Kutumia umeme units 75 kwa mwezi(tariff 4) ni kujidanganya ama kudanganya

Ahsante sana ndg kwa kuanzisha mada hii japo Kuna upungufu kidogo lakini Ina ukweli mwingi.

Mimi kwa zaidi ya miaka 5 nimekuwa natumia unit 60-65 kwa mwezi. Sikuzote nalipa gharama ya watumiaji wa kati. Kwa mwezi bili yangu Imekuwa elf30.

Nilifanya tathimini ya kina ninatumia unit 2 kwa siku. Nina friji moja ndogo, pasi, radio na heater ya kuchemsha maji ya kuoga. Siwashi taa za nje japo kwa dharula. Nina vyumba 3 na sebule.

Nilitegemea labda Kwakuwa unakuwa unanunua umeme kila mwezi unaingizwa kwenye kundi husika automatic. Lakini sio hivyo. Nilijaribu kufuatilia tanesco Kuna figisu nyingi. Mara andika barua nikaandika hakuna mabadiliko. Nimefuatilia Kuna watu wengi wanaotumia chini ya unit 75 lakini wanalipiswha bei ya juu.

Nina nyumba mkoa mwingine nililazimika zinitoke kidogo ndo nikaingizwa kwenye taarifu sahihi. Wanakaa wapangaji na bill haizidi elfu kumi Maana matumizi yao ni chini ya 75. Kwa nyumba ninakoishi kwa sasa nimeamua Ngoja nitulie tu ila kwa sababu nitahama soon. ila nikihamia kwangu mwezi ujao nitakomaa.

Tanesco wanawaibia wengi katika hili amini usiamini
 
Unit 75 kwa mwezi labda uwe una charge smartphone na kuwasha kingamuzi bila TV tuu...
Ndg yangu Unit 75 ni nyingi mno. Inawezekana hukuwahi kufanya tathimini. Mini ninahakika na hili kabisa. Pamoja na vyombo nilivyotaja hapo juu Nina TV ambayo inatumika tena mda mwingi.
 
Kutumia Chini ya Units 75 Umeme kwa mwezi basi utakuwa bachelor au mbahili,Mie nalamba zaidi ya units 200 kwa mwezi,Taa 8,Friji 24hrs,TV Nchi 42,Pasi,Brenda,Jagi la Chai.
Kama husemi uongo una leakage moja ya hatari. Mimi Nina vifaa kama hivyo natumia chini ya 75. Nakushauri ufanye utafiti wa waya zako.
 
Dah! Hili la umeme mi kila mwezi natumia unit zaidi ya 200, maana elfu 90 mpaka 100000 lazima nimalize, nyumba yangu ya kawaida ya kuishi, matumizi ya vifaa muhimu ni kawaida, friji, pasi, tv, feni, ac mara chache
Check wiring...pia uchakavu wa nyaya na pia earth rod kama haviko vizuri matumizi ya umeme huwa juu maana kuna umeme mwingi pia hupotea.tizama pia aina na watts ya taa unazotumia
 
Mkuu kwa sasa hakuna habari ya barua ya maombi ya tariff 4, pengine wewe unanunua umeme bila mpangilio.
Kwa ushauri basi; usi nunuwe umeme zaidi ya sh26000 kwa mwezi, hakikisha huzidishi kwa mda wa miezi 6, then wao tanesco automatically watakuingiza tariff 4
 
Hatutaki gharama za maisha zipande lakini usijidanganye watumiaji wa umeme kwa kiasi hicho hawapo, mtembee nchi ni kubwa sana hii sio Dar pekee. Wapo watu hutumia 20 units kwa mwezi na ni WENGI sana sana hasa zama hizi za umeme vijijini. Mtu yupo NJOMBE, friji, kiyoyozi, feni vya nini? Pasi jumapili tu au Ijumaa kunyooshea nguo za ibada, shambani tunaenda tumepiga pasi. Jiko la umeme bado ni hadithi (kwanza tunayaigopa, yanakula umeme hayo). Huwezi kutumia units 30 kwa taa na Tv pekee kwa mwezi. Kipindi kile cha service charges ilikuwa kama una matumizi chini ya 75 units unaomba kuondolewa service charge na hata nyumbani kule kijijini tulifanya hivyo maana tulikuwa hatutumii kiasi hicho.
hukumwelewa mtoa mada
 
taa ziko 15.
Kama kila taa ina 20W na ni energy saver zikiwaka wastani masaa 2 kwa siku kwa mwezi unit 18.

fridge 1.
Assumption ni ya kubwa ya mlango mmoja. 100W na themostat ni nzuri. Itawaka abt 4hrs kila siku km huzimi ukutani. Kwa mwezi unit 12.

TV mbili.
Hujataja aina. Ila km ni bapa za nchi 32 kila moja 85W. Zikiwaka 1hr kila siku kwa mwezi unit 5.1

Water pump
Km ni Pedrollo ndogo ya ndani 370W kila siku ikiwaka 0.5hrs kwa mwezi unit 5.6

rice cooker 1
Labda ya Kenwood 2kg ina 1500W unapikia kwa nusu saa daily. Kwa mwezi ubit 22.5

Pasi.
Labda Phillips ile ya kijivu. 1100W. Unapasia daily nusu saa wewe na mwenzio jumla unit 16.5 kwa mwezi.

JUMLA KUU unit 79.7 kwa mwezi. Kwa maneno yako "... sijawahi kuvuka unit 70 kwa mwezi ..." nina mashaka.

Maana hapo bado kuchaji simu excess za kuacha pasi on mda mwingi au kupasi nguo kdg kdg. Hujaweka Home theatre au redio kubwa, King'amuzi wala taa za nje. Blender wala toaster wala micro wave hujaweka.

Funguka jamaa.
Mkuu Naomba unifanyie makadirio ya matumizi yafuatayo ili nijue matumizi yangu yatakuwa kiasi gani makao mapya.

1. Taa 3 energy server wat18 zitawaka masaa 4
2. Taa 4 energy server wat18 zitawaka wastani wa dk 30 kila moja
3. Taa 2 energy server Wat18 zitawaka masaa 12 kwa siku.

4. Fridge ndogo mlango mmoja itawaka masaa 24
5. Tv flat screen inchi32 itawaka masaa 5 kwa siku

6. Birika la kuchemsa maji lichemshe mara 3 kwa siku
7. Pasi itumike dk 15 kwa siku

Ahsante sana
 
Pc na video hazina matumizi makali ya umeme,watu wanamaliza umeme kwa pasi(mwingine akishamaliza kunyoosha nguo hachomoi pasi wala kuzima hatari)jagi la umeme,jiko la umeme,friji kukesha. Ukitaka kujua unit 28 ni kubwa sana kwa mwezi subiri UFILISIKE (sikuombei mabaya)ila ndio ukweli huo,maisha haya.
Ukiwa peke yako
1.ukiwa chumbani unawasha taa/tv etc chumbani tu.
2.ukienda kazin/out hamna kinachotumika labda friji.

Lakini ukiwa na familia wewe uko chumbani na tv yako au pc watoto wako sebuleni na tv na playstation yao. Ukienda kazini/out nyumbani kuna watu wanaendelea kutumia umeme.
 
Kwangu natumia unit 56 tu kwa mwezi. Nyumba yangu nimeweka taa 4 za nje za Wat 18 kila upande, room za ndani zote nimeweka za wat 12 mwanga mkali tu. Tv Led nch 32 na kingamuzi cha zuku na pasi. Frijinatumia kwenye friza tu ambapo asbh inawashwa kwa masaa mawili na usiku lisaa limoja hapo hakuna kitu kinaharibika. Muhimu hakikisha asbh mapema sana unazima taa za nje ikiwezekana hata saa 11. Taa za room zizimwe kama mko sebleni.. So kwenye unit 75 nikitumia 56 kila mwezi na save 14 baada ya miezi mitano tu nakua sijibani tena mtaji unakua upo wa kutosha
Unalipa sh. Ngapi?
 
Napata shida kama ewura wamekurupuka. Uwekezaji wa kisiasa yaani political capitalization ndo chanzo cha maamuz ya áibu. Tang lini tanesco wapelek maombi bila briefing kwa waziri wa secta husika.hilo changa la macho
 
nalipa elf tisa mia moja kupata unit 75 ambazo natumia mwez mzima na zinabaki
Wengine tunauziwa units 56 kwa shs 20,000/ haizalishi utatumia kiasi gani kwa mwezi, just kwa sababu tuliwekwa ile tarrif nyingine tena bila kuuliza. Waliotoa mlungula kidogo wako kwenye hiyo tariff yako despite wanakila kitu majumbani mwao: full kiyoyozi, friji 24/7, electric cookers with oven ana grills 24/7 and so on.
 
Dr.akili kuna fridge linakula umeme wa Tsh 20,000 kwa siku moja basi hatari badilisha hilo litakuua mkuu...unatunza nini mpaka ughalimie kiasi hicho kwa siku moja angalua hesabu zako vizuri ingawaje kayaman hayupo sahihi..
Huyu jamaa mwenyewe kanishtua sijui hesabu za wapi hizo?
 
Mkuu kwa sasa hakuna habari ya barua ya maombi ya tariff 4, pengine wewe unanunua umeme bila mpangilio.
Kwa ushauri basi; usi nunuwe umeme zaidi ya sh26000 kwa mwezi, hakikisha huzidishi kwa mda wa miezi 6, then wao tanesco automatically watakuingiza tariff 4
Ushauri mzuri.ila muongozo huu umeupata wapi? maana mie pia matumizi yangu ya umeme yako ndani ya sifa unazozitaja toka 2009 nahangaikia kubadili tarifa yangu ila ni shida tupu.Hawako wawazi na hakuna customer care desk inayoeleweka.Nilikata tamaa nikaamua niache wajipigie tu maana hakuna namna.
 
Badilisha appliances mkuu. Hapo kuna tatizo kubwa kwenye vifaa vyako. Watt 20 za taa ni nyingi. Mie maeneo mengi watt 3
Sio vifaa vyangu hivyo. Nilimjibu mtoa mada. Btw...... balbu za wati 3 ni za aina gani? Unatumia maeneo gani?

Maana usijedhani unaokoa gharama za umeme kumbe humohumo unajiandalia balaa la macho mbeleni.
 
Mimi nina tv,friji,microwave,washing machine,music system,electric cooker,kettle,taa 16 ndani, nje taa 6 lakini umeme situmii zaidi ya 40,000/- kwa mwezi.

Why ? Kwasababu
1.niko peke yangu
2.natoka asubuhi narudi usiku siku sita kwa wiki. Muda ninaotumia umeme hauzidi masaa mawili, friji nazima.

Kwahio sio una nini ila ni kiasi gani unatumia hivyo vifaa vya umeme ulivyonavyo.
vitu vyote hivyo uko peke yako? naomba ushemeji nikupe mdogo wangu plz
 
Sio vifaa vyangu hivyo. Nilimjibu mtoa mada. Btw...... balbu za wati 3 ni za aina gani? Unatumia maeneo gani?

Maana usijedhani unaokoa gharama za umeme kumbe humohumo unajiandalia balaa la macho mbeleni.
Zipo fine ni LED. Zipo mjini kwenye maduka ya vifaa vya umeme. Ukisoma review yake mitandaoni, iko poa
 
Mkuu Naomba unifanyie makadirio ya matumizi yafuatayo ili nijue matumizi yangu yatakuwa kiasi gani makao mapya.

1. Taa 3 energy server wat18 zitawaka masaa 4
2. Taa 4 energy server wat18 zitawaka wastani wa dk 30 kila moja
3. Taa 2 energy server Wat18 zitawaka masaa 12 kwa siku.

4. Fridge ndogo mlango mmoja itawaka masaa 24
5. Tv flat screen inchi32 itawaka masaa 5 kwa siku

6. Birika la kuchemsa maji lichemshe mara 3 kwa siku
7. Pasi itumike dk 15 kwa siku

Ahsante sana

Najibu kwa namba unit ni kwa mwezi.
1. Unit 6.5
2. Unit 1
3. Unit 13
4. Unit 12. Km friji mpya haitazd 6hrs za kazi japo iko on 24hrs. Inatumia themostat. Jitahd ijae vitu inapunguza sn ulaji umeme. Vitu vinaambukizana baridi so thmstt inakata mda mrefu. Assumption 67W type LG.
5. Unit 13. Assumption 85W
6. Unit 22.5. Assumption Kenwood 2ltr. 3000W. Kila mchemsho labda 5mins.
7. Unit 8.25. Pasi ya Philips Diva. 1100W

JUMLA KUU Units 76.25 kwa mwezi!!

Ukipambana unaeza shuka japo hujaweka vitu km redio, chaja, toaster n.k.

Jitahd sn usiache friji tupu na hakikisha themostat yake ni nzima. Km hujanunua bado basi nunua mpya. Sio used. Original brands zinadumu zaidi ya miaka 10 bila hata kutumia fridge guard.

Usiwashe Tv unnecessarily. Masaa matano daily huna hata matembezi mazoezi n.k mkuu?

Jagi tumia iwapo gesi imeisha. Kuokoa gesi, km maji ya kuoga, weka tu kdg ili yachemke haraka.
 
Ndugu mm nipo kwenye tariff hiyo tokea mwaka 2013, na kwangu tuko wawili ila sometime napata wageni, 3 bedrooms taa ziko 15 ila haziwaki kwa wakati mmoja, fridge, tv mbili, water pump, rice cooker na pasi, na sijawahi kuvuka unit 70 kwa mwezi gharama ya umeme in 6000 na maji unit 5 shillingi 8000 na sijafanya makeke yeyote Yale!
Ndugu unamaanisha au?
 
Back
Top Bottom