Kuunguruma kwa kongamano la Wanataaluma Dar: Moto wayaka!

Wengine wanatafuta channel za kutokea hapo

Wengine wanatafuta kuonekana nao wamo

Hamna aliye na kipya, ukiangalia maswali yao tu utaona kama wanataaluma ndio hawa bora labda hao wabeba boksi.

Bluray Maneno mazito sana haya.

Unaweza kutoa ufafanuzi?

Kisha tunaomba utupatie Njia Mbadala unayofikiri inafaa ya majibu ya matatizo yetu na utekelezaji.
 
Moja ya mikakati mikuu iliyowekwa na Kongamano ni kubadili mindset ili kuwa na mitazamo chanya.

Karibu kama una jibu mbadala.

Ndugu mtsimbe ukiendelea kujibu kila vijembe ndani ya forums haswa na watu wanaotumia majina bandia unaweza kukuta kilichomkuta zitto kinageuka kwako pia sasa basi kwakuwa wewe ni raisi wa TPN majibu unayoyatoa yawakilishe TPN nzima au sema kama unaongea kama mtu huru na sio raisi wa TPN
 
Umesahau, na ulaji (au Posho) kwa waandaaji pia, yaani kamati ya maandalizi ikiongozwa na mwenyekiti wao(keep change!) Haha hahaa...blah bla blaaa kwa sana!

Kazi kweli kweli.

Mkuu Kongamano hili halikuwa na posho yoyote wala ulaji. Sana sana, unajilipia nauli na gharama zote za kuishi DSM na pia unalipia Ada ya Ushiriki TZS 50,000 kwa ajili ya kufidia gharama zote za mkutano. Unakaribishwa kufanya ukaguzi wa namna yoyote kujiridhisha.

Hakika nawapongeza sana wote walioshiriki kwani wameonyesha uzalendo wa hali ya juu na nimeamini kuwa bado wako Wanataaluma wenye uchungu na nchi hii ingawa pia baadhi ya Wanaotuangausha ni Wanataaluma Wenzetu.

Let us change our mind set and the way we think.
 
Ndugu mtsimbe ukiendelea kujibu kila vijembe ndani ya forums haswa na watu wanaotumia majina bandia unaweza kukuta kilichomkuta zitto kinageuka kwako pia sasa basi kwakuwa wewe ni raisi wa TPN majibu unayoyatoa yawakilishe TPN nzima au sema kama unaongea kama mtu huru na sio raisi wa TPN

Mzalendo;

Ninayo imani kuwa wengi humu ni Wanataaluma na wanayo haki ya kupata majibu ya maswali yao. Ili mradi mimi ni Mwanachama hapa JF ninayo nafasi ya kutoa ufafanuzi.

Nia ni kuwa kama wakielewa na kukubali na kuunganisha nguvu, sote tutaongea lugha moja na kuwa chachu ya kuleta mabadiliko ya kweli.

Katika Thread hii naongea kama Mtsimbe na si President. Tutakapoa toa Press Release ambayo itakuwa signed, nitaongea kama President kwa kuwa nitakuwa najibu kwa niaba ya TPN na Wanakongamano kwa kadiri majadiliano yalivyofanyika.
 
Mh, hii ngumu kweli kwetu watanzania, ni nani tanzania anaweza kuandaa kitu kikapokewa na positive mazee?

Yaani inavunja moyo kweli

MTM;

Nashukuru umeliona hili.

Hata hivyo wanayo haki ya ku-react namna hii kwani watu wamekata tamaa na longo longo za miaka mingi.

Ndiyo maana moja ya mikakati tuliyokubaliana ni nini kifanyike kubadili mindset zetu.

Stay blessed.
 
Ndugu mtsimbe ulifikiriaje kuhusu NATIONAL THINK TANK naona nchi nyingi zina hizi national thinktank au TPN huko mbeleni ina mpango wa kuwa NATIONAL THINK TANK kwa kutumia wanataaluma ambao watakuwa wamejisajili kwenye Jumuiya Hiyo ??
 
Yaani! Hata kabla ya kuona matokeo yake yakoje tumetangaza wameshindwa. Duuh! Mi naomba jamaa wachukue hii ni kama challenge na kuthibitisha they mean what they say by action.Mtoto kabla ya kuanza kutembea, huwa anatambaa.Siamini kama huu nao ni mkutano kama mikutano mingine unless waandaji wameamua kufanya hivyo.Bado wana chance ya kufanya kitu tofauti.

Asante Mzalendo kwa angalizo.

Naona kuna baadhi wanavuka daraja hata kabla hawajalifikia.

mambo yalikwenda vizuri sana na kila kitu kitawekwa hadharani, kipimwe na kupata maoni ya ziada.
 
Ndugu mtsimbe ulifikiriaje kuhusu NATIONAL THINK TANK naona nchi nyingi zina hizi national thinktank au TPN huko mbeleni ina mpango wa kuwa NATIONAL THINK TANK kwa kutumia wanataaluma ambao watakuwa wamejisajili kwenye Jumuiya Hiyo ??

Mzalendo Shy;

Nadhani hili ni wazo zuri sana hasa ukichukulia moja kati ya maazimio ni kuwaunganisha Wanataaluma wote WAZALENDO wa fani tofauti na Vyama vyote vya Kitaaluma na vya harakati za Maendeleo.

Tutakapoyafanyia kazi ambayo tumekubaliana na yakaonekana, hakika tutakuwa tumejihalalishia kuwa THINK TANK YA TAIFA.

Una maoni gani?
 
MTM;

Nashukuru umeliona hili.

Hata hivyo wanayo haki ya ku-react namna hii kwani watu wamekata tamaa na longo longo za miaka mingi.

Ndiyo maana moja ya mikakati tuliyokubaliana ni nini kifanyike kubadili mindset zetu.

Stay blessed.

Rafiki yangu hilo la kukatishana tamaa ni kitu kibaya sana na kushambuliana Kibinafsi ni kitu kibaya sana ndio maana hata kwenye ufunguzi Dada Janet alisema hili jambo kwa uwazi kabisa na mimi naomba kuongezea wale wanaopenda kukatisha tamaa wenzao ni wale wanaojiona hapo walipofika ndio alama ya mafanikio yao wanajali wao na familia zao tu hawafikirii wale walio wengi ambao ndio wafanyaji kazi zaidi sehemu mbalimbali .

Ni maajabu sana kuona mtaani kwenu kuna tatizo la maji , mmoja wa wana mtaa anaamua kununua tanki la maji kwa ajali yake halafu anaanza kuuza maji hayo kwa majirani mtu kama huyu hata mkiwa na mkutano kujadili masuala ya maji msitegemee aje hapo hata akija atajaribu kulinda biashara yake kwa nguvu zote
 
Mimi nina matumaini sana na hawa jamaa. Lakini, tutapima ni maazimio na utekelezaji wake. Wasije wakajikuta wanaitwa majina na kina Makamba!

Mwanakijiji;

Jana kulikuwa na wawakilisha na wanasheria kutoka Mtandao wa Vyama vya Kisheria.

Sijui niseme nini.

Katiba yetu pamoja na mapungufu yote, bado inatupa uwezo mkubwa sana wa kuleta mageuzi na kuwawajibisha watendaji wabovu, bila hata kwenda kwenye siasa. Jana binafsi nimejiona nasutwa sana nafsi kwamba kwa uvivu wetu tunashindwa kuzielew sheria za nchi yetu zinazotupa haki ya msingi. Si hivyo tu, hata katiba yetu iko wazi.

Ni hakika kuwa wengi hawajui hata katiba ya nchi inasema nini na ni nini nafasi yao.

Hakika tuna safari ndefu lakini inayowezekana kwa matumaini makubwa. Tusaidiane kuiboresha nchi yetu kwa manaufaa yetu na vizazi vijavyo.
 
Rafiki yangu hilo la kukatishana tamaa ni kitu kibaya sana na kushambuliana Kibinafsi ni kitu kibaya sana ndio maana hata kwenye ufunguzi Dada Janet alisema hili jambo kwa uwazi kabisa na mimi naomba kuongezea wale wanaopenda kukatisha tamaa wenzao ni wale wanaojiona hapo walipofika ndio alama ya mafanikio yao wanajali wao na familia zao tu hawafikirii wale walio wengi ambao ndio wafanyaji kazi zaidi sehemu mbalimbali .

Ni maajabu sana kuona mtaani kwenu kuna tatizo la maji , mmoja wa wana mtaa anaamua kununua tanki la maji kwa ajali yake halafu anaanza kuuza maji hayo kwa majirani mtu kama huyu hata mkiwa na mkutano kujadili masuala ya maji msitegemee aje hapo hata akija atajaribu kulinda biashara yake kwa nguvu zote

Mzalendo Shy;

Hakika umeenda kwenye kiini hasa. Ni kama vile unaainisha Matatizo yetu ya ubinafsi Wanataaluma kuwa:
Kwa kuwa nina kazi nzuri
na kwa kuwa nina familia nzuri
Na kwa kuwa watoto wangu wanasoma "International Academy"
Na kwa kuwa nina gari
Na kwa kuwa nina nyumba
Na kwa Kuwa nina kipato cha ziada
etc
etc
.
.
Basi matatizo mengine ya nchi si yangu na ayanihusu kabisa. Huu ndiyo ubinafsi mkubwa wa Wanataaluma wengi kiasi kwamba hawataki tena kushughulikia maendeleo ya Nch na Watanzania kwa ujumla japokuwa uwezo wanao.

They dont want to waste time and pay the prices for change kwa kuwa to them it will not make any difference. Na hapa pia ndiyo kwa namna fulani panachangia ufisadi usipungue.
 
Ni kongamano zuri kwani kihistoria wasomi watanzania hawajwahi kuwa na mwavuli wao binafsi wakujadili mustakabali wa taifa lao.

Waandaaji wazingatie tahadhari mbali mbali zitakazopelekea mwavuli huu kutekwa na wanasiasa au wale wote wenye kutamani zaidi vyeo kwa faida ya nafsi zao..

Mwanzo mzuri TPN tunatarajia maamuzi bora ya kutupeleka mbeleee...

Asante sana Mzalendo;

Maneno yako yanatia matumaini sana.

TPN imejianisha wazi kuwa hatufungamani na Siasa; Dini; Kabila; Jinsia; Rangi; wala hali ya maisha.

Wanasiasa wote waliokuwepo walikuja kwa nafasi zao kama Wanataaluma; kwa hiyo hoja zote zilikuwa ni za Kitaaluma tu.
 
Tatizo la Tanzania ni la kisiasa zaidi na siyo la kiuchumi. .

Give me Five mtu mzima.

Mzalendo; hebu tusaidie kuliweka wazi.

Ni vipi tatizo ni la kisiasa zaidi? Tulipokutana hatukuongelea mambo ya Uchumi tu, kulikuwa na mambo mengi sana.

Je, unadhani kuna tatizo la Kiutendaji na kama lipo ni lipi?

Kisha tupe Maoni Mbadala nini kifanyike kwa vitendo.
 
Hawa wanaojiita wana taaluma hawana jipya bali wanatumiwa kama front kujaribu kucounter effect za KONGAMANO lililoandaliwa na Mwalimu Nyerere foundation!! Kongamano hili litakuwa ijumaa na jumamosi yamepamgwa maandamano ya kuwalaani wote wanaomkosoa Jakaya kwenye kongamano la mwalimu; sasa kama sio mbinu za kujikosha na kutaka kuhalalisha ufisadi ni nini basi? Wanataaluma wa kweli ni wale waliokuja kutoa maoni yao kwenye kongamano la wazi la Mwalimu Nyerere na sio hawa wanaoweka kiingilio kwenye kongamano ili wale wanaowajua na wenye fikra kama zao ndio waweze kuhudhulia na kupata press coverage!! I will not be surprised kama mwana Mtandao maarufu V.C. wa UDSM Mukandara anatumika katika hizi mbinu chafu za kudhoofisha fikra endelevu!!

Mzalendo Bulesi;

Tuhuma ulizozitoa ni kubwa sana na I wish zingekuwa na ukweli. Bila shaka utakapoona Maazimio na Mikakati, utafuta kauli yako.

Hata hivyo, si vibaya ukutuambia njia Mbadala ya kushughulikia matatizo yetu kama unayo, na wapi utaanzia utekelezaji.
 
Binafsi naamini TPN itafika mbali. Ni muhimu tuwe wavumilivu na kutoa ushauri na changamoto za kuweza kuisaidia TPN kufanikiwa katika mipango yake. Naamini wengi wetu humu ni wataalam katika fani mbalimbali, nashauri tuangalie uwezekano wa kujiunga nayo na kuhakikisha inafika mbali kwa maslahi ya taifa letu na watu wake hasa vijana na watoto.

Mzalendo Sabi; Asante sana kwa maneno ya kutia moyo.

Hakika kinachotakiwa sasa hivi ni kuunganisha nguvu kuhakikisha kuwa wote tunapigania kitu kimoja. maendeleo na ya msingi na kwa vpaumbele vinavyohitajika.

Natoa wito; wote tuiunge mkno TPN na Wanataaluma wote Wazalendo katika kuyafanya kazi matatizo yetu kwa kutumia mbinu za Kitaaluma.
 
MKJJ, nadhani kuunguruma kwao kutategemea wanaungurumaje. Kukiwa na mwelekeo ama elements za kukosoa utendaji wa Serikali ama kutoa tu ushauri wa nini kifanyike yanaweza yakawa yale yale ya Kongamano la kukumbuka kifo cha Mwalimu. Kongamano hilo litashutumiwa, yatatajwa majina ya waliosema hili na lile.

Kwa 'ujinga' wangu nilidhani yaliyosemwa na Wazee kwenye Kongamano la Mwalimu Nyerere, kwanza yataheshimiwa kwa kuwa yametoka vinywani mwa Wazee wa nchi hii, baadaye yatachujwa, yatachukuliwa ya msingi, na hatimaye yatafanyiwa kazi na Chama (CCM) ama na Serikali kwa manufaa ya taifa letu. Lakini, baada ya matamshi ya Makamba na Rais mwenyewe, na yaliyokuwa yakiripotiwa kwenye vyombo vya habari, ni wazi wananchi wameaminishwa kwamba Kongamano lile lilikuwa likimuandama Rais!

Tusubiri tuone la wasomi kitapokelewaje.

Mzalendo Bora Maisha;

Nadhani Wanakongamano walikuwa makini sana kutokujiingiza katika siasa.

mambo yote yalijojadiliwa yalikuwa ni ya kimsingi na bila kumlaumu mtu badi kutafuta majibu na nini kifanyike. Katika hili kama kuna atakayelifanya la kisiasa; hakika mikakati iliyowekwa itaprove kuwa yuko wrong.
 
Mzee Mwanakijiji,

Wakati wa maazimio kwa Tanzania umepita; kuna maazimio mengi sana ila hakuna utekelezaji.

Hawa wana taaluma wetu ni bora waazimie kutekeleza mambo machache kuliko kuja na maazimio kibao ambayo yataishia kapuni.

Kuna watu nawaamini kwenye hicho chama chao ila Watanzania tumesalitiwa mara nyingi sana na hawa wasomi wenzetu. Mimi kwasasa siamini tena blah blah! Nionyeshe umefanya nini kwenye haya mapambano, kisha nitaamini kama kweli uko serious.

Vinginevyo nawatakia mafanikio mema!

Mzalendo;

You said it all. 100% True.

Let us join forces pale mikakati inakapoonekana ni ya uhakika na inatekelezeka.
 
Mwanakijiji;

Jana kulikuwa na wawakilisha na wanasheria kutoka Mtandao wa Vyama vya Kisheria.

Sijui niseme nini.

Katiba yetu pamoja na mapungufu yote, bado inatupa uwezo mkubwa sana wa kuleta mageuzi na kuwawajibisha watendaji wabovu, bila hata kwenda kwenye siasa. Jana binafsi nimejiona nasutwa sana nafsi kwamba kwa uvivu wetu tunashindwa kuzielew sheria za nchi yetu zinazotupa haki ya msingi. Si hivyo tu, hata katiba yetu iko wazi.

Ni hakika kuwa wengi hawajui hata katiba ya nchi inasema nini na ni nini nafasi yao.

Hakika tuna safari ndefu lakini inayowezekana kwa matumaini makubwa. Tusaidiane kuiboresha nchi yetu kwa manaufaa yetu na vizazi vijavyo.

Sanctus,

Kwanza pole sana kwa hekaheka ya mkutano wenu; kuandaa hata tafrija ndogo ni kazi kubwa na mwisho wake huwa uchovu mkubwa wa akili na mwili.

Ninasikitika kusema kwamba hayo unayoyaandika, ndiyo yamekuwa yakisemwa na kuandikwa na wasomi mbalimbali kwa nyakati tofauti. Mimi niko kwenye hivi vijiwe vya wasomi wa Kitanzania kuanzia mwaka 1993 na niliyoyasikia na niliyoyaona wakitenda ndiyo yamenifanya niachane kabisa na haya makongamano au mikutano isiyo na mwisho.

Matatizo ya Tanzania yanajulikana na kinachotakiwa ni utekelezaji. Wengine katika kila tulichojaribu kufanya TZ, kumekuwa na ukwamishaji wa ajabu kutoka kwa hao hao wasomi wetu. Inafika mahali unajiuliza hivi neno uzalendo lipo tena kweli kwa hawa wasomi wetu?

Usifikiri watu wako negative kwenye comments zao kwasababu tu hawataki mabadiliko, hapana, ni kwasababu wengi wamekumbana na ujinga mwingi unaofanywa na wasomi kwenye maeneo ambayo ungetegemea mtu hata angeweka uzalendo mbele.

Kuna watu tunawajua kabisa wanakwamisha baadhi ya juhudi za Watanzania wenzao kujiletea maendeleo, lakini ukiwakuta kwenye makongamano wao ndio mabingwa wa kuongelea uzalendo na opportunities zilizopo. Mtu unaweza kuchukia ukamtukana mtu kama huyo kwa unafiki na ukaambulia kesi ya bure.

Mimi nitaunga mkono mara moja wanataalauma ambao wanatekeleza kwa vitendo matatizo yaliyopo. Kwa mfano wa mazingira wanaotumia elimu zao na ujuzi wao kusafisha mazingira au kuwachukulia hatua wanaoharibu mazingira. Madaktari wanaotumia ujuzi wao kuzuia uozo wa kuhamishia wagonjwa wetu kwenda kutibiwa nje badala yake wanatoa ujuzi wao kwa vitendo ili hospitali zetu ziwe bora na ziweze kuwahudumia Watanzania wengi zaidi. Wanasheria ambao wanatumia ujuzi wao kuwafikisha mahakamani wale wanaoliibia taifa letu na pia kuzipinga kwa vitendo sheria mbovu ambazo zinazuia maendeleo.

Leo hii ninavyoandika, kuna Watanzania wengi wako mikoani wakijaribu kutatua matatizo ya Watanzania wenzao kwa vitendo lakini wanakwamisha na wasomi kwenye vyombo vyao mbalimbali kuanzia TRA, TCRA, Wizara, mikoa, wilaya na ofisi zingine zenye mamlaka ambazo ungetegemea hawa wasomi watumie elimu zao kutatua matatizo badala ya kuongezea matatizo.

Mimi nawatakia mafanikio kwenye chombo chenu; kadri watu wengi wanavyoandika hovyo hapa ndio iwe motivating factor kwenu ili mufanikiwe na muweze kutuonyesha sisi wote kwamba tulikuwa wrong. Nitafurahi kupata maazimio yenu ili nijue wapi na wengine tunaweza kuunganisha nguvu.
 
Hatma ya watanzania imo ktk mikono ya watanzania wakielimishwa.

Nadhani hawa wanataaluma wangekuja na mkakati wa kuwakomboa watanzania kifikra hasa hasa kuchechemiza mapinduzi katika elimu ili ndani ya miaka 20 ijayo tusiongozwe na watu style ya mzee mapesa yaani wasomi wasio na maadili.

nina hisia kwamba wanaweza kuja na hoja kinzani dhidi ya yaliyojiri ktk kongamano la MNF. Kama watafanya hivyo basi maneno ya mwalimu yatatimia kwamba kusoma kwingi ni kuelekea ujingani kama hautachukua tahadhari

Mzalendo Msanii;

Kama vile ulikuwepo.

Hilo liko katika moja ya maazimio na mkakati wake wa utekelezaji nimeupenda sana na naamini utafanya kazi.

Kubwa ni kuwa inatakiwa wote tuwe sehemu ya mageuzi na tusiwaachie wachache.
 
Sanctus,

Kwanza pole sana kwa hekaheka ya mkutano wenu; kuandaa hata tafrija ndogo ni kazi kubwa na mwisho wake huwa uchovu mkubwa wa akili na mwili.

Ninasikitika kusema kwamba hayo unayoyaandika, ndiyo yamekuwa yakisemwa na kuandikwa na wasomi mbalimbali kwa nyakati tofauti. Mimi niko kwenye hivi vijiwe vya wasomi wa Kitanzania kuanzia mwaka 1993 na niliyoyasikia na niliyoyaona wakitenda ndiyo yamenifanya niachane kabisa na haya makongamano au mikutano isiyo na mwisho.

Matatizo ya Tanzania yanajulikana na kinachotakiwa ni utekelezaji. Wengine katika kila tulichojaribu kufanya TZ, kumekuwa na ukwamishaji wa ajabu kutoka kwa hao hao wasomi wetu. Inafika mahali unajiuliza hivi neno uzalendo lipo tena kweli kwa hawa wasomi wetu?

Usifikiri watu wako negative kwenye comments zao kwasababu tu hawataki mabadiliko, hapana, ni kwasababu wengi wamekumbana na ujinga mwingi unaofanywa na wasomi kwenye maeneo ambayo ungetegemea mtu hata angeweka uzalendo mbele.

Kuna watu tunawajua kabisa wanakwamisha baadhi ya juhudi za Watanzania wenzao kujiletea maendeleo, lakini ukiwakuta kwenye makongamano wao ndio mabingwa wa kuongelea uzalendo na opportunities zilizopo. Mtu unaweza kuchukia ukamtukana mtu kama huyo kwa unafiki na ukaambulia kesi ya bure.

Mimi nitaunga mkono mara moja wanataalauma ambao wanatekeleza kwa vitendo matatizo yaliyopo. Kwa mfano wa mazingira wanaotumia elimu zao na ujuzi wao kusafisha mazingira au kuwachukulia hatua wanaoharibu mazingira. Madaktari wanaotumia ujuzi wao kuzuia uozo wa kuhamishia wagonjwa wetu kwenda kutibiwa nje badala yake wanatoa ujuzi wao kwa vitendo ili hospitali zetu ziwe bora na ziweze kuwahudumia Watanzania wengi zaidi. Wanasheria ambao wanatumia ujuzi wao kuwafikisha mahakamani wale wanaoliibia taifa letu na pia kuzipinga kwa vitendo sheria mbovu ambazo zinazuia maendeleo.

Leo hii ninavyoandika, kuna Watanzania wengi wako mikoani wakijaribu kutatua matatizo ya Watanzania wenzao kwa vitendo lakini wanakwamisha na wasomi kwenye vyombo vyao mbalimbali kuanzia TRA, TCRA, Wizara, mikoa, wilaya na ofisi zingine zenye mamlaka ambazo ungetegemea hawa wasomi watumie elimu zao kutatua matatizo badala ya kuongezea matatizo.

Mimi nawatakia mafanikio kwenye chombo chenu; kadri watu wengi wanavyoandika hovyo hapa ndio iwe motivating factor kwenu ili mufanikiwe na muweze kutuonyesha sisi wote kwamba tulikuwa wrong.

Mzalendo Mtanzania;

nakushukuru sana. Ni kama vile ulikuwepo kwenye Konamano maana haya pia yaliangaliwa. Ilikuwa ni kama tulikuwa tuna-Think outside the box na kufanya postortem kujua hivi shida yetu hasa ni nini au tumelogwa.

Ninaloonekana kwanza ni ukosefu wa Uzalendo; Ubinafsi na Mindset zetu. Haya lazima yabadilike kwa kutumia mikakati ya Kielimu, kampeni, mawasiliano na kuunda mtandao imara utakaofika kila mahali.

Matazitizo ya kiutendaji sasa yamepatiwa majibu na utafiti unaendelea. Mitandao ya wanasheria itafanya kazi na wanataaluma wazalendo kuhakikisha kuwa sasa hatua zinachukuliwa. pale ambapo hakuna majibu ya kisheria, then advocacy, kampeni, lobbying, pressure vitatumika.

nadhani ni vizuri tukiendelea kujua weakness zetu na kisha kujiwekea mikakati ya mabadiliko mabayo ni endelevu.
 
Back
Top Bottom