanaweza Kushiriki Kuleta Maendeleo Nchini
Kwanza tujiullize kwanini wengi wa wanataaluma hao wako nje halafu utagundua kwamba ndiyo sababu hiyo hiyo ambayo pengine uanataaluma wao hauhitajiki na wanasiasa ambao ndio shot callers,wanataaluma wenye mafanikio ni wale wenye kufanya yale wanasiasa wanayoyataka,regardless to National interests ama hata regular work ethics.Hata hivyo kwasababu bado tuna mapenzi na the coming generation,basi sidhani kama wanataaluma waliko nje watashindwa kushiriki kwenye kuleta maendeleo nchini kama wakiruhusiwa kufanya hivyo na kujengewa mazingira yenye kuruhusu kufanya hivyo,hiyo ni kama kweli wanataaluma wa kweli wanahitajika kwenye mustakabali wa the well being of our Nation.

Sanctus Mtsimbe said:
5. Wanataaluma na Dira ya Maendeleo ya Taifa Letu: Tukotoka; Tulipo, Tunakokwenda: Changamoto na Ufumbuzi
Hatuna direction yoyote kama Taifa,hatuna dira wala mwelekeo,mambo bado yako shaghalabhagala, yaliyokuwa yakipigiwa kelele decades zilizopita ni yale yale na in other situations even worst,we're stuck,ufumbuzi ni revolution ya namna moja ama nyingine,bila revolution how are we gonna "unscrew" ourselves?

Sanctus Mtsimbe said:
6. Je, Ni Wakati Gani Mwafaka Wanataaluma Walazimike Kuchukuka Hatua za Kuleta Mabadiliko Na kwa Vipi?
Mabadiliko kwenye nyanja yoyote ile hayawezi kuwa possible kama yasipokuwa facilitated na clean politics with clean politicians who puts the National interests first,then mabadiliko yeyote either ya kijamii ama kiuchumi ni ndoto,ukiweka maslahi ya Taifa kwanza basi uchumi unafuatia na jamii inaendelea na kuishi vizuri,unapata jamii yenye kujitosheleza.Sisi watanzania ni wanafki sana,hatuwezi kujadili kuleta mabadiliko ya kijamii na kiuchumi kama siasa ni mbovu na corrupt kama siasa zetu zilivyo,no wonder jamii inareflect siasa zetu,viongozi wetu wanajidai kuseparate na wakati ukweli ni kwamba wao wanachokifanya in reality mara baada ya kupata uongozi ni biashara na si kufacilitate mazingira mazuri ya kibiashara ama innovation nk,na kuyathamini mawazo innocent ya wataalam depending on nyanja zao na kuyapa kipaumbele, na ndio mana uchumi upo hapo ulipo,wanawapa wananchi maelezo ya kisiasa lakini in reality wanafanya mambo yanayougusa uchumi na maslahi ya Taifa kwa ujumla moja kwa moja.....Mambo ambayo ni kinyume kabisa na maadili ya uongozi bora.Na kwahivyo narudia ndugu Mtsimbe,revolution is the solution.

Sanctus Mtsimbe said:
7. Ni Mikakati Gani Watumie Wanataaluma Kupeana Habari na Taarifa Za Uhakika na kwa Muda Muafaka

Bado sifahamu kwa nini kuna baadhi wanafikiri mada hizo si za msingi na muhimu. Tunasubiri watoe mada mbadala ili tuzitumie siku za usoni.

Ukiangalia mada nyingi hapo utaona ni za kimikakati na Kiutendaji. Agenda namba 6, si kitu cha kuchezea.

Tunasubiri kupata agenda Mbadala kama zipo.

Kwenye namba sita kweli muhimu na ndio pa kuanzia,wanataaluma watendaji wengi ni wale wenye elimu lakini hawakuelimika na kwa hivyo kazi zao wanafanya kisiasa,hadi tuwe na wanasiasa na wanataaluma wenye kujali taaluma na kuzipa kipaumbele na si siasa na ulaghai.Mada hizi kweli ni za msingi,lakini pia ni muhimu kuwe na mazingira yenye kushawishi kuwa hakuna upotevu wa muda kwani kusema ukweli we are really really screwed!
 
Wana taaluma ni nani hao? Mafundi mchundo wamo? Wauguzi wamo? Wapishi wamo? Na kwa nini tuwasikilize? Wana nini kipya? Na nini kinakipa hiki chama cha TPN na hao watakaohudhuria haki ya kuwazungumzia wana taaluma wote? Mimi naona tunaongeza msululu wa vyama, vyombo ambavyo kwa kweli havitakuwa na maslahi yeyote kwa mwananchi wa kawaida.

Amandla..........

Mzalendo Fundi Mchundo;

Kwa tafsiri ya TPN:

Mwanataaluma ni mtu yeyote aliye na ujuzi wowote / taaluma yeyote bila kujali kiwango cha elimu yake.

Kwa hiyo Mafundi mchundo; Wauguzi;Wapishi n.k. as long as wanajitosheleza katika tasfsiri hii nao wamo.

Kwa nini tuwasikilize?

Preamble
Tanzania is among the poorest nations of the world where more than fifty percent of her population live below the poverty line; and that the main cause of poverty is under development which can be expressed in terms of unemployment, underproduction, high rate of illiteracy, low level of Science and Technology and imbalance in its trade balance caused by among others unmanageable external debt and lopsided international trade practices.

We founder members therefore:

· CONSIDERING the present environment in which we operate, lack of formal forum where we can contribute our expertise ,air our views and exchange our experience:

· HAVING REGARD to the National advantage to be derived from the effective and continuous co-ordination of activities and exchange of information on our professions:

· AWARE of the need for a forum for professionals to encourage the carrying out of studies, research and dialogue with other stakeholders on National problems and common interests and concerns to foster closer relationship between them:

· CONVINCED that the establishment of an Association would best serve these purposes:

Have decided to establish an organ known as TANZANIA PROFESSIONALS NETWORK (TPN) which aims to have a very strong base for building a better future and promoting and facilitating Socio - Economic Development.

OUR VISION
To transform Tanzania into a POWERFUL KNOWLEDGE BASED SOCIETY by the Year 2050.

OUR MISSION
To stimulate and promote effective use of the POWER OF THE BRAIN among Tanzanians in addressing and solving their various Social, Cultural, Economical; Environmental; Developmental and Psychological Problems.

Na nini kinakipa hiki chama cha TPN na hao watakaohudhuria haki ya kuwazungumzia wana taaluma wote?

Tanzania Professionals Network (TPN) is a Non-Governmental Organization which brings together Tanzania Professionals and body corporates within and outside the country to address cross-cutting issues. The top agenda being mobilizing our resources using the Power of Brain to empower economically Professionals and Tanzanians at large by using diverse opportunities which have already been identified.

TPN is registered under the Ministry of Home Affairs, Registrar of Societies under the Societies Act Cap. 337 R.E. 2002, with the Certificate of Registration certificate number SO. 9746
 
Na kwahivyo narudia ndugu Mtsimbe,revolution is the solution.

Mzalendo jMushi1;

Umeongea maneno mazito sana. Na bila ya shaka nitayafikisha katika kamati ya mikakati ya TPN ili yafanyiwe kazi.

Kwa maoni yako Mushi; REVOLUTION unayozungumzia ni ipi? Tunaanzia wapi na ni nini mkakati wake wa utekelezaji hasa ukizingatia mazingira ya sasa?
 
Sanctus Mtsimbe said:
OUR VISION
To transform Tanzania into a POWERFUL KNOWLEDGE BASED SOCIETY by the Year 2050.


OUR MISSION
To stimulate and promote effective use of the POWER OF THE BRAIN among Tanzanians in addressing and solving their various Social, Cultural, Economical; Environmental; Developmental and Psychological Problems
.

Ni kweli kuwa na a POWERFUL KNOWLEDGE BASED SOCIETY kunahitaji promotion ya efective use of POWER OF BRAIN ambayo ndiyo knowledge yenyewe,hapo ndipo kwenye tatizo sugu,wengi wana knowledge lakini utilization ni zero,kama nilivyosema hapo awali,je TNP mna mbinu gani za kuhakikisha kuwa walioelimika ama wenye ujuzi wanatumia ujuzi ama elimu zao towards solving those various Social,Economical,enviromental and psychological problems?Tuna matatizo kadhaa,kuna waliosoma lakini hawajaelimika,halafu kuna walioelimika lakini mazingira hayaruhusu mchango wao,na kama mchango wao ukiwepo si kwa maslahi ya Taifa,naomba tuweke msisitizo hapo,kuna a fundamental way to solve this problem,only kama tuki acknowledge na kuacha politics of nonsense...Politics zenye misingi ya kibinafsi,badala yake we need to implicate politics of common sense,politics that adhere to our National Interests....Je mission na vision za Taifa letu ni zipi?Je vinaendana ama kushabihiana na mission and vision of TNP?Kama ni tofauti basi lazima kutakuwa na conflict and we will be doomed before we even begin the mission.
Bila kuwa na the end to corrupt leadership hatwendi pahali hata kama tukifanya kongamano kwenye mwezi.
 
Mzalendo jMushi1;

Umeongea maneno mazito sana. Na bila ya shaka nitayafikisha katika kamati ya mikakati ya TPN ili yafanyiwe kazi.

Kwa maoni yako Mushi; REVOLUTION unayozungumzia ni ipi? Tunaanzia wapi na ni nini mkakati wake wa utekelezaji hasa ukizingatia mazingira ya sasa?

Mzalendo S. Mtsimbe;Viongozi wapya ama wenye mawazo mapya,ninapozungumzia mawazo mapya certainly ni mawazo tofauti na haya ya ki EPA,Richmond,Dowans,Buzwagi etc.

Mazingira ya sasa ya kisiasa ni lazima yabadilike ili kuwezesha hilo la wanataaluma kuchangia kwenye maendeleo ya Taifa,mazingira yabadilishwe na wanataaluma kabla ya lolote lile lenye kudaiwa kwamba ni "utumiaji wa taaluma kuleta maendeleo" kujadiliwa ama kufanyika.

Watanzania na waafrika kwa ujumla tuna tabia ya kuridhika na "mazingira" kama tunajua kuwa mazingira yaliyopo hayaruhusu progres ya kweli kwenye society yetu,then tukisema tuangalie namna ya kufanya "kwa mazingira yaliyopo" ni hali ya kuridhika na mazingira hayo.....Kwa mfano Mwiko ukivunjika haina maana kuwa ugali hautaliwa,ugali unaweza kuchelewa kuliwa lakini utaliwa provided tunajenga mazingira mazuri ya kupata mwiko mpya ama kuu reapair uliopo kwa namna ambayo utakidhi mahitaji ya ugali kuiva,ukitaka kuula ugali bila ya kujali mazingira yaliyopo ya mwiko kuvunjika,basi uwezekano ni mkubwa utaula mbichi.

Ndio situation tuliyomo,si lazima tujadili kuhusu maendeleo na wakati mazingira ya kupata maendeleo "endelevu" hayapo,we should work on mazingira first,..Kuhakikisha kwanza demokrasia ni ya kweli na uozo uliopo wa kiuongozi haupo tena....Kwa hiyo jibu langu ni kwamba kimsimamo sitaki "kuzingatia mazingira ya sasa" bali siyataki ama sikubaliani na mazingira ya sasa....Na siamini kabisa kwamba mazingira ya sasa yatatufikisha popote,labda some individuals kama ilivyo ada ya ubinafsi wa viongozi...Na kwahiyo basi REVOLUTION ninayoizungumzia ni ya kutuondoa kwenye mazingira haya ya sasa instead of working in the same enviroments with the same corrupts expecting different results.
 
am not sure kama niko ndani ya mada au nje lakini kuna vitu vinaniboa sana na haya wengi kati yao wataalam wa Kitanzania.

1.wanapenda sifa kuliko vitu tunavyovifanya,kuanzia waziri hadi mesenja wote wanadai credit tu,just wait 2010 utakavoona watu wanavyopanga mstari kupokea credit za UDOM etc.
2.ni wavivu-dont even start muda tunaopoteza "lunch" na "JF"
3.hawapendi kukosolewa,kuanzia mlinzi hadi mkurugenzi.
4.wana Tamaa-hadi secretary anataka kumiliki gari la 40M,wapi na wapi?kinachotokea ukienda kuimuona bosi utazungushwa weee hadi utoe hela ya "soda"
5.tu wadanganyifu,ni rahisi sana muuza super-market kuiba vitu kwa sababu tu hamna anayemuona/kumzuia,hasara kwa investors kesho supermarket inafungwa.
6.ni wababaishaji,kama unabisha mpe kazi mjenzi wa kitanzania au fundi cherehani sijui,utalia as if hela humpi,no wonder chinese are eating our bread.
7.wana elimu ndogo-hapa namaanisha "ujuzi" wa watu ukilinganisha kile kilichopo kwenye vyeti vyao,nishawahi kuombwa na mfanyakazi wa bank nimuelezee L/C inafanyaje kazi,nusura nimpe vibao.
ndio zile biashara mtu anajiita prof,dr,engineer mkurugenzi "peter".eeephw.last time amepublish anything viable was when he/she was defending whatever she has titles on during her academic encounters.
8.na mengineyo meengi..,si mahala pake hapa

sasa ukiangalia baadhi tu ya maono hayo hapo juu utaguindua kuwa ni kazi sana kwa kanchi haka kuendelea kama hakutakuwa na mabadiliko ya kiitikadi/kifikra/kimawazo.kwa kifupi hatutaendelea ng'o!

nafahamu ubadilishwaji wa fikra za watu sio kazi ya TPN lakini bila hili hawatafika mbali,kama vile wakilitazama hili kwanza.waulizane tu hapo kwenye mkutano/chama chao.ni wangapi wako tayari kulipwa kadri wafanyavyo kazi?wangapi wako tayari kukataa fedha za perdiem kutoka kwenye mikutano na safari hewa?!wangapi wako tayari kutokuwa matajiri sana ili nchi yao iendelee?
nadhani watabaki si zaidi ya 10.maana wafanyayo hayo huitwa wazembe,wajinga,wamelala etc.jamii inawadhihaki kwa kuwa si wezi.wote tunafahamu mishara ya TZ haiwezeshi mfanyakazi wa TZ kumiliki magari luxurious ma 3,kumiliki nyumba 4-5 etc.
we need to go back to basics kama wanavyosema baadhi ya wachangiaji huko juu.
 
Kuna wanaosema viongozi wetu/politics ni wala Rushwa hivyo ndio maana Tanzania ni masikini,

sawa ndio lakini hivi duniani kuna nchi kusiko na Rushwa?one of the most succesfull economies are also the most corrupt.

nionavyo mie,we have problems with our system.hii ndio inalea hawa wanasiasa wala rushwa,lets work on fixing the system not leaders/leaders will come and go,the system will be there to stay.

i believe we don't need a kikwete to fix poor services in public offices,do we?
Tunamlaumu sana kikwete,lakini the guy will come and go,even worse leaders than him will come.

swali kwa TPN,mmeandaa any specific solution ya tatizo Lolote lile ili wengine wafuate mfano wenu?
 
Na kwahiyo basi REVOLUTION ninayoizungumzia ni ya kutuondoa kwenye mazingira haya ya sasa instead of working in the same enviroments with the same corrupts expecting different results.

Kiongozi na Mzalendo Mushi nimekupa vizuri Mkuu;

Kwa maoni yako, suppose tunataka kuanza kutekeleza maoni yako, nilichopenda kujua tunaenda vipi kimikakati in terms of actions mpaka tufanikiwe? Nadhani hilo ndo kubwa kubwa na muhimu.
 
am not sure kama niko ndani ya mada au nje lakini kuna vitu vinaniboa sana na haya wengi kati yao wataalam wa Kitanzania.

1.wanapenda sifa kuliko vitu tunavyovifanya,kuanzia waziri hadi mesenja wote wanadai credit tu,just wait 2010 utakavoona watu wanavyopanga mstari kupokea credit za UDOM etc.
2.ni wavivu-dont even start muda tunaopoteza "lunch" na "JF"
3.hawapendi kukosolewa,kuanzia mlinzi hadi mkurugenzi.
4.wana Tamaa-hadi secretary anataka kumiliki gari la 40M,wapi na wapi?kinachotokea ukienda kuimuona bosi utazungushwa weee hadi utoe hela ya "soda"
5.tu wadanganyifu,ni rahisi sana muuza super-market kuiba vitu kwa sababu tu hamna anayemuona/kumzuia,hasara kwa investors kesho supermarket inafungwa.
6.ni wababaishaji,kama unabisha mpe kazi mjenzi wa kitanzania au fundi cherehani sijui,utalia as if hela humpi,no wonder chinese are eating our bread.
7.wana elimu ndogo-hapa namaanisha "ujuzi" wa watu ukilinganisha kile kilichopo kwenye vyeti vyao,nishawahi kuombwa na mfanyakazi wa bank nimuelezee L/C inafanyaje kazi,nusura nimpe vibao.
ndio zile biashara mtu anajiita prof,dr,engineer mkurugenzi "peter".eeephw.last time amepublish anything viable was when he/she was defending whatever she has titles on during her academic encounters.
8.na mengineyo meengi..,si mahala pake hapa

sasa ukiangalia baadhi tu ya maono hayo hapo juu utaguindua kuwa ni kazi sana kwa kanchi haka kuendelea kama hakutakuwa na mabadiliko ya kiitikadi/kifikra/kimawazo.kwa kifupi hatutaendelea ng'o!

nafahamu ubadilishwaji wa fikra za watu sio kazi ya TPN lakini bila hili hawatafika mbali,kama vile wakilitazama hili kwanza.waulizane tu hapo kwenye mkutano/chama chao.ni wangapi wako tayari kulipwa kadri wafanyavyo kazi?wangapi wako tayari kukataa fedha za perdiem kutoka kwenye mikutano na safari hewa?!wangapi wako tayari kutokuwa matajiri sana ili nchi yao iendelee?
nadhani watabaki si zaidi ya 10.maana wafanyayo hayo huitwa wazembe,wajinga,wamelala etc.jamii inawadhihaki kwa kuwa si wezi.wote tunafahamu mishara ya TZ haiwezeshi mfanyakazi wa TZ kumiliki magari luxurious ma 3,kumiliki nyumba 4-5 etc.
we need to go back to basics kama wanavyosema baadhi ya wachangiaji huko juu.

Mzalendo Kimweri'

You said it all. Kama vile ulikuwepo kwenye Kongamano.

Hayo niliyobold hapo juu ni moja ya hatua muhimu katika kutafuta ufumbuzi wa matatizo yetu.

Jisikie huru Mzalendo kushirikiana na TPN. Tutafika.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom